Desprospero
JF-Expert Member
- Feb 1, 2023
- 887
- 2,201
Wana wema!
Siasa za Lindi Jimbo la Mtama zimeanza kushika kasi ambapo harakati za kumtaka mdogo wake Hayati Bernard Membe, Steve Membe anatajwa kutakiwa kumrithi kaka yake jimbo la Mtama kama hatua ya kumuenzi huyo Mwamba wa Kusini.
Jitihada hizo inadaiwa kufanywa vigogo wa chama huku majina makubwa ya viongozi Wastaafu na walioko madarakani wakitaka kumuenzi Membe kwa kumfanya mdogo wake ambaye ni daktari kitaaluma Steve Membe kuchukua mikoba hiyo.
Mwenyewe Steve Membe amenukuliwa na moja ya t online akisema, "ni mapema mno kutamka juu ya hilo maana chama Cha CCM kina taratibu zake lakini kama wana-Mtama wametaka hivyo Mimi ni nani niwakatalie?"
Hatua hii inamuweka Mbunge wa Mtama kwa Sasa ambaye pia ni Waziri Nape Moses Nnauye katika wakati mgumu mno kisiasa jimboni hapa kuelekea 2025.