Ustaarabu, Makazi, Maendeleo na Maisha ya watanzania na watawala (machifu na watemi)

John-Q

JF-Expert Member
Oct 4, 2016
643
957
england.jpg

England United Kingdom
Dresdane German.jpg

Dresdane German

Habari wanajamvi natumai mu wazima wa afya.

Binafsi napenda utalii hasa utalii wa kihistoria kujua watu wa zamani na jamii zao waliishi vipi makazi, siasa, shughuli za kiuchumi nk.

Tukija sehemu yangu pendwa ya makazi navutiwa sana na architects, ukiangalia picha hizo juu ya Dresdane German (my favourite place on earth) na England United Kingdom hiyo miji na majengo yake yanawastan wa umri usipungua miaka 300, ukarabati wa miundo mbinu huwa unafanyika mara kwa mara ili ku accomodate jamii husik na zijazo.

Swali ambalo linanifikirisha kila siku na sijapata majibu sahihi, kwa wastani wa miaka hiyo 300 watanzania tulikua tunaishi vipi, ukiangalia miji yetu hasa hii mikubwa hauoni majengo yenye umri huo, na ukikuta majengo yenye historia ambayo wastan yana umri usiozidi miaka 150 basi yanahusishwa na ukoloni na wakoloni yaani walijenga wao mf. misikiti, makanisa, majengo ya utawala kama bomani, ikulu, magereza nk.

Swali langu, tulikua na machifu na watemi, walikua wanakaa wapi yaani Kingdoms zao ziko wapi, majengo yao walikua wanajenga vipi tu. Ni kwamba hatukua na teknolojia ya kujenga majengo yenye kubaki mpaka sasa ama mfumo wetu wa maisha wa kijamaa sana kwamba hauna tofauti za kimakazi.

Ilitegemewa kwa jiji kama DSM, ukute old DSM iliyojengwa na wazawa ambayo ni still standing na watoto wa kizazi kipya na watalii wa nje na ndani wanatembea kuangalia na kujifunza zaidi utatembelea na kuona majengo yaliojengwa na wakoloni kidogo na wahamiaji wa kihindi waliojenga nyumba zao miaka ya 1920s to 1950s.

Naomba kuuliza, wakati Dresdane, England, Greece, Turkey, Paris, St. Peters berg, Venice, Rome, Milan zinajengwa sisi huku tulikua tunaishi vipi na wageni (wakoloni) wasingekuja miji yetu ingekuaje mpaka sasa?
 
Back
Top Bottom