Usiyoyajua kuhusu Coco Beach!

Miaka kadhaa iliyopita nilikuwa mdau wa kutembelea fukwe zetu zilizopo Dar na kwingine upepo unakovuma.story ya leo itagusa matukio ya COCO BEACH!
Tukio la kwanza nimeende Coco na mwenza wangu kula upepo wa bahari yetu ya hindi.nimepark gari.ilikuwa mida ya saa kumi na mbili na nusu,kigiza kinaanza.tukashuka na kwenda pembezoni mwa bahari kuyakaribia maji chumvi. kulikuwa na wadau wengine wanatamalaki hapo pia.

kama kawaida ya wapendanao tulikuwa zero distance busu kwa mbali.tukaamua tukae pembezoni kwenye mawe tukipiga stori za hapa na pale,mara akaja askari hana uniform kajitambulisha na kudai kitendo chetu cha kukaa kwa kukaribiana na kukiss kando ya bahari ni kufanya mapenzi hadharani, nikauliza kivipi? hakuna aliyevua nguo hapo wala kumshika mwenzie.ikawa tumezua zogo.nikamaliza ile tafrani na yule askari.

Tukio la pili nilienda Coco safari nyingine niliamua sasa nikae kwenye gari na mwenza wangu.kosa nililofanya sikufunga milango ya gari.kuna vijana huwa wanapitisha biashara zao pembeni ya gari kama gari ni tinted bado wanapita mbele ya gari na kuchungulia watu walioko kwenye gari kujua kama ni wapenzi na kama mmezama kwenye mahaba hata kama hamfanyi ngono kwenye gari wanaenda kutoa taarifa kwa maaskari.ambao wanakuja kuwakamata na kuwabambikia kesi! siku hiyo walifungua gari na kudai tuna kiss karibu na eneo la waziri mkuu.

pale Coco kuna makazi yake.(sio Majariwa)tukakamatwa mpaka oysterbay kituoni.tulipaki nje askari mmoja aliingia ndani mwingine alibaki nasisi.tulibishana hatimae tukayamaliza.
Mara nyingine ya mwisho tulienda pale Coco beach club.kwenye parking ile nimekaa kidogo wakaja askari watano na siraha zao wanaopatrol kule baharini tukawafungulia milango wakaona hakuna lolote pia tulijibu maswali yao kwa ufasaha na uzoefu wakasepa zao.

kabla hatujaondoka kwakuwa tulikaa kwenye gari mda mrefu tukipiga story na kuagiza tunachotaka na kula kwenye gari wakatokea askari wengine wawili wenye uniform tofauti na wa mwanzo wakawa wanapiga mahesabu ya kutuzingira na kufungua milango ya gari na kushtukiza kama kuna chochote kinafanyika.niliona mchezo mzima kwenye site/driving mirror.mmoja alianza kutambaa(craw) kulijia gari letu.

kwakuwa mda wote nikiwa kwenye gari huwa nakuwa makini na linakuwa limewashwa.nikaliondoa kwa kasi.sijawahi rudi tena kule labda nikiwa na hamu ya mishikaki ya Samaki kwa kipara ndio naenda na kuacha gari mbali na nikiwa peke yangu.

Fundisho ukiwa na gari popote lock milango yake pia elewa ukiwa COCO Beach na mwenza chukua tahadhali vinginevyo unaweza kugeuzwa mradi na polisi wetu.pia usiwaamini wale wauza biashara wanaokujia kwenye gari au pale ulipo kaa wanashirika na askari wa kule.

Wish you a lovely long week end,keep your faith in what you believe.
'
Hii hata Agakhan
 
mkuu democracy kila mtu na kitu anachopenda na kwenda unakotaka.mfano kwangu hata kwako sidhani kama unaweza kupata mishikaki ya samaki na ndizi za kuchomwa.au outing ya kawaida.kwanini ukae nyumbani 24/7 that is boring life.

Swali langu ni kwanini ukae ndani ya gari ukiwa Coco Beach kula, kunywa, nk ukiwa ndani ya gari? Hii ni kulingana na maelezo yako.
 
Swali langu ni kwanini ukae ndani ya gari ukiwa Coco Beach kula, kunywa, nk ukiwa ndani ya gari? Hii ni kulingana na maelezo yako.
mkuu naona hujasoma post vizuri ukaelewa.nimese mara ya kwanza nilikamatwa nje ya gari.sasa unataka nikae nje tena nikamatwe kirahisi.naenda kule kuna vitu nategemea kupata (food stuffs ) pia kuona scene tofauti na nyumbani.
 
Ukitaka utulivu nenda beach za kulipia tu mi nilipigwa roba kunduch beach nikiwa na demu wangu simu,walet vyote vilisepa
 
Asante hata hivyo kwa kunipa taarifa siku nikienda pale lazima nijikoki tayari kwa fujo bila uoga maana huwa sipendi uonevu was kijinga.
poua mkuu.tunashare experience.kama mtu na Dada yake kakamatwa kisa wako.beach kwenye gari na kupakaziwa wanafanya ngono ni uonevu wa hali ya juu.
 
Mimi niko hapa coco beach, gari full tinted sijaizima nusu saa sasa niko na mrembo! Nawasubiri hao wajingawajinga!
 
Nafikir Makonda kashasoma huu uzi na ameuelewa vijana tunavyopata shida na kukaa kwa waswas Coco Beach tutapenda kuona anachukua hatua kwa hao polis njaa
 
Back
Top Bottom