Utajiri wa Dr. Dau unashtua

Utajiri wa Dr. Dau unashtua

Nimekuwa nafuatilia Suala la DR Dau na NSSF nimeshindwa kuelewa kwanini amekuwa na watetezi wengi kiasi hiki hapa jamvini! Je ni kweli dr wetu hana makando kando ya UFISADI kiasi watu wengi hivyo kumtetea? Je ikaja gundulika ana makando kando hawa watetezi wake wateweza kuaminika tena hapa jamvini? Hii vita mara ionekane kama ni uislam vs ukristo mara ihamishwe ionekane ni chuki!? La hapa kuna jambo sijapata ona mtu mwenye watetezi wengi hivi!

Sisikii kama Kabwe anapigwa vita kwa sababu ya dini yake. Wala sijasikia Kitilya, prof. Mahalu, William Mhando, Mramba au Yona walipelekwa mahakamani kwa sababu ya dini zao. Ila Dau tu ndiyo anaandamwa kwa dini yake.

Kweli pesa ina uwezo mkubwa, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kununua utu, mioyo hata akili za watu!
 
Nitashukuru sana kwa wenye kufahamu kutufahamisha "credibility" ya gazeti hili, wamiliki na wahariri wake ni ya kiwango kipi.

Kwa mtazamo wa haraka haraka, habari imekaa kipropaganda zaidi kama sehemu ya mikakati ya mashambulizi baina ya pande zinazohasimiana serikalini.
 
Mkuu,
Newcastle football club haina shareholders kwasababu inamilikiwa asilimia 100 na Ashley.

UK kuna sharia, ukifanikiwa kununua asilimia 77 ya shares, unaruhusiwa kuiondoa kampuni kwenye stock exchange.

Ukifanikiwa kununua shares asilimia 90 una uwezo wa kuwalazimisha asilimia 10 iliyobaki kuuza shares zao.

Tarehe 17 July 2007 ndio siku Mike Ashley alifanikiwa kufikisha asilimia tisini ya shares na wengine waliobaki wakalazimika kuziuza za kwao.

Hiyo club iliondolewa kwenye stock exchange tarehe 18 July 2007. Unless mnaongelea kwamba Dau alikuwa na shares kabla ya muda sawa ila kwasasa mnamwonea tu.

Mwenye umiliki wa Newcastle club kwa asilimia 100 ni Ashley na wala sasa huwezi kununua share ya Newcastle.

Kwa UK kuwa shareholder sio siri, Ukitaka kujua shareholders wote wa kampuni utawajua. Kama sio kwa majina yao basi utajizua kampuni ambazo zinawawakilisha.

Simfahamu Dau, wala sijui ni fisadi au sio fisadi. Ila hii issue ya Newcastle sio ya kweli.
Mkuu,
Kuna habari nyingi zinaletwa hapa ilikuwaondoa Watanzania kwenye habari za kweli. Ukizisoma hata nusu tu utajua zimejaa uongo wa wazi wazi lakini utashangaa wengi wanashikia bango kama niza kweli.

Gazeti la Dira linaandika habari za uongo lakini cha kushangaza aliyeandikwa wala alipeleki gazeti mahakamani!!

Kwa mtazamo wangu, hizi habari zinaanzishwa na hao wenye kashfa ilikuwaondoa Watanzania kwenye kashfa za kweli na kuonyesha kwamba wanaonewa.
 
Siyo mimi niliyeeleza kuwa Dau ana hisa Newcastle. Gazeti la Dira ndiyo limeandika. Nina imani watakuwa na vielelezo ambavyo wewe na mimi, wote hatuna. Siamini gazeti linalohaririwa na mtu mwenye kiwango kizuri cha uelewa kama gazeti la Dira linaweza kuzua jambo bila ya kuwa na vielelezo vyovyote maana hatari ya kufanya hivyo wanaijua.

Jambo la kushangaza ni watu wengine kueleza kuwa haiwezekani Dau akawa ana hisa bila vielelezo vyovyote vya kuonesha kuwa kwa nini hawezi kuwa mmiliki wakati Newcastle ilikuwa public company mpaka 2007. Gazeti la Dira halijaeleza Dau alikuwa mwanahisa wa Newcastle kipindi gani maana kampuni ilikuwa public kwa miaka 10. Na hilo nunyi watetezi wa Dau hamlisema, mkifanya hivyo makusudi, mkitaka kupotosha kama vile Ashley aliimiliki kampuni hiyo tangu kuanzishwa kwake.

Hilo la Dau kuwa mmiliki wa Newcastle nadhani aliyeleta habari JF ameandika katika lugha rahisi ile ya kuwa kila mwanahisa ni mmiliki lakini gazeti la Dira halijaandika kuwa Dau ni mmiliki badala yake limeandika kuwa ana hisa nyingi.
Ownership structure ya Newcastle ipo wazi lakini unashindwa kuangalia na baadalak yake wanangalia gazeti la Dira kama reference daah! Nimecheka sana.
 
Kwani Uongo?
Jiulize kwa nini somo la dini kwa shule za kikristo zilikuwa zinakubalika kama somo halali na NECTA wakati huo huo somo la dini kwa shule za kiislamu lilikuwa halitambuliki na NECTA kama somo halali? . Mnataka mpaka wabunge wapige kelele ndio mnafanya mapitio na kulikubali?
Kwa nini mtindo wa kutumia Examination Number ulikuja kutoa vijana wengi wa kiislamu kwenda secondary kuliko mtindo wa kutumia majina?. Milkuwa mnasubiri mpaka Marehemu Ali Kigoma Malima ndio aje awasaidie akili ya kutenda haki?
Kwa nini huwa kwenye uongozi wa nafasi zote zikiwemo za kisiasa mnajiona ninyi(wakristo) ni viongozi bora kuliko Viongozi walio waislamu? wakati huo huo huwa mnaongozi kuboronga sana katika nafasi hizo. Chunguza kwenye vipindi vyote vitano ni viongozi gani uongoza kuachia fedha mtaani?
Kwa nini kwenye shule za secondary za Govt na Private mnaruhusu watoto kufundishwa masomo ya Dini za kikriso na kukataza masomo ya dini za kiislamu?
Kwa nini wadada na watoto wanaovaa hijab hutakiwa ama kuvua au kuvumilia kunyanyaswa wakti wakiwa wmevaa vazi hilo huku mnawaacha Masiste wavae kama hivyo pasipo kunyanyaswa na kudharauliwa?.
Unataka zaidi?
SOMA kitabu chenye kichwa cha habari UHUSIANO KATI YA KANISA NA SERIKALI YA TANZANIA BARA KATI YA MWAKA 1958 MPAKA MWAKA 1985 Kilichotungwa na Padri wenu(Padri John Sivalon).

Mwishowe kabisa fuata link hii>>>>>

Nyerere,kanisa katoliki na muendelezo wa mfumo kristo dhidi ya Uislam Tanzania
Ujuha huo wakati gani somo la uislam lilikataliwa? Prove

Nipe ushahidi wa kuwa baada ya kuanza kutumia namba ufaulu wa waislam umepanda kuitumia hata takwimu za miaka mitano iliyopita.

Wapi imesemwa kuwa wakristo wanajiona ni viongozi bora zaidi ya waislam? Hizo ndiyo inferiority complex niliokuambia, Kuna viongozi waislam wazuri tena waliofanya kazi za kutukuka na wenye akili wanawatambua kama watanzania si waislam. Ila mwizi au fisadi hana dini mind you.

Shule ipi ya government inayokataza kufundishwa dini ya uislam? Unaota?

Mwisho don't drag me into foolish argument, I am sure you will beat me with your experience.
 
Sisikii kama Kabwe anapigwa vita kwa sababu ya dini yake. Wala sijasikia Kitilya, prof. Mahalu, William Mhando, Mramba au Yona walipelekwa mahakamani kwa sababu ya dini zao. Ila Dau tu ndiyo anaandamwa kwa dini yake.

Kweli pesa ina uwezo mkubwa, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kununua utu, mioyo hata akili za watu!
Chief Msambichaka umeongea vyema sana. Lakini si fedha tu inayoweza kununua akili za watu, hata hizi imani za kidini zimewafanya baadhi ya watu wamekuwa mazwazwa na kutetea uzuzu uzuzu tu.
 
Tttt
Mbona unapanic? Usichoelewa ni nini? Kiingereza hujui, unasingizia lugha ya kigeni kumbe na kiswahili hujui? BAsi ngoja nikuandikie kimatumbi maana halisi ya unachohoji:-

Sosipae kupepa, abamchwewa simmatini kumbaliwane, isikisi 100%? Tobeanti sikiati 80%? 60%? 40%? nadi 20%? Billioni 100 sangasawela palimbwe?

Najua sasa umeelewa!.teh teh teh
 
Utajiri wa aliyekuwa Mkurugenzi wa NSSF, Dr. Ramadhani Dau unafika zaidi ya Tsh 100 Bilioni.

- Ni mmoja wa wamiliki wa timu ya Newcastle ya Uingereza.

- Kampuni zake pekee ndizo zinazopewa tenda ya kufanya kazi NSSF.

Chanzo: Dira ya Mtanzania - 18 Aprili 2016
Jamani hizo ni tuhuma tu hebu thibisha umiliki wake wa new castle [maana hata kama una share 2 unakuwa mmiliki]
hizo kampuni zake zitajwe basi maana humu ndani mbona wanatajwa watu wa aina hiyo na mali zao zikitajwa?
 
Nimekuwa nafuatilia Suala la DR Dau na NSSF nimeshindwa kuelewa kwanini amekuwa na watetezi wengi kiasi hiki hapa jamvini! Je ni kweli dr wetu hana makando kando ya UFISADI kiasi watu wengi hivyo kumtetea? Je ikaja gundulika ana makando kando hawa watetezi wake wateweza kuaminika tena hapa jamvini? Hii vita mara ionekane kama ni uislam vs ukristo mara ihamishwe ionekane ni chuki!? La hapa kuna jambo sijapata ona mtu mwenye watetezi wengi hivi!
Vuta subira tu ni swala la wakati, bahati mzuri CAG Assad ni mwislamu na ndiye aliyendaa repoti ya huyu Dr Dau na NSSF yake, ile repoti itakapokuwa wazi utasikia Assad wanamwita Murtad au kafir au kibaraka wa mfumo kristo.

Wao kiongozi mzuri kwao ni kama Marehemu Profesa Kighoma Malima, yani ukijamba udini, ukilala udini na ukiamka udini. Profesa Malima ndio muasisi wa chama cha NRA akampachika kibaraka wake pale Aboubakar Ulotu huku yeye akiwa waziri wa serikali ya Ccm, baada ya kifo chake hawa mujahidina wote ndio wakakimbilia CUF na kuhakikisha wanamn'goa kafiir James Mapalala na kumpa Uenyekiti ndugu yao katika imani Profesa Lipumba, kama huijui historia hii huwezi kuijuwa ajenda ya watu hawa.

Ukiona mujahidina wanamuita mtu mcha Mungu tilia shaka sana mienendo ya huyo mchamungu wao, ndio maana wasomi wa kiislamu wasiojifungamanisha na mujahidina usikii wakipigiwa upatu na utetezi huu.

Kijana mdogo kabisa wa kiislamu Risheed Bade ameondolewa ukamishna mkuu wa TRA ndio roho ya Taifa lakini hawa wavaa kandambili wala huwasikii wakimtetea na wala hawana mpango naye kwa sababu ni mwislamu moderate na bia anakunywa. Hii ndio siri wengi msiyoijuwa iliyojificha juu ya wapiga debe wa Dr Dau.

Ukitaka kuujuwa unafki wa waislamu angalia nchi kama Zanzibar 99% wapo wao peke yao je wanatendeana vile uislamu wao unavyotaka? Wanafki wakubwa hawa.
 
Nimekuwa nafuatilia Suala la DR Dau na NSSF nimeshindwa kuelewa kwanini amekuwa na watetezi wengi kiasi hiki hapa jamvini! Je ni kweli dr wetu hana makando kando ya UFISADI kiasi watu wengi hivyo kumtetea? Je ikaja gundulika ana makando kando hawa watetezi wake wateweza kuaminika tena hapa jamvini? Hii vita mara ionekane kama ni uislam vs ukristo mara ihamishwe ionekane ni chuki!? La hapa kuna jambo sijapata ona mtu mwenye watetezi wengi hivi!
wala usihangaike hayo ni Ma zombie yameajiriwa kwa kazi hiyo,
 
Utajiri wa aliyekuwa Mkurugenzi wa NSSF, Dr. Ramadhani Dau unafika zaidi ya Tsh 100 Bilioni.

- Ni mmoja wa wamiliki wa timu ya Newcastle ya Uingereza.

- Kampuni zake pekee ndizo zinazopewa tenda ya kufanya kazi NSSF.

Chanzo: Dira ya Mtanzania - 18 Aprili 2016
Huyo ni balozi wa Tanzania .
 
Mbona unapanic? Usichoelewa ni nini? Kiingereza hujui, unasingizia lugha ya kigeni kumbe na kiswahili hujui? BAsi ngoja nikuandikie kimatumbi maana halisi ya unachohoji:-

Sosipae kupepa, abamchwewa simmatini kumbaliwane, isikisi 100%? Tobeanti sikiati 80%? 60%? 40%? nadi 20%? Billioni 100 sangasawela palimbwe?

Najua sasa umeelewa!.
nimecheka sana .
 
Ujuha huo wakati gani somo la uislam lilikataliwa? Prove

Nipe ushahidi wa kuwa baada ya kuanza kutumia namba ufaulu wa waislam umepanda kuitumia hata takwimu za miaka mitano iliyopita.

Wapi imesemwa kuwa wakristo wanajiona ni viongozi bora zaidi ya waislam? Hizo ndiyo inferiority complex niliokuambia, Kuna viongozi waislam wazuri tena waliofanya kazi za kutukuka na wenye akili wanawatambua kama watanzania si waislam. Ila mwizi au fisadi hana dini mind you.

Shule ipi ya government inayokataza kufundishwa dini ya uislam? Unaota?

Mwisho don't drag me into foolish argument, I am sure you will beat me with your experience.


Fuata Link hii uone hali ilivyo, Tatizo lipo:-

Mohamed Said: WAISLAM WA TANZANIA NA TATIZO LA UDINI KATIKA WIZARA YA ELIMU

WAISLAM WA TANZANIA NA TATIZO LA UDINI KATIKA WIZARA YA ELIMU
UM5d4OfKGZAOGzoyOL2k5ofU7gKUq8up-rSPW94rWq1CU0oly4DuZx0nhqPDBRsHV1Y1-QwcV7s6cEfgbDES2YV1DERqomujIb8mhJE0ThZ38ztuIb7yN3F-JAIBLHNYQ-ZS95Gsgnt3ftui-8GfkgJ1U7JyLXPmpYiUd0m7o1FtBE_QkdyKIHzyiqHeZKffKBAnnGXheHLdhvU0FaGpK9clckpP1nq9L1Q95c_d_t0X_Usrdu0FFRv3dAES0GmlBUD_sRVoUBfiJrkIzDJ1RSLnYHhm6ZJlotJWcHhOesANLUPU3pErqJRACQkqIjrU1ZeUosCWXHzwxciZB2kqvbxbC2dXxeWquDhnvP7F1hgeGqld21AEp4bFHUu-DiZeMNpIwWkW9IVkWSqXTQTW1ToO1PqqSozdgk2BBWPBZILvEmedz2-3Qi9R3Andwtl-xxxU2e9Jp4PbiVvlgJhkzzr2PH-hRg4gxEe64ogHNac_vJZbOj98n_dKdKuQVZKOsSovFVnXp18c5bGYKCwq--ISKgPCAbeQAZPbbXpGSQ4tpWL91wZOniRFzxcedUjRd6Bx=w480-h320-no

Maandamano ya Waislam Dhidi ya NECTA Chini ya Dr. Joyce Ndalichako
Ndugu Waziri,
Kwa muda mrefu sasa, kumekuwa na maswali mengi wakijiuliza Waislamu, moja likiwa inakuwaje katika maeneo yenye Waislamu wengi ambapo idadi ya wanafunzi Waislamu inakuwa zaidi ya asilimia 70, lakini wanapochaguliwa kwenda sekondari, idadi ya watoto wa Kiislamu huporomoka na kuwa chini ya asilimia 20.

Swali na kitendawili hiki kimekuwepo kwa muda mrefu bila kupatiwa majibu. Hata lilipofikishwa Bungeni mwaka 1999 na aliyekuwa Mbunge wa Kigamboni, Mzee Kitwana Selemani Kondo, bado halikupatiwa jibu.
ar6kGfiPOg9afYE4gRWDHVHw5QlMyS5lAevP3Tkmi7yCy-T29eF24_IoxP0Vj-ydMrS2Vrlq5k_Wyc7NRkHQudZj1UesOxPrLJByxcSrdX9ES1QmAGeO54UhfCMHNH6DmYP4b5Dcfn6dgVf3LWDsVqnkEOh6kBcGo3QBm83kqvlCisa5-S8_GmCLVSYHAPrzERHoxycfe_DDkoPkmt60qF2eBLO3bu0619cOhBKHkbuwq8FQPWiDU47Ry_hUqvz6quhI0zjKM4msLGRYjVWoLcGmazH0pDfhc_j1VncF6es34y2A3lOQgfugBZzp3ZsAzqgQ-iqG-zyfdNg8bM-htQy2AVhy2i09Dcg0dPV39ZA3ff_W9Nc4anEkRh9jn-GyEW_WgNqlW3Ryc6QJoO93sIIoqw4Ue7EGy5rjK3HwK2_LqbEb0htqFT3UgJ-8HhyTVmLPJQTVd4tKVTrxDfD918g5mSkpfSS8E_tdZdvLrbyJlJBtkkNhkNeQ_pOAZ1VsH8xmiq7ZKVM0WPZmMhLdajan7JPvSuj4FVA2HfouFqttQTT5CFSUyI40Ngir413nNA2Oxw=w280-h320-no

Kitwana Selemani Kondo
Akihoji juu hali hiyo, Mzee Kitwana Kondo alitoa mfano jinsi hali ilivyokuwa katika shule ya Pembamnazi iliyokuwa na Waislamu watupu na kwa miaka mingi mfululizo kulikuwa hakuna hata mtoto mmoja aliyekuwa akichaguliwa kwenda sekondari kutoka katika shule hiyo. Aidha alisema kuwa, katika mkoa wa Dar es Salaam na Pwani, takwimu zinaonyesha kuwa idadi ya watoto wa Kiislamu katika shule za msingi ilikuwa zaidi ya asilimia 70 lakini inapokuja kuchaguliwa kwenda sekondari, idadi ya Waislamu iliporomoka na kuwa chini ya asilimia 20.

Akizungumza Bungeni tarehe 2 Februari, 1999 alisema kuwa katika watoto waliofanya mtihani wa darasa la saba mwaka 1998, idadi ya Waislamu ilikuwa asilimia 71 na Wakristo 29%. Hata hivyo akasema, ilipotoka orodha ya waliochaguliwa kwenda sekondari, idadi ya Wakristo ikawa asilimia 79 (79%) na Waislamu 21%.

Je, hiyo ilikuwa na maana kuwa watoto wa Kiislamu kwa asili yao hawana akili? Alitaka kujua Mzee Kitwana Kondo. Lakini hakuweza kupata jibu.

Mheshimiwa Waziri,
Ni wazi kuwa Waziri wa Elimu au Waziri Mkuu ambaye ndiye msimamizi wa mambo ya serikali Bungeni asingeweza kutoa majibu ya uhakika kwa sababu swali lilihitaji kufanyika uchunguzi huru wa kina na makini kwanza.

Mheshimiwa Waziri,
Mwaka 1987 aliyekuwa Waziri wa Elimu, Profesa Kighoma Ali Malima, aliweka utaratibu mpya wa ufanyaji wa mtihani wa darasa la saba ambapo namba zilitumika toka kufanya mtihani, kusahihisha na kuchagua wanafunzi wa kwenda kidato cha kwanza. Namba zilivishwa majina baada ya taratibu zote hizo kukamilika. Mwaka huo idadi ya watoto wa Kiislamu waliokwenda kidato cha kwanza iliongezeka kwa asilimia 40 ikilinganishwa na miaka ya nyuma.

Hata hivyo, mara aliondolewa Waziri Malima katika wizara hiyo na utaratibu wa zamani ukarejeshwa ambapo yalikuwa yakichaguliwa majina na idadi ya Waislamu ikaporomoka na kurudi chini ya asilimia 20.

Mheshimiwa Waziri,
Hali kama hii hapana shaka inazua maswali mengi ambayo yanahitaji majibu na majibu hayo hayawezi kupatikana bila ya kufanyika uchunguzi.


Labda tuongeze mifano ili kuliweka wazi zaidi jambo hili. Mwaka 1983 mwanafunzi aliyekuwa akiitwa Kopa Abdallah akisoma katika shule ya msingi Kichangani, Kilosa, alikosa kuchaguliwa kwenda sekondari. Yeye binafsi, wazazi wake na hata walimu wake hawakuamini matokeo yale kutokana na alivyokuwa akifanya vizuri kuliko wanafunzi wote. Baadae ilikuja kugundulika kuwa nafasi yake alipewa mwanafunzi aliyekuwa akiitwa Antoni Samirani ambaye alikuwa na uwezo mdogo sana ikilinganiswa na Abdallah. Kilichofanyika ni kuwa jina la Abdallah lilifichwa na baadae Antoni akapewa jina hilo kimya kimya na kwenda kusoma sekondari akitumia jina Abdallah wakati yeye ni Antoni.

Taarifa zinasema kuwa Kopa Abdallah alipogundua hakuweza kufanya kitu akaishia kuwa dereva.

Hali kama hiyo ilimkuta pia Adam Ramadhani aliyekuwa akisoma shule ya msingi Rutihinda jijini Dar es Salaam na kumaliza darasa la saba mwaka 1999. Yalipotoka matokeo ya mtihani wa darasa la saba na kuonekana kuwa Adam hakuchaguliwa, baba yake hakuamini kuwa mtoto wake anaweza kufeli kutokana na uwezo aliokuwa nao na zaidi akitizama walivyochaguliwa watoto ambao Adam alikuwa mwalimu wao shuleni na mitaani.

Katika kufuatilia suala hilo wizarani, ilikuwa aibu kwa wizara baada ya kuonekana kuwa walichaguliwa watoto wa Kikristo wenye alama za chini kabisa huku akiachwa Adam Ramadhani aliyekuwa na alama za juu kuliko wote.

Mheshimiwa Waziri,
Mifano kama hii ni mingi mno na ipo katika ngazi zote kwa maana kutoka elimu ya msingi kwenda sekondari, kutoka kidato cha nne kwenda kidato cha tano na kutoka kidato cha sita kwenda Chuo Kikuu. Kwamba hata kutoka kidato cha nne kwenda kidato cha tano, wapo watu waliopata kushuhudia majina ya wanafunzi wa Kiislamu yakiwekwa pembeni japo walikuwa na sifa za kuchaguliwa.

Mheshimiwa Waziri,
Ukiacha hujuma katika kuwaacha wanafunzi Waislamu wenye sifa kuendelea na masomo, matatizo huanzia kwenye kuamua nani amefaulu na nani kafeli. Tuhuma zilizopo ni kuwa wapo wanafunzi wanapewa madaraja ya juu wakati alama zao ni za chini na wapo wanaopewa madaraja ya chini wakati alama zao ni za juu. Na hii ni kwa masomo yote.

Mheshimiwa Waziri,
Kumekuwa na utamaduni katika nchi hii wa kukataa ukweli. Kufuatia uchunguzi uliofanywa na Kamati za Bunge, tumeshuhudia wizi na ufisadi wa kutisha ukifichuliwa Bungeni hivi karibuni hali iliyopelekea mpaka Mheshimiwa Rais kubadili Baraza lake la Mawaziri.

Sasa baada ya kuyasema yote hayo, tunasema kuwa Baraza la Mitihani la Tanzania, limekuwa likilalamikiwa kwa zaidi ya miaka 30, lakini malalamiko hayo yamekuwa yakipokewa kwa sikio la uziwi. Imefikia mahali tunasema kuwa hatuna tena imani na Baraza hilo.

Mheshimiwa Waziri,
Ilikupata ukweli wa malalamiko na shutuma hizi, na ili kujibu lile swali juu ya watoto wa Kiislamu ambalo halikupata jibu Bungeni, tunaitaka serikali kufanya yafuatayo:
  1. Tume huru iundwe kuchunguza Baraza la Mitihani la Tanzania na utendaji wake kazi kwa kipindi cha miaka kumi iliyopita.
  2. Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani (NECTA) ajiuzulu mara moja ili kulinda heshima ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzaani na Baraza la Mitihani. Watendaji wakuu wa kitengo cha mitihani na wanaohusika na mfumo wa Kumputa ya Baraza la Mitihani nao wawajibishwe mara moja.
  3. Hatua za kisheria na kibinadamu zichukuliwe dhidi ya watumishi wa Baraza la Mitihani watakaothibitika kuhusika na kashfa hii.
  4. Muundo wa Baraza la Mitihani uzingatie uwiano wa kidini, kitendo cha chombo nyeti kama hiki kujazana watu wa dini moja kunaliondolea Baraza la Mitihani sura ya kitaifa, kwani takwimu zinaonyesha Makatibu Wakuu Watendaji na Manaibu Katibu Wakuu wamekuwa Wakristo na Wenyeviti wa Baraza hilo ni Wakristo tangu lilipoanzishwa mwaka 1973, mpaka hii leo na takwimu tunazo.
Mheshimiwa Waziri,
Tunaomba ieleweke kuwa tunachotaka ni kupatikana haki na kufanyika uadilifu kwa watu wote. Hatudai wala hatutaki upendeleo kwa Waislamu na wala hatutaki kuona mtu yeyote anaonewa au kuporwa haki yake, awe Mwislamu au mtu wa dini nyingine.

Tunachoamini ni kuwa kama Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi haina cha kuficha, basi itaunda Tume hiyo kwa haraka na kuhakikisha kuwa ni Tume ya kuaminika itakayofanya kazi yake kwa umakini, kwa kina na kwa uadilifu wa hali ya juu kabisa.

Lakini kama Wizara yako itaona kuwa haiwezi kuunda Tume ya uchunguzi, tunacho kuhakikishia ni kuwa sisi tutafanya kila liwezekanalo na kwa namna yoyote kuhakikisha kuwa Tume hiyo inaundwa. Na ikigundulika kuwa kuna hujuma zinafanyika katika utendaji wa Baraza, basi itabidi uwajibikaji uanze kwenye Wizara kabla ya kuwawajibisha watendaji wa Baraza la Mitihani.

Ni imani yetu kuwa utayapokea madai ya Waislamu na kuyafanyia kazi kwa umakini na kwa haraka ili kujenga mustakbali mwema wa nchi hii na watu wake.

Tunaomba kuwasilisha,


Mwenyekiti
Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu
 
Back
Top Bottom