Utajiri wa Daniel Yona unatisha!

..............ama kweli habari za tajiri muulize maskini,wekeni na za MY-GAL bac..........
 
kuna daniel yona wawili, sr. na jr.

unajua mleta mada anamzungumzia yupi?
Nazungumzia yule kibaka aliyetuibia kodi zetu na sasa mwenye 'kesi' (Ambayo kwa kweli ni dongo la macho kwa watanzania) na kibaka mwenzie Mramba. Natamani watu hawa waliotufikisha hapa wawajibishwe kwa kuikabili adhabu ya kupigwa risasi hadharani wao na wote waliotusababishia feddheha ya watoto wetu kukaa mavumbini na wengine kukosa dawa hospitalini.
 
Wiki hii tulishuhudia Mwinyi akitinga mahakamani kudai kuibiwa milini 37 ambazo mfanyakazi wake baada ya kukusanya kodi kwa wapangaji wa nyumba za Mwinyi (mzee ruksa) hakuziwakilisha kwa Mwinyi. Hatukujua utajiri alio nao, sehemu hiyo ya utajiri ambayo ni kutokana na kodi za wananchi umejulikana kutokana na mwajiriwa wake kumfanyia mizengwe ya kuona mbona amejaza na bado anataka, ngoja nizihifadhi na familia yangu ipate sehemu ya walipa kodi asifaidi peke yake.
 
Ndugu zangu, juzi nimefika Makongo Juu. Nilionyeshwa mahekalu ya Daniel Yona hadi nikaogopa.

Amejitwalia eneo kubwa mno. Kajenga mahekalu mengi. Mengine anaishi, mengine amepangisha wazungu. Nikaambiwa mengine ni ya mkewe. Pia kuna shule ambazo ni mali yao. Utajiri huu jamani si wa kawaida.

Hivi kweli makabwela wa nchi hii watakubali wizi huu hadi lini? Anayetaka na afike eneo hilo ajionee haya ninayosema. Inakera sana, hasa wakati huu ambao watoto wetu hawana madawati, maabara wala mlo wa uhakika. Lazima tuchukue hatua za kurejesha mali hizi!

Nawasilisha

Umeziona mali za Rostam, Kikwete, Lowassa, Nkullo, Ngereja na Ridhwan? hebu tuanze kwanza kwa kuzijadili hizo halafu kishe tugeukie wenye mali chini yao
 
Kwa kuwa leo ni jumapili naomba niwajibu kama yesu na ambaye hajawahi kuiba katika maisha yake hata sh kumi au sh mia na awe wa kwanza kumsema yona
 
Kimsingi wanasiasa ni wanatumia Madaraka vibara (kula rushwa ) na kuishi Kama wake peponi.cha kufanya kwa sasa ni kuimarisha tume ya maadili ya viongozi wa umma ili kuweza kudhibiti wanasiasa na watumishi wengine wa serikali
 
Cha kufanya ni lazima kifungu kinachompatia raisi kinga ya kushitakiwa kifutwe katika katiba. Mahakama kuu lazima iwe huru na mwanasheria mkuu lazima jina lake lipitishwe na Bunge. wewe hakikisha umeyafanya haya halafu uone jinsi mali za umma zilizoibiwa zitakavyo rudi haraka kwa umma. Hakuna maendeleo kabisa, miaka 50 baada ya uhuru shule 80% za msingi bado wanatumia vyoo vya kuchimba ! Halafu unamkuta mtu kama yona anatajilikia pesa za umma. Hii kweli haiingii akirini. sisi lazima tupeleke madai yetu ktk katiba tuu.
 
Ndugu zangu, juzi nimefika Makongo Juu. Nilionyeshwa mahekalu ya Daniel Yona hadi nikaogopa.

Amejitwalia eneo kubwa mno. Kajenga mahekalu mengi. Mengine anaishi, mengine amepangisha wazungu. Nikaambiwa mengine ni ya mkewe. Pia kuna shule ambazo ni mali yao. Utajiri huu jamani si wa kawaida.

Hivi kweli makabwela wa nchi hii watakubali wizi huu hadi lini? Anayetaka na afike eneo hilo ajionee haya ninayosema. Inakera sana, hasa wakati huu ambao watoto wetu hawana madawati, maabara wala mlo wa uhakika. Lazima tuchukue hatua za kurejesha mali hizi!

Nawasilisha

Ndugu yangu,fanya kazi na jitume ili nawe upate mafanikio katika maisha yako,wewe umeona na hujui amepataje,badala ya kupoteza muda na nguvu zako kujadili ya wenzio jitume ili nawe uwe bora.(Life is one thing road with a lot of sings,so when you riding through the road don't complicate your mind!free from hate mischief and jealous!)
 
Kumiliki mijumba at his age, na vyeo alivyopitia mbona ni kitu rahisi sana? kulalamika sometimes kumezidi. mi ni kijana, niko kwenye ajira na kamshahara kangu wala sio kakubwa na sina rushwa lkn mdogomdogo najiandaa kupiga msingi wa nyumba ya 2. Sasa hivi kuna wajinga tayari wananiita fisadi mtoto bila kujua kamkopo kangu kamilion kumi ni tofali na cement ya nyumba nzima. nikifika umri wa Yona lzm niwe na nyumba atleast tano mjini. hayo ndo malengo yangu, wewe je? tutenganishe ufisadi na fursa, msomi kama Yona aliyeenda Uk na kina Mengi kupiga ACCA miaka hiyo na akaipata kabla ya kina Mengi bado unataka awe maskini? huo utakuwa upuuzi.

Ujenzi ni mgumu sana tena kwa dar hapa na ww usitudanganye kwa mshahara wako wa serikali unawezaa jenga nyumba mbili, kwa vyovyote vile utakuwa ni mwizi,
 
Ndugu zangu, juzi nimefika Makongo Juu. Nilionyeshwa mahekalu ya Daniel Yona hadi nikaogopa.

Amejitwalia eneo kubwa mno. Kajenga mahekalu mengi. Mengine anaishi, mengine amepangisha wazungu. Nikaambiwa mengine ni ya mkewe. Pia kuna shule ambazo ni mali yao. Utajiri huu jamani si wa kawaida.

Hivi kweli makabwela wa nchi hii watakubali wizi huu hadi lini? Anayetaka na afike eneo hilo ajionee haya ninayosema. Inakera sana, hasa wakati huu ambao watoto wetu hawana madawati, maabara wala mlo wa uhakika. Lazima tuchukue hatua za kurejesha mali hizi!

Nawasilisha

Mkuu naona unatakiwa kufanya research zaidi, zile nyumba haziwezi kuitwa utajiri wa kutisha. Zile nyumba za Yona ukiangalia zilivyoanza kujengwa na kuongezwa polepole unaweza kuona kuwa ni juhudi za polepole naziona toka nikiwa mtoto ninapopita kwenda nyumbani, na zile nyumba si mahekalu naweza kuita ni nyumba za kawaida kwa mwenye uwezo. Jarubu kupanda juu kidogo kulia kwa mzee kaduma au nchini kidogo kwa Mporongomyi au nenda juu zaidi kwa Rugemalira wa IPTL ndio unaweza kujua kuwa watu wa kule walikuwa wanadunduliza.

Mahekalu yako mikocheni......
 
tumezidi kulala, kama prof mahalu alishinda kesi, sitoshangaa mramba, yona na mgonja kushinda kesi kwa kishindo
 
house_porch.jpg

Pima hoja zangu kuhusu nyumba hii kwamba haijajengwa Dar ila imechukuliwa kutoka nyumba za ulaya au bara la Marekani kaskazini. Linganisheni na nyumba hapo chini utakuja kuona ukwlei wa hoja zangu. Ninachotaka tuweke picha ya ukweli badala ya kudanganya JF.

Nyumba hiyo hapo juu haijaezekwa kwa bati au vigai bali ni aina vulani ya plastic iliyochanganywa na saruji, mpira na takataka nyingine ni uezekaji maarufu katika nyumba nyingi za kawaida Ulaya Na Marekani. Uezekaji huu haupo kabisa Tanzania.

images
images
images

images
images
images

Hizi ni nyuma za ulaya au marekani ambazo mjengo wake unashabihiana na nyumba hiyo. Tukumbuke kuwa nyumba nyingi za Dar utakuwa milango na madirisha huwekwa nondo kujihadhari na wizi, hapo hakuna cha nondo. Mbaya zaidi window shutters kuwa double kitu ambacho hakipo kabisa hapa kwetu Tanzania kwa sababu window shutter huwa sehemu ya baridi kali, hata Marekani kusini hakuna double window shutter, utazikuta Canada na northern states kwa sababu ya baridi kuweza kuhifadhi zaidi joto. Nchi za ulaya kama Scandinavia bila double window shutters hitter haisaidii sana na zaidi utatumia zaidi utility na kushtukia bill ya kukukatisha tamaa kuilipa.

95% nyumba hiyo imeshukuliwa picha ya nyumba za ulaya na wala si nyumba anayotuambia ameijenga Yona. Kama anataka kutuhakikishia ukweli aipige picha nyumba hiyo kwa mbali kidogo ikionyesha madhari ya mazingira ya Dar es Salaam na nyumba za jirani la sivyo kauli yangu ina uzito stahiki.

asante mkuu scope aminia.
 
Ndugu zangu, juzi nimefika Makongo Juu. Nilionyeshwa mahekalu ya Daniel Yona hadi nikaogopa.

Amejitwalia eneo kubwa mno. Kajenga mahekalu mengi. Mengine anaishi, mengine amepangisha wazungu. Nikaambiwa mengine ni ya mkewe. Pia kuna shule ambazo ni mali yao. Utajiri huu jamani si wa kawaida.

Hivi kweli makabwela wa nchi hii watakubali wizi huu hadi lini? Anayetaka na afike eneo hilo ajionee haya ninayosema. Inakera sana, hasa wakati huu ambao watoto wetu hawana madawati, maabara wala mlo wa uhakika. Lazima tuchukue hatua za kurejesha mali hizi!

Nawasilisha

Tuanze na wewe uliyeyashuhudia ulifanya nn au unakusudia kufanya nn au wewe sio kabwela??
 
Back
Top Bottom