Utalii wa msosi

Red Giant

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
15,658
20,889
Umewahi toka matembezi ili kufuata msosi?

Vitu vidogovidogo maishani vinaweza kukuletea furaha sana. Mi nilikua natoka mpaka feri. Nikifika naingia mle wanakaanga samaki. Nanunua pweza wa moto au samaki yeyote mkubwa, tena bei cheap tu. Wananiwekea kwenye bahasha. Hapo naenda beach pale nyuma ya Ikulu. Natulia zangu naangalia meli na wavuvi huku nikipiga samaki taratibu.

Sometimes kama nimechelewa kurudi nakaa kwa wale mama ntilie wa feri. Napiga wali samaki na kisamvu. Ulikuwa msosi tofauti sana kulinganisha na miwali ya Canteen vyuoni.

Nimekuwa hivyo, nikienda sehemu napenda kula vyakula vinavyopatikana maeneo hayo. Nafikiri hamna kitu siwezi kula. Umewahi funga safari kwenda kupiga msosi?
 
Nishawahi panda gari kufuata korodani za mbuzi na ng'ombe za kuchomwa sehemu fulani hivi Daslam na ile chachandu ilikua ni balaa..
 
Back
Top Bottom