Uso kwa uso na MwanaJF ndani ya Internet Cafe!!

Katavi

Platinum Member
Aug 31, 2009
41,983
12,701
Leo nilikuwa na mizunguko mjini, na nilikuwa na kazi iliyohitaji niifanyie ndani ya internet cafe. Baada ya kumaliza kazi ile ilibidi niingie JF kujua nini kimejiri. Kwa kuwa internet cafe ile haikuwa na privacy jamaa aliyekuwa kompyuta ya jirani alikuwa akifuatilia nilichokuwa nafanya. Baada ya kulog in, alionekana kushangaa sana.........

"Wewe ndio Katavi"?? Mbona kijana sana", kabla sijaendeleza mazungumzo TANESCO wakachukua chao, nikasepa bila ya kuondeleza mazungumzo, sijui ni nani yule!!!
 
Kwa hyo nanyie mechanism yenu ya kuongea ilikuwa inafanywa na umeme au!!?
 
Katavi umenichekesha, sasa umeme ulikuzuia nini kumjibu? Yeye mzee sana?
 
Leo nilikuwa na mizunguko mjini, na nilikuwa na kazi iliyohitaji niifanyie ndani ya internet cafe. Baada ya kumaliza kazi ile ilibidi niingie JF kujua nini kimejiri. Kwa kuwa internet cafe ile haikuwa na privacy jamaa aliyekuwa kompyuta ya jirani alikuwa akifuatilia nilichokuwa nafanya. Baada ya kulog in, alionekana kushangaa sana.........
"Wewe ndio Katavi"?? Mbona kijana sana", kabla sijaendeleza mazungumzo TANESCO wakachukua chao, nikasepa bila ya kuondeleza mazungumzo, sijui ni nani yule!!!

Nimekuona, unafanana na avatar yako. Ha ha haaa!
 
You are very lucky.

Kanunue ticket ya bahati nasibu na ujuwe una uhakika wa kujinyakulia zawadi nono. Lady luck is smiling at you.
 
Katavi umenichekesha, sasa umeme ulikuzuia nini kumjibu? Yeye mzee sana?
Sio kuwa umeme ulinizuia ila dah!! Yule jamaa alivyoshangaa hadi watu wote wakageuka kuangalia. Umeme ulipokatika aligeuka kidogo nami nikatumia upenyo huo kuondoka...
 
Labda kilichomshangaza ni huo ujana wako lol... Jamaa alidhani Katavi ni kibabuuu!
 
Back
Top Bottom