Usisomeshe mtoto shule za gharama kwa matarajio kwamba atapata ajira, utaishia kuumia tu

We naweeeeh Kwani lazima wote tulime bustani ili iwejee ujinga mtupu..
Wacheni watu waishi maisha yao na wewe ishi yako ..
Tafuta pesa kaka hizo zote ni dalili za kutokua na pesa acha makasiriko
Sawa mkuu,,
 
We sema huna hela Ndio maneno yanakutoka pole yako...
Ni sawa mtu anakaa masaki na wewe unakaa manzese useme wa masaki anajidai kukaa masaki
Mwenye pesa anaonekana usoni,,si lazima uigize maisha..

Kwani masaki hakuna watu wenye njaa?

Zile nyumba Tu,,kuna watu wanaishi mle na mfukoni hana kitu.
 
Siyo goigoi. Hii ni kanuni ya tajiri atazidi kuwa tajiri na masikini atazidi kuwa tajiri.
Mfano leo mtoto wa Bakhera au Mo aende akasome kayumba? Masikini huwa anaamini ili mtoto akue kimaadili lazima apitie maisha magumu, kulima, kubeba maji kichwani, kulala njaa n.k ila tajiri huwa anaamini ili mtoto akue kimaadili lazima apitie mazingira mazuri, asome shule za gharama, alale sehemu nzuri, afanye kazi nyepesi.
Mtoto wa tajiri akimaliza chuo, baba yake anamfungulia duka la Hardware la kwake, anapewa nyumba na gari wakati mtoto wa masikini yupo mtaani anatembea na bahasha mkononi kutafuta ajira. Akipata mshahara laki 4, cycle ya poverty inarudi pale pale.
Sawa mkuu,,kama mtoto kutokujuwa hata kufagia au kuwa goigoi ni dalili za utajiri basi idadi ya matajiri wataongezeka Tanzania ikifika 2030..
 
Hakika mkuu hiyo ni proved kabisa,,

Shule za private ni biashara.so wanambinu za ufaulu ili wawe hot sokoni..
Nina watoto huko na nimechunguza vitu vingi sana, najua mambo mengi.
Najua tofauti za hizo shule zenyewe, maana kuna za wahindi, zenye standard ya ulaya na USA, za watanzania lakini zimeboreshwa nk.
Najua utofauti wa kayumba na hizi english medium.
Kuna miezi kadhaa mtoto wangu alisoma kayumba, niliongea mengi na walimu wa hiyo shule wakati namhamisha mtoto wangu kumrudisha english medium.

Najua struggle zinazofanyika.
Bahati mimi ni mmoja wa wazazi ambao mtoto akirudi nyumbani likizo ananikuta mimi ni mwalimu mwingine namsubiria.

Kiufupi nina mengi ya kusema kuhusu hizo shule. Ikiwemo viwango vya walimu wanaoajiriwa huko na mishahara yao na treatment zao.

Nina mengi gwa kukaja.
 
Mtoto anatoka nyumbani saa 5 am na kurudi saa 6 pm ,
Muda mwingi yupo shuleni na kwenye school bus,
Huo muda wa mzazi kumnyoosha mtoto anaupata wp?

Utakuta mtoto ana miaka 9 lakini akitembea anahema kama ana miaka 59,,
Sababu hana mazoezi wala purukushani zozote.
Wala hapati changamoto zozote za usafiri na shule kwa ujumla.

Lazima muelewe kwamba hata changamoto za kondakta kwa mwanafunzi pia kunamjenga mtoto,

Mjenge mtoto kupambana mapema,,.
Na sio kumfanya mzembe na goigoi..
Matajiri watasema huna hela
 
Somesha mtoto shule za hela akachangamane na watoto wa matajiri, viongozi, wanasiasa Ili apate exposure na connection,kwani bila connection life haiendi.
ni fasheni tu, mi mwenyewe nimesoma na watoto wa mawaziri, wakuu wa wilaya na mikoa, wanasiasa na wafanyabiashara, kisha nikafundisha hizo shule, ni za kawaida sana
 
Huwezi kubishana na mimi mkuu, nimesoma hizo shule za gharama na sikukuta cha ajabu, kwa shule ya msingi siku hizi zipo shule za serikali wanafundisha kiingereza na watoto kiingereza hakiwapigi chenga, wengi hupeleka watoro ahule za gharama wajifunze kiingereza, ndo hicho hicho wanafundishwa hata hizo shule za serikali
Sawa sawa, nime-stop arqueing with yoi
 
Kule anakutana na watoto wa matajiri, wanasiasa na wa viongozi mbali mbali anapata future connections. Akisoma Kayumba kama mimi baba ake anakutana na kina Siyawezi, Avinitishi, Mwajuma ndala ndefu,mtoto wa mama Mudy muuza Kangala,Mtoto wa mzee Juma muuza genge etc.....

Sijutii kumpeleka mtoto wangu shule nzuri na zenye garama. Kama wewe kipato kidogo sawa mpeleke unapoweza ila usishauri wengine kufuata unavyofikiria.

Huu ni Umaskini ndo unaokusumbuwa na kukufanya uone hii ni sawa mtoto kwenda na fagio na dumu la maji shule
So unatengeneza chawa wa baadae?
 
Kumekuwa na tabia ya baadhi ya wazazi wakisomesha watoto wao shule za gharama za private toka chekechea, msingi, o level na advance mpaka chuo kwa mategemeo kwamba watakuwa na ajira zenye malipo ya juu, watoto wakimaliza chuo hawana ajira aua ajira zinakuwa za chini, kwa o yanageuka kuwa maumivu:

Nimekuwekea hapa mbinu za kumsombesha mtoto wako kwa gharama nafuu na kupata elimu sawa na wale wanaoenda private

SHULE YA MSINGI - Hapa lengo kuu la kupeleka watoto shule za private huwa ni mtoto ajifunze kiingreza, piga ua galagaza somesha mtoto wako shule za mitaala ya kiingereza kwa sababu akifika sekondari na chuo atatumia lugha ya kiingereza, kuna shule za english medium zinakidhi kila kitu kutekeleza hili, hakuna aja ya kulipia mamilioni kwenye shule za private, Mwanangu kamaliza darasa la tatu saizi anaweza kusoma / kusikia / kuongea / kuandika kiingereza kwa level nzuri tu, anaimba miziki ya kiingereza, anaweza kuelewa movies bila tafsiri, n.k. Hata nikimletea mitihani ya kiingereza ya shule kama st mary anabutua vizuri kabisa.

SHULE YA SEKONDARI - Hapa mtaji wa kujua lugha ya kiingereza unahitajika sanaili kumpiga jeki asome kwa urahisi, Hapa nasihi sana asome shule ya day, aidha iwe ni shule yenye walimu wa kutosha na inafanya vizuri mitihani ya taifa iwe ni shule ya serikali aliyochaguliwa au hizi shule za umoja wa wazazi ambazo mara nyingi hazizidi laki 4.

Binafsi enzi zangu wazazi wangu walinipeleka shule za boarding za gharama kwa sababu wazazi wenzao wengi walifanya hivyo (mkumbo) pia wakiamini kwamba ndio ntajifunza maisha na kuepukana na vishawishi, Mimi muhusika nilieenda huko nlikutana na hali tofauti kabisa, ukiwa mlegevu utaonewa, ukiwa mtu wa makundi utavuta bangi, kulikuwa na mashoga, n.k. watoto wa ma rpc, majaji, wabunge, wakurugenzi wa taasisi, n.k walikuwepo. Kuna ile dhana ya kwamba mtoto aende huku kwa lengo la kupata marafiki wazito, hii nayo siwezi kuipa uzito maana kuna watoto wa vigogo walikuwa wakikuona unawalamba lamba wananyanyasa sana wenzao na kuwafanya kuwa watumwa.

Kiufupi mambo ya boaring hayana sana umuhimu kwa sasa, baki na moto wako nyumbani, Siku hizi kuna vitabu vya maswali na majibu vya kumuandaa mwanafunzi kujua kuyajibu kwenye chumba cha mtihani, Tuition zipo kibao nyingi sana, mtoto anafeli vipi???

FORM 5 NI TAKATAKA PELEKA CHUO - Kuliko kujiminya kumsomesha mtoto shule ya milioni 2 ni heri umpeleke chuoni kwa milioni 1 aanze kujifunza taaluma yake mapema, hata serikali yenyewe huwa inatoa selection chache sana mithiri ya bahati nasibu kuwafadhili wanafunzi kwenda kusoma vyuoni, hii ni sababu tosha kwamba chuoni ndio kuna elimu bora kuzidi form 5.

Nakumbuka hata nilivyomaliza form 6 na kuingia chuo, wale watu waliosomea certificate na diploma badala ya kwenda form 5, kwao karibu kila kitu kilikuwa ni marudio, maisha ya uhuru wa chuoni walikuwa wameshayazoea, walikuwa tayari wameanza taaluma zao mapema huku sisi tunasomea kombi, walikuwa wameshafanya mazoezi ya kazi kwa vitendo huko maoofisini kuvimbishia cv huku sisi ni weupe, vyeti vyao vilikuwa vina hadhi ya kuajiriwa serikalini wakati sisi na vyeti vyetu vya form 6 hata kiwe na division 1 hupati ajira, n.k. Pia nao wanapata mikopo kama waliomaliza form 6.

VITABU - Hakikisha mtoto wako anasoma vitabu kwajili ya elimu binafsi, kuna vitabu kama rich dad poor dad, How to make friends and influence people, n.k hakikisha anasoma hivi, Mwanangu napanga aanze kusoma hicho cha how to influence people mwakani. vitabu ni resource muhimu zaidi, ajabu ni kwamba kuna wahitimu wengi wa vyuoni hawajawahi hata kujisomea kitabu kimoja

Kwa mtinfdo huu utaweza kupunguza gharama
Makasiriko ya nn?
 
Trust me elimu ni bure siku hizi ssbabu resources ziko kila kona.

Sems tumekazs fuvu tunataka kutsmbiana tu
 
Wengine waliambiwa:"It was just a matter of time. Sasa ulitaka usinisomeshe?" Huku mama yake akikenua meno kama ngiri!
Inaumiza kwelikweli!!
 
Uzi wa wasio na ela huu.....full kujiliwaza
Sio kweli ni muhimu mtoto apate elimu nzuri pia tujue tunazalisha kizazi cha aina gani kwa mtindo huu uliopo hatuwasaidii. watoto maana tumekuwa na watoto wa nadharia sana watoto ambao hawapendi kujishughulisha akitafutiwa kazi anakataa mtoto ambae hawezi kuwa baba imara au mama imara Toto lipolipo tu kama kuku wa. kisasa
 
Back
Top Bottom