Friji la mtumba
JF-Expert Member
- Apr 7, 2024
- 277
- 434
Ndugu zangu wababa na wavulana wenzangu,
Nimekaa nikafikiri, nikasema ngoja niwape ukweli bila chenga – KUOA ni raha, ni utamu, ni burudani ya moyo na mwili, ila kwa wale walio tayari na wanaelewa maana ya kuwa na mtu wako wa kudumu.
Na sasa ngoja nizungumzie kwa staha lakini bila kujizuia – tendo la ndoa ukiwa umeoa halifanani hata kidogo na mchezo wa kujificha ficha gesti au "naomba usiku mmoja". Huko ni sprint, huku ndani ya ndoa ni marathon.
Kuna utulivu, kuna mawasiliano, kuna kucheza na siyo mashambulizi tu. Mke anajua mapenzi yako, mwili wako, na muda wako wa mabadiliko ya hali ya hewa. Hapa kazi inafanyika kwa hisia na heshima, sio presha ya dakika 10 kabla ya mlinzi kubisha mlango.
Na ukishamaliza? Hamlali mbali. Huna wasiwasi wa "nimtume Uber aende?". Hapo hapo unalala, unashikilia, unacheka, labda mkiwa fiti mnarudi round mbili au tatu – bado ni halali yako.
Kaka zangu, kama bado hujaoa kwa sababu unafikiri ndoa ni kifungo – basi ujue bado upo hujajisoma. Ndoa nzuri ni kama chama cha akiba na mikopo ya mapenzi, unachangia upendo kila siku, faida yake inakuja kwa amani ya moyo, utulivu wa mwili, na burudani ya maisha.
Wanaume wenzangu, hebu tusaidiane:
Wewe ambaye umeoa – ni raha gani kubwa umewahi kuipata ndani ya ndoa?
Na wewe ambaye bado hujaoa – ni nini kinakufanya usikimbilie huu utamu?