Utajiri wa gesi umepotelea wapi?

sir longo GAS YA MSIMBATI NI YA MUDA MREFU? UTAJIRI AMBAO ULIZUNGUMZWA NI WA GAS YA MSIMBATI NA NDIYO ULILETA VURUGU KULE MTWARA NA NDIYO UNAOZUNGUMZWA NA MLETA THREAD, NAHS WEWE NDYO HUFATILII MAMBO.
 
Umaekula like yangu mkuu, bila kujali ukweli wa takwimu ulizonazo,umeandika kiadilifu bila ushabiki wala povu..
 
Hahaha yani wewe hukuona swali kwenye kichwa cha habari yake au umeamua tu kutoliona ili umshutumu?! Yeye nimeona ameuliza swali tena liko bolded.
 
Serikali laghai huwa hazina mipango madhubuti inayoeleweka zaidi ya blah blah zenye kulaghai wananchi wake kwenye majukwaa ya kisiasa
Word. Wamakonde walimwagiwa sana maji ya kuwasha na kupigwa mabomu na risasi, kisa wasizuie uwekezaji wa wazungu. Leo kimyaaaaa. Na mgao wa umeme uko pale pale, ilhali tuliambiwa gesi ikiingia nchini basi mgao wa umeme ungekua historia.
 
Hilo nalo lilipita kama la Dr. shika
 
Extraction ya hiyo gas si mchezo. Inataka technolojia ya kueleweka
 
gesi ya msimbati ni ya kitambo, lkn manufaa ya kuisafirisha kwa bomba had dar, yameanza kuonekana, kwa sasa asilimia kubwa ya umeme ktk grid ya taifa ni wa maji na gas. tumeshaanza kuachana na umeme wa mafuta(iptl...) ambao ni ghali zaidi. ila gas iligunduliwa miaka ya 2005 ambayo iliyo nyingi ipo onshore. mikakati ya kuichimba na kujenga NLG plant inaendelea. maendeleo ni process ndugu zangu.
 
Halafu unakuta spika huyo huyo naye anaunda tume kuchunguza madini ya almasi mwadui,nchi hii haiishi maigizo.
 
Ndio uelewe kwa nini tunaitwa Wadanganyika.
 
Lakini si nyie ndio mlikuja kwa mbwembwe zote sasa povu la nini unatoa?
 
Mkuu hao wapinzani wataongelea wapi wakati mikutano ya siasa imepigwa ban?
Serikali ya viwanda ndo yunakomaa nayo. Acheni siasa ati..

Kuna nafasi kwenye huu uchaguzi, pia kwenye vipindi mbalimbali vya TV nk.Na huku kwenye mitandao ya kijamii ndio unajimwaga upendavyo. Najua sio rahisi lakini inawezekana.
 
Achana na mambo ya ajabu ajabu ya uchumi wa gesi...kwa sasa tuko kwenye uchumi wa viwanda...mambo ya gesi yashakuwa zilipendwa.
Umenichekesha sana. Kwa kweli watu wanajua kucheza na vichwa vya Watanzania.
 
gas haijaanza kuchimbwa iko kwenye mchakato! majibu ya wanasiasa
 
sir longo GAS YA MSIMBATI NI YA MUDA MREFU? UTAJIRI AMBAO ULIZUNGUMZWA NI WA GAS YA MSIMBATI NA NDIYO ULILETA VURUGU KULE MTWARA NA NDIYO UNAOZUNGUMZWA NA MLETA THREAD, NAHS WEWE NDYO HUFATILII MAMBO.
NI kweli, gas ambayo ilileta vurugu kule Mtwara ni gas ya Msimbati. HATA HIVYO, utajiri wa gas inayozungumzwa sio gas ya Msimbati! Gas ya Msimbati ni ya kawaida sana.

Gas ambayo Muhongo alikuwa anataka kutoana macho na akina Mengi ipo deep sea na kiasi kikubwa kimegundulika mkoani Lindi.
 
Hilo nalo lilipita kama la Dr. shika
Extraction sio tatizo kwa sababu makampuni yenye uzoefu na hizo shughuli ndiyo yalikuwa yanafana na imeshafanyika kwa kiasi kikubwa.

Issue ni kwamba, inaonekana gas sio kipaumbele cha JPM kama ilivyokuwa kwa JK.
 
Nakumbuka tuliambiwa uneme kukatika itakua mwiko! Dah ni bora kufikiri kwa nn kwa namna yoyote ukimrusha juu paka mkubwa lazima atatua chini kwa miguu kuliko kukumbuka ahadi kama hzo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…