Utabiri kwa kutumia karata za tarot

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,633
697,529
4596d32d9940a23a62efc6c12f5c25f5.jpg

Binadamu pamoja na maarifa yake yote kashindwa kujua kitu kimoja!...kesho yake si waamini Mungu, miungu wala wapagani si wanazuoni mahiri wala wanasayansi waliobobea wote maarifa yao yamegota kwenye leo na sasa hivi zaidi ya hapo ni upofu na giza.

Hali hii imesababisha kutokea kwa elimu ya utabiri na unajimu kwamba wewe kesho yako itakuwa hivi au vile

Hii elimu ni pana na kongwe sana na imegawanyika katika makundi haya;

-kwa kutumia nyota
-kwa kutumia viganja vya mikono
-kwa kutumia majira ya mwaka, miezi na tarehe za kuzaliwa
-kwa kutumia herufi na majina
-Na kutumia hii ya karata za tarot

Katika zote hizo ni hii ya kutumia karata za tarot ambayo hutoa majibu ya uhakika na uhalisia zaidi na uchezaji wake ni rahisi Tarot yaweza kuwa ndio elimu ya utabiri na unajimu kongwe zaidi duniani ikiwa na zaidi ya miaka 500

Kwenye kusoma karata za tarot huwa kuna mafungu yaani karata tatu sita tisa kumi na mbili na kuendelea lakini iliyo maarufu ni tatu na sita ni katika uchezaji huo karata utakazochagua ukija kulinganisha majibu yake na ukafananisha na mambo yako utapata majibu ya kushangaza mno

Hebu jaribu kuingia kwenye mtandao sasa ugonge tarot card reading halafu utaniambia...na baada ya hapo hutahangaika tena na tabiri zingine zisizotoa majibu ya uhakika!!! jaribu sasa

1f271d86b99111e0cecf1a397398dcbe.jpg
 
7f96859ee0d6f6b7ace3c68e600f9932.jpg

Sina hakika sana na haya mambo ingawa wengi waliniambia nina nyota Kali enzi nipo gizani miaka hiyo kabla sijaiona nuru...
Lakini je kuna uhalisia kwenye hilo? Na je vipi ulipocheki na karata ya tarot?
 
Lakini je kuna uhalisia kwenye hilo? Na je vipi ulipocheki na karata ya tarot?
Kiaina inaendana, kuna miaka nilikuwa nafatilia sana nyota na kwakuwa nimezaliwa nyota ya ng'e nikawa mfuatiliaji mzuri...kinachonitatiza kwenye haya mambo tangu nipo gizani mpaka leo kila ninachokisoma kuhusu Mimi ni cha kweli yaani kilishawahi tokea au kitatokea...pia sikuwa nikiamini Alama ya M kiganjani na ninayo mikono yote na kila kilichoandikwa kuhusu alama hizo inarandana namie
 
Kuwa makini sana wewe ni malighafi moja muhimu sana kwenye mambo ya kiza
 
mshana jr nakuomba sana, kama hujui undani kitu usikilete jukwaani. MziziMkavu kuna kipindi alileta elimu kuhusu numerology, kwa kuwa mimi huwa sipendi kupinga kitu bila kujiridhisha, nikaamua kuifuatilia, na bahati nzuri nikampata mbashiri ambaye anatumia tarot card, pia ni physic, anatumia numerology, horoscope, nilichogundua sasa. Yawezekana lengo lako ni zuri tu kwamba kutoa elimu juu ya mambo mbalimbali, lakini kuwa makini sana, kwa elimu hizo unaweza kuta siku moja unaulizwa kwa nini ulipotosha watu.
 
Hebu naomba unieleweshe pale nilipopotosha kuhusu tarot nami nitaomba radhi...hii elimu ni pana sana na nilichoandika hapo ni kidogo sana na kuthibitisha andiko langu nimesema wazi anayetaka aingie mtandaoni akajionee mwenyewe
Kama kuna wengine waliandika ni sahihi pia wala siwezi kupinga lakini kunishutumu bila kuweka ithibati hujatenda haki...vema ukawa highlight huko ulikoona nimepotosha kwa njia hii tutakuwa na mjadala wenye tija
Karibu....!
 
4596d32d9940a23a62efc6c12f5c25f5.jpg
Binadamu pamoja na maarifa yake yote kashindwa kujua kitu kimoja!...kesho yake si waamini Mungu, miungu wala wapagani si wanazuoni mahiri wala wanasayansi waliobobea...wote maarifa yao yamegota kwenye leo na sasa hivi zaidi ya hapo ni upofu na giza
Hali hii imesababisha kutokea kwa elimu ya utabiri na unajimu kwamba wewe kesho yako itakuwa hivi au vile
Hii elimu ni pana na kongwe sana na imegawanyika katika makundi haya
-kwa kutumia nyota
-kwa kutumia viganja vya mikono
-kwa kutumia majira ya mwaka, miezi na tarehe za kuzaliwa
-kwa kutumia herufi na majina
Na kutumia hii ya karata za tarot
Katika zote hizo ni hii ya kutumia karata za tarot ambayo hutoa majibu ya uhakika na uhalisia zaidi na uchezaji wake ni rahisi
Tarot yaweza kuwa ndio elimu ya utabiri na unajimu kongwe zaidi duniani ikiwa na zaidi ya miaka 500
Kwenye kusoma karata za tarot huwa kuna mafungu... yaani karata tatu sita tisa kumi na mbili na kuendelea lakini iliyo maarufu ni tatu na sita..ni katika uchezaji huo karata utakazochagua ukija kulinganisha majibu yake na ukafananisha na mambo yako utapata majibu ya kushangaza mno
Hebu jaribu kuingia kwenye mtandao sasa ugonge tarot card reading halafu utaniambia...na baada ya hapo hutahangaika tena na tabiri zingine zisizotoa majibu ya uhakika!!! jaribu sasa
1f271d86b99111e0cecf1a397398dcbe.jpg
Huishiwi nondo mshana jr! Big up
 
Watu wanaotafuta bahati wanaweza kushauriwa vibaya na mganga ukajikuta unapata ulemavu kwa kukatwa kiungo au hata kupoteza maisha
LAKINI pia imani za kishetani na freemason wakikugundua watafanya kila jitihada wakuvutie kwako
Utasikia wengine wanaomba connection ya kujiunga na free Mason
 
mshana jr sikumaanisha kwamba maelezo yako ni batili, nilichokusudia kueleza ni kwamba tarot card iko kinyume na mpango wa Mungu. Kwa hivyo hiyo tuseme inawahusu wasio muamini Mungu. Mungu anasema, tusijisumbue kuhusu kesho, tuiache ijisumbukie yenyewe tu. Ni kweli hiyo kitu ipo, na ina maandiko mengi tu kuielezea, lakini iko kinyume na Mungu.
 
Back
Top Bottom