Utajiri wa Kamanda Barlow Unatisha! Soma hapa...

Utajiri wa Kamanda Barlow Unatisha! Soma hapa...

Father of All Achakusema na kuhukumu usichokifahamu. Tusubiri majibu ya uchunguzi. Je unafahamu gari alilokuwa anaendesha wakati umauti unamkuta halikuwa lake ila aliazimwa? Usipende kuropoka. Nafikiri wewe ndo unatakiwa u-Live and rest in hell after this world.
 
Bado naye yule mkur***nz mweny jina kama la Zuberi maana naye hapa mwanza tetesi tunazozipata zinatisha, tunasikia hadi kanyang'anya viwanja vya watu halafu wanajenga magorofa yao ziwani.

Mr.bweka siyo?
 
Utajiri wa Kamanda Barlow waanikwa

Frederick Katulanda, Mwanza

SIKU chache baada ya Jeshi la Polisi kutoa taarifa yake ya uchunguzi kuhusu kifo cha aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Liberatus Barlow, umeibuka utata wa mali alizokuwa akimiliki, huku akidaiwa kumiliki utajiri wa kutisha likiwamo jengo la ghorofa.

Habari za kiuchunguzi zilizopatikana zinaeleza kuwa mbali ya jengo hilo, Kamanda Barlow anadaiwa pia kumiliki magari zaidi ya saba yakiwamo malori mawili aina ya Fuso, malori mawili ya mchanga, gari dogo aina ya Toyota Cresta pamoja na Toyota Hilux Double Cabin.

Magari hayo yanadaiwa kuhifadhiwa eneo la Nyakato mjini Mwanza, yakisimamiwa na mfanyabiashara mmoja kwa niaba yake.

Mbali na magari hayo kamanda hyo anatajwa kumiliki nyumba ya kifahari mkoani Mara, ambayo aliijenga alipokuwa RPC mkoani humo, huku nyumba nyingine ikiwa maeneo ya Capri-Point jirani na Ikulu ndogo mkoani Mwanza, inayoelezwa kuwa aliinunua baada ya Serikali kutangaza uuzaji wa nyumba zake kwa watumishi wake.

Umiliki wa mali hizo umeibua maswali mengi, wengi wakitaka kujua iwapo zinalingana na kipato cha Kamanda Barlow, licha ya kuwa na cheo cha Kamanda wa Polisi wa mkoa.

Jengo la ghorofa

Moja ya mali za Kamanda huyo ambazo zimeanza kuwa gumzo mjini Mwanza ni jengo la ghorofa ambalo ujenzi wale ulikuwa ukiendelea katika kiwanja Namba 173 Block G, eneo la Nyakato Mahina kwa kibali Na. 6400 (Building Permit), kilichotolewa na ofisi ya Mhandisi Jiji la Mwanza kikiruhusu kujenga jengo la ghorofa tatu.

Mhandisi wa Jiji

Mhandisi wa Jiji la Mwanza, Boniface Nyambele alikiri Kamanda Barlow kuomba kibali cha kujenga jengo la ghorofa katika kiwanja hicho na kwamba, hata ujenzi wake walikuwa wakiufuatilia kwa karibu.

“Kibali kilichotolewa hapa kilikuwa ni kwa ajili ya kujenga jengo la ghorofa tatu, alipoanza ujenzi alieleza kuwa anataka kujenga ghorofa tano, lakini baada ya kukagua jengo hili tulikuta foundation yake ikiwa na uwezo wa kuhimili ghorofa tatu tu, tulimzuia,” alisema Nyambele.

Hata hivyo, mmoja wa wasimamizi wa ujenzi wa jengo hilo, ambaye hakutaka kutajwa jina lake alisema kuwa marehemu Kamanda Barlow, aliwasisitiza kujenga ghorofa tano.

Alisema kwamba kila mara kamanda huyo alikuwa akiwaeleza kuwa masuala ya vibali kutoka Jiji wanapaswa kumwachia yeye licha ya wakaguzi kumkatalia.

“Baada ya kuwa tumejenga hapa ,mwezi mmoja kabla ya kufariki alituita na kumweleza fundi wetu mkuu kuwa alikuwa amebadili mawazo ya kujenga jengo la ghorofa tatu na kwamba, mpango wake sasa ulikuwa ni kuongeza ghorofa nyingine mbili juu,” alisema mmoja wa wasimamizi wake wa ujenzi na kuongeza:

“Alipoelezwa kama kisheria haikubaliki, alidai hayo hayamuhusu atasimamia yeye huko kwenye sheria.”

Mwandishi wa habari hizi alifika eneo linapojengwa ghorofa hilo na kushuhudia ubao unaoonyesha kuwa kibali cha ujenzi wa jengo hilo kimetolewa kwa Liberatus Barlow.

Wizi ulikwamisha ujenzi

Hata hivyo, majuma machache kabla ya kifo chake, eneo hilo la ujenzi kulitokea wizi wa nondo za ujenzi, ambapo baada ya tukio hilo mwangalizi wa jengo hilo na baadhi ya mafundi wake walikamatwa na kuwaweka mahabusu kwa siku nne katika Kituo cha Polisi Nyakato Mwatex huku ikielezwa kuwa kamanda huyo aliwatoa baada ya kukubaliana nao kumlipa nondo zilizopotea.

“Siku ya wizi huo ujenzi ulisimama na tulikamatwa na kulazimishwa kulipa nondo 10 alizodai zimeibwa, lakini msimamizi wetu nakumbuka aliamua kulipa yeye badala yetu na kesi iliishi baada ya kuwekwa ndani siku nne. Alilipa nondo 60 badala ya 10 na huo ulikuwa mwisho wake wa kuendelea na kazi pamoja nasi, ” alisema kijana huyo aliyewahi kufanya kazi ya kibarua katika jengo hilo.

Umiliki wa magari na utata

Mali nyingine zinazodaiwa kumilikiwa na Kamanda Barlow ni pamoja na magari, ambapo katika idadi ya magari hayo, gari moja aina ya Toyota Hilux ambalo ndilo alipata nalo ajali limeonekana kuwa na utata katika umiliki wake kutokana na namba hiyo ya usajili kubainika kuwa siyo yake kwa vile ilisajiliwa kwa gari aina ya Nisan Premier inayomilikiwa na wamiliki wawili.

Ingawa umiliki wa magari mengine unadaiwa kusajiliwa kwa majina ya mfanyabiashara maarufu jijini Mwanza, lakini umiliki wa gari ambalo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Evarist Ndikilo, alipotangaza kifo cha kamanda huyo, alilitangaza pia kuwa ni mali ya marehemu, imebainika kuwa alilipata wiki moja kabla ya kifo chake.

Katika uchunguzi wa Mwananchi Jumapili, imebainika kuwa hata bima ya gari hilo iliyoonyesha imekatwa kutoka Kampuni ya Bima ya Zanzibar, ilikuwa haitambuliki.

Kamanda Barlow alilichukua gari hilo kwa mmoja wa wafanyabiashara jijini Mwanza, ambaye bado jeshi hilo la polisi linamsaka kutokana na utata wa umiliki wake, kuonyesha namba hiyo siyo halisi ya gari hilo.

Meneja wa Kampuni ya Bima

Meneja wa Tawi la Kampuni ya Bima Zanzibar Mkoa wa Mwanza, Suzan Masele alipotakiwa kutoa ufafanuzi wa suala hilo, alisema kuwa stika ya bima ya gari hilo alilokuwa nalo Kamanda Barlow, wamefuatilia kwenye mfumo wao wa malipo wakabaini kuwa haipo.

"Tumeangalia katika system (mfumo) yetu hakuna bima ya malipo hayo, kwa hiyo ni feki," alisema.

Aidha, utata wa umiliki wa gari hilo pamoja na bima yake ulithibitishwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Said Mwema, ambaye alisema jijini Mwanza kuwa jeshi lake lilikuwa likiendelea na uchunguzi wa umiliki wa gari hilo, pamoja na bima yake kujua ukweli na jinsi lilivyoingia mikononi kwa marehemu siku kadhaa kabla ya kifo chake.

“Suala la gari alilokuwa akilitumia marehemu mpaka siku mauti yanamkuta, pamoja na bima yake, hatuwezi kulieleza hapa, kwa sasa bado tunachunguza,” alisema IGP, alipoulizwa na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kumaliza kutoa taarifa za awali za uchunguzi wa kifo Kamanda Barlow.

Kumbe kazi ya U - RPC inalipa! Kama ndivyo ni heri Ma - RPC wote wachunguzwe!

Tuongelee makosa yake, mimi binafsi sijaona utajiri unaotisha. Thamani ya magari hayo yote haifiki hata VX moja. Enyi watanzania, mbona tunataka kuishi ki-masikini hivi? Mtanzania wa kawaida kupitia mikopo magari sasa sio issue, itakuwaje kwa kamanda wa polisi? Mbona familia kibao hivi sasa hususani wakazi wa Dar es Salaam, zinamiliki magari si chini ya matatu. Baba, Mama, na moja la biashara?

Sijaona utajiri hapo, ni jinsi tu ya kujikwamua kimaisha. Nampongeza kwa hilo, maisha ya polisi ni magumu.

MPANGO A....Binafsi naungana na wewe , kimsingi hata mimi sioni utajiri wowote hapa hata kidogo, hizo ni mali za kawaida sana kwa mtu ambaye amewahi kuitumikia serikali kama yeye....hapa issue ni makosa yake tu...ni kwa jinsi gani alipata hizo mali zenye utata, bima feki etc....hapo ndio palipo na issue.
Ukiiangalia sana hii issue ya utata wa magari na baadhi ya vitu nyake, kuna connection(Ring/Syndicate) ya wizi wa magari, rushwa na ubabambikiaji wa kesi hewa etc. Sasa usalama wetu kama raia umekabidhiwa kwa mny'ang'anyi, wezi, majambazi na wahuni ambao huyu ni mmoja wao.
 
Ni jambo la kawaida katika nchi hii , mmesahau hata chenge alipogonga wale wadada wawili wa bajaji, gari yake ilikutwa haina bima wala motor vehicle licence kwa miaka 3 japo kuwa ni mwanasheria na AG mstaafu.
 
Hizi mali za mashaka ni ushahidi kuwa watendaji wetu wengi ni majambazi wasioweza kutoa maelezo ya jinsi walivyochuma. Barlow maisha yake, kifo chake hata kipato chake ni picha ya majambazi wanaoifanya Tanzania iwe omba omba. Bahati mbaya ni kwamba jinai hii inaanzia ikulu hadi kwa mfagiaji.

Heri Mungu awapunguze wanangu wezi walionishinda ili wale wasafi hasa wakulima na wafanyakazi wa kipato cha chini wapunguziwe mzigo na madhara. Je hao nao wakipata nafasi watafanya nini? Zingatia sana hili Mtanzania. Vinginevyo unaweza kukuta unamchukia Barlow kumbe unajichukia mwenyewe.

Hapo kwenye RED nasema.... Eeeemen!!!

Mimi nimekuwa nikijitahidi sana kuomba misiba ya watu wa aina hii ili angalau mambo yaanze upya badala ya kurithiwa kama uongozi wa chama tawala
 
MPANGO A....Binafsi naungana na wewe , kimsingi hata mimi sioni utajiri wowote hapa hata kidogo, hizo ni mali za kawaida sana kwa mtu ambaye amewahi kuitumikia serikali kama yeye....hapa issue ni makosa yake tu...ni kwa jinsi gani alipata hizo mali zenye utata, bima feki etc....hapo ndio palipo na issue.
Ukiiangalia sana hii issue ya utata wa magari na baadhi ya vitu nyake, kuna connection(Ring/Syndicate) ya wizi wa magari, rushwa na ubabambikiaji wa kesi hewa etc. Sasa usalama wetu kama raia umekabidhiwa kwa mny'ang'anyi, wezi, majambazi na wahuni ambao huyu ni mmoja wao.
Utajili huo unawea usiwe wa kutisha sana lakini una maana kubwa sana. Kwamba ktk utumishi wake wa polisi kwa elimu yake na muda ambao amekuwa hapo kwenye u-RPC hangeweza kuwa na mali ya aina hiyo kihalali! Hata siku moja!

Kinachojitokeza hapo ni kwamba hawa siyo walinzi wa Raia na mali zao bali sasa hivi wanalinda usalama wa wezi na majambazi. Wanapewa mgao wa majambazi, makosa ya barabarani, nk.

Utata wa mali hizo ndo huo unaojitokeza hata ktk umiliki wa hilo gari pamoja na bima. Alijua kwa cheo chake hakuna wa kumuuliza upuuzi anaoufanya. Siyo barabarani tu, hadi huko kwenye ujenzi anakoomba jengo lipelekwe hadi gorofa 45 badala ya 3.

Lazima tuulize utajili wake huu ni wa nani au umetoka wapi. Ni wale wale akina Tibaigana na mahoteli ya Mukuranga. Ni wale wale akina Zombe na uuwaji wao. Ni wale wale akina Kova na migorofa wanayoinua na ni wale wale akina Lowasa na estates zao.

Kwa ujumla ni nchi ya kizembe. Ni banana republic. Ni nchi tusiyokuwa na usalama wowote.
 
MchunguZI
Upo sahihi kabisa, lakini mkuu mwisho wa siku ipo siku nayo si ndefu sana.....ni jana tumeshuhudia Berluscon amepewa hukumu yake, je kuna atakae simama? itafika tu tu hata iweje na hawa wote njia yao itakuwa moja....that is what i still believe, hata kama si sasa lakini muda utasema wenyewe.
Dhuluma, wizi, ufisadi na kila aina ya ulafi umepitiliza kwa hawa washenzi wakubwa...tunajua kuna mnyororo mrefu sana sana. Kifupi nchi hii inahitaji mzalendo mmoja tu kuweza kuleta mabadiriko la lazima atoke nje ya system...na ili awe nje ya system means lazima yafanyike mapinduzi either ya kijeshi au ya kidemokrasia (ambayo yatachukua muda)....lakini all in all kuna njia tu...believe me or not.
 
Vita dhidi ya ujambazi ni ngumu sana kwa nchi kama Tanzania kwa sababu asilimia 98 ya waliopewa dhamana ya kupambana nayo ni majambazi. Polisi wa ngazi za juu na chini wote ni majambazi. Si rahisi sana kuimaliza hiyo vita.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
na huyo ni mmoja tuuu sasa makamanda wakuu wa mikoa yote ya tanzania tukianza kuwachunguza mmoja mmoja tunaweza tusiamini tutakayoyasikia
 
Mwanangu Revolutionalist tuko wengi tunaoomba mabaya yawapate wabaya wetu ingawa wengi wanaona aibu au kuhisi woga kusema hivyo. Mimi siku zote naomba hilo dege la rais lidunguke tena akiwamo na mkewe na watu wake ili nasi tupumue. Kwangu kifo cha mwanangu Barlow ambaye aliasi maagizo yangu na kuwa fisadi ilikuwa sherehe na ushindi mkubwa dhidi ya ufisadi.Sasa angalia wasivyo na maana wanaanza kufichuana hata jamaa hajaoza. Laana hiyo.
 
Napata machungu ujambazi unatokea mahali askari wanakuja baada ya saa moja je askari wetu ni wasafi kiasi hicho?
 
Jeshi, polisi vyote vinanuka rushwa, dhuluma na ujambazi uliokithiri. Taasisi zetu zote zimeoza.

Si ndo maana haya majambazi yalimpora Dr Slaa ushindi wake halali 2010?!!
Wanajua kabisa kuwa kile chuma kikiingia pale Magogoni hakuna gozi gozi!
 
Mbona kuna viongozi wengi sana wako madarakani matajiri sana? Marehemu Barlow alikuwa mmoja wa maskini kwa viwango vyao. Mnakumbuka ya yule SIMBO aliyestaafu JWTZ juzi kati? Habari ndio hiyo.
 
Mbona kuna viongozi wengi sana wako madarakani matajiri sana? Marehemu Barlow alikuwa mmoja wa maskini kwa viwango vyao. Mnakumbuka ya yule SIMBO aliyestaafu JWTZ juzi kati? Habari ndio hiyo.
.....Kumbe wengi wanaishi "kimjinimjini" kama Ridhiwani. tukirudisha nchi mikononi mwa wananchi itabidi akina Ridhiwani watuoneshe na sisi hao wajomba wanaowaweka mjinimjini ili sote tuishi kimjinimjini.
 
Hizi mali za mashaka ni ushahidi kuwa watendaji wetu wengi ni majambazi wasioweza kutoa maelezo ya jinsi walivyochuma. Barlow maisha yake, kifo chake hata kipato chake ni picha ya majambazi wanaoifanya Tanzania iwe omba omba. Bahati mbaya ni kwamba jinai hii inaanzia ikulu hadi kwa mfagiaji.

Heri Mungu awapunguze wanangu wezi walionishinda ili wale wasafi hasa wakulima na wafanyakazi wa kipato cha chini wapunguziwe mzigo na madhara. Je hao nao wakipata nafasi watafanya nini? Zingatia sana hili Mtanzania. Vinginevyo unaweza kukuta unamchukia Barlow kumbe unajichukia mwenyewe.

Tishio la kuisha kwa tembo linasababishwa na wakubwa kwenye vituo vya hifadhi hali kadhalika katika maeneo mengine wanakula kulingana na urefu wa kamba.Tufanye maamuzi 2015,kwa kubadilisha mfumo huenda inaweza kuwa hatua nzuri katika kuliokoa taifa letu.
 
Back
Top Bottom