Nawaletea hapa nadharia kuu tatu ambazo zitamtupa lowasa nje ya mbio za urais
1. NADHARIA YA KWANZA -JULIUS CAESAR
Huyu alikuwa ni mtawala wa dola la kirumi miaka mingi hata kabla ya Kristu, Mtawala aliyeheshimika katika dola kubwa kabisa lililopata kuwepo kwenye uso wa dunia. kulikuwa na tetesi kuwa mke wa kaisari alikuwa ametembea nje ya ndoa, habari zikaenea kama nyika katika dola la kaisari, kaisari akaunda tume ya watu weledI wachunguze kama kweli malkia alikuwa anazini nje ya ndoa yake. Tume ikafanya kazi yake pasi shaka, ikathibitisha kuwa ULIKUWA NI UONGO MKUBWA SANA ULIOPIKWA KUMCHAFUA MALKIA, kwa mshangao mkuu, kaisari akamtaliki mkewe, alipoulizwa kwa nini amefanya vile wakati habari zile zilikuwa potofu, akajibu kuwa MKE WA KAISARI HAPASWI HATA KUSINGIZIWA UONGO
MY TAKE: LOWASA ANASEMWA KWA MAMBO MENGI, KUHUSIKA KWAKE NA RICHMOND, UKWASI WA KUTISHA ALIOJILIMBIKIZIA TANGU AKIWA MKURUGENZI WA AICC, WAZIRI , NA WAZIRI MKUU. JULIUS NYERERE ALIWAHI KUONYA KWA HILI. kiti cha urais ni kitakatifu na kitukufu, hakipaswi hata kukaliwa na mtu anayehisiwa kuwa ni mwizi, hata kama zitaundwa tume lukuki kumsafisha. Tanzania ina watu zaidi ya milioni arobaini, haiwezekani akosekane kiongozi mmoja kwa mfano wa kaisari, haiwezekani nchi nzima imekosa kiongozi mweledi na kukimbilia wanaojisafisha bila kutakata.
Nadharia ya pili. -wanafilosofia wa zamani walikuwa ni watu wasiopenda kutawala, kinyume na wanasiasa, lakini wanafilosofia hawa walikuwa watawala wazuri, ukiwalazimisha kutawala watatawala kwa muda mfupi na kipindi chao cha utawala kikiisha wanataka haraka kurudi tena kwenye filosofia, tofauti yao na wanasiasa wa siku hizi wanapenda kutawala na wanapotawala wanakuwa dhaifu na ni viongozi wabovu, hivyo hata baada ya kipindi chao kupita bado wanaganda hawataki kuachia kutawala.
My take: lowasa ni mwanasiasa anayependa mno madaaraka, anapenda kutawala potelea mbali hata kama hana sifa za kutawala, ndo maana anatumia pesa, ulaghai , kuchafuana ili atawale, kipindi chake kikiisha anaweza kubadilisha katiba ili aendelee kutawala. Tanzania nchi iliyojaliwa rasilimali nyingi miaka ya karibuni, ni lazima tumtafute mwanafilosofia tumlazimisha awe rais hata kama hataki, atufanyie mambo makubwa hata anapomaliza muda wake tutamani aendelee lakini akatae na kurudi kwenye filosofia