Utafiti: Wanawake hawapendi pesa

tpaul

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2008
Posts
27,664
Reaction score
29,054
Sitaki kuwapotezea muda kwa maelezo marefu. Kila kitu kiko wazi. Tafiti za mahusiano zilizofanywa na wataalamu wa mahusiano zinaonyesha wanawake wengi hawatazami ukubwa wa pochi, bali ukubwa wa muda unaotolewa . Wengi wanasema pesa sio shida bali umakini na mawasiliano ya kweli ndivyo vinavyogusa moyo zaidi.
Wanaume wengi wamezoea kudhani kutoa hela ni ishara ya upendo, kumbe wengine wanachohitaji ni muda wako tu.

MAONI YANGU
Afadhali sasa ule uwongo uliodumu kwa muda mrefu kuhusu wanawake kupenda pesa sasa umepata ufumbuzi. Kuanzia sasa wanaume wanapaswa kutambua kuwa pesa si chochote si lolote katika mahusiano. Mwanamke anahitaji muda wako tu.

Utafiti huu umekuja wakati muafaka kwani wanaume tulishatumia pesa nyingi sana katika mapenzi pasipo kujua. Kwa kuwa sasa ukweli umejulikana, hii ni ahueni kubwa sana kwa wanaume waliokuwa wanadhani wanawake wanapenda fedha kumbe si kweli. Hadi wanawake wanaitwa "gold diggers" pasipo kujua kwamba hawapendi pesa bali wanahitaji muda tu!

Pongezi za kipekee ziwaendee watafiti waliogundua hili jambo mapema kabla mifuko ya wanaume haijatoboka zaidi. Mungu awabariki sana.
​
 
Pesa sio kila kitu kwa Mwanamke... upendo,heshima, na kumpelekea tomo
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…