Utajiri wa rafiki yangu ulivyofanya nikamuamini Shetani

Utajiri wa rafiki yangu ulivyofanya nikamuamini Shetani - 18.


Nilifanikiwa kufika Mbeya na kuanza kuzunguka kukusanya viazi huku nikiendelea kuwatumia madalali ili kufanikisha kwa haraka niweze kurudi mjini kuuza mzigo.

Nilitumia takribani wiki 1 kununua mzigo na kupakia kwenye fuso kisha kuuleta mjini Dar es Salaam, nilipofikisha mzigo mjini hali haikuwa kama nilivyodhani mwanzo, wale madalali ambao niliongea nao tangu mwanzo nilipokutana nao walianza kuniambia mzigo kwasasa umekuwa mwingi na umeshuka bei.

Niliamua mwenyewe kupita na kufanya utafiti kwenye masoko ya Ilala, Buguruni na Mabibo na kugundua ya kwamba wale madalali walikuwa na nia ya kunipiga kwasababu hakukuwa na mzigo mwingi wala nini! Nilichoamua ni kuanza kuuza ule mzigo mwenyewe, ule mzigo kiukweli ulinikata sana na namshukuru Mungu niliambulia kiasi kidogo cha pesa kwasababu kuna magunia mengine ya viazi yalioza kwasababu ya kukaa chini muda mrefu bila kuuzwa.

Nilichogundua ni kwamba wale madalali mwanzo walikuwa wakinipanga ili nilete mzigo mjini na nikisha ufikisha wao ndiyo wanipangie bei ya kuuza, wao wajipatie pesa nyingi kupitia mzigo wangu halafu mimi nipate faida kidogo, sasa nilipowakataa wakasambaza maneno kichini chini kwamba mzigo wangu haufai hivyo kila mteja akawa anaupita tu kama anaaga maiti kiukweli ile hali ilinifedhehesha sana hadi kuna watu ambao ni wema walinishauri niuuze wote kwa jamaa mmoja pale Mabibo ambaye alikuwa ni dalali na alinipatia fedha nusu ya mtaji, kiukweli kwasababu ndiyo ilikuwa mara ya kwanza kuifanya ile biashara sikutaka kabisa kuendelea nayo kwasababu ilikuwa na fitina kubwa mno na mpaka leo sielewi watu wengine wanawezaje kufanya biashara ya viazi.

Baada ya kuona hiyo biashara imenishinda kwasababu ya fitina ya mswahili, niliamua kurudi zangu kwenye usajili wa laini za simu huku nikiendelea na majukumu mengine ya usimamizi wa miradi ya Brother Ally Mpemba.

Baadae nilichokuja kugundua ni kwamba, hakukuwa na fitina za mswahili wala nini, ile hela ambayo nilikuwa nikiipata kila Ijumaa ya mwisho wa mwezi kiukweli kila nilipojaribu kuifungulia biashara iligoma kabisa kwasababu ukiachilia mbali biashara hiyo ya viazi, nilifungua duka la nguo za kike pale Tandika na kuna jamaa mmoja kutoka Iringa nilimuajiri aniuzie, ilikuwa ni siri sana na sikutaka mtu yeyote ajue kuhusu hilo, lile duka halikufikisha hata miezi 6 likawa linaporomoka, mtaji na faida havikujulikana vinapotelea wapi.

Nikajaribu kumchunguza yule bwana mdogo nikadhani huenda akawa ananipiga kumbe haikuwa hivyo, lile duka nikaamua kuliuza na bidhaa baadhi zilizokuwa zimebaki, kwakuwa mwanzo nilipata ugumu kuelewa ila kadiri siku zilivyosonga ndipo akili na ufahamu vikanijia nikafahamu ya kwamba ile hela ilikuwa na matatizo, sasa nilichoamua ni kwamba ile hela niingize kwenye ujenzi wa nyumba yangu nitakayokaa huko Chanika kwenye uwanja wangu(Nitakuja kueleza kilichotokea maana hali ilikuwa mbaya kuliko nilivyodhani).

Sasa kwakuwa nilikuwa na kiasi cha fedha ambacho nilibaki nacho, niliamua kununua ramani ya nyumba na kwenda kuanza ujenzi kwenye uwanja wangu kule Chanika ili ule uwanja usiendelee kuota nyasi, baada ya kupiga msingi na jamvi niliamua kuachia hapo ili niendelee kuvuta nguvu za kupandisha boma.

Sasa kuna siku Ally Mpemba alinipigia simu akawa amenitaka nionane nae pale kwake ili tupange mipango kadhaa kwasababu yeye alikuwa anahitaji kusafiri kama alivyokuwa ameniambia awali, tulikubaliana tungeonana Jumapili ya wiki hiyo pale nyumbani kwake kwasababu pia hata mimi Jumapili mara nyingi nilikuwa napumzika.

Niliondoka zangu kuelekea kwa Ally na bahati nzuri nilimkuta akiwa nyumbani.

Ally Mpemba "Salama?"

Mimi "Salama kaka"

Baada ya salamu na mazungumzo mafupi, jamaa aliingia ndani ambako alichukua muda mrefu kidogo ndipo akawa ametoka.

Ally Mpemba "Pika chakula ule master, hapa ni kama kwako wala usione taabu!"

Mimi "Kaka usijali niko vizuri"

Ally Mpemba "Ulikula muda gani?"

Mimi "Nimekula muda si mrefu!"

Ally Mpemba "Sawa kama ndivyo"

Aliendelea "Mimi nimekuita weye kwasababu hapo awali nilikueleza ya kwamba nina safari ya kwenda Oman, hivyo nikakuomba unisitiri master!"

Mimi "Sawa kaka"

Ally Mpemba "Kuna jambo nahitaji nikwambie na nakuomba Union unionyeshe uaminifu wako kama nilivyokuamini"

Mimi "Kaka ina maana huniamini tu!"

Ally Mpemba "Mimi nakuamini tangu siku ya kwanza ila nadhani unakumbuka nilikutahadharisha ya kwamba kuna mambo ukiyapayuka kwa watu wengine utakachokutana nacho basi utajua mwenyewe!"

Aliendelea "Ndugu zangu siwathamini kama ninavyokuthamini weye, hivyo thamani ninayokupatia ni kubwa mno"

Aliendelea "Hivyo mimi naondoka na itanichukua takribani mwezi mmoja huko, nakuomba usimamie shughuli zangu hasa ile niliyokukabidhi huko kwengine Farah atasimamia!"

Mimi "Sawa kaka nimekuelewa!"

Ally Mpemba "Vipi mambo yako lakini yanakwenda?"

Mimi "Yanakwenda kaka"

Ally Mpemba "Sawa jitahidi ufanye vema kama ulivyoambiwa na nakuhakikishia wewe ukiwa mwaminifu hakika utakuwa mkubwa hapa Bara kote na hata huko pwani hakuna atakaye kugusa kwa utajiri!"

Niliendelea kumsikiliza Ally Mpemba namna alivyonitia moyo kuhusu ile bangili lakini sikutaka kumwambia kabisa kuhusu biashara zangu zote mbili zilivyonipatia hasara ikabidi nikaushe.

Ally Mpemba "Kuna jambo ambalo kabla ya kuondoka naomba ulifahamu maana ni lazima ndipo uweze kufanya maamuzi ya kunisitiri"

Aliendelea "Bila shaka Huyu kiumbe ninayeishi naye hapa kwangu unamfahamu!"

Mimi "Ndiyo kaka namfahamu"

Ally Mpemba "Sasa nadhani unaelewa huwa nisipokuwepo nakuomba unisaidie kumwandalia chakula"

Mimi "Ndiyo kaka"

Ally Mpemba "Naomba leo nikueleze ukweli na usije kujaribu kumueleza mtu, mimi na wewe tumekuwa wamoja na siri yako ni yangu na naomba siri yangu iwe yako, huwezi kufanikiwa kama hutaweza kutunza jambo!"

Aliendelea "Huyo unayemuona hapa she's my blood sister na ndiye mwanamke ninayempenda kuliko wanawake wote duniani, jina lake si Maya kama unavyodhani, jina lake ni Zahra, hakuna mtu yeyote anayejua Zahra yuko hapa ila wewe, hivyo nakuomba uwe makini na siri hii na nakuomba sana!"

Kiukweli Ally Mpemba alionyesha hali fulani ya huruma na upole baada ya kumuongelea Maya, nilikuwa nikimuangalia Ally Mpemba alionyesha usoni ni mtu wa huruma sana lakini kiuhalisia hakuwa kama ulivyomdhania.

Ally Mpemba "Nikitoka Oman nitakuja kukueleza vizuri ila nachotaka ujifunze na unisitiri!"

Aliendelea "Oman sina mke kama nilivyokwambia hapo awali ila kuna jambo kubwa ambalo na wewe utalifanya siku moja, nikirudi nitakujuza ila kwasasa nakuomba unisitiri!"

Kiukweli hali haikuwa rahisi kama nilivyodhani ila kwakuwa nilikuwa tayari nishaingia kwenye mfumo wa Ally Mpemba sikuwa na jinsi ilibidi nitekeleze na kufanya nilichoambiwa ili kuendelea kujipatia pesa.

Ally Mpemba "Nitakapoondoka nakuomba kila ijumaa uwe unalala kwenye chumba changu hicho!"

Mimi " Sawa kaka nimekuelewa"

Ally Mpemba "Naomba usiwe unashituka kwasababu Zahra atakuwa anakuja mnalala naye na atakachokuwa anataka umfanyie naomba umfanyie usiogope!"

Mimi "Hawezi kuniletea fujo kaka?"
Ally Mpemba "Hawezi, yeye akishakula huwa hana shida, hakikisha kila Ijumaa haufungi mlango wa chumba changu, yeye atakuwa anaingia na mnalala nae kisha akitaka chochote mpatie"

Aliendelea "Bila shaka master wewe ni rijali na kama huwezi kabisa basi mimi kuna dawa nitakupatia utakuwa unakunywa ili uweze kuwa imara kitandani!"

Mimi "Hapana kaka wala usijali niko Imara sana!"

Ally Mpemba "Sawa nitashukuru sana kama umeamua kunisitiri!"

Mimi "Kaka asije akajua mimi siyo wewe akaniletea vurugu!"

Ally Mpemba "Hapana hawezi kufanya hivyo, akishaingia chumbani atalala kitandani na wewe nakuomba usipoteze muda wala usione huruma, mshughulikie kikweli kweli, ikifika asubuhi ataamka mwenyewe ataondoka chumbani kwake!"

Mimi "Sawa kaka nimekuelewa!"

Ally Mpemba "Japo anayo harufu ila nakuomba usionyeshe hali ya kujuta maana hiyo harufu ndiyo pesa yenyewe!"

Aliendelea "Ukifanya vema utapata zaidi na utakuwa mkubwa sana"

Mimi "Sawa kaka nimekuelewa kabisa na sitokuangusha"

Ally Mpemba "Usije kuruhusu mtu yeyote kuingia humu ndani zaidi yako!"

Mimi "Sawa"


Ally Mpemba "Sasa jiandae kesho twende pale TRA ukachukue TIN, kuna jamaa pale nishampa hela nitamkabidhi kwako akufanyie mchakato wa leseni ya gari!"

Basi baada ya yale mazungumzo Ally Mpemba alinikabidhi laki 5 kisha akaniambia kesho asubuhi mida ya 2 tuonane ili tuelekee TRA kwa ajili ya ishu ya leseni. Kiukweli nilibaki kushangaa namna Ally Mpemba alivyokuwa na ujasiri wa kulala na dada yake kitanda kimoja na kumuingilia kimwili. Haikuwa kazi ndogo ila niliamua kupiga moyo konde kwasababu nilikuwa ninataka pesa na mimi niliamua kuwa na roho ngumu.

Baada ya siku tatu kufatilia masuala ya leseni, namshukuru Mungu nilijipatia leseni yangu ya kwanza kabisa kwa ajili ya uendeshaji wa gari. Nilipopata leseni Ally Mpemba alinipatia ile gari yake iliyokuwa mpya aina ya Aud A4, kiukweli nilipata kiburi sana kwa kujiona mimi ndiye mimi, sasa kabla Ally hajaondoka kuelekea Oman alinipatia maelekezo namna ya kuimiliki ile gari.

Ally Mpemba "Master nakuomba tu kwenye hii gari mpya ninayokukabidhi ukiamua kuwabeba marafiki zako basi wakae viti vya nyuma,hii siti ya mbele asije akaikalia mtu yeyote labda kama akitokea ndugu yangu,tafadhali sana nakuomba!"

Mimi "Ndugu zako siwafahamu kaka zaidi ya mama yako mdogo pamoja na Farah"

Ally Mpemba "Hao ndiyo ninaomaanisha, kama Farah akikuona na akihitaji lift usiache kumbeba na asikae nyuma bali akae kiti cha mbele, wengine wote usithubutu kuwabeba mbele"

Mimi "Nimekuelewa kaka nitakuwa muangalifu!"

Ally Mpemba "Sawa mimi nadhani Alhamisi ijayo naondoka, hakikisha Jumatano utakuja kulala hapa ili nikiwa naondoka kuna pesa nikukabidhi pia nikukabidhi na funguo"

Mimi "Utachukua muda mrefu huko?"

Ally Mpemba "Haitapungua mwezi!"

Mimi "Sawa kaka"

Baada ya kuniambia niwe muangalifu na ile siti ya mbele nilivuta picha lakini sikupata majibu, lakini nikakumbuka mara zote nimekuwa nikimuona na ile range akiwa amebeba mtu basi huishia kukaa nyuma na siti ya mbele hukaa bila mtu na mimi pia mara zote nimekuwa nikipanda ile Range ndivyo ilivyokuwa!.

Kweli, baada ya siku kufika Ally Mpemba aliondoka akawa amenikabidhi funguo za nyumba yake pamoja na kiasi cha shilingi milioni 3 na akawa ameniambia amempatia Farah maelekezo endapo zikiisha nimuone atanipatia nyingine, pesa aliyonipatia ilikuwa ya matumizi ya kawaida ya kununulia vyakula vya Maya pamoja na matumizi yangu. Nilifurahi sana maana niliona kila kitu sasa kipo mikononi mwangu na nilipanga kiukweli marafiki na ndugu wanitambue mimi ni nani kupitia lile Audi A4.

Baada ya Ally Mpemba Kuondoka hiyo Alhamisi, ilipofika Ijumaa kama kawaida nilienda zangu kazini pale Kkoo kusajili line za simu, ilipofika mida ya saa 10 jioni nilimuaga Farah nikamwambia nitawahi kufunga kuna mahali nawahi.

Farah "Mbona mapema leo!"

Mimi "Kuna mahali nawahi Aunt!"

Farah "Sawa, si unarudi lakini au ndiyo hadi kesho!"

Mimi "Hiyo hadi kesho dada"

Niliondoka zangu nikaenda kununua vyakula vya maya kama kawaida kisha nikaelekea nyumbani kwa Ally Mpemba, nilipofika kama kawaida nilichukua kitambaa kile cheupe nikatandika pale mezani kisha nikaweka vile vyakula, baada ya kuweka vile vyakula nilifunga mlango kisha nikawasha mchuma nikatoka zangu kuelekea kupata chakula ili niwahi kurudi kufungua kile chumba cha Maya.

Nilipomaliza nilirudi mdogo mdogo na ile gari huku nikiendesha kwa madaha kama yangu vile, ilipofika mida ya saa 1 usiku niliwasha taa kisha nikawa nimetoka zangu nje, kiukweli sikutaka kabisa kumuangalia Maya, nilichoamua ni kwenda kuzurura na ikifika mida ya 3 usiku nirudi kulala. Kweli, niliporudi nyumbani kwa Ally Mpemba kama kawaida niliingia chumbani kwake nikawasha taa na sikufunga mlango, kile chumba kilikuwa ni kizuri na kisafi kupita mfano, sikutaka kabisa kuzima taa, niliingia bafuni kuoga kisha nikarudi kujitupa kitandani kulala huku nikiendelea kumsubiri Zahra(Maya)niliyeambiwa na Ally ya kwamba nikiacha chumba wazi ataingia mwenyewe.

Kweli, haikupita hata nusu saa nilimuona Zahra akiingia chumbani akiwa uchi kama ambavyo siku zote huwa.


Inaendelea: Sehemu ya 19
Balaa
 
Wako vizuri na ukumbuke tu kwamba wote hao ni Kanda maalum TARIME - RORYA
Watu wa kanda maalum
Nimekumbuka Magere alivyozunguka kuitafuta sh mia ya mwaka 1993
Ila Tarime jamani
They don't give up kabisa


So far kuna part zimenichekesha kwenye hii stori;-
Part 1 ni ile shemeji yake Master anavyoongea na Master kuhusu ile hela alimpa ndugu yake

Part 2 Ally Mpemba anamtumia msg Umughaka eti huna akili na utakufa kifo kibaya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watu wa kanda maalum
Nimekumbuka Magere alivyozunguka kuitafuta sh mia ya mwaka 1993
Ila Tarime jamani
They don't give up kabisa


So far kuna part zimenichekesha kwenye hii stori;-
Part 1 ni ile shemeji yake Master anavyoongea na Master kuhusu ile hela alimpa ndugu yake

Part 2 Ally Mpemba anamtumia msg Umughaka eti huna akili na utakufa kifo kibaya

Sent using Jamii Forums mobile app
Hawa wanaume wa kikurya ni wanaume kweli kwa kupambana. Mpaka wanawekewa kanda maalumu ya kipolisi mchezoo
 
Yaani hawakati Tamaa
Jamaa kutoka kutapeliwa mamillioni hadi kuanza upya kwa kufanya vibarua vya matofali

Yule mwenzie alienda hadi kuzimu kupata huo utajiri

Sent using Jamii Forums mobile app
🤣🤣🤣🤣🤣🤣
Hawa sio lelemama
Halafu usijepata boy mkurya ukadhan utakuwa unamzungusha kwenye vijiwe vya chips...mama utapiga ugali tena sio wenu pekee na wa kuliwa na mashemeji pia maana sku zote mkurya anatembea kwenye group
 
Umeongea kwa uchungu sana.
Ila jamaa kazingua kinoma sijaona kama kina Ally mpemba na mzee wamemzubaisha au Maya ila ni yeye pekee na nyege zake
Atupe mwendelezo tu ila stimu zimekata kabisa kufatilia
yani nmeumiaa kinoma

sikuifatilia tangu ep 20, ndo nikasoma soma jana nikajutana na huo ujinga daah nmeumiaa.. tumetoka Tarime matukio kibao afu Demu anakuja kuzingua aaah sikubali kabisa
 
Kumbuka siku ya kwanza alipokutana na Rehema, alisikia sauti kabla hata hajamuona Rehema.
Kuna mtu unaletewa aje akuokoe.
aah mi kuokoana staki.. Mtu mwenye makalio makubwa anakuokoaje bwana
Vaa uhusika wa rey then rudia kauli yako
aah heri nivae uhusika wa Ally mpemba sio Rey mkata kamba
Afu jamaa hapo juu ametusanua kuwa ndo mkewe... mi sisomi tena mana mwisho nshauona yani tumeenda mpaka Quba afu tunarudi liwale aah staki mimi
Ha ha ha ha huwaga wanaanzia mbali hivo hivo ili uzoee.
aah uko mbali unasafisha tu ...kwenye mtihani mgumu ndo unakwama hata wao wanaona hapa ngumu kumesa.
 
Utajiri wa rafiki yangu ulivyofanya nikamuamini Shetani - 24.


Mimi "Alinionyesha album ya picha "

Farah "Kitendo cha Ally kukuonyesha Album ya picha ya familia yake anakuamini sana kama mimi nilivyokuamini tangu mwanzo "

Aliendelea "wewe ni mtu mwema sana master kama hujui Ally anakuamini sana"

Kadiri Farah alipozidi kuongea kiukweli ndiyo nilizidi kuchanganyikiwa kwasababu ni kama sikumuelewa,mwanzo alianza vema sana kuzungumza lakini kadiri muda ulivyozidi niliona mabadiriko.

Farah "Unataka kuniona?"

Mimi "Ndiyo dada Farah nahitaji kukuona uenda kuna kitu utanisaidia!"

Farah "Huwa naonwa na mume wangu tu,sasa nikiondoa Nicab tambua wewe ni mume wangu!"

Mimi "Ndiyo maana nimekuomba dada"

Farah "Siwezi kukutolea hapa hadharani Nicab watu wote wanitazame"


Aliendelea "Kuna lingine?"

Mimi "Hapana Dada"


Niliondoka kuelekea nje kuendelea na kazi zangu lakini kiukweli siku hiyo hata kazi haikwenda vizuri,niliamua kuondoka zangu kuelekea nyumbani kupumzika tu.

Sasa nakumbuka Ally Mpemba akawa amerudi na alipokuwa akinikuta pale Kkoo pembeni ya duka lake nilikuwa nikimsalimia anaitikia kama hataki,ile hali kiukweli ilikuwa ikinipatia taabu sana,niliona nimtafute angalau nimuombe msamaha.Nijaribu kumwambia dada Farah aniombe msamaha kwa Ally lakini pia akasema ndugu yake hataki kunielewa.

Ile kazi ya Catering nayo ni kama iliota mbawa kwangu kwasababu sikuwahi kuambiwa tena wala kupewa ratiba ya kitu gani kilichokuwa kinaendelea,kitu nilichokuwa nakitegemea ni ile bangiri tu ambayo kila mwisho wa mwezi ilikuwa ikinipatia fedha,sasa nakumbuka hata mwisho wa mwezi huo ni kama hali ikaanza kuwa mbaya sana,ile bangiri ilibana kama kawaida na nikatoa damu nyingi sana lakini cha ajabu sikupata fedha hata tone.Kiukweli ile hali ilinitisha sana na kibaya nilipojaribu kuivua ilikuwa haitoki,nilidhani uenda ikawa inanibana nikachukua sabuni na kupaka kulainisha mkono lakini wapi!,sikuishia hapo tu bali nilichukua na mafuta ya kupikia nikajipaka mkononi kulainisha lakini nilipoitoa haikutoka.

Sikutaka kabisa kupoteza muda,nilijaribu kumpigia Ally Mpemba simu angalau ajaribu kuongea na Mzee wa Chumbe lakini jamaa simu zangu alikuwa hashiki kabisa na kuna muda alikuwa akizima.Ile hali ilibaki kama siri yangu lakini niliona nitafute mtaalamu anisaidie vinginevyo ningeendelea kukaa kimya hali ingekuwa mbaya sana.Nilimtafuta yule mshikaji wangu ambaye nilikuwa nikifanya nae kazi kule Dege aliyeitwa Mwakisaka angalau nimueleze hali niliyokuwa naipitia kama mwanaume mwenzangu,ingawaje sikumwambia ukweli lakini jamaa hakuwa na neno.

Mwakisaka "Kimya sana kaka"

Mimi "Mapambano tu ndugu yangu"

Mwakisaka "Nilikutafuta mara kadhaa ukawa hupatikani!"

Mimi "Sasa hivi natumia namba hii kaka ya Tigo"

Mwakisaka "Wapi sikuhizi "

Mimi "Bado nipo palepale Gongo la Mboto kaka"

Mwakisaka "Mwanangu mi niko Dodoma napambana"

Mimi "Mambo mazuri huko nini kaka!"

Mwakisaka "Mwanangu huku kuna hela,siunajua tena watu wanajenga sana huku"

Mimi "Sawa kaka,sasa kuna ishu naomba nikushirikishe kaka"

Mwakisaka "Niambie mwanangu"

Mimi "Mwanangu hivi kuna mtaalamu yeyote ambaye ni mzuri unaweza kuwa unamfahamu?"

Mwakisaka "Mtaalamu wa...?"

Mimi "Mganga kaka"

Mwakisaka "Vp ulikuwa na shida nini!"

Mimi "Yeah kuna ishu nilikuwa nataka kuziweka sawa kaka,siunajua mjini hapa!"

Mwakisaka "Nakuelewa sana kaka!"

Aliendelea "Ishu yako kubwa ni nini "

Mimi "Nilitaka tu wa kuniangalizia mambo yangu kaka"

Mwakisaka "Kama ni kuangalia mambo mbona wapo kibwena!"

Mimi "Ndo unisaidie sasa kaka"

Mwakisaka "Kwasasa nipo kibaruani,nipe muda hata jioni au kesho nitakupa jibu kaka!"

Mimi "Sawa kaka"


Baada ya mazungumzo na Mwakisaka niliamucha jamaa apambane na kazi yake na nikaendelea kuvuta subra kama alivyokuwa ameniahidi.Kazi kwa upande wangu ikawa ngumu sana kiasi kwamba hata nikienda pale Kariakoo kwa ajili ya usajili wa line za simu nilikuwa napata wateja 2 hadi 3 kwa siku kitu ambacho haikuwa kawaida,zamani nilikuwa nikiweka meza tu ile nimefungua unakuta wateja ni wengi sana kiasi kwamba mpaka nilikuwa nafurahi.

Nilimtafuta Mwakisaka baada ya siku mbili maana niliona jamaa uenda akawa ametingwa na mambo lukuki.Sasa nilipojaribu kumtafuta jamaa akawa ameniambia atanipigia baada ya dakika kumi na kweli baada ya dakika hizo akawa amenipigia.

Mimi "Kaka niambie basi ndugu yangu"

Mwakisaka "Kaka kuna mtaalamu mmoja yupo pale Namanyere,unapafahamu?"

Mimi "Namanyere sipafahamu kaka ila napasikia"

Mwakisaka "Sasa jamaa anapatikana kule na ni mtaalamu kweli kweli kaka naamini kwa shida yako ya kuangalia mambo yako basi atakusaidia"

Mimi "Nipatie lokesheni kaka namna ya kufika kwake"

Mwakisaka alinielekeza namna nzuri ya kufika kwa huyo mtaalamu na akawa amenipatia namba yake ya simu ili niwasiliane nae kabla ya kuondoka.Sasa nakumbuka nilipowasiliana na jamaa ilipofika usiku Ally Mpemba alinipigia simu.

Ally Mpemba "Acha kuangaika wewe unachokitafuta utakipata!"

Mimi "Kaka nahangaika kwa kitu gani?"

Ally Mpemba "Mimi nakuonya tu,usije sema sikukwambia "

Aliendelea "Haya mambo umeharibu mwenyewe ila sasa hivi unataka kuwatafuta watu ubaya,shauri yako!"

Mimi "Kaka nisamehe ndugu yangu,najua nilifanya makosa makubwa sana naomba unisamehe!"

Ally Mpemba "wewe fanya ulichokuwa unataka kufanya kaka ila ukijaribu utakiona cha moto!"

Aliendelea "Kuna muda unanisababishia matatizo lakini kwasababu dhamira yangu ni kuukimbia umasikini hivyo nakupuuza tu!"

Baada ya jamaa kuniambia kwa jazba alikata simu.Nilijaribu kumpigia tena lakini akawa hapokei tena.Rehema kuna muda aliniambia alikuwa anahitaji kama nina uwezo nimpeleke chuo akasomee ualimu,yeye hakufahamu kama kwa kipindi hicho nilikuwa ninapitia hali ngumu ya kimaisha na ukosefu wa fedha;Kwakuwa nilimpenda na nilikuwa nina ndoto nae,niliona lile pagale langu la kule Chanika niliweke sokoni ili niweze kumpeleka chuo Rehema.Namshukuru Mungu lile pagale niliweza kuliuza kupitia madalali na hivyo nilipata kiasi cha fedha ambacho kilitosha kabisa kumpeleka Rehema chuo cha ualimu na fedha nyingine ikabaki nikawa nimeihifadhi,Rehema nilimpeleka chuo cha ualimu Mhonda.

Maisha yalivyozidi kwenda Kombo kuna siku ilibidi nimfuate Ally Mpemba pale Aggrey nikajaribu kuonana nae na akanisikiliza ila akaniambia nijitahidi siku itakayofuata niende kwake nikaonane nae.

Kesho yake kweli nilikwenda hadi kwake na jamaa akanipatia kazi nyingine ya kufanya.

Ally Mpemba "Kwakuwa umetambua kosa lako na mimi kusema ukweli nililipa gaharama za uharibifu wako kwangu"

Aliendelea " Ila kama umeona nafaa tena kuwa na wewe nitakutazama na ikishindikana nadhani utapotea,huo ndio ukweli na wala nisikufiche"

Mimi "Kaka sasa hivi siwezi kufanya ujinga tena nimejifunza"

Ally Mpemba "Mimi hivi karibuni nafungua mgahawa ila naomba wafanyakazi unitafutie wewe na nitakupa kazi maalumu"

Mimi "Sawa kaka hakuna tatizo!"


Jamaa aliniambia kwenye mgahawa wake huo anao ufungua mimi ndiye niwe msimamizi na atanielekeza namna ya kuwa nawatoa kafara wafanyakazi kila baada ya miezi 6 hadi mwaka ili tuendelee kupiga pesa,ule mgahawa hadi leo ninapoandika hapa upo na unapiga kazi kama kawaida na wafanyakazi kila mwaka ni lazima afe mmoja,hiyo niliasisi mimi.

Ally Mpemba "Utakuwa tayari tufanye kazi?"

Mimi "Nipo tayari kaka"

Ally Mpemba "Ok wewe kaendelee na shughuli zako na utakapokuwa tayari kukamilika nitakujulisha"

Mimi "Kaka lakini hali yangu si nzuri kiuchumi"

Ally Mpemba "Uliharibu wewe kaka,utajiri hauko kama unavyodhani,nilazima uulinde kwa wivu mkubwa sana"

Aliendelea " Subiri nakuja"

Jamaa aliingia ndani akawa ametoka na hela kadhaa,sasa baada ya kuhesabu kiasi kile ilikuwa ni shilingi laki 5.

Ally Mpemba "Chukua hizo zikusogeze angalau kidogo"

Inaendelea: Sehemu ya 25
Wewe mwisho mpemba akuoe shauri yako ndugu yangu 😂😂😂
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom