Utajiri wa Kamanda Barlow Unatisha! Soma hapa... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Utajiri wa Kamanda Barlow Unatisha! Soma hapa...

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mwana Mpotevu, Oct 28, 2012.

 1. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #1
  Oct 28, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,294
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Utajiri wa Kamanda Barlow waanikwa

  Frederick Katulanda, Mwanza

  SIKU chache baada ya Jeshi la Polisi kutoa taarifa yake ya uchunguzi kuhusu kifo cha aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Liberatus Barlow, umeibuka utata wa mali alizokuwa akimiliki, huku akidaiwa kumiliki utajiri wa kutisha likiwamo jengo la ghorofa.

  Habari za kiuchunguzi zilizopatikana zinaeleza kuwa mbali ya jengo hilo, Kamanda Barlow anadaiwa pia kumiliki magari zaidi ya saba yakiwamo malori mawili aina ya Fuso, malori mawili ya mchanga, gari dogo aina ya Toyota Cresta pamoja na Toyota Hilux Double Cabin.

  Magari hayo yanadaiwa kuhifadhiwa eneo la Nyakato mjini Mwanza, yakisimamiwa na mfanyabiashara mmoja kwa niaba yake.

  Mbali na magari hayo kamanda hyo anatajwa kumiliki nyumba ya kifahari mkoani Mara, ambayo aliijenga alipokuwa RPC mkoani humo, huku nyumba nyingine ikiwa maeneo ya Capri-Point jirani na Ikulu ndogo mkoani Mwanza, inayoelezwa kuwa aliinunua baada ya Serikali kutangaza uuzaji wa nyumba zake kwa watumishi wake.

  Umiliki wa mali hizo umeibua maswali mengi, wengi wakitaka kujua iwapo zinalingana na kipato cha Kamanda Barlow, licha ya kuwa na cheo cha Kamanda wa Polisi wa mkoa.

  Jengo la ghorofa

  Moja ya mali za Kamanda huyo ambazo zimeanza kuwa gumzo mjini Mwanza ni jengo la ghorofa ambalo ujenzi wale ulikuwa ukiendelea katika kiwanja Namba 173 Block G, eneo la Nyakato Mahina kwa kibali Na. 6400 (Building Permit), kilichotolewa na ofisi ya Mhandisi Jiji la Mwanza kikiruhusu kujenga jengo la ghorofa tatu.

  Mhandisi wa Jiji

  Mhandisi wa Jiji la Mwanza, Boniface Nyambele alikiri Kamanda Barlow kuomba kibali cha kujenga jengo la ghorofa katika kiwanja hicho na kwamba, hata ujenzi wake walikuwa wakiufuatilia kwa karibu.

  "Kibali kilichotolewa hapa kilikuwa ni kwa ajili ya kujenga jengo la ghorofa tatu, alipoanza ujenzi alieleza kuwa anataka kujenga ghorofa tano, lakini baada ya kukagua jengo hili tulikuta foundation yake ikiwa na uwezo wa kuhimili ghorofa tatu tu, tulimzuia," alisema Nyambele.

  Hata hivyo, mmoja wa wasimamizi wa ujenzi wa jengo hilo, ambaye hakutaka kutajwa jina lake alisema kuwa marehemu Kamanda Barlow, aliwasisitiza kujenga ghorofa tano.

  Alisema kwamba kila mara kamanda huyo alikuwa akiwaeleza kuwa masuala ya vibali kutoka Jiji wanapaswa kumwachia yeye licha ya wakaguzi kumkatalia.

  "Baada ya kuwa tumejenga hapa ,mwezi mmoja kabla ya kufariki alituita na kumweleza fundi wetu mkuu kuwa alikuwa amebadili mawazo ya kujenga jengo la ghorofa tatu na kwamba, mpango wake sasa ulikuwa ni kuongeza ghorofa nyingine mbili juu," alisema mmoja wa wasimamizi wake wa ujenzi na kuongeza:

  "Alipoelezwa kama kisheria haikubaliki, alidai hayo hayamuhusu atasimamia yeye huko kwenye sheria."

  Mwandishi wa habari hizi alifika eneo linapojengwa ghorofa hilo na kushuhudia ubao unaoonyesha kuwa kibali cha ujenzi wa jengo hilo kimetolewa kwa Liberatus Barlow.

  Wizi ulikwamisha ujenzi

  Hata hivyo, majuma machache kabla ya kifo chake, eneo hilo la ujenzi kulitokea wizi wa nondo za ujenzi, ambapo baada ya tukio hilo mwangalizi wa jengo hilo na baadhi ya mafundi wake walikamatwa na kuwaweka mahabusu kwa siku nne katika Kituo cha Polisi Nyakato Mwatex huku ikielezwa kuwa kamanda huyo aliwatoa baada ya kukubaliana nao kumlipa nondo zilizopotea.

  "Siku ya wizi huo ujenzi ulisimama na tulikamatwa na kulazimishwa kulipa nondo 10 alizodai zimeibwa, lakini msimamizi wetu nakumbuka aliamua kulipa yeye badala yetu na kesi iliishi baada ya kuwekwa ndani siku nne. Alilipa nondo 60 badala ya 10 na huo ulikuwa mwisho wake wa kuendelea na kazi pamoja nasi, " alisema kijana huyo aliyewahi kufanya kazi ya kibarua katika jengo hilo.

  Umiliki wa magari na utata

  Mali nyingine zinazodaiwa kumilikiwa na Kamanda Barlow ni pamoja na magari, ambapo katika idadi ya magari hayo, gari moja aina ya Toyota Hilux ambalo ndilo alipata nalo ajali limeonekana kuwa na utata katika umiliki wake kutokana na namba hiyo ya usajili kubainika kuwa siyo yake kwa vile ilisajiliwa kwa gari aina ya Nisan Premier inayomilikiwa na wamiliki wawili.

  Ingawa umiliki wa magari mengine unadaiwa kusajiliwa kwa majina ya mfanyabiashara maarufu jijini Mwanza, lakini umiliki wa gari ambalo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Evarist Ndikilo, alipotangaza kifo cha kamanda huyo, alilitangaza pia kuwa ni mali ya marehemu, imebainika kuwa alilipata wiki moja kabla ya kifo chake.

  Katika uchunguzi wa Mwananchi Jumapili, imebainika kuwa hata bima ya gari hilo iliyoonyesha imekatwa kutoka Kampuni ya Bima ya Zanzibar, ilikuwa haitambuliki.

  Kamanda Barlow alilichukua gari hilo kwa mmoja wa wafanyabiashara jijini Mwanza, ambaye bado jeshi hilo la polisi linamsaka kutokana na utata wa umiliki wake, kuonyesha namba hiyo siyo halisi ya gari hilo.

  Meneja wa Kampuni ya Bima

  Meneja wa Tawi la Kampuni ya Bima Zanzibar Mkoa wa Mwanza, Suzan Masele alipotakiwa kutoa ufafanuzi wa suala hilo, alisema kuwa stika ya bima ya gari hilo alilokuwa nalo Kamanda Barlow, wamefuatilia kwenye mfumo wao wa malipo wakabaini kuwa haipo.

  "Tumeangalia katika system (mfumo) yetu hakuna bima ya malipo hayo, kwa hiyo ni feki," alisema.

  Aidha, utata wa umiliki wa gari hilo pamoja na bima yake ulithibitishwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Said Mwema, ambaye alisema jijini Mwanza kuwa jeshi lake lilikuwa likiendelea na uchunguzi wa umiliki wa gari hilo, pamoja na bima yake kujua ukweli na jinsi lilivyoingia mikononi kwa marehemu siku kadhaa kabla ya kifo chake.

  "Suala la gari alilokuwa akilitumia marehemu mpaka siku mauti yanamkuta, pamoja na bima yake, hatuwezi kulieleza hapa, kwa sasa bado tunachunguza," alisema IGP, alipoulizwa na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kumaliza kutoa taarifa za awali za uchunguzi wa kifo Kamanda Barlow.
   
 2. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #2
  Oct 28, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Hizi mali za mashaka ni ushahidi kuwa watendaji wetu wengi ni majambazi wasioweza kutoa maelezo ya jinsi walivyochuma. Barlow maisha yake, kifo chake hata kipato chake ni picha ya majambazi wanaoifanya Tanzania iwe omba omba. Bahati mbaya ni kwamba jinai hii inaanzia ikulu hadi kwa mfagiaji.

  Heri Mungu awapunguze wanangu wezi walionishinda ili wale wasafi hasa wakulima na wafanyakazi wa kipato cha chini wapunguziwe mzigo na madhara. Je hao nao wakipata nafasi watafanya nini? Zingatia sana hili Mtanzania. Vinginevyo unaweza kukuta unamchukia Barlow kumbe unajichukia mwenyewe.
   
 3. Ufunguo

  Ufunguo JF-Expert Member

  #3
  Oct 28, 2012
  Joined: Aug 18, 2012
  Messages: 219
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hapo ndo ujue kwamba hata viongozi wa nchi hawafuati sheria. Hawafai kabisa, hiyo ni ishara ya tu ya maovu mengi. Tuamke watanzania
   
 4. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #4
  Oct 28, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,572
  Likes Received: 82,066
  Trophy Points: 280
  Jeshi, polisi vyote vinanuka rushwa, dhuluma na ujambazi uliokithiri. Taasisi zetu zote zimeoza.
   
 5. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #5
  Oct 28, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,294
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Father of All

  Inauma sana nchi hii inajengwa na wenye moyo wengi sana na inabomolewa kwa nguvu zote na wenye meno wachache.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. N

  Ndjabu Da Dude JF-Expert Member

  #6
  Oct 28, 2012
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 3,650
  Likes Received: 408
  Trophy Points: 180
  No wonder few felt sorry about his sudden death. He reaped by the sword, and he died by it!

  He might have gotten that cake in his lifetime through coercion, corruption and most dubious means imaginable given his pitiful wages as civil servant. But thank God, he didn't get to live long enough to eat and savor that rotten cake.
   
 7. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #7
  Oct 28, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,294
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  TAKUKURU nao hawakosekani humo pia
   
 8. J

  JERUSALEMU JF-Expert Member

  #8
  Oct 28, 2012
  Joined: Sep 19, 2012
  Messages: 2,739
  Likes Received: 1,796
  Trophy Points: 280
  Nchi hii inatakiwa tufike mahali kila mtu mwenye mali achunguzwe na hasa wafanyakazi wa serikali. wengi ni wapokea rushwa na ndio maana nchi haiendi mbele.
   
 9. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #9
  Oct 28, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  yaani napata kizunguzungu na maluilui kuitafakari nchi yetu maana kila mtu kwenye sector yake anajimilikisha anavunja sheria n.k. Lakini hii nikutokana na kuwa na uongozi usio na uzalendo na wenye kujinufaisha kwa familia zao bila kuangalia wengine wanapata taabu zipi.
   
 10. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #10
  Oct 28, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,294
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Ipo haja ya sisi wananchi kufanya maamuzi magumu bila kuogopa. Enough is Enough, let's walk the talk now!
   
 11. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #11
  Oct 28, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Kinachouma zaidi ni kuona hawa majambazi wenye vyeo wanaheshimiwa huku nao wakijiona wajanja. Jamii isipoacha kuwaabudia tutaishia wote kuwa majambazi tunawanafiki wananchi kuwa tunawatumikia wakati tunawaibia.

  Ingawa wengi wananishangaa kwanini nafurahia vifo vya watu kama hawa, ukweli ni kwamba wakipungua angalau nasi tunapunguza mateso. Ni sawa na mtu nweye nyumba ilyojaa panya. Akifa panya unasherehekea maana yake ni kwamba nafaka zako zitapona angalau kwa kupungua huo mdomo mmoja.

  Na hii ndiyo maana alipokufa huyu mwanangu nilisema Rest In Hell wengi walinishangaa. Mie si mzazi wa kuendekeza njaa na kufumbia macho jinai.
   
 12. Ngongoseke

  Ngongoseke JF-Expert Member

  #12
  Oct 28, 2012
  Joined: Jan 1, 2012
  Messages: 3,212
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Sijui kwanini nilizaliwe kwenye nchi hii,full majambazi, wenye dhamani yakulinda mali zetu ndio wanaongoza kwa wizi sasa wengine sijui wafanye nini
   
 13. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #13
  Oct 28, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  Unachunguzaje hapo, magari yote hayapo kwa jina lake. Hadi kamanda wa polisi ana.bima fake. Hapachunguziki yaani, hapa tunahitaji overhaul ya system nzima. Huu ushemeji na ushkaji ni tatizo.
   
 14. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #14
  Oct 28, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,294
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  ndugu yangu tatizo hatuwezi kujichagulia sehemu ya kuzaliwa, naamini ingewezekana basi Tanzania ingebakiwa na mafisadi tu ili wajifisidi wenyewe kwa wenyewe
   
 15. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #15
  Oct 28, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,294
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Inakatisha tamaa sana. Kama mlinzi wa kwanza wa sheria na amani katika mkoa anakuwa ndie kinara mvunjaji sheria namba moja, who remains safe hapa??? Tukimbilie wapi???
   
 16. bullet

  bullet JF-Expert Member

  #16
  Oct 28, 2012
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 959
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  Nimegundua kwa nini wakuu wa police wa mikoa na hata wilaya wanapagawa wakisikia mikutano na kampeni za vyama vya upinzani(si mna kumbuka Arusha na Iringa na kwingineko?)

  Fikiria iundwe tume huru ya kutafiti utajiri wa makamanda hao wa mikoa na wilaya, mbona watu watazimia kwa mashikizo ya damu kwa matokeo ya tume hiyo(nasisitiza iwe huru si kama ile ya Nchimbi).
   
 17. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #17
  Oct 28, 2012
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 864
  Trophy Points: 280
  Mwacheni apumzike mbele ya haki ya kudumu. Hata kama hakutenda haki wakati wa uhai wake, huko aliko atakuwa anatendewa haki yake.
   
 18. J

  JERUSALEMU JF-Expert Member

  #18
  Oct 28, 2012
  Joined: Sep 19, 2012
  Messages: 2,739
  Likes Received: 1,796
  Trophy Points: 280
  KINACHO TAKIWA NI POLITICAL WILL. Tukiwa na dhamira ya kweli wachunguzi wa nje wanajiriwa kufanya kazi maalumu kwa kipindi maalumu. uchunguzi unatakiwa uanzie kwa POLISI. TRA na kila idara ya serikali kama watu ni wasafi.kuna baadhi ya idara watu wanadhani wapo pale kwaajili ya kutengeneza pesa tu.
   
 19. babukijana

  babukijana JF-Expert Member

  #19
  Oct 28, 2012
  Joined: Jul 21, 2009
  Messages: 4,811
  Likes Received: 1,146
  Trophy Points: 280
  huyu mtu alikua mlafi w kilakitu,wake za watu,mali,madaraka etc,yawezekana waliomuua pia aliwazulumu
   
 20. Victoire

  Victoire JF-Expert Member

  #20
  Oct 28, 2012
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 10,447
  Likes Received: 7,187
  Trophy Points: 280
  imekula kwake mali hazina majina yake,bora hata angekuwa anaandika ya watoto au mke wake,imekula kwake
   
Loading...