Utajiri wa Kamanda Barlow Unatisha! Soma hapa...

Bado naye yule mkur***nz mweny jina kama la Zuberi maana naye hapa mwanza tetesi tunazozipata zinatisha, tunasikia hadi kanyang'anya viwanja vya watu halafu wanajenga magorofa yao ziwani.
 
Hivi inawezekana kuwa Mkuu wa Polisi (RPC) anashindwa kununua hata Gari lake binafsi (Toyota Hilux DC) kwa mapato halali? Ama kwa hakika "kuna watu walizaliwa kuwa wanyanganyi...!
 
Jeshi, polisi vyote vinanuka rushwa, dhuluma na ujambazi uliokithiri. Taasisi zetu zote zimeoza.


Kama wakubwa huko juu wanakula, kwanini wavuja jasho huko chini wasichukue chao mapema kama kirefu cha CCM kinavyosema.
 
kinachonishangaza mm ni kwamba kafa akiwa na mwanamke ambaye tayari ni hawara wa mtu mwingine kwahiyo ni mwizi wa penzi la mnyonge, hadi mali za nchi hii.

jamani inamaana hakuna hata kimoja ambacho aliweza japo kukifanya fair? sasa masala yote aliyoombewa ya nn? kamuibia mkewe penzi bado kaja kaliibia taifa mali halafu mnamwombea. alipaswa kuzikwa kama mbwa ama kuku tu manakesala zote hizi ni bure kwake may be zitasaidia wengine walioko toharani lol!
 
Yaani Tz kila aliye kwenye kitengo cha kudhibiti uharifu ndio mratibu mkuu wa uharifu, huyu tumegundua kwa kuwa kifo chake ni cha utata lkn naamini tungepata fursa ya kugundua mali za wakurugenzi wa TAKOKURU,Upelelezi wa jinai, mahakimu na uhamiaji tungeandamana kuomba sekta zote hizo yifutwe.
 
Miwani ya trafiki na tra haikuwa inaiona hiyo gari. Ukiwaona wanavyokamata mgari ya na pikipiki za wasaka nyoka walala hoi, utadhani kweli ni wachapa kazi. Ukiona hawasimmishi gari la kiraia ujue wanalifahamu ni la mkubwa fulani. Sheria za nchi hii haziwahusu wakubwa kamwe. Kimatendo hatupo sawa mbele ya sheria. Wakubwa wanapeta tu. Wizi mtupu. Rpc kwa kipato chake hawezi jenga ghorofa tano.
 
Tafsiri ya utajiri wa mapolisi na watawala ni watu kujaa magerezani, watu kuwa na vilema, watu kufa kwa mashinikizo ya mioyo, watu kuuawa kama majambazi.
Tatizo la polisi na watawala ni wao kujiona ni vyuma na hawajaumbwa kwa damu na nyama iliyoshikilwa na mifupa.
Wanafikiri wao waliumbwa tofauti hivyo wanahaki ya kudhulumu kila kitu.

HAKIKA AUAYE KWA UPANGA ATAKUFA KWA UPANGA.
 
kinachonishangaza mm ni kwamba kafa akiwa na mwanamke ambaye tayari ni hawara wa mtu mwingine kwahiyo ni mwizi wa penzi la mnyonge, hadi mali za nchi hii.

jamani inamaana hakuna hata kimoja ambacho aliweza japo kukifanya fair? sasa masala yote aliyoombewa ya nn? kamuibia mkewe penzi bado kaja kaliibia taifa mali halafu mnamwombea. alipaswa kuzikwa kama mbwa ama kuku tu manakesala zote hizi ni bure kwake may be zitasaidia wengine walioko toharani lol!
Dah...
kijungu.jpg
 
Miwani ya trafiki na tra haikuwa inaiona hiyo gari. Ukiwaona wanavyokamata mgari ya na pikipiki za wasaka nyoka walala hoi, utadhani kweli ni wachapa kazi. Ukiona hawasimmishi gari la kiraia ujue wanalifahamu ni la mkubwa fulani. Sheria za nchi hii haziwahusu wakubwa kamwe. Kimatendo hatupo sawa mbele ya sheria. Wakubwa wanapeta tu. Wizi mtupu. Rpc kwa kipato chake hawezi jenga ghorofa tano.
 
Mwacheni apumzike mbele ya haki ya kudumu. Hata kama hakutenda haki wakati wa uhai wake, huko aliko atakuwa anatendewa haki yake.
haina ya kumwacha apumzike mwizi mkubwa akabwe tu majizi mengine labda yataogopa,viva cdm
 
Lakini kwa nini haya yote yanasemwa mtu angali maeshafariki?.............Kwa nini haya hayakusemwa akiwa hali ili ahojiwe alikopata mimali yote hiyo.....Tusije tukasikia kumbe naye alikuwa jambazi sugu
 
Ukweli ni kuwa haya majitu ni majizi makubwa na uhai unapotoka ndipo haya yote yanafichuka na kiukweli ukiwa unatumia madaraka yako vibaya lazima utajiingiza katika madhala makubwa
 
mnashangaa nini aliyewahi kuwa kamanda msaidizi wa mkoa wa Dar es salaam alishiriki kuwapiga risasi wafanyabiashara wa madini wakawaua wakawanyang'anya hela zao kisha wakasema ni majambazi.baada ya kelele tume ikaundwa ikasema si kweli.kesi mahakamani polisi wakaacha kumshika mmoja wa watuhumiwa ambaye inasemekana kufyatua risasi.
Ingawa mi si mwanasheria lakini nadhani kuna kitu kula njama ya kuua,wote wako nje,nani anawachagua hawa?system.
Mauaji yote yaliyofanywa na polisi umeona Mwema amehuzunika?wapi yote hii miuaji kama wanasiasa waliowateua
 
Tayari imeshakuwa ajenda kwa wakosa sera ndo.mtaimba majukwaani wee mkiacha ya msingi na ya maendeleo.
 
Utajiri wa Kamanda Barlow waanikwa

Frederick Katulanda, Mwanza

SIKU chache baada ya Jeshi la Polisi kutoa taarifa yake ya uchunguzi kuhusu kifo cha aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Liberatus Barlow, umeibuka utata wa mali alizokuwa akimiliki, huku akidaiwa kumiliki utajiri wa kutisha likiwamo jengo la ghorofa.

Habari za kiuchunguzi zilizopatikana zinaeleza kuwa mbali ya jengo hilo, Kamanda Barlow anadaiwa pia kumiliki magari zaidi ya saba yakiwamo malori mawili aina ya Fuso, malori mawili ya mchanga, gari dogo aina ya Toyota Cresta pamoja na Toyota Hilux Double Cabin.

Magari hayo yanadaiwa kuhifadhiwa eneo la Nyakato mjini Mwanza, yakisimamiwa na mfanyabiashara mmoja kwa niaba yake.

Mbali na magari hayo kamanda hyo anatajwa kumiliki nyumba ya kifahari mkoani Mara, ambayo aliijenga alipokuwa RPC mkoani humo, huku nyumba nyingine ikiwa maeneo ya Capri-Point jirani na Ikulu ndogo mkoani Mwanza, inayoelezwa kuwa aliinunua baada ya Serikali kutangaza uuzaji wa nyumba zake kwa watumishi wake.

Umiliki wa mali hizo umeibua maswali mengi, wengi wakitaka kujua iwapo zinalingana na kipato cha Kamanda Barlow, licha ya kuwa na cheo cha Kamanda wa Polisi wa mkoa.

Jengo la ghorofa

Moja ya mali za Kamanda huyo ambazo zimeanza kuwa gumzo mjini Mwanza ni jengo la ghorofa ambalo ujenzi wale ulikuwa ukiendelea katika kiwanja Namba 173 Block G, eneo la Nyakato Mahina kwa kibali Na. 6400 (Building Permit), kilichotolewa na ofisi ya Mhandisi Jiji la Mwanza kikiruhusu kujenga jengo la ghorofa tatu.

Mhandisi wa Jiji

Mhandisi wa Jiji la Mwanza, Boniface Nyambele alikiri Kamanda Barlow kuomba kibali cha kujenga jengo la ghorofa katika kiwanja hicho na kwamba, hata ujenzi wake walikuwa wakiufuatilia kwa karibu.

“Kibali kilichotolewa hapa kilikuwa ni kwa ajili ya kujenga jengo la ghorofa tatu, alipoanza ujenzi alieleza kuwa anataka kujenga ghorofa tano, lakini baada ya kukagua jengo hili tulikuta foundation yake ikiwa na uwezo wa kuhimili ghorofa tatu tu, tulimzuia,” alisema Nyambele.

Hata hivyo, mmoja wa wasimamizi wa ujenzi wa jengo hilo, ambaye hakutaka kutajwa jina lake alisema kuwa marehemu Kamanda Barlow, aliwasisitiza kujenga ghorofa tano.

Alisema kwamba kila mara kamanda huyo alikuwa akiwaeleza kuwa masuala ya vibali kutoka Jiji wanapaswa kumwachia yeye licha ya wakaguzi kumkatalia.

“Baada ya kuwa tumejenga hapa ,mwezi mmoja kabla ya kufariki alituita na kumweleza fundi wetu mkuu kuwa alikuwa amebadili mawazo ya kujenga jengo la ghorofa tatu na kwamba, mpango wake sasa ulikuwa ni kuongeza ghorofa nyingine mbili juu,” alisema mmoja wa wasimamizi wake wa ujenzi na kuongeza:

“Alipoelezwa kama kisheria haikubaliki, alidai hayo hayamuhusu atasimamia yeye huko kwenye sheria.”

Mwandishi wa habari hizi alifika eneo linapojengwa ghorofa hilo na kushuhudia ubao unaoonyesha kuwa kibali cha ujenzi wa jengo hilo kimetolewa kwa Liberatus Barlow.

Wizi ulikwamisha ujenzi

Hata hivyo, majuma machache kabla ya kifo chake, eneo hilo la ujenzi kulitokea wizi wa nondo za ujenzi, ambapo baada ya tukio hilo mwangalizi wa jengo hilo na baadhi ya mafundi wake walikamatwa na kuwaweka mahabusu kwa siku nne katika Kituo cha Polisi Nyakato Mwatex huku ikielezwa kuwa kamanda huyo aliwatoa baada ya kukubaliana nao kumlipa nondo zilizopotea.

“Siku ya wizi huo ujenzi ulisimama na tulikamatwa na kulazimishwa kulipa nondo 10 alizodai zimeibwa, lakini msimamizi wetu nakumbuka aliamua kulipa yeye badala yetu na kesi iliishi baada ya kuwekwa ndani siku nne. Alilipa nondo 60 badala ya 10 na huo ulikuwa mwisho wake wa kuendelea na kazi pamoja nasi, ” alisema kijana huyo aliyewahi kufanya kazi ya kibarua katika jengo hilo.

Umiliki wa magari na utata

Mali nyingine zinazodaiwa kumilikiwa na Kamanda Barlow ni pamoja na magari, ambapo katika idadi ya magari hayo, gari moja aina ya Toyota Hilux ambalo ndilo alipata nalo ajali limeonekana kuwa na utata katika umiliki wake kutokana na namba hiyo ya usajili kubainika kuwa siyo yake kwa vile ilisajiliwa kwa gari aina ya Nisan Premier inayomilikiwa na wamiliki wawili.

Ingawa umiliki wa magari mengine unadaiwa kusajiliwa kwa majina ya mfanyabiashara maarufu jijini Mwanza, lakini umiliki wa gari ambalo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Evarist Ndikilo, alipotangaza kifo cha kamanda huyo, alilitangaza pia kuwa ni mali ya marehemu, imebainika kuwa alilipata wiki moja kabla ya kifo chake.

Katika uchunguzi wa Mwananchi Jumapili, imebainika kuwa hata bima ya gari hilo iliyoonyesha imekatwa kutoka Kampuni ya Bima ya Zanzibar, ilikuwa haitambuliki.

Kamanda Barlow alilichukua gari hilo kwa mmoja wa wafanyabiashara jijini Mwanza, ambaye bado jeshi hilo la polisi linamsaka kutokana na utata wa umiliki wake, kuonyesha namba hiyo siyo halisi ya gari hilo.

Meneja wa Kampuni ya Bima

Meneja wa Tawi la Kampuni ya Bima Zanzibar Mkoa wa Mwanza, Suzan Masele alipotakiwa kutoa ufafanuzi wa suala hilo, alisema kuwa stika ya bima ya gari hilo alilokuwa nalo Kamanda Barlow, wamefuatilia kwenye mfumo wao wa malipo wakabaini kuwa haipo.

"Tumeangalia katika system (mfumo) yetu hakuna bima ya malipo hayo, kwa hiyo ni feki," alisema.

Aidha, utata wa umiliki wa gari hilo pamoja na bima yake ulithibitishwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Said Mwema, ambaye alisema jijini Mwanza kuwa jeshi lake lilikuwa likiendelea na uchunguzi wa umiliki wa gari hilo, pamoja na bima yake kujua ukweli na jinsi lilivyoingia mikononi kwa marehemu siku kadhaa kabla ya kifo chake.

“Suala la gari alilokuwa akilitumia marehemu mpaka siku mauti yanamkuta, pamoja na bima yake, hatuwezi kulieleza hapa, kwa sasa bado tunachunguza,” alisema IGP, alipoulizwa na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kumaliza kutoa taarifa za awali za uchunguzi wa kifo Kamanda Barlow.

muulizeni kama hzo mali kazikwa nazo...tamaa ya binadam bwana
 
Back
Top Bottom