Usiyoyafahamu kuhusu Malawi

Usiyoyafahamu kuhusu Malawi

Malawi ni nchi isiyo na bahari iko kusini mwanTanzania. Mpaka 2006 wananchi wa Malawi hawakuhitaji visa kuingia Uingereza. Visa ilianza baada ya Wanigeria wengi kuingia Uingereza kwa passport za Malawi.

Kuna Hospital Lilogwe ambayo ni maalum kwa wataalamu wa kigeni na watalii wanaoishi na kutembelea Malawi. Wafanya kazi wa hospital hii baada ya kufanya kazi kwa miaka miwili wana uwezo wa kuomba kazi moja kwa moja katika wizara ya afya ya Uingereza National Health Services.
Wachina wameshafika huko ?
 
Nilipoishi huko 2013, 2014 wizara yao ya elimu iliruhusu wanafunzi wa shule za msingi za vijijini wasome bila kulazimishwa kuvaa sare wala viatu. Zaidi ya nusu ya watoto hao walikuwa wakiwa pekupeku na/au bila sare. Kusingekuwa na ruhusa hiyo watoto wengi wasingesoma.

Sijui iwapo kufika sasa 2018 wazazi wote wa vijijini wanamudu mambo ya sare/viatu kwa watoto wao walio shule?
 
Nilishawahi kuwa huko kikazi kwa muda wa mwaka mmoja na nusu. Nilikuwa Blantyre...nikiishi sehemu inaitwa Namiwawa.
Wamalawi ni wakarimu sana. Nilipendelea sana Samaki aina ya chewa na vyakula vyao kwa ujumla.
Ukikutana na mwanamke wa kiMalawi mzuri anakuwa mzuri kweli kweli. Huwa naenda kutembea kila wakati ninapopata nafasi.

"Ukikutana na mwanamke wa kimalawi mzuri anakuwa mzuri kweli kweli". Tafadhali mkuu fafanua hii kauli yako, kwani ukikutana na mwanamke wa kiTZ mzuri hawi mzuri kikweli kweli??😁😁
 
Wakazi wa kwanza wa Malawi walikuwa wawindaji Wasan.

Katika karne za kwanza BK walifika wahamiaji Wabantu wenye ujuzi wa kilimo na uhunzi.

Hakuna habari za kimaandishi kabla ya kufika kwa Wazungu.

Tangu karne ya 16 ufalme wa Wamaravi ulikuwepo upande wa kusini wa ziwa.

Wamaravi walipanua utawala wao. Lakini katika karne ya 19 walishambuliwa sana na Wayao walio endesha biashara ya watumwa waki wakamata katika eneo la ziwa na kuwa peleka hadi pwani ya Bahari Hindi kama vile Kilwa.

Mwaka 1859 Mwingereza David Livingstone alifika ziwani.

Wamisionari wali mfuata, hasa Wapresbiteri kutoka Uskoti, waliotafuta wafuasi wa Ukristo na kumpambana na wafanyabiashara ya utumwa.

Mwaka 1891 serikali ya Uingereza iliweka nchi upande wa magharibi na kusini kwa ziwa chini ya ulinzi wake ikawa „Nyassaland
Protectorate“, halafu tangu 1907 koloni la Unyasa.

Wakati wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia Waingereza wali ogopa kushambuliwa kutoka Afrika ya Mashariki ya Kijerumani wakachukua hatua za kudai huduma za nyongeza
 
Lugha yao kuu ni kichichewa, ambacho wenye nacho hasa zaidi ni mkoa wa Kati. Ni lugha ambayo pia huzungumzwa Zimbabwe na Zambia.Wachewa wa nchi hizi tatu hufanya matamasha ya Kimila ya pamoja kila baada ya kipindi fulani.

Lugha nyingine kubwa ni kitumbuka cha mkoa wa kaskazini. Watumbuka hawakipendi sana kichichewa, japo kichichewa ni lugha rasmi ya taifa. Enzi nikiwa huko katika mkoa wa kaskazini elimu ya msingi ilikuwa ni kwa kitumbuka na kiingereza!

Kuna makabila mengine madogomadogo.
 
Hii ilisababisha ghasia ya John Chilembwe dhidi ya wakoloni.

Baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia Waingereza waliunganisha
Unyasa na Rhodesia (leo Zambia na Zimbabwe) kuwa Shirikisho la Afrika ya Kati mwaka 1953.

Shirikisho hilo hali kudumu hadi mwisho wa ukoloni kutokana
mielekeo tofautitofauti katika sehemu tatu za shirikisho.

Katika Unyasa daktari Hastings Kamuzu Banda alijitokeza kuwa mwanasiasa aliyependelewa na wananchi wengi, akawa waziri mkuu wakati wa Unyasa kupata madaraka ya kujitawala katika mambo ya ndani na baadaye rais wa kwanza wa taifa.

Mwaka 1964 Unyasa (Nyassaland) ilikuwa nchi huru kabisa lakini bado sehemu ya Jumuiya ya Madola chini ya malkia wa Uingereza kwa miaka miwili ya kwanza.

Mwaka 1966 Banda alitangaza kura ya katiba mpya iliyo pokewa na wananchi.

Nchi ilipata jina la
Malawi na chama cha Malawi Congress Party kikawa chama pekee.

Banda aliendelea kutawala, akatangazwa kuwa rais kwa muda
wote wa maisha yake mwaka 1971.
 
"Ukikutana na mwanamke wa kimalawi mzuri anakuwa mzuri kweli kweli". Tafadhali mkuu fafanua hii kauli yako, kwani ukikutana na mwanamke wa kiTZ mzuri hawi mzuri kikweli kweli??😁😁
Kama umeshafika Zambia,Zimbabwe,Malawi na Msumbiji utanielewa nimemaanisha nini!
Asilimia kubwa ya wanawake wa maeneo hayo wamefanana na babu/baba zao. Ndio maana nikasema ukikutana na mwanamke wa kiMalawi mzuri anakuwa mzuri kweli kweli kwa msisitizo.
 
"A woman beauty is in the eyes of the beholder "
 
Malawi ni nchi isiyo na bahari iko kusini mwanTanzania. Mpaka 2006 wananchi wa Malawi hawakuhitaji visa kuingia Uingereza. Visa ilianza baada ya Wanigeria wengi kuingia Uingereza kwa passport za Malawi.

Kuna Hospital Lilogwe ambayo ni maalum kwa wataalamu wa kigeni na watalii wanaoishi na kutembelea Malawi. Wafanya kazi wa hospital hii baada ya kufanya kazi kwa miaka miwili wana uwezo wa kuomba kazi moja kwa moja katika wizara ya afya ya Uingereza National Health Services.
Yani wanaigeria wanaharibu image ya Africa.. We can't even date wazungu kisa tunaonekana tunatafuta papers wakati watu ni wasomi
 
Back
Top Bottom