Utabiri kwa kutumia karata za tarot

Utabiri kwa kutumia karata za tarot

Inawezekana kwakuwa muda mwingi niko barabarani na natembelea sehemu nyingi kuna nini kwani?

Kuna siku nilikuhisi kuwa ni mshana jr. Wa jf pale msikitini kuna kijana mmoja hv mlikuwa mkibishana kuhusu kufa kwa yesu/issa yeye anasema hakufa...wewe unasema alikufa kwa kuwa kuna andiko linasema "kila nafsi itaonja mauti". ( samahani lakini kama hukuwa wewe).
 
Usijali hapana sio mimi huwa najiepusha sana na malumbano ya namna hiyo
 
970bdc05c4b944a65ed1bce2757881d3.jpg

Mmhh Mshana nimekutana na hii kitu katika pitapita zangu huko mtaani.

Na hii pia
f772876627b160ae7cc48ec2f46c3247.jpg

Mmhh....
 
Sasa wanakutabiria vipi wakati hata jina lako hauandiki zaidi ya kubofya karata sita then majibu yanakuja, eti mkuu mshana jr
Challenging question. ...ukiisoma sana tarrot unaona kama kuna connection kati ya wewe na yenyewe kupitia kidole chako lakini pia ni kama ushetani fulani hivi au katika hali ya kawaida ni basic assumptions tuu
 
Hebu naomba unieleweshe pale nilipopotosha kuhusu tarot nami nitaomba radhi...hii elimu ni pana sana na nilichoandika hapo ni kidogo sana na kuthibitisha andiko langu nimesema wazi anayetaka aingie mtandaoni akajionee mwenyewe
Kama kuna wengine waliandika ni sahihi pia wala siwezi kupinga lakini kunishutumu bila kuweka ithibati hujatenda haki...vema ukawa highlight huko ulikoona nimepotosha kwa njia hii tutakuwa na mjadala wenye tija
Karibu....!
Usimshawishi mtu yeyote kujaribu tarot kama unaamini ubaya wake, pengine hujajua vizuri ubaya wa jambo lolote la kubashiri.
 
Doh mshana kwa kujibu kiistaarubu nakupa 100%
 
Umesahau na utabiri kwa kutumia wanyama,wadudu na ndege wa porini na majumbani, bila kusahau utabiri kwa kutumia mayai ya kuku na utabiri kwa kutumia waoto wadogo.

4596d32d9940a23a62efc6c12f5c25f5.jpg

Binadamu pamoja na maarifa yake yote kashindwa kujua kitu kimoja!...kesho yake si waamini Mungu, miungu wala wapagani si wanazuoni mahiri wala wanasayansi waliobobea wote maarifa yao yamegota kwenye leo na sasa hivi zaidi ya hapo ni upofu na giza.

Hali hii imesababisha kutokea kwa elimu ya utabiri na unajimu kwamba wewe kesho yako itakuwa hivi au vile

Hii elimu ni pana na kongwe sana na imegawanyika katika makundi haya;

-kwa kutumia nyota
-kwa kutumia viganja vya mikono
-kwa kutumia majira ya mwaka, miezi na tarehe za kuzaliwa
-kwa kutumia herufi na majina
-Na kutumia hii ya karata za tarot

Katika zote hizo ni hii ya kutumia karata za tarot ambayo hutoa majibu ya uhakika na uhalisia zaidi na uchezaji wake ni rahisi Tarot yaweza kuwa ndio elimu ya utabiri na unajimu kongwe zaidi duniani ikiwa na zaidi ya miaka 500

Kwenye kusoma karata za tarot huwa kuna mafungu yaani karata tatu sita tisa kumi na mbili na kuendelea lakini iliyo maarufu ni tatu na sita ni katika uchezaji huo karata utakazochagua ukija kulinganisha majibu yake na ukafananisha na mambo yako utapata majibu ya kushangaza mno

Hebu jaribu kuingia kwenye mtandao sasa ugonge tarot card reading halafu utaniambia...na baada ya hapo hutahangaika tena na tabiri zingine zisizotoa majibu ya uhakika!!! jaribu sasa

1f271d86b99111e0cecf1a397398dcbe.jpg
 
Umesahau na utabiri kwa kutumia wanyama,wadudu na ndege wa porini na majumbani, bila kusahau utabiri kwa kutumia mayai ya kuku na utabiri kwa kutumia waoto wadogo.
Duu nitalitafiti hili na nitakuconsult nitakapokwama
 
Usimshawishi mtu yeyote kujaribu tarot kama unaamini ubaya wake, pengine hujajua vizuri ubaya wa jambo lolote la kubashiri.
fazili nini maana ya JF kuitwa jukwaa la Great thinkers? Hapa tunaandika maarifa uzoefu na majadiliano....hapa hakuna ushawishi naamini kila mmoja wetu hapa ni mtu mzima anayeweza kuchambua na kuchanganya mambo
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom