Mtokambali
JF-Expert Member
- Nov 1, 2010
- 222
- 99
Jamani wadau,nafurahi kuwaarifu kuwa juzi mchana nikiwa kwenye daladala ya kutoka Mbezi kwenda Posta maeneo ya tiptop Manzese nilibahatika kushuhudia member mmoja wa JF akifungua ukurasa wake kwenye simu. Yaani jina lake na sura yake ni vitu viwili tofauti kabisa,utashangaa humu ndani anasound kama mwanaume mzee wa makamo kumbe dada mdogo tu....nilikuwa nimesimama nimeshika bomba wakati yeye anasurf na Blackberry yake kakaa kwenye siti,nimetupia jicho sikuamini kama huyo ndiye.....!!!! Be careful humu ndani,unaweza kuwa unachati na babu mzee ukidhani ni binti mrembo. Ni hayo tu.