Utamkumbuka Benard Membe kwa lipi?

JF Member

JF-Expert Member
Dec 14, 2014
7,398
9,680
Membe.jpg

Picha: Benard Membe

Kwa kawaida Hawa watu walioshika nyanja za juu za uongozi na wakagombea urais Huwa Wana miguso katika jamii.

Sasa Uzi huu utakuwa kwa ajili ya kumbukumbu ya Membe.

Kati ya Mambo yanayokumbukwa kwa ajili ya Mh.. Membe kutoka kwa jamii ni kama haya hapa.

1. Kula pesa za Libya.

2. Kusimamia misimamo yake wakati wote.

3. Kutataa kumsamehe Msibani waziwazi siku chache kabla ya kifo.

4. Waziri ambae hakuhusishwa na ufisadi wa Moja kwa Moja kutokana na majukumu yake hapa nchini.

N k.
 
Sasa mkuu yaani na wewe ulitaka ule pesa za libya...Huwezi jua labda na yeye aliliwa,,,,maana waarabu hawatoi pesa bure...Afu nani alikuambia watanzania walikua na shida na pesa za waarabu wa libya???
 
Ninachojua wabongo tunapenda Sana kuchafuana ila

Membe kwa kazi za ujasusi alizozifanya kwa taifa ili hapaswi kupewa vijembe kama watu wanavyofanya.

Mtu unalala, unaamka, unatembea,unakula, unavimbewa, unakunya na kukesha baa, unaona nchi ipo huru unaropoka tu na huelewi wakina nani wanafanya ufanye hayo ...!

Achana na wanasiasa uchwara wengi wa ccm katika watu muhimu taifa limepoteza Basi Ni Mahiga na Membe R.I.P.

Tuache chuki mambo ya kusema mtu wakati una ushahidi!! Pesa za libya zilikuwa pesa ndogo Sana hazifiki hata bilioni 10 na ziliibiwa kwa ajiri ya uchaguzi wa ccm sio Membe aliyeiba izo pesa!!!

Fanyeni siasa zenu lakini mtu kama alifanya mazuri mpeni maua yake!!

Kwangu mimi Membe simdai katuokoa na mambo mengi Sana kama taifa tungekuwa tunajuta sasahivi kuwa na madicteta uchwara, Rais fisadi Lowassa, vyama uchwara vya upinzani kushika dola.

Kosa lake kubwa ni kutaka kuwa rais wakati ni mtumishi wa idara hii tu ndio imemponza maana ni mwiko mtumishi wa idara kuwa Namba moja!!!

Rest in peace Membe!!
 
Hivi mkuu JPM hakua na mapungufu?????

Alikuwa nayo tena mengi

Ila katuachia mengi zaidi mazuri

Katuonyesha kuwa nchii hii inaweza ikanyooshwa na watu wakawa wanalialia kuomba msamaha kwa ufisadi wao.

Nchi ilinyooka jmani

Nikiri wazi yule jamaa alikuwa ni mwamba

Hakuna msoga wala upumbavu wote walikuwa wanajificha makwao
 
Akiwa waziri wa mambo ya nje alihakikisha mission ya Moroni/commmoro inakamilika kikamilifu na kwa mafanikio ya kuwafurisha waasi lkn pia Sudan na sehemu mbalimbali.

Wakati wake aliimarisha mahusiano kati ya mataifa mbalimbali Duniani.

Utengamano wa maziwa makuu.

Mambo ni mengi sana, yanayo fahamika wazi ni mavhache lakini ambayo hayafahamiki wazi lkn mazuri kwa Taifa letu ni mengi sana.
 
Mna uhakika zile barua kutoka kwa viongozi wanaojiita wameshika dini hazikuwa na ungaunga wowote uliochoronga mfumo wa hewa wa mheshimiwa?
 
Ninachojua wabongo tunapenda Sana kuchafuana ila

Membe kwa kazi za ujasusi alizozifanya kwa taifa ili hapaswi kupewa vijembe kama watu wanavyofanya...

Siasa imepaka mavi wengi,sababu ya ujasusi wa ndugu yetu kuingia matopeni ni siasa.

Majasusi wanaonekana mbuzi sababu ya siasa.
Wanajeshi wazalendo wanaonekana vituko sababu ni siasa.
Polisi bora kabisa wanachafuka kwa siasa.

Hakuna aliye salama mbele ya siasa.
 
Back
Top Bottom