Utajiri wa Kamanda Barlow Unatisha! Soma hapa...

Utajiri wa Kamanda Barlow Unatisha! Soma hapa...

na huyo ni mmoja tuuu sasa makamanda wakuu wa mikoa yote ya tanzania tukianza kuwachunguza mmoja mmoja tunaweza tusiamini tutakayoyasikia

Mkuu hawa polisi wetu na wakubwa wao ni kichaka cha majambazi na ujangili wa kutisha. Si unakumbuka kwenye sakata la magendo ya sukari na mahindi kuvuka mipaka ya nchi, malori yalikuwa yanasindikizwa na hao polisi mpaka Pinda akaomba msaada wa JWTZ. Pia nasikia Mahita akiwa mkuu wa polisi nchi nzima alijenga nyumba karibu kila mkoa.
 
Mahita ana hospitali pia dar na hizo nyumba ndio usiseme. alivuna sana kipindi kile ujambazi umechachamaa
 
Wanaajiriwa na nani, na tukishapata ukweli unafanyiwa kazi na nani? Theu are all part of the system! Hujaona issue ya radar? Kwetu hakuna alie guilty, uchinguzi wa bure umefanywa na wenyewe huko lakini kwetu hatuna mhusika hata mmoja. Tunaenda kudai change bila hata kujiuliza alietuingiza chaka yuko wapi! Hamna kitu hapa baba. Na political will inatoka kwa mshkaji mkuu ama shosti mkuu?
KINACHO TAKIWA NI POLITICAL WILL. Tukiwa na dhamira ya kweli wachunguzi wa nje wanajiriwa kufanya kazi maalumu kwa kipindi maalumu. uchunguzi unatakiwa uanzie kwa POLISI. TRA na kila idara ya serikali kama watu ni wasafi.kuna baadhi ya idara watu wanadhani wapo pale kwaajili ya kutengeneza pesa tu.
 
Kuna sehemu nilisoma kwenye gazeti kwamba huyu jamaa alikuwa mchapa kazi sana na viongozi wake walikuwa wanamwamini, nikaguna nakujisemea labda! sasa kwa huo utajiri wake wa mashaka najaribu kufikiria ni nani tumwamini tumkabidhi ofisi zetu za UMMA........hata bima feki, tena kamanda wa Mkoa?
 
Haya yote ni matokeo ya mfumo wa Chukuwa Chako Mapema. Kila kiongozi, mtumishi wa umma anachojua ni kujikusanyia mali by whatever means possible. Worse enough siasa za kulindana za CCM ndizo zimetufikisha hapa
 
Huyu mtu amelipwa duniani, Huyu ni mwizi na mzinzi. Anatakiwa afungwe japo kafa. Polisi fanye uchunguzi zidi yake na sio zidi ya walio mua tu. Haiingii akilini mtu kumua kwa ajili ya mapenzi. Huyu bwana atakua kaua wengi sana katika kuiba kwake then wameamua na yeye kumrudi.
 
Kuna sehemu nilisoma kwenye gazeti kwamba huyu jamaa alikuwa mchapa kazi sana na viongozi wake walikuwa wanamwamini, nikaguna nakujisemea labda! sasa kwa huo utajiri wake wa mashaka najaribu kufikiria ni nani tumwamini tumkabidhi ofisi zetu za UMMA........hata bima feki, tena kamanda wa Mkoa?

bado naamini Sekretarieti ya maadili ya viongozi imeshindwa kazi
 
Utajiri wa Kamanda Barlow waanikwa

Frederick Katulanda, Mwanza

SIKU chache baada ya Jeshi la Polisi kutoa taarifa yake ya uchunguzi kuhusu kifo cha aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Liberatus Barlow, umeibuka utata wa mali alizokuwa akimiliki, huku akidaiwa kumiliki utajiri wa kutisha likiwamo jengo la ghorofa.

Habari za kiuchunguzi zilizopatikana zinaeleza kuwa mbali ya jengo hilo, Kamanda Barlow anadaiwa pia kumiliki magari zaidi ya saba yakiwamo malori mawili aina ya Fuso, malori mawili ya mchanga, gari dogo aina ya Toyota Cresta pamoja na Toyota Hilux Double Cabin.

Magari hayo yanadaiwa kuhifadhiwa eneo la Nyakato mjini Mwanza, yakisimamiwa na mfanyabiashara mmoja kwa niaba yake.

Mbali na magari hayo kamanda hyo anatajwa kumiliki nyumba ya kifahari mkoani Mara, ambayo aliijenga alipokuwa RPC mkoani humo, huku nyumba nyingine ikiwa maeneo ya Capri-Point jirani na Ikulu ndogo mkoani Mwanza, inayoelezwa kuwa aliinunua baada ya Serikali kutangaza uuzaji wa nyumba zake kwa watumishi wake.

Umiliki wa mali hizo umeibua maswali mengi, wengi wakitaka kujua iwapo zinalingana na kipato cha Kamanda Barlow, licha ya kuwa na cheo cha Kamanda wa Polisi wa mkoa.

Jengo la ghorofa

Moja ya mali za Kamanda huyo ambazo zimeanza kuwa gumzo mjini Mwanza ni jengo la ghorofa ambalo ujenzi wale ulikuwa ukiendelea katika kiwanja Namba 173 Block G, eneo la Nyakato Mahina kwa kibali Na. 6400 (Building Permit), kilichotolewa na ofisi ya Mhandisi Jiji la Mwanza kikiruhusu kujenga jengo la ghorofa tatu.

Mhandisi wa Jiji

Mhandisi wa Jiji la Mwanza, Boniface Nyambele alikiri Kamanda Barlow kuomba kibali cha kujenga jengo la ghorofa katika kiwanja hicho na kwamba, hata ujenzi wake walikuwa wakiufuatilia kwa karibu.

“Kibali kilichotolewa hapa kilikuwa ni kwa ajili ya kujenga jengo la ghorofa tatu, alipoanza ujenzi alieleza kuwa anataka kujenga ghorofa tano, lakini baada ya kukagua jengo hili tulikuta foundation yake ikiwa na uwezo wa kuhimili ghorofa tatu tu, tulimzuia,” alisema Nyambele.

Hata hivyo, mmoja wa wasimamizi wa ujenzi wa jengo hilo, ambaye hakutaka kutajwa jina lake alisema kuwa marehemu Kamanda Barlow, aliwasisitiza kujenga ghorofa tano.

Alisema kwamba kila mara kamanda huyo alikuwa akiwaeleza kuwa masuala ya vibali kutoka Jiji wanapaswa kumwachia yeye licha ya wakaguzi kumkatalia.

“Baada ya kuwa tumejenga hapa ,mwezi mmoja kabla ya kufariki alituita na kumweleza fundi wetu mkuu kuwa alikuwa amebadili mawazo ya kujenga jengo la ghorofa tatu na kwamba, mpango wake sasa ulikuwa ni kuongeza ghorofa nyingine mbili juu,” alisema mmoja wa wasimamizi wake wa ujenzi na kuongeza:

“Alipoelezwa kama kisheria haikubaliki, alidai hayo hayamuhusu atasimamia yeye huko kwenye sheria.”

Mwandishi wa habari hizi alifika eneo linapojengwa ghorofa hilo na kushuhudia ubao unaoonyesha kuwa kibali cha ujenzi wa jengo hilo kimetolewa kwa Liberatus Barlow.

Wizi ulikwamisha ujenzi

Hata hivyo, majuma machache kabla ya kifo chake, eneo hilo la ujenzi kulitokea wizi wa nondo za ujenzi, ambapo baada ya tukio hilo mwangalizi wa jengo hilo na baadhi ya mafundi wake walikamatwa na kuwaweka mahabusu kwa siku nne katika Kituo cha Polisi Nyakato Mwatex huku ikielezwa kuwa kamanda huyo aliwatoa baada ya kukubaliana nao kumlipa nondo zilizopotea.

“Siku ya wizi huo ujenzi ulisimama na tulikamatwa na kulazimishwa kulipa nondo 10 alizodai zimeibwa, lakini msimamizi wetu nakumbuka aliamua kulipa yeye badala yetu na kesi iliishi baada ya kuwekwa ndani siku nne. Alilipa nondo 60 badala ya 10 na huo ulikuwa mwisho wake wa kuendelea na kazi pamoja nasi, ” alisema kijana huyo aliyewahi kufanya kazi ya kibarua katika jengo hilo.

Umiliki wa magari na utata

Mali nyingine zinazodaiwa kumilikiwa na Kamanda Barlow ni pamoja na magari, ambapo katika idadi ya magari hayo, gari moja aina ya Toyota Hilux ambalo ndilo alipata nalo ajali limeonekana kuwa na utata katika umiliki wake kutokana na namba hiyo ya usajili kubainika kuwa siyo yake kwa vile ilisajiliwa kwa gari aina ya Nisan Premier inayomilikiwa na wamiliki wawili.

Ingawa umiliki wa magari mengine unadaiwa kusajiliwa kwa majina ya mfanyabiashara maarufu jijini Mwanza, lakini umiliki wa gari ambalo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Evarist Ndikilo, alipotangaza kifo cha kamanda huyo, alilitangaza pia kuwa ni mali ya marehemu, imebainika kuwa alilipata wiki moja kabla ya kifo chake.

Katika uchunguzi wa Mwananchi Jumapili, imebainika kuwa hata bima ya gari hilo iliyoonyesha imekatwa kutoka Kampuni ya Bima ya Zanzibar, ilikuwa haitambuliki.

Kamanda Barlow alilichukua gari hilo kwa mmoja wa wafanyabiashara jijini Mwanza, ambaye bado jeshi hilo la polisi linamsaka kutokana na utata wa umiliki wake, kuonyesha namba hiyo siyo halisi ya gari hilo.

Meneja wa Kampuni ya Bima

Meneja wa Tawi la Kampuni ya Bima Zanzibar Mkoa wa Mwanza, Suzan Masele alipotakiwa kutoa ufafanuzi wa suala hilo, alisema kuwa stika ya bima ya gari hilo alilokuwa nalo Kamanda Barlow, wamefuatilia kwenye mfumo wao wa malipo wakabaini kuwa haipo.

"Tumeangalia katika system (mfumo) yetu hakuna bima ya malipo hayo, kwa hiyo ni feki," alisema.

Aidha, utata wa umiliki wa gari hilo pamoja na bima yake ulithibitishwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Said Mwema, ambaye alisema jijini Mwanza kuwa jeshi lake lilikuwa likiendelea na uchunguzi wa umiliki wa gari hilo, pamoja na bima yake kujua ukweli na jinsi lilivyoingia mikononi kwa marehemu siku kadhaa kabla ya kifo chake.

“Suala la gari alilokuwa akilitumia marehemu mpaka siku mauti yanamkuta, pamoja na bima yake, hatuwezi kulieleza hapa, kwa sasa bado tunachunguza,” alisema IGP, alipoulizwa na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kumaliza kutoa taarifa za awali za uchunguzi wa kifo Kamanda Barlow.

TATIZO Wananchi HAMFUATILII MAKAMANDA wa POLICE walivyoMATAJIRI

WOOTE TANGU na BAADA ya VITA VYA UHUJUMU UCHUMI Wote wanaopangiwa MWANZA ni KISIMA cha UTAJIRI

Mfano

1. TRYPHONE MAJI
2. DAUDI
3. REECHUNGURA

Na Wengine wengi hadi MAKAO MAKUU WANAJUA HAYO...
 
MPANGO A....Binafsi naungana na wewe , kimsingi hata mimi sioni utajiri wowote hapa hata kidogo, hizo ni mali za kawaida sana kwa mtu ambaye amewahi kuitumikia serikali kama yeye....hapa issue ni makosa yake tu...ni kwa jinsi gani alipata hizo mali zenye utata, bima feki etc....hapo ndio palipo na issue.
Ukiiangalia sana hii issue ya utata wa magari na baadhi ya vitu nyake, kuna connection(Ring/Syndicate) ya wizi wa magari, rushwa na ubabambikiaji wa kesi hewa etc. Sasa usalama wetu kama raia umekabidhiwa kwa mny'ang'anyi, wezi, majambazi na wahuni ambao huyu ni mmoja wao.

Kweli kabisa mkuu, tuangalie makosa yake, hapa hakuna utajiri. Vitu hivyo ni vya kawaida sana kwa mtu mwenye cheo cha kamanda wa polisi.
 
Huu utajiri wanaotaja hapa jamani mbona siuoni? Hivi kweli mtu anayemiliki katoyota cresta na vifuso viwili vya kuhemea njaa kumbe ni 'tajiri wa kutisha'? Hii ni kauli ya kujidhalilisha wenyewe. Hizi ni mali za kawaida sana kwa mtumishi wa serikali mwenye mshahara mdogo anayejitahidi kwa ujasiriamali apate pesa ya kusomeshea wanae, maana hakika mishahara wanayolipwa haiwezi kusomesha watoto, achilia mbali kupata milo mitatu kwa siku.
Niwape mfano wa ndugu yangu mmoja ni mwalimu wa shule ya msingi. Mshahara wake laki tatu unusu kwa mwezi, wastani wa elfu 11 kwa siku, malipo sawa na kibarua (saidia fundi) wa ujenzi hapa Arusha. Lakini mwalimu huyu ana cresta kama hiyo ya Barlow, pale sokoni amepaki KIA tani 3 huwa inafata mchele Magugu, ana trekta moja, Landrover 109 (Mandolini) guest house, nyumba ya kupangisha, mashamba ya vitunguu Mangola na sasa hivi ameajiri vijana mtaani na TOYO zisizopungua nane. Huyu naye ni tajiri wa kutisha, au vipi? Lakini hamjajiuliza anafanyaje. Alianza kulima mahindi Babati kwenye mashamba ya kukodi. Akanunua trekta akawa anakodishia wenzake. Akafuga nguruwe, nilimtembelea shambani kwake nikakuta nguruwe zaidi ya 200, aliniambia alichukua mkopo wa milioni 10 Azania, na anatarajia atakapowauza hao nguruwe kwa bei ya laki 3 kila mmoja atapata takribani milioni 60. Watumishi wa serikali wanaweza kufanya ujasiriamali na kupata mali, lakini hizi vitu ndogondogo kama vicresta si utajiri jamani tuache kukuza mambo.
Nakubali kujadili na kushangaa kuhusu gari ya marehemu kamanda kuwa na namba feki na bima feki. Lakini hakuna cha kushangaza kuhusu kiasi kile cha mali.
 
huo ndo ujinga ambao tunao kama mtu ni mwovu ni mwovu tu na Mungu anasema liliofungwa duniani limefungwa na mbinguni pia
Sawa kabisa, una maana dini imetufanya wajinga? ukipigwa kofi upande wa kushoto mgeuzie na kulia pia. nimenukuu tu
 
Mwacheni apumzike mbele ya haki ya kudumu. Hata kama hakutenda haki wakati wa uhai wake, huko aliko atakuwa anatendewa haki yake.
Rafiki yangu kuna wengine wengi kama yeye bado wapo hai na hawatendi haki. Je tuwaache tu waendelee kutokutenda haki tusubiri hadi wafikwe na mauti ili wakatendewe haki huko kwa Mungu?
 
Rafiki yangu kuna wengine wengi kama yeye bado wapo hai na hawatendi haki. Je tuwaache tu waendelee kutokutenda haki tusubiri hadi wafikwe na mauti ili wakatendewe haki huko kwa Mungu?

bora nawe umwambie
 
kwa mtiririko huu, huyu mtu alikuwa alikuwa na maadui wengi sana! Na Mungu ni mwingi wa kujua na busara ana makusudi yake ya kumuondoa duniani maana kuwepo kwake kungesababisha maafa makubwa zaidi... all in all katangulia nasi tutafuata
 
haina ya kumwacha apumzike mwizi mkubwa akabwe tu majizi mengine labda yataogopa,viva cdm
Rafiki yangu kuna wengine wengi kama yeye bado wapo hai na hawatendi haki. Je tuwaache tu waendelee kutokutenda haki tusubiri hadi wafikwe na mauti ili wakatendewe haki huko kwa Mungu?
bora nawe umwambie

Tafuteni dawa ya kuwadhibiti wangali hai; kusubiri hadi wafe ndipo tupige domo hapa hakusaidii kwa sababu hakuna hatua mtakazowachukulia wakiwa wameshatangulia huko mbele ya haki. Mnapoteza kuzungumza mali za marehemu hata kama si za halali badala ya kuangalia ni akina nani wengine walio hai wanaotumia madaraka yao vibaya na kujipatia mali kinyume cha sheria.

Kuhusu usajiri wa magari wenye utata, unaweza kukuta kuwa halikuwa kosa lake kwani mimi binafsi niliwahi kukutwa na adha hiyo baada ya kutumia jamaa waliojiita kufanya kazi za Clearing and Forwarding wakiwa na ofisi yao pale mtaa wa Nkurumah, wakanitolea magari mawili bandarini na kuyafanyia usajiri ambapo baadaye ikagundulika kuwa usajili huo ulikuwa na utata mkubwa sana hadi nikalazimika kulipia zaidi ya thamani ya magari yenyewe. Matatizo ya aina hiyo yanakuwa hayasababishwi na mtu mwenyewe bali mfumo wetu wa forodha unaoruhusu rekodi kupotea au kubadilika.
 
Nadhani kwa waliomjua Kamanda alikuwa ni kiboko ya wezi na wahalifu, then hata mwandishi maada yake na uhalisia wa alichoandika ni tofauti, kwani kuwa na nyumba mbili ndio utajiri wa kutisha, ukiangalia na kutafakari vizuri jamaa ghorofa aandike jina lake na kulianika kweupe halafu eti magari aandike majina ya rafiki zake haiji akilini magari hayo thamani yake hata robo ya ghorofa alilokuwa anajenga haifiki nadhani ni ushabiki tu, mbona akina Sumaye, Lowasa, Nape ,Makamba, wanautajiri wa kutisha saana na hawaandikwi, Pia kamanda katumikia kama Mkuu wa Interpol Tanzania muda mrefu, je alikuwa anapaswa madola mangapi na alikuwa hawekezi si atakuwa mjinga, tuchambue kabla ya kushabikia mada
 
Naungana nawe hapo hakuna utajiri wo wote nilisoma historia yake na pia niliwahi kufanya naye kazi miaka ya zamani saana , jamaa alikuwa anahimiza vijana kuwekeza na kuchukua mikopo tena aliwahi kusema msiwafungie wake zenu ndani wafungulieni miradi mbalimbali ili muwezi kuwa na maisha bora na kumbukeni kidogo mnachopata kukitumia vizuri,
Huu utajiri wanaotaja hapa jamani mbona siuoni? Hivi kweli mtu anayemiliki katoyota cresta na vifuso viwili vya kuhemea njaa kumbe ni 'tajiri wa kutisha'? Hii ni kauli ya kujidhalilisha wenyewe. Hizi ni mali za kawaida sana kwa mtumishi wa serikali mwenye mshahara mdogo anayejitahidi kwa ujasiriamali apate pesa ya kusomeshea wanae, maana hakika mishahara wanayolipwa haiwezi kusomesha watoto, achilia mbali kupata milo mitatu kwa siku.
Niwape mfano wa ndugu yangu mmoja ni mwalimu wa shule ya msingi. Mshahara wake laki tatu unusu kwa mwezi, wastani wa elfu 11 kwa siku, malipo sawa na kibarua (saidia fundi) wa ujenzi hapa Arusha. Lakini mwalimu huyu ana cresta kama hiyo ya Barlow, pale sokoni amepaki KIA tani 3 huwa inafata mchele Magugu, ana trekta moja, Landrover 109 (Mandolini) guest house, nyumba ya kupangisha, mashamba ya vitunguu Mangola na sasa hivi ameajiri vijana mtaani na TOYO zisizopungua nane. Huyu naye ni tajiri wa kutisha, au vipi? Lakini hamjajiuliza anafanyaje. Alianza kulima mahindi Babati kwenye mashamba ya kukodi. Akanunua trekta akawa anakodishia wenzake. Akafuga nguruwe, nilimtembelea shambani kwake nikakuta nguruwe zaidi ya 200, aliniambia alichukua mkopo wa milioni 10 Azania, na anatarajia atakapowauza hao nguruwe kwa bei ya laki 3 kila mmoja atapata takribani milioni 60. Watumishi wa serikali wanaweza kufanya ujasiriamali na kupata mali, lakini hizi vitu ndogondogo kama vicresta si utajiri jamani tuache kukuza mambo.
Nakubali kujadili na kushangaa kuhusu gari ya marehemu kamanda kuwa na namba feki na bima feki. Lakini hakuna cha kushangaza kuhusu kiasi kile cha mali.
 
Sawa kabisa, una maana dini imetufanya wajinga? ukipigwa kofi upande wa kushoto mgeuzie na kulia pia. nimenukuu tu

hapa ninamaanisha tuwe kama india mtu akiiba mali za umma ahukumiwe kwa kifo na azikwe kama mbwa. hakuna aja ya kuwalea waovu hawa
 
Back
Top Bottom