Utajiri halali! Dhana isiyo na chembe ya ukweli

Utajiri halali! Dhana isiyo na chembe ya ukweli

Hakuna mkamilifu chini ya jua, unaweza ukawa sio tajiri ila ukawa mwovu. Kwani matajiri pekee ndio waovu? Dhambi yako inaweza kuwa tofauti na mwingine but wote ni wadhambi. Tuache kuona matajiri ni watu wadhambi Halafu wasio matajiri ni watu clean .
Kuna niliposema hivyo? Au hukusoma na kuelewa kilichoandikwa?
 
Je huyu ngamia aliyetajwa hapa kama sio mnyama maandiko yalimaanisha ngamia yupi au ni kiumbe kipi au ni kitu gani chenye kusimama badala ya neno ngamia? hebu naomba mtueleze na wengine tujuwe, natanguliza shukrani zangu za dhati.
Ni kamba itumikayo kwenye nanga
IMG_20181214_090132.jpeg
 
Maneno ya Mungu yanasema hivi.... Ni rahisi kwa ngamia(sio mnyama) kupenya kwenye tundu la sindano kuliko tajiri kuurithi ufalme wa Mungu....!
Warithi wa ufalme wa Mungu ni akina nani? Wana sifa na vigezo gani? Ni wanyofu na wasafi wa moyo, watenda haki waliojitenga na dhambi na matendo yote ya giza, wasiodhulumu wala kupora cha mhitaji...
Ili uweze kuwa tajiri ama ili uweze kuupata utajiri kwa kiasi kikubwa itabidi ujitenge na matendo ya unyofu, huruma, utu wema na ushikamane na ulimwengu wa giza, makafara dhuluma na ni lazima uwe na roho ngumu na katili japo kwa kificho....!
Itabidi utafute njia za kupata bidhaa kwa bei rahisi sana halafu uuze kwa faida kubwa
Itabidi uwe mkwepa kodi na mdanganyifu kwenye mapato kwa nia ya kutunisha kibubu chako
Itabidi ununue hata kuuza mali ya wizi, dhuluma ama magendo ili tu usitetereke kiuchumi
Itabidi waajiriwa wako uwalipe kidogo lakini wazalishe kingi
Itabidi ufanye makafara na ushirikina kwa nia ya kulinda utajiri na himaya yako
Itabidi utumie mbinu zote halali na haramu ili kuendelea kukuza na kutunisha akaunti zako na biashara zako..

Ukishafanikiwa kimaisha na kuwa mfanyabiashara tajiri kwa viwango tofauti, kiunafiki kabisa na kuficha makucha yako, utairudia jamii kwa kutoa sadaka, misaada na zaka kwenye nyumba za ibada na majukwaa ya kijamii.. Hutafanya kwa siri kwakuwa unataka usafishike mbele za macho ya jamiii... Lakini kile unachokoa ni sehemu ndogo kabisa kwenye kile ulichowaibia wale unaowapa kwa mlango wa misaada....

Yote juu ya yote tunauhitaji utajiri kwa nguvu zetu zote ili kukidhi mahitaji ya natamanio ya kimwili na starehe za dunia, sifa na utukufu wa kununua.... Lakini asikudanganye mtu hakuna utajiri wa haki hata siku moja
Mshana Jr, asante nimekupata.
 
Hapo masikini wametukosha hatuna haja ya kuangaika na utajiri ngoja tubaki huku huku anayebisha sawa.
 
Msingi wa kuelekea kwenye utajiri

Hatua ya kwanza
Elimu ya wastani.. Secondary mpaka chuo
Kuanzisha biashara kwa msingi kiduchu au msingi wa kawaida
Kupata makazi na mahitaji muhimu
Kustawisha biashara na kuanza kutengeneza faida ya kawaida... Mpaka hapa hakuna shida kabisa

Hatua ya pili
Hapa biashara imestawi sasa na faida yenye ziada nzuri ipo... Linakuja wazo la kupanua biashara kwa kuwekeza kwenye maeneo mengine
Ukiwa sasa ni mbobezi kiasi chake unawekeza kwenye maeneo mengine mawili matatu na mambo yanakuwa alhamdulilah... Unaaza kukutana na marafiki wapya, status za juu kidogo.... Wanakusimulia mafanikio... Una anza kuvutiwa na kutamani mafanikio zaidi...
Ukiwaangalia wamekuzidi kwa magari ya gharama, majumba vitega uchumi nknk... Unatamani kufanana nao... Na shida ina anzia hapa

Hatua ya tatu
Utajiri wa dhambi
Unampata mmoja unayemwamini kati ya wale... Anakutamanisha na kukushawishi ujiunge na chama cha mafanikio kwa kutumia njia za mkato
Unaanza kufundishwa biashara za magendo
Unaanza kufundishwa biashara za dhuluma
Unaaza kufundishwa kutoa makafara na kufanya mazindiko
Unaaza kufundishwa kufanya biashara haramu
Unashawishika na kujaribu... Matokeo yanakuwa chanya.... Shap kwa haraka unakuwa wa next level

Hatua ya nne
Uko kwenye mafanikio, unaitwa milionea ama bilionea.... Jina wengi wangependa waitwe... Una heshima na nafasi katika jamii... Unatambulika na kuwa mfano na alama ya mafanikio.... Lakini mara unaambiwa fulani ni mnoko sana usipomfix mapema ataharibu mtandao wako wa biashara... Unatafakari yeye na utajiri wako kipi kikubwa... Unamwondoa...
Unaambiwa safari hii bila kafara la binadamu utaanguka... Kwahiyo chagua aanguke nani...
Utajiri ni mtamu asikwambie mtu... Akuambiaye kuna utajiri wa halali hajui nini maana ya utajiri au ana maanisha utajiri level one
Swadakta.
 
Kiufupi utajir wa halali kabisa ni kama haupo...kila moja ana siri yake moyoni....labda wale matajir wa kuajiriwa....harakati za mtaani zina mauza uza mengi sana
Matajiri wa kuajiriwa ndio usiseme kabisa.
 
Mfano rais wa nchi ka mshahara wake tu hawezi kuwa ni tajiri? Ni maskini huyu??

Mfano mtu anafanya kazi UN kwa mshahara tu si tajiri huyu??

Tajiri ni nani??
Rais analipwa mil 9 per month,hii ni kwa mujibu wa yeye mwenyewe.

Unadhani kwa huo mshahara utamfanya awe tajiri au atakua ni middle income person?
 
Maneno ya Mungu yanasema hivi.... Ni rahisi kwa ngamia(sio mnyama) kupenya kwenye tundu la sindano kuliko tajiri kuurithi ufalme wa Mungu....!
Warithi wa ufalme wa Mungu ni akina nani? Wana sifa na vigezo gani? Ni wanyofu na wasafi wa moyo, watenda haki waliojitenga na dhambi na matendo yote ya giza, wasiodhulumu wala kupora cha mhitaji...
Ili uweze kuwa tajiri ama ili uweze kuupata utajiri kwa kiasi kikubwa itabidi ujitenge na matendo ya unyofu, huruma, utu wema na ushikamane na ulimwengu wa giza, makafara dhuluma na ni lazima uwe na roho ngumu na katili japo kwa kificho....!
Itabidi utafute njia za kupata bidhaa kwa bei rahisi sana halafu uuze kwa faida kubwa
Itabidi uwe mkwepa kodi na mdanganyifu kwenye mapato kwa nia ya kutunisha kibubu chako
Itabidi ununue hata kuuza mali ya wizi, dhuluma ama magendo ili tu usitetereke kiuchumi
Itabidi waajiriwa wako uwalipe kidogo lakini wazalishe kingi
Itabidi ufanye makafara na ushirikina kwa nia ya kulinda utajiri na himaya yako
Itabidi utumie mbinu zote halali na haramu ili kuendelea kukuza na kutunisha akaunti zako na biashara zako..

Ukishafanikiwa kimaisha na kuwa mfanyabiashara tajiri kwa viwango tofauti, kiunafiki kabisa na kuficha makucha yako, utairudia jamii kwa kutoa sadaka, misaada na zaka kwenye nyumba za ibada na majukwaa ya kijamii.. Hutafanya kwa siri kwakuwa unataka usafishike mbele za macho ya jamiii... Lakini kile unachokoa ni sehemu ndogo kabisa kwenye kile ulichowaibia wale unaowapa kwa mlango wa misaada....

Yote juu ya yote tunauhitaji utajiri kwa nguvu zetu zote ili kukidhi mahitaji ya natamanio ya kimwili na starehe za dunia, sifa na utukufu wa kununua.... Lakini asikudanganye mtu hakuna utajiri wa haki hata siku moja
Umenena Chief

Tamaa ya Utajiri na mafanikio ya Haraka,ndio maana amani hukosekana katika jamii zetu
 
Hoja yako unataka aminisha jamii kuwa umaskin ni sehemu ya utakatifu,,na mtu kuwa na Mali ni dhambi kwa mtazamo wako duni kwamba Mali au utajiri lazma udhulumu,uibe,unyonye watu nk..
Sio kweli sabb kuna utajiri unaopatikana kwa haki na unaopatikana nje ya haki..pande zote mbili kuna mchakato wake!!

Usitake kuturudisha kwenye wokovu wa kimaskini kama wa enzi zileeeee...afu mnageuka na kutucheka eti mbona wanasema Mungu wao tajiri wakat wao maskini..

Fedha na dhahabu ni Mali ya Bwana..mithali...
Povu lenye heshima
 
Utajiri Bora kabisa kwa Mwanaadam
Ni mtu kuridhika na chake na kutokodolea macho cha mtu

Walisema

CHA MTU MAVI,UKIKIONA KITEMEE MATE
 
Mada nzuri sana kaka, kwa kimombo kidogo japo kilikuja na jahazi “a road to success has never been an easy one” hata kupanda cheo au kutumikia nyumba za ibada kuna visanga vingi sanaa.

Kwenda mbinguni pia yale yale sio kazi rahisi, basi hata kua tajiri pia sio kazi rahisi.
 
Ila kwenye thread yako umenikumbushia mzee mengi.. Maana nasikia yeye ni muumini wa freemason, sasa kwenye ile misaada anayotoa + party za vilema huenda anachukua nyota za watu na anatoa kafara in the process Mshana Jr
Hayo ni maneno ya kike tena wanawake wa tandale kwenu. Huyu Mengi familia yake (kaka yake) ni matajiri hata kabla ya uhuru!
Mengi alianza kuengeneza kalabu za wino, akaja viwanda vya mafuta ya kujipaka etc.
Fanyeni kazi achene umbea wa tandale kwenu!
 
Ni kweli hakuna hata chembe ya ukweli . Anza hapo kijijini kwako , matajiri wana utahiri halali ? Mara usikie kwenye familia kuna tatizo la ajabu mf. Msomi kurudi kijijini na kuanza ulevi na mambo ya ajabu . Yote hayo yanajibiwa kwa kauli moja "Mungu hakupi vyote " acheni kumsingizia Mungu . Hakuna utajiri kutoka kwa Mungu ila ni "maujanja ya aibu ya dunia "
 
uongo mtupu huuu

Kwanza tutajie huyo swahaba ni gani?

Na ni kitabu gani hapo?

Uongoooo mtupuuuuuuuuu,huyo labda sahaba wa mswahili.
Kuna hadithi moja ya maswahaba (walioachwa kulea ujumbe na mtume) waislamu walipojaribu kuuishi uislamu waligundua dhambi zote zinaa achika isipokuwa riziki haramu ,wakamfata yule swahaba na kumuuliza ''Je yawezekana binadamu kuishi kwa riziki halali tuu?'' Jamaa akaomba afikilie kwanza akajisemea nikiwaambia yawezekana ntamfurahisha mungu ,ntakuwa nimewadanganya wao ,nikisema haiwezekani ntamuuzi mungu nakuwapa amani wao. Akawajibu hivi'' Mimi stojibu swalil enu ,ila ntawatolea mfano muamue wenyewe wa riziki moja halali ,akasema nendeni jangwani (akimaanisha ardhi asiyomiliki mtu) kisha usiwe umepaka mafuta mdomo (akimaanisha mafuta yaweza kuwa hujayapata kihalali) panua mdomo kuelekeza juu na nyoosha ulimi subiri hadi mvua inyeshe ( Jangwani mvua hunyesha baada ya miaka 40 ) ,Kisha lile tone litakalo tua ulimini fumba mdomo meza ,utakuwa umekula riziki halali.
 
Back
Top Bottom