Ustawi wa soko katika siku za mapumziko wathibitisha ufufukaji wa Uchumi wa China

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,036
VCG11421866990.jpg
Katika siku nane za mapumziko ya Siku ya Taifa la China, watu wameshuhudia ustawi wa soko, kwani mamilioni ya watu wamefanya utalii, na wateja walijaa kwenye maduka na mikahawa. Kuongezeka kwa shauku ya watumiaji kwa mara nyingine tena inaonyesha uthabiti mkubwa na uhai wa uchumi wa China, hivyo kuthibitisha tena kuwa uchumi wa China unafufuka vizuri.

Wachina wanaita siku za mapumziko kutokana na Siku ya Taifa ya kila mwaka kama “Wiki ya Dhahabu”. Kwani katika siku hizo, watu hufanya utalii, pamoja na mambo mengine mengi ya kujifurahisha ambayo hawana nafasi ya kufanya katika siku za kawaida.

Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Wizara ya Utamaduni na Utalii ya China, katika siku hizo nane, zaidi ya Wachina milioni 826 walifanya utalii wa ndani, na pato la utalii nchini China lilifikia zaidi ya Renminbi yuan bilioni 753, sawa na zaidi ya dola bilioni 100 za Kimarekani. Licha ya miji maarufu ya kiutalii, ikiwemo Beijing, Shanghai na Xi’an, miji midogo na yenye ukubwa wa kati pia imewavutia watalii wengi.

Wakati huohuo, Wachina wengi pia wametalii katika nchi za nje. Shirika la Televisheni la Marekani CNBC liliripoti kwamba katika “Wiki ya Dhahabu” ya China, idadi ya watalii wa China katika nchi za nje imeongezeka kwa kiasi kikubwa. Ili kuvutia watalii wa China, nchi nyingi zimejiandaa mapema.

Korea Kusini ilitoa “Mpango wa Kuvutia Watalii wa China” na kutangaza kwamba itaondoa ada za kuomba visa ya kielektroniki.

Mamlaka ya Utalii ya Australia ilifanya hafla ya kukaribisha kikundi cha kwanza cha watalii cha China kuwasili nchini humo wakati wa “Wiki ya Dhahabu”. Mkuu wa Ofisi ya Mamlaka ya Utalii ya Saudi Arabia eneo la Asia Pacific Dai Hansen amesema nchi hiyo inajitahidi kuwa moja ya nchi yenye watalii wengi zaidi wa China duniani.

Mikahawa ni sehemu nyingine inayowavutia zaidi Wachina wakati wa “Wiki ya Dhahabu”. Takwimu zinaonesha katika siku hizo za mapumziko, matumizi ya kula mikahawani nchini China yaliongezeka kwa asilimia 254 ikilinganishwa na mwaka 2019 kipindi kama hiki, na hata miji mingi imewavutia watalii kutokana na chakula chao maalum.

Kutazama filamu pia kumechaguliwa na Wachina wakati wa “Wiki ya Dhahabu”. Takwimu zinaonesha kuwa katika siku hizo, jumla ya pato la tiketi za filamu nchini China ilifikia bilioni 2.734, ambalo ni ongezeko la asilimia 83 ikilinganishwa na mwaka jana kipindi kama hicho.

Kutokana na Michezo ya Asia iliyofanyika huko Hangzhou, China, matumizi ya Wachina katika michezo pia yameongezeka kwa kiasi kikubwa katika kipindi cha “Wiki ya Dhahabu”.

“Wiki ya Dhahabu” ni dirisha la kutazama uchumi wa China. Ustawi wa soko katika kipindi hicho cha mwaka huu unaonesha kuwa uchumi wa China na unafufuka vizuri, na Wachina wana imani kubwa kuhusu maisha ya siku za baadaye.
 
Back
Top Bottom