Drama ya Mapenzi: Kaka Anayekopesha kwa Riba na Tamaa za mke mchepukaji zasababisha ndoa kuvunjika na mauti

Hanifer Mjanja

JF-Expert Member
Dec 10, 2019
216
327
Kuna kaka (baba) mmoja anakopesha kwa riba, akawa ana date dada mmoja mke wa mtu.... Yule dada na mumewe wakapata dharura, akashauri mumewe wakope pesa kwa mchepuko (mumewe hajui kama mkopeshaji ana date na mkewe) wakaweka nyumba yao kama dhamana.

Penzi likanoga, mume akimpa mke marejesho akabidhi mke anakula akijua baby wangu(mchepukowe) hana noma... Kaka mkopeshaji yeye ana count tu deni na riba inaongezeka, alimuuliza yule dada vipi mumeo mbona pesa hakipi anamwambia baby bhana tuna hili na lile pesa nitakupa mimi.

Kumbe marejesho anapewa ananunua vipodozi na nguo nzuri apendeze kwa mchepuko mkopeshaji...

Kikichokuja kutokea...

Kaka mkopeshaji anakoishi sasa ndio ile nyumba ambayo dada na mumewe waliweka dhamana...
Ilibidi aibinafsishe maana deni na riba ilikuwa kubwa ikashindikna kulipwa. Bibie alijua wako kwenye mapenzi pesa halipi kaka yeye biashara yake na mapenzi havina uhusiano.

Ndoa ile iliingia migogoro ikafa, na yule baba hakukawia nae akafariki, yule dada alihama mji... Imebaki historia chungu japo watu huwa wanamlaumu kaka mkopeshaji kuwa hakuwa na utu. Akamlia mkewe na nyumba akabeba.

My take: WANAWAKE TUACHE TAMAA!
 
Kuna kaka (baba) mmoja anakopesha kwa riba, akawa ana date dada mmoja mke wa mtu.... Yule dada na mumewe wakapata dharura, akashauri mumewe wakope pesa kwa mchepuko (mumewe hajui kama mkopeshaji ana date na mkewe) wakaweka nyumba yao kama dhamana.....
Kuna ukweli kuhusu hii stori?

Tokea lini mtu akopeshe kwa riba bila idhini ya serikali?

Ndoa si kitu kibaya , ni nzuri sana katika kuanzisha family unit yenye watoto wenye maadili. Shida ni pale mwanaume unamuoa mwanamke ambaye ni Bed to Bed midfielder bila kuangalia historia yake na wala bila kuchunguza body language au mambo anayofanya.
 
Kuna ukweli kuhusu hii stori?

Tokea lini mtu akopeshe kwa riba bila idhini ya serikali?

Ndoa si kitu kibaya , ni nzuri sana katika kuanzisha family unit yenye watoto wenye maadili. Shida ni pale mwanaume unamuoa mwanamke ambaye ni Bed to Bed midfielder bila kuangalia historia yake na wala bila kuchunguza body language au mambo anayofanya.
Unaishi Uingereza nini? Hilo swali lako umeuliza kama mtu asieishi Tz hii hii. Eti tangia lini mtu akopeshe kwa riba bila idhini ya serikali.
 
Duuh...Mungu atuongoze sue tunaojindaa kuingia kwny maisha ya ndoa...Hali si nzur huko nje....hakuna maneno mazuri yanatoka huko ya kutupa matumaini kwamba angalau ndoa ni jambo zuri...ni vitisho na kuaribiana future tu
Sali sana, muombe Mungu akupe wa kufanana nae. Sasa na wewe usiwe mharibifu, Mungu atasikiliza maombi yako kaka yangu.
 
Back
Top Bottom