Utajiri wa Kamanda Barlow Unatisha! Soma hapa...

Utajiri wa Kamanda Barlow Unatisha! Soma hapa...

Hizi mali za mashaka ni ushahidi kuwa watendaji wetu wengi ni majambazi wasioweza kutoa maelezo ya jinsi walivyochuma. Barlow maisha yake, kifo chake hata kipato chake ni picha ya majambazi wanaoifanya Tanzania iwe omba omba. Bahati mbaya ni kwamba jinai hii inaanzia ikulu hadi kwa mfagiaji.

Heri Mungu awapunguze wanangu wezi walionishinda ili wale wasafi hasa wakulima na wafanyakazi wa kipato cha chini wapunguziwe mzigo na madhara. Je hao nao wakipata nafasi watafanya nini? Zingatia sana hili Mtanzania. Vinginevyo unaweza kukuta unamchukia Barlow kumbe unajichukia mwenyewe.

soma hii niliandika muda kidogo mkuu, hili ni tatizo kubwa sana hata ndani ya mfumo wa ufisadi wenyewe. https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...ni-ufisadi-usiokua-na-nidhamu.html?highlight=
 
imekula kwake mali hazina majina yake,bora hata angekuwa anaandika ya watoto au mke wake,imekula kwake

Wataambulia ghorofa, mara nyingi watu wengi wakiwa wanavuta pumzi wanajua hawawezi kufa hivyo mali zao huziweka rehani wakiamini ipo siku wataziweka sawa
 
Sijui kwanini nilizaliwe kwenye nchi hii,full majambazi, wenye dhamani yakulinda mali zetu ndio wanaongoza kwa wizi sasa wengine sijui wafanye nini

Ndo maana hata kwenye chaguzi zetu wanasimama kidete kuhakikisha CCM inashinda ili kuendelea kulinda mfumo wao wa ujambazi waliojitengenezea! Sisi wananchi tunaoendelea kuishabikia CCM haki ya nani ni mataahira. Eti kapuku naye utamsikia akisema CCM ina wenyewe na wenyewe ni sisi!! Tumb....ff!! Ona wenye ccm yao wanavyokula wewe mjinga wewe!!

Hatuna budi kuungana kwa umoja wetu ili hiki chama cha majambazi tukitose. Labda mali zetu zitarudi. Sasa huyu marehemu si anyang'anywe hizo mali jamani!!??
 
SIKU chache baada ya Jeshi la Polisi kutoa taarifa yake ya uchunguzi kuhusu kifo cha aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Liberatus Barlow, umeibuka utata wa mali alizokuwa akimiliki, huku akidaiwa kumiliki utajiri wa kutisha likiwamo jengo la ghorofa.

Habari za kiuchunguzi zilizopatikana zinaeleza kuwa mbali ya jengo hilo, Kamanda Barlow anadaiwa pia kumiliki magari zaidi ya saba yakiwamo malori mawili aina ya Fuso, malori mawili ya mchanga, gari dogo aina ya Toyota Cresta pamoja na Toyota Hilux Double Cabin.

Magari hayo yanadaiwa kuhifadhiwa eneo la Nyakato mjini Mwanza, yakisimamiwa na mfanyabiashara mmoja kwa niaba yake.

Mbali na magari hayo kamanda hyo anatajwa kumiliki nyumba ya kifahari mkoani Mara, ambayo aliijenga alipokuwa RPC mkoani humo, huku nyumba nyingine ikiwa maeneo ya Capri-Point jirani na Ikulu ndogo mkoani Mwanza, inayoelezwa kuwa aliinunua baada ya Serikali kutangaza uuzaji wa nyumba zake kwa watumishi wake.

Umiliki wa mali hizo umeibua maswali mengi, wengi wakitaka kujua iwapo zinalingana na kipato cha Kamanda Barlow, licha ya kuwa na cheo cha Kamanda wa Polisi wa mkoa.

Jengo la ghorofa

Moja ya mali za Kamanda huyo ambazo zimeanza kuwa gumzo mjini Mwanza ni jengo la ghorofa ambalo ujenzi wale ulikuwa ukiendelea katika kiwanja Namba 173 Block G, eneo la Nyakato Mahina kwa kibali Na. 6400 (Building Permit), kilichotolewa na ofisi ya Mhandisi Jiji la Mwanza kikiruhusu kujenga jengo la ghorofa tatu.

Mhandisi wa Jiji
Mhandisi wa Jiji la Mwanza, Boniface Nyambele alikiri Kamanda Barlow kuomba kibali cha kujenga jengo la ghorofa katika kiwanja hicho na kwamba, hata ujenzi wake walikuwa wakiufuatilia kwa karibu.

"Kibali kilichotolewa hapa kilikuwa ni kwa ajili ya kujenga jengo la ghorofa tatu, alipoanza ujenzi alieleza kuwa anataka kujenga ghorofa tano, lakini baada ya kukagua jengo hili tulikuta foundation yake ikiwa na uwezo wa kuhimili ghorofa tatu tu, tulimzuia," alisema Nyambele.

Hata hivyo, mmoja wa wasimamizi wa ujenzi wa jengo hilo, ambaye hakutaka kutajwa jina lake alisema kuwa marehemu Kamanda Barlow, aliwasisitiza kujenga ghorofa tano.

Alisema kwamba kila mara kamanda huyo alikuwa akiwaeleza kuwa masuala ya vibali kutoka Jiji wanapaswa kumwachia yeye licha ya wakaguzi kumkatalia.

"Baada ya kuwa tumejenga hapa ,mwezi mmoja kabla ya kufariki alituita na kumweleza fundi wetu mkuu kuwa alikuwa amebadili mawazo ya kujenga jengo la ghorofa tatu na kwamba, mpango wake sasa ulikuwa ni kuongeza ghorofa nyingine mbili juu," alisema mmoja wa wasimamizi wake wa ujenzi na kuongeza:

"Alipoelezwa kama kisheria haikubaliki, alidai hayo hayamuhusu atasimamia yeye huko kwenye sheria."

Mwandishi wa habari hizi alifika eneo linapojengwa ghorofa hilo na kushuhudia ubao unaoonyesha kuwa kibali cha ujenzi wa jengo hilo kimetolewa kwa Liberatus Barlow.

Wizi ulikwamisha ujenzi

Hata hivyo, majuma machache kabla ya kifo chake, eneo hilo la ujenzi kulitokea wizi wa nondo za ujenzi, ambapo baada ya tukio hilo mwangalizi wa jengo hilo na baadhi ya mafundi wake walikamatwa na kuwaweka mahabusu kwa siku nne katika Kituo cha Polisi Nyakato Mwatex huku ikielezwa kuwa kamanda huyo aliwatoa baada ya kukubaliana nao kumlipa nondo zilizopotea.

"Siku ya wizi huo ujenzi ulisimama na tulikamatwa na kulazimishwa kulipa nondo 10 alizodai zimeibwa, lakini msimamizi wetu nakumbuka aliamua kulipa yeye badala yetu na kesi iliishi baada ya kuwekwa ndani siku nne. Alilipa nondo 60 badala ya 10 na huo ulikuwa mwisho wake wa kuendelea na kazi pamoja nasi, " alisema kijana huyo aliyewahi kufanya kazi ya kibarua katika jengo hilo.

Umiliki wa magari na utata

Mali nyingine zinazodaiwa kumilikiwa na Kamanda Barlow ni pamoja na magari, ambapo katika idadi ya magari hayo, gari moja aina ya Toyota Hilux ambalo ndilo alipata nalo ajali limeonekana kuwa na utata katika umiliki wake kutokana na namba hiyo ya usajili kubainika kuwa siyo yake kwa vile ilisajiliwa kwa gari aina ya Nisan Premier inayomilikiwa na wamiliki wawili.

Ingawa umiliki wa magari mengine unadaiwa kusajiliwa kwa majina ya mfanyabiashara maarufu jijini Mwanza, lakini umiliki wa gari ambalo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Evarist Ndikilo, alipotangaza kifo cha kamanda huyo, alilitangaza pia kuwa ni mali ya marehemu, imebainika kuwa alilipata wiki moja kabla ya kifo chake.

Katika uchunguzi wa Mwananchi Jumapili, imebainika kuwa hata bima ya gari hilo iliyoonyesha imekatwa kutoka Kampuni ya Bima ya Zanzibar, ilikuwa haitambuliki.

Kamanda Barlow alilichukua gari hilo kwa mmoja wa wafanyabiashara jijini Mwanza, ambaye bado jeshi hilo la polisi linamsaka kutokana na utata wa umiliki wake, kuonyesha namba hiyo siyo halisi ya gari hilo.

Meneja wa Kampuni ya Bima

Meneja wa Tawi la Kampuni ya Bima Zanzibar Mkoa wa Mwanza, Suzan Masele alipotakiwa kutoa ufafanuzi wa suala hilo, alisema kuwa stika ya bima ya gari hilo alilokuwa nalo Kamanda Barlow, wamefuatilia kwenye mfumo wao wa malipo wakabaini kuwa haipo.

"Tumeangalia katika system (mfumo) yetu hakuna bima ya malipo hayo, kwa hiyo ni feki," alisema.

Aidha, utata wa umiliki wa gari hilo pamoja na bima yake ulithibitishwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Said Mwema, ambaye alisema jijini Mwanza kuwa jeshi lake lilikuwa likiendelea na uchunguzi wa umiliki wa gari hilo, pamoja na bima yake kujua ukweli na jinsi lilivyoingia mikononi kwa marehemu siku kadhaa kabla ya kifo chake.

"Suala la gari alilokuwa akilitumia marehemu mpaka siku mauti yanamkuta, pamoja na bima yake, hatuwezi kulieleza hapa, kwa sasa bado tunachunguza," alisema IGP, alipoulizwa na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kumaliza kutoa taarifa za awali za uchunguzi wa kifo Kamanda Barlow.

Mwananchi.
​
​
​
 
naendelea kutafakari wapi tunaenda! kama hivi ndivyo basi hata hao makamanda ambao wako hai
hali itakuwa hiyo2, wakimaliza kujiuliza ya barlow, waanze kujichunguza na wao wenyewe!
 
............. He! si mnajionea wenyewe..... walio wasafi ni akina nani? ukienda kwa viongozi wa serikali.... ukija kwa watu wa TRA..... ukiangalia wanajeshi..... watumishi wa mahakama........ uhamiaji........nchi imekuwa kama shamba kuwa la mahindi yaliyonawiri mali ya bibi......... na manyani wameachiwa wale jinsi watakavyo...... ndo nasema hao TAKUKURU wanafanya kazi gani? kama kweli wangekuwa wako makini wangeangalia hao ma RPC kwa mikoa yoteeeee na utajiri wao mbona tutashangaa.... nchi inazidi kuenganisha kati ya walionacho na wasionacho..... wako wanaoshindwa kulipa ada za watoto mashuleni nakulalia mlo mmoja wa kula usife..... huku kuna wao wanaoamua kula kila kitu watakacho na kusasaza eeh Mungu tusaidie. !!!!!!!!1
 
makamanda wa polisi kuanzi ngazi ya wilaya wana nafasi kubwa sana ya kutajirika. zaidi wanapata kutoka kwa makamanda waliopo chini yao. yaani kama ikitokea issue ya hela kwa njia yoyote ni lazima watampelekea mkuu wao. kwa namna hii mlafi anaweza kukusanya kiasi kikubwa tu. ikiwa kuna ambaye hawasilishi gawio ujue ataswekwa mahali ambapo kuiona senti ni kazi sana. hii haiko kwa polisi pekee karibu kila sekta yaani kuna syndicate ya ulaji na kulindana. hata kupeana vyeo kunategemea hali hii. hakuna uzalendo bali sifa kubwa ni kulinda maslahi ya hiyo syndicate. ndiyo maana kila mtu analilia cheo akae ofisini aingie kwenye syndicate. mtu anasoma akiwa kazini si kwa sababu anahitaji huo ujuzi kutekeleza majukumu bali akae mahali ale kiulaini. Ujuzi nini bwana. Watanzania tuna safari nndefu!
 
nadhani tunapotosha dhana ya utajiri wa kutisha, mimi nilidhani ni mali zinazofikia mabilioni ya fedha, kumbe vigorofa vitatu na vigari viwili. Tusikuze mambo, labda tujiulize amepata wapi hizo mali zote wakati mshahara wake ni mdogo.
 
Ila si kwamba nataka kumtetea huyu Jamaa, Watanzani wanapenda sana kuhukumu bila kujiuliza, Huyu jamaa mimi nimewahi kukutana naye akiwa RPC Mara, na alikuwa na Mashamba yake makubwa nje ya Mji wa Musoma huko Buhemba na alikuwa analima si mchezo na kila wikendi ilikuwa ni lazima akatembelee mashamba yake, na jamaa alikuwa anapenda kilimo sana kwa maelezo yake so tusipende kuhukumu tu kwamba kaiba, Ina maana akitokea Mwalimu wa Chekechea akawa na Magari atakuwa ameiba? kuna watu wameinvest kwenye maeneo kama kilimo na kilimo ndo investment pekee ambayo ukibahatika inakutoa mazima
 
Hizi mali za mashaka ni ushahidi kuwa watendaji wetu wengi ni majambazi wasioweza kutoa maelezo ya jinsi walivyochuma. Barlow maisha yake, kifo chake hata kipato chake ni picha ya majambazi wanaoifanya Tanzania iwe omba omba. Bahati mbaya ni kwamba jinai hii inaanzia ikulu hadi kwa mfagiaji. Heri Mungu awapunguze wanangu wezi walionishinda ili wale wasafi hasa wakulima na wafanyakazi wa kipato cha chini wapunguziwe mzigo na madhara. Je hao nao wakipata nafasi watafanya nini? Zingatia sana hili Mtanzania. Vinginevyo unaweza kukuta unamchukia Barlow kumbe unajichukia mwenyewe.
Naona hii nchi mungu ameamua kuikomboa kwa staili ya aina yake kwanza kwa kuonyesha madhambi ya watawala ili wananchi wajiandae kujitawala
 
Utajiri wa Kamanda Barlow waanikwa

Frederick Katulanda, Mwanza

SIKU chache baada ya Jeshi la Polisi kutoa taarifa yake ya uchunguzi kuhusu kifo cha aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Liberatus Barlow, umeibuka utata wa mali alizokuwa akimiliki, huku akidaiwa kumiliki utajiri wa kutisha likiwamo jengo la ghorofa.

Habari za kiuchunguzi zilizopatikana zinaeleza kuwa mbali ya jengo hilo, Kamanda Barlow anadaiwa pia kumiliki magari zaidi ya saba yakiwamo malori mawili aina ya Fuso, malori mawili ya mchanga, gari dogo aina ya Toyota Cresta pamoja na Toyota Hilux Double Cabin.

Magari hayo yanadaiwa kuhifadhiwa eneo la Nyakato mjini Mwanza, yakisimamiwa na mfanyabiashara mmoja kwa niaba yake.

Mbali na magari hayo kamanda hyo anatajwa kumiliki nyumba ya kifahari mkoani Mara, ambayo aliijenga alipokuwa RPC mkoani humo, huku nyumba nyingine ikiwa maeneo ya Capri-Point jirani na Ikulu ndogo mkoani Mwanza, inayoelezwa kuwa aliinunua baada ya Serikali kutangaza uuzaji wa nyumba zake kwa watumishi wake.

Umiliki wa mali hizo umeibua maswali mengi, wengi wakitaka kujua iwapo zinalingana na kipato cha Kamanda Barlow, licha ya kuwa na cheo cha Kamanda wa Polisi wa mkoa.

Jengo la ghorofa

Moja ya mali za Kamanda huyo ambazo zimeanza kuwa gumzo mjini Mwanza ni jengo la ghorofa ambalo ujenzi wale ulikuwa ukiendelea katika kiwanja Namba 173 Block G, eneo la Nyakato Mahina kwa kibali Na. 6400 (Building Permit), kilichotolewa na ofisi ya Mhandisi Jiji la Mwanza kikiruhusu kujenga jengo la ghorofa tatu.

Mhandisi wa Jiji

Mhandisi wa Jiji la Mwanza, Boniface Nyambele alikiri Kamanda Barlow kuomba kibali cha kujenga jengo la ghorofa katika kiwanja hicho na kwamba, hata ujenzi wake walikuwa wakiufuatilia kwa karibu.

“Kibali kilichotolewa hapa kilikuwa ni kwa ajili ya kujenga jengo la ghorofa tatu, alipoanza ujenzi alieleza kuwa anataka kujenga ghorofa tano, lakini baada ya kukagua jengo hili tulikuta foundation yake ikiwa na uwezo wa kuhimili ghorofa tatu tu, tulimzuia,” alisema Nyambele.

Hata hivyo, mmoja wa wasimamizi wa ujenzi wa jengo hilo, ambaye hakutaka kutajwa jina lake alisema kuwa marehemu Kamanda Barlow, aliwasisitiza kujenga ghorofa tano.

Alisema kwamba kila mara kamanda huyo alikuwa akiwaeleza kuwa masuala ya vibali kutoka Jiji wanapaswa kumwachia yeye licha ya wakaguzi kumkatalia.

“Baada ya kuwa tumejenga hapa ,mwezi mmoja kabla ya kufariki alituita na kumweleza fundi wetu mkuu kuwa alikuwa amebadili mawazo ya kujenga jengo la ghorofa tatu na kwamba, mpango wake sasa ulikuwa ni kuongeza ghorofa nyingine mbili juu,” alisema mmoja wa wasimamizi wake wa ujenzi na kuongeza:

“Alipoelezwa kama kisheria haikubaliki, alidai hayo hayamuhusu atasimamia yeye huko kwenye sheria.”

Mwandishi wa habari hizi alifika eneo linapojengwa ghorofa hilo na kushuhudia ubao unaoonyesha kuwa kibali cha ujenzi wa jengo hilo kimetolewa kwa Liberatus Barlow.

Wizi ulikwamisha ujenzi

Hata hivyo, majuma machache kabla ya kifo chake, eneo hilo la ujenzi kulitokea wizi wa nondo za ujenzi, ambapo baada ya tukio hilo mwangalizi wa jengo hilo na baadhi ya mafundi wake walikamatwa na kuwaweka mahabusu kwa siku nne katika Kituo cha Polisi Nyakato Mwatex huku ikielezwa kuwa kamanda huyo aliwatoa baada ya kukubaliana nao kumlipa nondo zilizopotea.

“Siku ya wizi huo ujenzi ulisimama na tulikamatwa na kulazimishwa kulipa nondo 10 alizodai zimeibwa, lakini msimamizi wetu nakumbuka aliamua kulipa yeye badala yetu na kesi iliishi baada ya kuwekwa ndani siku nne. Alilipa nondo 60 badala ya 10 na huo ulikuwa mwisho wake wa kuendelea na kazi pamoja nasi, ” alisema kijana huyo aliyewahi kufanya kazi ya kibarua katika jengo hilo.

Umiliki wa magari na utata

Mali nyingine zinazodaiwa kumilikiwa na Kamanda Barlow ni pamoja na magari, ambapo katika idadi ya magari hayo, gari moja aina ya Toyota Hilux ambalo ndilo alipata nalo ajali limeonekana kuwa na utata katika umiliki wake kutokana na namba hiyo ya usajili kubainika kuwa siyo yake kwa vile ilisajiliwa kwa gari aina ya Nisan Premier inayomilikiwa na wamiliki wawili.

Ingawa umiliki wa magari mengine unadaiwa kusajiliwa kwa majina ya mfanyabiashara maarufu jijini Mwanza, lakini umiliki wa gari ambalo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Evarist Ndikilo, alipotangaza kifo cha kamanda huyo, alilitangaza pia kuwa ni mali ya marehemu, imebainika kuwa alilipata wiki moja kabla ya kifo chake.

Katika uchunguzi wa Mwananchi Jumapili, imebainika kuwa hata bima ya gari hilo iliyoonyesha imekatwa kutoka Kampuni ya Bima ya Zanzibar, ilikuwa haitambuliki.

Kamanda Barlow alilichukua gari hilo kwa mmoja wa wafanyabiashara jijini Mwanza, ambaye bado jeshi hilo la polisi linamsaka kutokana na utata wa umiliki wake, kuonyesha namba hiyo siyo halisi ya gari hilo.

Meneja wa Kampuni ya Bima

Meneja wa Tawi la Kampuni ya Bima Zanzibar Mkoa wa Mwanza, Suzan Masele alipotakiwa kutoa ufafanuzi wa suala hilo, alisema kuwa stika ya bima ya gari hilo alilokuwa nalo Kamanda Barlow, wamefuatilia kwenye mfumo wao wa malipo wakabaini kuwa haipo.

"Tumeangalia katika system (mfumo) yetu hakuna bima ya malipo hayo, kwa hiyo ni feki," alisema.

Aidha, utata wa umiliki wa gari hilo pamoja na bima yake ulithibitishwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Said Mwema, ambaye alisema jijini Mwanza kuwa jeshi lake lilikuwa likiendelea na uchunguzi wa umiliki wa gari hilo, pamoja na bima yake kujua ukweli na jinsi lilivyoingia mikononi kwa marehemu siku kadhaa kabla ya kifo chake.

“Suala la gari alilokuwa akilitumia marehemu mpaka siku mauti yanamkuta, pamoja na bima yake, hatuwezi kulieleza hapa, kwa sasa bado tunachunguza,” alisema IGP, alipoulizwa na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kumaliza kutoa taarifa za awali za uchunguzi wa kifo Kamanda Barlow.
Kinachonisikitisha ni kwamba, na kwa hili mhariri huwezi kubisha hata kidogo, Barlow angekuwa hai usingeandika hii habari, never! Mwananchi unatuandikia hii habari leo tuifanye nini sasa?
 
kinachonishangaza mm ni kwamba kafa akiwa na mwanamke ambaye tayari ni hawara wa mtu mwingine kwahiyo ni mwizi wa penzi la mnyonge, hadi mali za nchi hii.

jamani inamaana hakuna hata kimoja ambacho aliweza japo kukifanya fair? sasa masala yote aliyoombewa ya nn? kamuibia mkewe penzi bado kaja kaliibia taifa mali halafu mnamwombea. alipaswa kuzikwa kama mbwa ama kuku tu manakesala zote hizi ni bure kwake may be zitasaidia wengine walioko toharani lol!
umesemama sawa lkn tumefundishwa tusihukumu huenda ameenda mbiguni kama alitubu pale walipokuwa wamemlenga
 
Kaibiwa nondo 10 kalipwa 60 na huyo ni kamanda wa polisi mkoa, sasa nauliza hao wa chini yake vipi?
Inaonyesha huyu kamanda alikuwa anajihusisha na magenge ya ujambazi na bila shaka na yeye alikuwa jambazi
R.I.P kamanda mwizi.
 
Wala hakuna cha kujadili hapa, tunaonyesha mshangao wa vitu vya wazi. Kuwa usalama wa Taifa hili huko mikononi mwa watu gani hilo linajulikana na husemwa almost everyday. Hii si habari kabisa, ni mazungumzo baada ya habari
 
Nahisi nimekuelewa Eliza kwamba haya mambo yapo sana na Barlow sio wa kawanza wala wa mwisho, right?
 
Ila si kwamba nataka kumtetea huyu Jamaa, Watanzani wanapenda sana kuhukumu bila kujiuliza, Huyu jamaa mimi nimewahi kukutana naye akiwa RPC Mara, na alikuwa na Mashamba yake makubwa nje ya Mji wa Musoma huko Buhemba na alikuwa analima si mchezo na kila wikendi ilikuwa ni lazima akatembelee mashamba yake, na jamaa alikuwa anapenda kilimo sana kwa maelezo yake so tusipende kuhukumu tu kwamba kaiba, Ina maana akitokea Mwalimu wa Chekechea akawa na Magari atakuwa ameiba? kuna watu wameinvest kwenye maeneo kama kilimo na kilimo ndo investment pekee ambayo ukibahatika inakutoa mazima

Umenena vema. LAKINI

Kuwa mkulima hakumfanyi aruhusiwe kuwa na magari yasiyojulikana yamepatikana wapi na yenye usajili wa mashaka na kuhitajika uchunguzi.

Kuwa mkulima hakummhalalishii yeye kuwa na namba bandia za usajili wa magari.

Kuwa mkulima hakumfanyi yeye aruhusiwe kuwa na bima feki ya magari.

Bado anaonewa??????
 
umesemama sawa lkn tumefundishwa tusihukumu huenda ameenda mbiguni kama alitubu pale walipokuwa wamemlenga

huo ndo ujinga ambao tunao kama mtu ni mwovu ni mwovu tu na Mungu anasema liliofungwa duniani limefungwa na mbinguni pia
 
Back
Top Bottom