Nataka kumuoa msichana aliyeachana na rafiki yangu

KIBOD3

Senior Member
Sep 11, 2016
125
176
Habari zenu,

Nina rafiki ambaye siyo wa karibu sana alikuwa kwenye mahusiano na mtarajiwa wangu sasa baada ya kuachana kwao nilifanikiwa kumshawishi tukaingia katika mahusiano kwa siri kubwa sana (kiukweli nilikuwa nampenda tangu hapo zamani) sasa nataka niende kwao nikajitambulishe
 
Yote yanawezekana tu ila tahadhari.

Ilishatokea binti alikuwa na mahusiano na jamaa, binti alikuwa anaiba mpaka pesa kwao anampeleka mshkaji lakini ni kama vile jamaa hakutilia maanani.

Basi walipotezeana kumbe jamaa rafiki yake akaanza kumchombeza binti sasa zile stress mchumba akaingia king wakawa wanakutana kimya kimya.

Siku moja jamaa akamwambia mshkaji wake twende kuna sehemu nataka unisindikize kumbe jamaa alikuwa kaongea na demu kwamba kuna sehemu waliyokuwa wakikutana sana mara nyingi, demu yaani akisikia tu sauti ya mshkaji hajiwezi kabisa.

Basi wakaondoka mpaka kule, wakafika wakawa wanasubiri ndio anamuona sasa demu anakuja, jamaa kashafahamu binti ni dhaifu kwake akamfata kwenda kumkumbatia huku rafiki katulia tu akigugumia maumivu.

Wale wapenzi waluridana na binti aliloporoka yote.

Kuwa makini tu, ila linawezekana
 
Habari zenu
Nina rafiki ambaye siyo wa karibu sana alikuwa kwenye mahusiano na mtarajiwa wangu sasa baada ya kuachana kwao nilifanikiwa kumshawishi tukaingia katika mahusiano kwa siri kubwa sana (kiukweli nilikuwa nampenda tangu hapo zamani) sasa nataka niende kwao nikajitambulishe
Sasa unachosuniri ni nini kama una nia nae kweli? Alafu kingine vitu vidogo kama hivi si vyakuomba ushauri bali utekelezaji tu. Chakukusaidia tu yafanye mahusiano hayo yawe bora kuliko yale aliyotoka na huyo rafiki yako vinginevyo hatamsahau.
 
Habari zenu
Nina rafiki ambaye siyo wa karibu sana alikuwa kwenye mahusiano na mtarajiwa wangu sasa baada ya kuachana kwao nilifanikiwa kumshawishi tukaingia katika mahusiano kwa siri kubwa sana (kiukweli nilikuwa nampenda tangu hapo zamani) sasa nataka niende kwao nikajitambulishe
Kosa kubwa sana kwa mmbwa mwitu kung'ang'ania fupa lililomshinda fisi kulitafuna.

Ubinadamu ni kazi/Humanity is a work.

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom