Utajiri halali! Dhana isiyo na chembe ya ukweli

Utajiri halali! Dhana isiyo na chembe ya ukweli

The world is a full of secret,,, be hamble,,, learn it slowly Mshanajr


Umegusa mengi ila ukweli ni mgumu kuutambua na kuutumia pia
 
Umaskini ni kitu kibaya sana, na mawazo ya kimaskini ni kitu kibaya zaidi...Maskini wengi ndo hawataenda mbinguni kabisa, kwanza ndo watenda dhambi na wahalifu wakubwa zaidi na ni wengi, na zaidi ya yote wanawivu uliopitiliza.
 
Tangu enzi na enzi za manabii bishara zilikuwepo na wapigaji walikuwepo, wapo waliokuwa wanaweka maji kwenye mazao au kwenye maziwa.
Na wapo wanaoapa kuwa haimlipi ila anapata kidogo sana.
Wapo wanaosema anauza kwa hasara, lakini ni wachache sana wanaofanya biashara zao bila dhulma na kutoa sadaka kwa sana.
 
Tatizo mnashindwa kuelewa kitu kidogo, mfano umekopa benki ili uulinde mkopo wako lazima ufanye zindiko kwanza, then ufanye zindiko la biashara, la sivyo utaambulia pua.
 
Kwa hyo mshana unasemaje kuhusu vijana wanao hustle kwa kupigana na kupambana kila siku ili waje kuwa matajiri wasaidie ndugu jamaa na marafiki zao pia maisha yao yawe ya furaha???
 
Kwa hyo mshana unasemaje kuhusu vijana wanao hustle kwa kupigana na kupambana kila siku ili waje kuwa matajiri wasaidie ndugu jamaa na marafiki zao pia maisha yao yawe ya furaha???
Kila mtu anahitaji utajiri, pesa mingi tu, mabunda kwa mabunda tena ya ughaibuni...kumiliki Pesa nyingi humfanya mtu kuwa na furaha kila akiziangalia.... Mtu asiyependa utajiri mwangalie mara mbili inawezekana ni mchawi huyo.... Ninachosema ni kwamba hakuna kitu kinaitwa utajiri wa haki kwa asilimia 100
 
Maneno ya Mungu yanasema hivi.... Ni rahisi kwa ngamia(sio mnyama) kupenya kwenye tundu la sindano kuliko tajiri kuurithi ufalme wa Mungu....!
Warithi wa ufalme wa Mungu ni akina nani? Wana sifa na vigezo gani? Ni wanyofu na wasafi wa moyo, watenda haki waliojitenga na dhambi na matendo yote ya giza, wasiodhulumu wala kupora cha mhitaji...
Ili uweze kuwa tajiri ama ili uweze kuupata utajiri kwa kiasi kikubwa itabidi ujitenge na matendo ya unyofu, huruma, utu wema na ushikamane na ulimwengu wa giza, makafara dhuluma na ni lazima uwe na roho ngumu na katili japo kwa kificho....!
Itabidi utafute njia za kupata bidhaa kwa bei rahisi sana halafu uuze kwa faida kubwa
Itabidi uwe mkwepa kodi na mdanganyifu kwenye mapato kwa nia ya kutunisha kibubu chako
Itabidi ununue hata kuuza mali ya wizi, dhuluma ama magendo ili tu usitetereke kiuchumi
Itabidi waajiriwa wako uwalipe kidogo lakini wazalishe kingi
Itabidi ufanye makafara na ushirikina kwa nia ya kulinda utajiri na himaya yako
Itabidi utumie mbinu zote halali na haramu ili kuendelea kukuza na kutunisha akaunti zako na biashara zako..

Ukishafanikiwa kimaisha na kuwa mfanyabiashara tajiri kwa viwango tofauti, kiunafiki kabisa na kuficha makucha yako, utairudia jamii kwa kutoa sadaka, misaada na zaka kwenye nyumba za ibada na majukwaa ya kijamii.. Hutafanya kwa siri kwakuwa unataka usafishike mbele za macho ya jamiii... Lakini kile unachokoa ni sehemu ndogo kabisa kwenye kile ulichowaibia wale unaowapa kwa mlango wa misaada....

Yote juu ya yote tunauhitaji utajiri kwa nguvu zetu zote ili kukidhi mahitaji ya natamanio ya kimwili na starehe za dunia, sifa na utukufu wa kununua.... Lakini asikudanganye mtu hakuna utajiri wa haki hata siku moja
Hayo si maneno ya Mungu. Mungu hana lugha za kijinga namna hiyo.

Utajiri ni halali kabisa.
 
Unaujua msoto alioupitia??? kutoka kuwa tajir namba moja duniani mpak kuwa fukara namba moja duniani lakn jamaa kasimamia ukucha kumtegemea Mungu....Tajir gan wa sasa anaweza pitia msukosuko kama huo akabaki upande wa Mungu?? biashara ikiyumba kidog tu anakimbia kwa mganga wake au freemason...
Vigezo na masharti kuzingatiwa.
 
Ni kweli kabisa tena matajiri ni wabinafsi mno, kuna sehemu nlisoma Beyonce alitengeneza design yake ya nguo ambayo aliuza bei ghali mno lakini wanawake waliokua wanamfanyia kazi hyo walikua wanalipwa chini ya dollar moja kwa saa lakini alijigamba kwamba lengo lake ni kumuinua mwanamke wa chini
 
Back
Top Bottom