Je, Membe kosa lake kubwa ni kutaka kuwa Rais wakati yeye ni jasusi?

technically

JF-Expert Member
Jul 3, 2016
11,975
48,843
Poleni na msiba ila kwangu mimi Membe kwa kazi aliyoifanya sina ninachomudai. Tumepoteza mtu mwadilifu Sana pengine moja ya vijana waliopikwa na Nyerere pia mtu wa kitengo ambaye alifanya kazi zake kwa ufanisi wa Hali ya juu Sana.

Kama kuna watu tumepoteza kama taifa Basi ni Membe na Mahiga Hawa watu wawili walikuwa engine ya nchi hii haswa.

Wametuepusha na vitu vingi Membe alisaidia sana harakati za kuondoa Rais dicteta nchi hii na kuvunja mfumo wake wote aliokuwa anautengeneza kutawala Tanzania milele.

Membe ndiye alisaidia mwaka 2015 tusipate Rais fisadi ingawa anatukanwa lakini yeye ndiye alisimama kidete sasahivi labda nchi ingekuwa imeshauzwa kabisa.

Udikteta ni hatari kwa nchi kama ilivyo kwa ufisadi fikiria kama Magufuli angendelea kutawala milele Hali ingekuwaje uko mtaani?

Fikiria kama Lowassa angeingia Ikulu hali ya ufisadi ingekuwaje sasa hivi?

Lakini Membe alisimama kama mtu Kati kuzuia majaribio yote mawili na alifanikiwa.

Tunamdai nini watu watasema pesa za Libya? No pesa za Libya waliiba ccm kwa ajiri ya uchaguzi sio Membe.

Tunawaambia kila siku nchi hii ina tatizo la mfumo hamtaki.

Membe apumzike kwa amani kapigana vita yake kwa umakini mkubwa Sana na ameimaliza kosa lake kubwa ni kutaka kuwa Rais wa Tanzania wakati yeye ni spy hakuna kitu kama icho katika mfumo wa Tanzania na ameshaambiwa ilo kabla.

Apumzike kwa amani alikuwa mtu na nusu apewe maua yake kwenye kaburi lake.

R.I.P
 
2015 Membe mwenyewe alikuwa akiitaka ile nafasi, bahati mbaya ushindani ulioibuka ndani ya chumba cha mkutano baada ya jina la Lowassa kukatwa, ukasababishwa Membe nae akatwe ili kutuliza hali ya mambo.

Hizo sifa nyingi ulizompa hapo juu sioni kiuhalisia kama alikuwa nazo, kwangu alikuwa anasubiri kubebwa na rafiki yake Kikwete awe Rais wa JMT, lakini yeye binafsi sikuwahi kumuona kama mwanasiasa mwenye ushawishi wa aina yoyote ili kufanikisha hiyo ndoto yake.

Kwa hali hiyo, naona ungemlaumu zaidi yule aliyetaka Membe awe Rais wakati akijua alikuwa jasusi, Membe ni kama alishawishiwa tu achukue fomu agombee akiaminishwa atakuwa, lakini bahati mbaya mambo yakaenda sivyo.
 
Poleni na musiba ila kwangu mimi Membe kwa kazi aliyoifanya sina ninachomudai. Tumepoteza mtu mwadilifu Sana pengine moja ya vijana waliopikwa na Nyerere pia mtu wa kitengo ambaye alifanya kazi zake kwa ufanisi wa Hali ya juu Sana...
George Bush Sr aliwahi kuwa Mkuu wa CIA kabla ya kuja kuwa Rais. Ile CIA ambayo hakukuwa na Intelligence Community juu yake. Sasa cha ajabu kwa Tanzania nini? Mahiga alikaimu ukuu wa Idara, 2015 alichukua fomu.
 
Samia anatakiwa akemee ushangiliaji wa misiba
1. Amkemee na kumfuta kazi Nape kwa kauli yake ya "Mungu ameamua ugomvi"
2. Amfukuze kazi Januari kwa kauli ya baba yake ya kulamba asali na watu wazuri hawafi.

Atumie kanuni ya Mungu ya "Nawapatiliza wana maovu ya baba zao hata kizazi cha tano na cha sita.".

Bila hivyo nchi inagawanyika vipande
 
Back
Top Bottom