Utajiri wa Daniel Yona unatisha!

Mwitongo

JF-Expert Member
Jan 30, 2009
312
360
Ndugu zangu, juzi nimefika Makongo Juu. Nilionyeshwa mahekalu ya Daniel Yona hadi nikaogopa.

Amejitwalia eneo kubwa mno. Kajenga mahekalu mengi. Mengine anaishi, mengine amepangisha wazungu. Nikaambiwa mengine ni ya mkewe. Pia kuna shule ambazo ni mali yao. Utajiri huu jamani si wa kawaida.

Hivi kweli makabwela wa nchi hii watakubali wizi huu hadi lini? Anayetaka na afike eneo hilo ajionee haya ninayosema. Inakera sana, hasa wakati huu ambao watoto wetu hawana madawati, maabara wala mlo wa uhakika. Lazima tuchukue hatua za kurejesha mali hizi!

Nawasilisha
 
usicheze na madini ya ya wenyewe, na bahati mume muwahi na gesi ya ya kusini
 
Mwitongo

Kila mbuzi anakula urefu wa kamba yake ndugu.hata hivyo kesi yake ipo mahakamani
 
Last edited by a moderator:
Kila mbuzi anakula urefu wa kamba yake ndugu.hata hivyo kesi yake ipo mahakamani

Sidhani kama hiyo kesi itakuwa na tija kwa masikini. Mahakimu wameshakatiwa chao, sana sana atafungwa miaka miwili, anarudi kula maisha kama kawaida!
 
ndugu ungetuwekea na mapicha hapa, pia kijana wake dani yona ana bonge ya kitu hapa tegeta line ya umeme wa kwenda zanzibar ni hotel siyo hivyo tu mali ni nyingi sana wanazo, wametuibia sana tena sana.
Ni watu ambao leo hii nchi hii ikichukuliwa na wenye uzalendo wa kweli hakika mafisadi watarudisha mali zetu zote walizotuibia wakati wako kwenye madarak. Pole ndugu ndo hali halisi ya mambo na watawala wa nchi yetu
 
kati ya mabilionea wa kwanza kwanza tangu Azimio la Zbar (kufuta maadili ya viongozi)
 
Hii ni chachandu tu! Mlo kamili upo Makongo Juu ndugu zangu!!
 
Mwitongo

swali sio utajiri mkuu, UNATAKA KILA MTU AWE MASKINI???

Cha maana ni kujua aliupata kihalali??

Kulalamikia utajiri wa mtu bila kujua alipataje ni sawa na enzi zile kijijini mtu akiweka bati tu, basi lazma apigwe kipapai
 
Last edited by a moderator:
Siye wabongo watu wa kuridhika sana nimeshuhudia kesi ya rich mond wakituaminisha hawajui muhusika na labda walishalipwa pesa yao na siye twakaa kimya tuuu.....kha
 
Kuwa tajiri hata kama ni kupindukia sio vibaya kama ni kutokana na nguvu zako. Na hili linawezekana sana hapa bongo kwa watu waliokuwa na opportunities kama kina D.Yona, F.Masha, F.Mosha, etc (Soma cv zao) actually wakiwa fukara tunatakiwa kuwacheka!

Ila Haya ndo mambo tunasema kila siku, ukiwa kiongozi wa umma unatakiwa kuwa clean "in fact, and in appearance"! Na hapa nadhani ndipo Yona anapo chemsha, kutokana na tuliyo yasikia Kiwira tu, tunashindwa tenganisha kati ya mali za wizi na za halali.



Kwa kuwa hili jukwaa ya thinkers! Tu - reason kidogo hii kesi.

kwa madaraka, na opportunities alizo wahi shika huyu bwana Yona, miaka nenda garuka, kuwa na utajiti huu wa makongo, sijui nyumba ya tegeta - tena ya mwanae mimi sioni ajabu!

Isitoshe kila nyumba iliyopo pale ilijengwa kabla jamaa hajawa mbunge, na nyumba anayo ishi ni ile ile (hata alipokuwa waziri) amabyo aliijenga toka akiwa THB - bila shaka ni kwa mkopo! Tena iko barabarani - vumbi loote lina ingia ndani!

Nasikia Yona alinunua eneo lake pale kama eka 8 kwa sh 120 - mwaka 1968 so sio hatari kuwa na mali hizo leo miaka zaidi ya 40.

Ni sawa na wanaokamata ma-ardi leo kibaha eka 1 - sh laki 3. Baada ya miaka 20 itakuwa kaa makongo.
 
Atashindwaje tajiri wakati aliwahi kushika wizara nyeti inayoongoza kwa kudidimiza uchumi wa nchi huku mawaziri wake wakiendelea kuneemeka tena wakiishia kuondolewa kwa kashfa kwenye nyadhifa zao.
 
Atashindwaje tajiri wakati aliwahi kushika wizara nyeti inayoongoza kwa kudidimiza uchumi wa nchi huku mawaziri wake wakiendelea kuneemeka tena wakiishia kuondolewa kwa kashfa kwenye nyadhifa zao.

Ile kampuni yake na BWM inaitwaje?
Si nasikia walijiuzia ule mgodi kwa bei ya kutupwa???
 
Back
Top Bottom