Matatizo mengine ni ya watu wenye hali fulani na economic status fulani za kuwa na magari, sisi wa TZ 11, hayo hayatukuti tena hizo patrol, zinafanywa kwenye fukwe waendazo wenye magari, sisi watu wa madogo kuporomoka kama kwetu Shimo la Udogo, fukwe zetu ni Mtoni Kijichi, huko hakuna patrol ya aina yoyote, mkienda beach na mwezio, kigiza kikianza tuu kuingia watoto wanarudi nyumbani, wakubwa wanabaki ufukweni hadi kujivinjari kwa raha zenu.
Ndio maana mitaa ya uswahilini sana hata guest hakuna!, guest za nini wakati viambaza tuu vinatosha?!.
Utajiri raha lakini pia ni shida na umasikini ni shida ila pia kuna raha zake!.
Pasco