Utajiri wa rafiki yangu ulivyofanya nikamuamini Shetani

Kwa uelewa Wangu(Low thinking capacity)

Ally mpemba alikua anaitumia nyota ya UMUGHAKA kukamilisha mambo yake ya kujipatia utajiri, yaani kulikua na Connection kubwa sana kati ya pete aliyoivaa Master na ally mpemba mwenyewe.

Na ndio maana Master alikua akizingua tu Ally mpemba na yeye uku mambo hayaendi poa kiasi cha kumchukia kabisa Master.

Refer pia kuna Sehemu Ally alimlalamikia Master kwamba anataka kumfanya Maskini. Pale master alipovunja Mashart ya kutopakia mtu asiye wa ukoo wa Ally siti ya mbele

Master alikua amelibeba jini la Ally mpemba na ndo lilikua linampa Blindness ya kumpa pesa kidogo kusudi asishtukie mchongo mzima. Alikua akitumika kama chambo na pia kama Ndoano.

Utajiri una siri nyingi sana Wajameni na madubuwasha ya Ajabu. Usipo ya Face huwezi kuelewa kamwe.
Uko vizuri
 
KUNA MTU ALIWAHI KUSEMA HAPA KWENYE HUU UZI "UMUGHAKA HANA AKILI NDIO MAANA BABA YAKE ALIMFUKUZA NYUMBANI" NAONA HII NI KWELI MAANA ALLY NAE KAMWAMBIA HIVYO HIVYO.

Kama wewe unaungana na mchawi Ally basi nawe huna akili. Inaona kuroga ni sahihi?
 
Utajiri wa rafiki yangu ulivyofanya nikamuamini Shetani - 25



Mimi "Nashukuru sana kaka"

Ally Mpemba "Usijali brother,haya ni maisha tu ila unapaswa uwe makini"

Aliendelea "Tatizo lako master huwa unajisahahu sana hadi kuepelekea kunisababishia matatizo,kuna muda napenda tufanye mambo makubwa sana ila naona bado una changamoto zako!"

Mimi "Lakini kaka nishajifunza na sitorudia kufanya makosa "

Ally Mpemba "Ngoja tuone "

Baada ya mazungumzo na Ally niliondoka zangu kuelekea maskani huku nikiwa nafuraha kwssababu jamaa alikuwa amenipatia laki tano.Mambo yalianza kurudi kwenye mstari baada ya kupitia matatizo ya kiuchumi kwa siku kadhaa.

Kila ulipokuwa ukifika mwisho wa mwezi kama kawaida ile bangiri niliyokuwa nimeivaa ilikuwa ikibana sana na damu zikinitoka lakini mwisho wa siku sikuwa napata fedha kabisa na nilipokuwa nikimuuliza Ally Mpemba yeye aliniambia ni kwasababu nimekiuka masharti,sasa ile hali kiukweli iliendelea kunitesa sana na nisingeweza kuishi na kitu ambacho kinaendelea kunitesa na manufaa siyaoni.

Nilimuomba sana Ally Mpemba aweze kuniombea kwa Sheikh yule wa Chumbe kama kuna jambo lolote niweze kufanya ili ikiwezekana nitolewe ile bangiri ambayo iliendelea kunitesa,Ally Mpemba alionekana kama kuwa mbishi lakini alipoona nakomaa sana aliniambia atanirudisha tena kwa mzee lakini ni baada ya Mwezi utakaofatia.Sikuelewa ni kwanini jamaa alikuwa anakomalia mimi kuendelea kuivaa bangiri ambayo ilikuwa ikiendelea kuniumiza na haikunipa chochote zaidi ya kunitoa damu zangu.

Sasa nakumbuka jamaa aliniambia kabla ya kunipeleka kwa Mzee inapaswa kwanza nianze kutafuta wafanyakazi wa ile hotel/mgahawa wake.Kweli,sikutaka kabisa kupoteza muda kwasababu alikuwa ameniahidi atakuwa ananilipa kila mwezi kama msimamizi,yeye alijiweka kando kabisa ingawaje watu walikuwa wakifahamu ni mgahawa wa jamaa.

Niliwashirikisha mademu na washikaji tuliokuwa tukifanya nao kazi ya usajili wa line kila nilipokuwa nikienda ofisini pale buguruni,niliwapata mademu 3 na mshikaji mmoja ambao wao walikubali,kikichofanya wakubali pia ni kwasababu mauzo ya line kwa wakati huo yalianza kupungua,pia wale mademu ni kama walikuwa wamechoka na ishu za kusajili line maana waliona ni kama ilikuwa ikiwadharirisha.Pamoja na hao lakini nakumbuka jamaa aliongea na yule Mama aliyekuwa mpishi wa ile Catering yake akawa amemtafutia wafanyakazi wengine.Jumla mara ya kwanza kulikuwa na wafanyakazi 6,wakike 4 na wakiume wawili.

Baada ya kuanza kazi kwa ule mgahawa mimi pia nikawa nimeacha kazi rasmi ya usajili wa line nikaanza kusimamia ule mgahawa,mimi nilikuwa nakusanya mauzo yote kwa siku na ndiye nilikuwa msimamizi mkuu wa ule mgahawa.Mgahawa huu ulikuwa mtaa wa mkunguni nyuma ya Big bon jirani kabisa na Soko kuu la Kkoo.

Kiukweli tulikuwa tunauza sana na hatukuuza kama ujuavyo wewe bali ilikuwa ni nguvu za kishirikina.Nakumbuka kuna siku Ally Mpemba alipoona mgahawa unachanganyia sana aliinita nyumbani kwake,nilipofika tukawa tumejadili namna ya utoaji wa kafara maana alikuwa ameniambia tangu mwanzo ni kazi ambayo ningekuwa naifanya mimi.

Mimi "Niambie kaka namna ya kufanya"

Ally Mpemba "Kabla ya kufanya chochote orodhesha majina ya wafanyakazi wote kisha mimi nitayatuma kwa Sheikh Unguja"


Nilianza kumuorodheshea majina ya wafanyakazi wote wa ule mgahawa na kweli nilipompatia aliwasiliana na Sheikh akawa anamtajia,sasa baada ya muda kupita kuna majina Sheikh akawa ameyataja pale ambayo yote yalikuwa ya wanawake,walikuwa takribani 3,sasa wale wengine waliobaki hawakuwa na maana,Ally Mpemba aliniambia ikiwezekana niwafukuze waondoke kwasababu hawakuwa na umuhimu wowote kwenye ule mgahawa.

Kiukweli ilinipatia taabu sana kuwafukuza kwasababu hakukuwa na sababu maalumu ambayo ningewaeleza,nilianza kuwafanyia visa na nilikuwa mkali sana,niliamua kufanya uaminifu kwa Ally Mpemba ili kumridhisha kwasababu hapo nyuma nilikuwa nimemkwaza,sasa nilichokifanya ni kuwatafutia sababu wale wafanyakazi ambao Ally Mpemba aliniambia hawakuwa na faida na niliwalipa fedha zao na kuwaondoa,japo walinisihi sana nisiwafukuze lakini kiukweli sikuwa na namna,nilikuwa naumia sana lakini ndugu zangu sikuwa na jinsi.Sasa wale waliobaki nilijaribu kuwapeti peti kwa marupurupu na kuwasifia ya kwamba wao wanapiga sana kazi kuliko wale niliowaondoa,kiukqeli hawakuelewa jambo lolote na wao walifurahi wakawa wanajipa kichwa kama kweli walikuwa wanafanya kazi kumbe ilikuwa ni mtego wa panya,kupitia wale wale wafanyakazi niliwaomba wanitafutie wafanyakazi waliokuwa wanajituma kama wao ili kujaza nafasi zilizokuwa wazi.Walifurahia sana na wakasema watawashitua ndugu zao ili waje wapambane.
Lile zoezi la kuwatimua halikuchukua siku moja bali ilikuwa ni prosesi ambayo ilichukua muda kwa takribani majuma mawili ili kuwatafutia sababu,hivyo nilivyomaliza hilo zoezi nilimwambia Ally Mpemba ya kwamba nimemaliza na nilikuwa natafuta wafanyakazi wengine wa kujaza nafasi,Ally Mpemba alinipongeza sana kwakupiga kazi na akaniambia mwisho wa Mwezi tutaondoka kulekea Unguja mara moja halafu tuwahi kugeuka.

Kweli,mwisho wa mwezi baada ya kuwa nimetoa damu kupitia bangiri langu la mkononi tukawa tumeondoka kuelekea Unguja kwa Sheikh,tulivyofika nakumbuka yule mzee alimwambia Ally Mpemba wale wafanyakazi itabidi kila baada ya miezi 6 awe anakufa mmoja kwasababu akisema iwe kila mwaka itakuwa mbali sana na majini yake aliyokuwa akiyafuga hayakutaka iwe mwaka,ndipo nikaja kugundua kwamba kumbe jamaa alikuwa akifuga majini na ndiyo yalikuwa yakimpa utajiri ule wote.
Yule mzee alimwambia Ally Mpemba ampatie shilingi milioni moja na Ally alifanya hivyo,baada ya kuipokea ile hela alianza kuifanyia dawa na baada ya kumaliza alimrudishia ile hela Ally Mpemba kisha akawa amemwambia ya kwamba.

Mzee "Hiyo hela hakikisha utakapokuwa unataka kuwalipa mshahara,utakuwa unachukuwa elfu kumi hapa na kisha unachanganya na fedha nyingine ndiyo unawalipa"

Ally Mpemba "Sawa Sheikh"

Mzee "Usiwalipe wewe,huyu kijana ndiye anapaswa kulifanya hilo jukumu"

Ally Mpemba "Hizi pesa anapaswa kukaa nazo yeye?"

Mzee "Siyo lazima akae nazo huyu,ila kama yakiwa yanafanyika malipo hakikisha ni lazima elfu kumi moja inatoka hapa kwenye hizo hela nilizokupatia"

Aliendelea "Na itakuwa kwa mmoja wapo wa mfanyakazi mliyemkusudia"

Ally Mpemba "Sawa nimekuelewa vema"


Kilichokuwa kinafanyika ni kwamba,kama kuna mfanyakazi ambaye tulikusudia afe baada ya miezi sita kutimia,nilikuwa nachukua elfu kumi moja kwenye ile milioni nachanganya na mshahara wake kisha nampatia,kwa mfano kama mshahara ilikuwa laki tatu basi ilikuwa namuandalia mfanyakazi laki mbili na tisini ambayo ilikuwa fedha ya kawaida na baada ya hapo nachukua na elfu kumi kutoka kwenye ile milioni moja kisha inakuwa laki tatu halafu ndipo namlipa mfanyakazi tuliyekusudia.

Baada ya maelekezo yale,Ally Mpemba alimwambia yule mzee afanye namna sasa ile bangiri iweze kunipatia fedha kwasababu tayari nishakuwa mwema kwake,lakini nilimuomba pia yule mzee anibadilishie ile bangiri kwasababu haikuwa na muonekano mzuri hata kidogo,kuna muda nilikuwa naonekana kama mganga wa kienyeji kwasababu tu ya mbangiri ule.

Yule mzee alinipatia Pete ndogo sana ambayo aliniambia niivae kwenye kidole cha kati na akasisitiza itafanya shughuli kama iliyokuwa ikifanya ile bangiri;kiukweli niliipenda sana ile pete kimuonekano kwasababu ilikuwa nzuri na ndogo pia,ingekuwa ngumu sana mtu kugundua,sasa lakini yule mzee akasisitiza sana ya kwamba nisije nikathubutu kuivua ile Pete kama ilivyokuwa kwa bangiri tu.

Baada ya kupata kilichotupeleka hatimaye tukarudi Dar es salaam,tulipofika Dar es salaam Ally Mpemba aliniambia zile fedha atakaa nazo na itakapofika mwisho wa mwezi ule wa sita atanipatia elfu kumi ili nijumlishe na fedha ya malipo ya mfanyakazi tutakayemkusudia.

Kiukweli ile Pete ilipokuwa ikifika mwisho wa mwezi ilikuwa ikibana kama ilivyokuwa bangiri na nilikuwa nikifanya kuituliza kama mwanzo,baada ya damu kumwagika nilikuwa nikipata fedha kama kawaida na zilikuwa nyingi kushinda mara ya kwanza,baada ya kupata zile fedha nilikuwa nikizihifadhi benki nikiwa na lengo la kuanza tena ujenzi upya.Niliendelea kupiga kazi kwenye mgahawa wa Ally Mpemba kwa uaminifu mkubwa na wale wafanyakazi wakawa wamewaleta wafanyakazi wengine,lakini kabla ya kuwaajiri Ally Mpemba akapendekeza kwanza majina yatumwe kwa Sheikh kule Unguja na majibu yakitoka vizuri tuwaajiri,majina yalirudi na kuonekana baadhi wanafaa na wengine hawafai(Hii ilikuwa inahusisha nyota ya bahati) wale waliofaa tuliwaajiri na wale ambao hawakufaa niliwatafutia sababu.

Ilipofika mwezi wa sita mwishoni kuna mdada ndiye tukawa tumekubaliana na Ally Mpemba nilimlipe pesa kupitia ile prosesi na kiukweli majibu yalikuwa mazuri,baada ya kumlipa ile fedha mkononi yule mdada aliipokea na mambo mengine ya kawaida yaliendelea,ingawa wote niliwalipa mkononi kila mmoja na fedha yake lakini yule mdada yeye ndiye tulikubaliana mwisho wa mwezi huo wa sita awe kitoweo kwa biashara ya Ally Mpemba.Taarifa tulizopata ni kwamba alipofika kwao aliugua ghafla na wakati anakimbizwa hospitali alifia njiani,ilikuwa ni huzuni kwa wafanyakazi wenzake waliokuwa wamezoeana lakini hakuna aliyefahamu ule mchezo,mambo yalikaa sawa hatimaye wakasahau na kazi ikaendelea kama kawaida.

Ally Mpemba yeye aliendelea kuingiza fedha nyingi sana na kwakuwa nilikuwa mshirika wake mkubwa nilikuwa naelewa kila kitu.
Baada ya muda kuwa umepita nakumbuka mwanamke wangu Rehema alipata likizo akawa amekuja kwao kisha akawa amekuja kunisalimu.


Itaendelea..............
baby zu 25
 
Utajiri wa rafiki yangu ulivyofanya nikamuamini Shetani - 26


Maisha yaliendelea kuwa matamu sana kwa wakati huo na hakuna aliyefahamu kile tulichokifanya mimi na Ally kwenye ule mgahawa,watu wengi walikuja kujipatia chakula na kuondoka,kiukweli tulikuwa tunauza sana,kuna muda tulikuwa tunauza hadi tunachoka wenyewe.

Mimi kwa upande wangu maisha yangu yalininyookea na nilikuwa nikisevu fedha kwa ajili ujenzi wa nyumba tena,pamoja na kulipwa na Ally Mshahara kama msimamizi wa ule mgahawa lakini pia nilikuwa nikipitisha panga kubwa kwenye mauzo ya siku,kiukweli nilikuwa ninapiga sana pesa na ukizingatia kila mwisho wa mwezi nilikuwa nikijipatia fedha kwa njia ile ya Pete.

Mwanamke wangu Rehema alipokuja nyumbani,mambo ni kama yakaanza kubadilika,alikuwa mkali sana baada ya kuona nikiwa mkononi nimevaa Pete na akahisi uenda nilivishwa na mwanamke mwingine,kitu ambacho haikuwa kweli.

Rehema "Unadhani naweza kukuamini kama unavyodhani?"

Aliendelea "Niliwahi kukwambia nyie wanaume huwa mnatamaa sana,sasa umeona ushanitumia vya kutosha ukaona kabisa uvishwe Pete na mwanamke wako"

Aliendelea "Basi hata ungeniheshimu tu kwa kuivua na kuificha ili nikiondoka ndipo uivae!"

Mimi "Hayo ni mawazo mfu mpenzi wangu,siwezi kuvishwa Pete na mwanamke mwingine,inapaswa uniamini!"

Rehema "Usidhani kunisomesha ndiyo kigezo cha kunifanyia ujinga wako,tunaweza kuachana vile vile!"

Mimi "Kwani Ray siwezi kununua Pete na kuivaa tu?"

Rehema "Usinifanye mimi mtoto mdogo,wewe ungekuwa wa kununua Pete nadhani mimi ndiye ningekuwa wa kwanza kuvalishwa,sasa mimi hujawahi nivalisha Pete halafu unaniambia madudu gani sijui!"

Usiku mzima ulikuwa wa kupigizana kelele na Rehema na kiukweli hakuelewa kitu pamoja na kumueleza,siku hiyo kiukweli Rehema aligoma kabisa kunipatia maji ya kunywa ijapokuwa nilikuwa nina kiu ya kufa mtu,kila nilipokuwa nikajaribu kumgusa anigeuzie mtungi nichote maji ninywe yeye alidai niende nikanywe kwa mwanamke aliyenivisha ile Pete.Kiukweli usiku ule sikufanikiwa kabisa kuchota maji ya kunywa na nilikesha na kiu hadi asubuhi.

Sasa ilipofika asubuhi wakati mimi najiandaa kuelekea kazini na yeye aliamka akasema anarudi nyumbani kwao na nikimhitaji tena nihakikishe hanioni na hiyo Pete kwenye kidole.Nilijaribu kumtuliza lakini akawa mkali sana akawa ameondoka akaelekea kuoanda daladala.

Nilifunga mlango nikaondoka zangu kazini;Ilipofika usiku baada ya kutoka hapo kazini nilijaribu kumpigia simu Rehema lakini ilikuwa inaita tu haipokelewi,basi niliondoka hadi Ubungo msewe kwao Rehema na nilipofika nilivua ile Pete nikaiweka mfukoni kisha nikampigia simu,alipopokea nikamwambia nipo nje atoke tuzungumze!.Nilimbembeleza na nikamwambia ile Pete isije kuleta ugomvi kwani nimeivua na kuitupa,japo alinielewa lakini aligoma kabisa kuondoka na mimi akasema angekuja kesho yake,sikuwa na namna ilibidi niondoke zangu kurudi nyumbani,sasa wakati narudi nyumbani nikawa nimesahau kuivaa tena ile Pete na nilipofika nyumbani nikawa nimeingia kuoga na kulala,sasa ilipofika asubuhi wakati navaa ile jeans nilikuwa nimeivaa jana yake nilijaribu kuitafuta ile Pete mfukoni ili niivae lakini sikuweza kuiona,nilijitahidi kuitafuta sana hadi kukung'uta ile jeans lakini wapi !.

Niliamua kuondoka hivyo hivyo kuelekea job,sasa nikiwa kwenye gari Rehema akawa amenipigia simu ya kwamba anaenda nyumbani hivyo akawa anaulizia funguo nimeziweka wapi,nilipofika pale kituo cha Ngozi niliamua kushuka na kuingia upande wa pili ili nipande gari lingine nirudi nyumbani kumsubiri Rehema aliyekuwa njiani nimpatie funguo.Nilipofika nyumbani kuna hali nilianza kuhisi ambayo haikuwa nzuri,nilianza kuhisi baridi kama mtu ambaye alikuwa na malaria,kadiri muda ulivyokuwa ukienda ndipo hali yangu nayo ilikuwa mbaya sana.

Rehema alipofika nyumbani alikuta nimelala na aliniuliza kama ninamwa lakini nilimkatalia,alijaribu kunishika shingoni akakuta homa imekuwa kali,alikwenda pharmacy kuninulia dawa za kutuliza homa lakini nilipotumia bado hali haikuwa nzuri,sasa kwakuwa nilikuwa tayari nishafahamu kilichokuwa kinaendelea,nilichukua simu yangu nikawa nimempigia Ally Mpemba lakini simu ikawa inaita tu jamaa hakupokea.Baada ya muda kupita jamaa akawa amenitumia sms iliyosomeka "Wewe huna akili na utakufa kifo kibaya sana!".

Baada ya kuisoma ile sms niliifuta kabisa ili Ray atakaposhika simu yangu asije kuiona;Niliona ningeendelea kukaa kimya ningekufa kipumbavu kama alivyoniambia Ally Mpemba,nilichukua simu yangu nikampigia mama yangu Tarime pamoja na Dada yangu mkubwa wa Mwanza na nikawa nimewajulisha hali yangu haikuwa nzuri,sasa mama aliona mpaka nimempigia simu kiukweli hali yawezekana haikuwa nzuri,yeye alimpigia simu Anko wangu kitu ambacho sikutaka kabisa yeyote kutoka upande huo afahamu,na nilijua anko akifahamu ataanza ngonjera zake.Niliamua kuzima simu kabisa ili yeyote atakayenitafuta asinipate.

Hali yangu ilikuwa mbaya sana hadi Rehema akaamua kunipeleka dispensary pale Gongo la mboto kwa ajili ya kuchukua vipimo,majibu yalipotoka sikuonekana na tatizo lolote lakini kiukweli nilikuwa naumwa,sasa wakawa wameniambia ninywe maji mengi kwasababu hali kama hiyo huwa ni kawaida.

Wakati Rehema anadhani ni ugonjwa wa kawaida mimi nilikuwa nimeshafahamu tatizo ilikuwa ni ile Pete niliyoivua na kupotelea kusiko julikana,niliona nikiendelea kuzubaa naweza kupotea kabisa,tulivyorudi nyumbani mimi niliondoka nikawa nimerudi pale Msikitini Gongo la mboto(Masijid ijumaa),kuna Sheikh mmoja nilikuwa nafahamiana naye nikawa nimefika kumuulizia lakini nikaambiwa siku hiyo hajaonekana hapo,sasa kuna Sheikh mmoja sikutaka kumficha kitu chochote kwasababu niliona kabisa nikiendelea kupuuzia naweza kupoteza maisha.
Nilimwambia kuna Pete nilikuwa ninayo lakini haikuwa nzuri ilikuwa ikinisaidia kwenye mambo yangu ya biashara na baada ya kuivua tu nikaanza kuugua,yule Sheikh aliniambia nimsubiri amalize swala kisha tuondoke.Kweli,nilivumilia hadi akawa amemaliza kuswali na alipotoka nje nilimuwahi nikamwambia nilikuwa namsubiri,alinichukua tukaondoka tukawa tunapiga stori za hapa na pale hadi tulipofika kwake mitaa ya mzambarauni,tulipofika kwake namshukuru Mungu Sheikh akaanza kunisomea dua za kufa mtu,alinisomea sana na hatimaye akawa ameniambia kuna mafuta ninapaswa nikayanunue kwenye maduka ya kisuna ambayo nitakuwa ninayaweka kwenye maji kabla ya jua kuchomoza kisha nakwenda kuoga.

Yule Sheikh aliniandika jina la yale mafuta nikaenda kuyanunua na kiukweli baada ya ya kutoka pale hali yangu ikawa nzuri kiasi.

Asubuhi baada ya kupambazuka niliyatumia yale mafuta na hali yangu ikawa nzuri japo si sana lakini kiukweli nilimshukuru sana Sheikh.

Baada ya kuwa nimepata japo ahueni,niliondoka nikaelekea Kkoo kwenye mgahawa wa Ally Mpemba ili kama nikimkuta nijaribu kuzungumza nae maana nilikuwa nampigia simu zangu jamaa hapokei,nilipofika pale kuna mwanamke mmoja mwenye asili kama ya Ally nilimkuta nikawa nimeambiwa na wale wafanyakazi wa pale kwamba yeye ndiye alikuwa msimamizi wa pale.Niliwaza sana laikini sikupata majibu kwasababu haiwezekani mimi kutokuonekana siku moja tu Ally Mpemba akaamua kuniweka pembeni.

Niliondoka hadi kwenye duka lake la pale Aggrey lakini sikumkuta,nilijaribu tena kumpigia simu hakupatikana kabisa.Niliamua kwenda hadi pale kwenye duka la Gerezani kujaribu kumtafuta lakini nilipokwenda nilikuta lile duka limefungwa,sikutaka kukata tamaa kirahisi nikaona nielekee kwake Magomeni.Nilipofika Magomeni nilikuta geti limefungwa na nilipojaribu kugonga hakuna aliyekuwepo ndani,niliamua kuondoka na kurudi zangu nyumbani mdogo mdogo nikiwa nimekata tamaa kabisa.

Rehema alikaa kwangu takribani wiki moja kisha akawa amerudi kwao ili akajiandae aweze kurudi chuo.

Baada ya Rehema kuondoka mimi pia niliondoka kuelekea Sumbawanga huko Namanyere kwa mtaalamu ambaye hapo awali Mwakisaka alikuwa amenielekeza na kunipa mawasiliano yake.


Itaendelea..............
baby zu 26
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom