Utafiti: Ndoa nyingi zimeshakufa ingawa watu bado wanaishi kama mke na Mume

Mkuu kumbuka hao wadada wa kazi watakuwa ni wamama wa nyumbani tu, hawawasaidii kutafuta pesa wala kuhudumia familia, watakuwa wanawategemea waume zao kiuchumi

Mimi nazungumzia wale wanawake ambao, mnataka wawasaidie kutafuta pesa na kuhudumia familia, na bado mnataka wafanye majukumu ya nyumbani kama wadada wa kazi hilo ni gumu sana

Hoja yangu ni kwamba lazima mchague kimoja mpoteze kimoja hamuwezi kupata vyote, ni either uoe mama wa nyumbani ambaye atafanya majukumu ya nyumbani ila atakuwa tegemezi kwako kiuchumi, au uoe mfanyakazi au mfanyabiashara ambaye hatafanya majukumu ya nyumbani lakini atakusaidia kuhudumia familia na hatakuwa tegemezi kwako kiuchumi
Uzuri kuna wanawake wanaofanya vyote bila kelele.
 
Nitandika Kwa kifupi najuwa mmu watu hawapendi magazeti.

Wazungu unafki huu hawaiwezi, kuishi na mtu eti kisa mna watoto lakini upendo umekufa.

Mi ni mtu wa society Kwa utafiti wangu wa miaka isiyopunguwa 10 nimegunduwa ndoa si kitu muhimu tena Kwa jamii ya Kitanzania, anayebisha hili shauri yake.

Ndoa za Watanzania wengi ni Sawa na Jehenamu kunyimana unyumba na tafrani zote.

Siku nilikuwa mediator ingawa sipendi kabisa kusuruhisha matatizo ya ndoa, findings zangu na ushauri wangu ni huu.

1. Kuoa au kuolewa siyo Jambo la lazima zingatia hili, Mimi nina ndoa lakini sikushauri kuingia kwenye ndoa kama hujui ndoa ni nini.

2. Kuna swala la ulevi Kwa ujumla, hili nimeona linaleta shida Sana kwenye ndoa, wote mmekutana kwenye pombe baadaye unamkataza mwenza wako asinywe pombe, jitafakari Sana hapo.

3. Hili ni tatizo, linawahusu wanawake wote, kumekuwa na tabia ya wanawake kutaka kuwarusha stage za ujuwaji waume zao, kumbe binadamu NI lazima apite hizo stage ili ajuwe mema na mabaya.

Kijana wa miaka 28 mpaka 40 unataka Aishi kama mtu wa miaka 50 kisa amekuwa wewe dada Hilo haiwezekani na likiwezekana elewa umetolewa na zezeta

Solution: Kwenye kupata wenzake , kila mtu ajitahidi kupata choice na quality zake, ukitaka mcha Mungu tegesha makanisani huko nako si kwamba Wana ucha Mungu wowote.

Point hapa vile umemkuta mwenzao wako bila kuangalia tako au uhandsome wake au pesa zake, elewa hivyo ndivyo alivyo usitalajie kwamba wewe utambadirisha, shida kubwa ya ndoa nyingi kuwa ICU ukichunguza Kwa makini utagunduwa tu kuna mwanandia mmoja anaamini yeye ndio mwenye akili mwenzake Hana akili.

Tutaendelea kwenye comment sess
 
Kuna watu wanatumika kama agent wa shetani kuwatisha watu kuhusu ndoa,acheni watu waoe. Tatizo siku hizi ndoa zinazungumzwa vijiweni kama Simba na Yanga which is not right. Kuna proper ways za kudeal na changamoto za ndoa ambazo wazee wetu walizitumia na maisha yakasonga.
 
Siyo ndoa za mikataba tu, Bali Kile kiapo kiandikwe upya.

Kiapo cha ndoa kinasema utamvumilia katika shida na Raha na maradhi, lakini jinsia ya Ke wengi wao kiapo hiki wamekariri kipengele cha wakati wa raha tu.

Kuna Jamaa yangu mmoja ilibidi Mimi niingilie Kati nimwambie mke wake ukweli Jamaa Hana pesa, kuna pesa anaidai kwangu ziko kwenye process ya kulipwa.

Imagine kuna mwanamke hataki kusikia lugha ya kumwambia wiki hii mipango yangu kipesa haiko Sawa kama Una akiba okowa jahazi nyumbani, sasa kuna haja gani ya kuwa na ndoa hapo? Ndoa ya upande mmoja?
Ulishawah jiuliza kwanini mwanaume anatakiwa aishi na mwanamke kwa akili ungejua hili hata hii thread usingeandika

Nikukumbushe matamanio ya wanadamu wengi ni kutaka kuishi kwenye comfortzone nawakati kihualisia haiko hivvyo
 
Bado sijaoa.

Lkn natamani na naweka mipango. Mwanamke ashiriki kwenye shughuri za familia za kujenge uchumi.

Aajiriwe kwenye shuguri za familia na alipwe mshahara.

Nje ya hapo. Ni kutafutiana lawama tu. Mara mke wa mtu yuko NMB ana safari ya kikazi mkoa x Week nzima not with me.
 
Huyo anaedhani eti wadada wa kazi watakuwa wake bora a ajidanganya. Hapo walipo wapo kazini wanatekelezq majukumu yao, ni kama wewe tu unavyoheshimu kazi yako. Akishaolewa anakuwa mke na anaweza hata asifanye hayo majukumu unayoyasema. Nina mifano ya wadada wa kazi , wameolewa na ni mama wa nyumbani lakini nao pia wamewekewa wadada. Uhalisia ni tofauti.
 
Sema Ndoa yako ndiyo iliyo kushinda, Ndoa nyingi kivipi wewe umefanya tafiti wapi, leta data hapa zinazo onyesha juu ya unacho kisema. Wewe sema ndoa yako imekushinda tujue cha kukusaidia au kukushauri.

Changamoto za hapa na pale hazikosekani shida ni kuendekeza mfumo dume, mwanaume una taka kuwa juu kwa msemo wa Mwanaume akosei na Mwanamke hataki kujishusha kumsikiliza mume nini anasema maana amesha ambiwa Mwanamke bila hata mwanaume anaweza, sasa hapa ndoa itawezekana vipi.

Mzee kama una endekeza mfumo dume kwenye ndoa yako karne hii ya 21 utakula za Uso kwenye kila ndoa unayo ingia we Kilaza.

Na kama utajitetea hupo kwenye ndoa jibu kwanini haupo kwenye ndoa, watu tupo kwenye ndoa na maisha yanaenda japo kabla ya kuingia kwenye ndoa nilisha kutana na watu wengi kama wewe wanaosema ndoa mbaya mara ndoa ndoano.

Watu wapo busy kuogopesha watu kuingia kwenye ndoa ila wao wapo kwenye ndoa na kutoka hawataki.

Kama mliokotana barabarani mkuu pambana sana.

Ndoa ni tamu zaidi ya sanaaa kama hamku okotana.

Hope ume nielewa mzee.
Umemfokea mno aise
 
Back
Top Bottom