Usisomeshe mtoto shule za gharama kwa matarajio kwamba atapata ajira, utaishia kuumia tu

Tatizo lako Unadhan shuleni ni elimu tu... Tunaangalia na malezi... Shuke Ina darasa lenye wanafunzi 400 afu na wew una peleka mwanao huko....
Ya nin Wakati umejaliwa hela ya ada?
Nita peleka kwenye darasa la wanafunzi 50.
Hela kwangu haina maana kama nitamtesa mwanangu
kama ni kituo cha kulea watoto sawa ila sio sehemu sahii zaidi kuliko shule zingine za kawaida. Hii ni sawa na kwenda mwanza ukachagua usafiri wa ndege au basi, mwanza utafika tu
 
Umepotoka
. 1. Hatusomeshi mtoto ili apate ajira.
2. Shuleni ni zaidi ya elimu.. Si kama unavodhani
3. Sampling yako umefanya utafiti kwa mwanao tu then Unataka ugeneralize
4. Kesho njoo na hoja Za hosptal binafs watu wasiende kutibiwa huko kwa kuwa ni gharama
Kwani hitaji linajali gharama? Ndio maana kuna hospitali za rufaa kutatua changamoto ya ugonjwa ulioshindakana hospitali za mwanzo. Shule na hospitali ghali mtu ana option kuchagua, hii ni kama kuchagua ule chakula cha gharama gani, upate usafiri gani, mtoto akalelewe kwenye vituo gani, yote haya ni mtindo wa maisha tu haimaanishi kwingine si bora
 
Huu ni upuuzi.

Shule inamfundisha mtoto lugha tatu kubwa, ana nafasi ya kutembelea nchi kubwa kujifunza na anapata exposure unasema asisome huko sababu hakuna ajira🤣🤣🤣🤣.

Kama uwezo hakuna sawa, ila kama upo peleka mtoto mahali ambapo ni The best.

Kwani mwanao akipata nafasi ya kusomeshwa bure shule yoyote utakayochagua utampeleka kijichi primary school?
 
Siyo goigoi. Hii ni kanuni ya tajiri atazidi kuwa tajiri na masikini atazidi kuwa tajiri.
Mfano leo mtoto wa Bakhera au Mo aende akasome kayumba? Masikini huwa anaamini ili mtoto akue kimaadili lazima apitie maisha magumu, kulima, kubeba maji kichwani, kulala njaa n.k ila tajiri huwa anaamini ili mtoto akue kimaadili lazima apitie mazingira mazuri, asome shule za gharama, alale sehemu nzuri, afanye kazi nyepesi.
Mtoto wa tajiri akimaliza chuo, baba yake anamfungulia duka la Hardware la kwake, anapewa nyumba na gari wakati mtoto wa masikini yupo mtaani anatembea na bahasha mkononi kutafuta ajira. Akipata mshahara laki 4, cycle ya poverty inarudi pale pale.
Zamani sn wakati tunasoma shule za msingi,
Tulibeba mafagio.
Tukafundishwa kulima bustani,
Tukafundishwa kazi za Sanaa,
Leo naweza kulima na kufanya kazi za shamba.

Kumpeleka mtoto shule za gharama kwa Kisingizio cha kubeba fagio au,
Kupata usumbufu kwenye usafiri.

Elewa unamjenga mtoto goigoi asiyejuwa hata kufanya usafi nyumbani.
Mtoto goigoi asiyejuwa hata kulima bustani..
 
Mkuu nimejiridhisha kuna bao la mkono ktk shule za private.

Niliangalia matokeo ya darasa la 7 2021/2022 kuna shule moja ya private. wamepasi shule nzima
Kwa alama A na B ..wastani.
C wala D..hakuna

Hii aiwezekani na kwa akili ya kawaida ,,
If you want to be common in life use common sense yaani akili.ya kawaida isyojihangaisha kwa lolote

If you want your child to be common send your child to Common school sio ya tofauti Sana Kama hizo za gharama kubwa ambazo sio common .
 
Wazo la safe,secure and high paying job ni idea za agranian age....we are not in that age anymore......
 
Wengi husomesha watoto shule za gharama kama njia ya kujionyesha wao wana maisha bora kuliko wengine.

We sema huna hela Ndio maneno yanakutoka pole yako...
Ni sawa mtu anakaa masaki na wewe unakaa manzese useme wa masaki anajidai kukaa masaki
 
Zamani sn wakati tunasoma shule za msingi,
Tulibeba mafagio.
Tukafundishwa kulima bustani,
Tukafundishwa kazi za Sanaa,
Leo naweza kulima na kufanya kazi za shamba.

Kumpeleka mtoto shule za gharama kwa Kisingizio cha kubeba fagio au,
Kupata usumbufu kwenye usafiri.

Elewa unamjenga mtoto goigoi asiyejuwa hata kufanya usafi nyumbani.
Mtoto goigoi asiyejuwa hata kulima bustani..

We naweeeeh Kwani lazima wote tulime bustani ili iwejee ujinga mtupu..
Wacheni watu waishi maisha yao na wewe ishi yako ..
Tafuta pesa kaka hizo zote ni dalili za kutokua na pesa acha makasiriko
 
Zamani sn wakati tunasoma shule za msingi,
Tulibeba mafagio.
Tukafundishwa kulima bustani,
Tukafundishwa kazi za Sanaa,
Leo naweza kulima na kufanya kazi za shamba.

Kumpeleka mtoto shule za gharama kwa Kisingizio cha kubeba fagio au,
Kupata usumbufu kwenye usafiri.

Elewa unamjenga mtoto goigoi asiyejuwa hata kufanya usafi nyumbani.
Mtoto goigoi asiyejuwa hata kulima bustani..
Ndo janga la wanaume wa dar ilo.
Yaan anapiga yowe akimuona mende
 
Sekta ya madini na kilimo zikitiliwa mkazo zitaajiri vijana wote na kumaliza tatizo la machinga na bodaboda mijini.
Tirion 2 tu zinatosha kumaliza tatizo la ajira nchini na kuzalisha mapato mara 10 ya hio
 
Kumekuwa na tabia ya baadhi ya wazazi wakisomesha watoto wao shule za gharama za private toka chekechea, msingi, o level na advance mpaka chuo kwa mategemeo kwamba watakuwa na ajira zenye malipo ya juu, watoto wakimaliza chuo hawana ajira aua ajira zinakuwa za chini, kwa o yanageuka kuwa maumivu:

Nimekuwekea hapa mbinu za kumsombesha mtoto wako kwa gharama nafuu na kupata elimu sawa na wale wanaoenda private

SHULE YA MSINGI - Hapa lengo kuu la kupeleka watoto shule za private huwa ni mtoto ajifunze kiingreza, piga ua galagaza somesha mtoto wako shule za mitaala ya kiingereza kwa sababu akifika sekondari na chuo atatumia lugha ya kiingereza, kuna shule za english medium zinakidhi kila kitu kutekeleza hili, hakuna aja ya kulipia mamilioni kwenye shule za private, Mwanangu kamaliza darasa la tatu saizi anaweza kusoma / kusikia / kuongea / kuandika kiingereza kwa level nzuri tu, anaimba miziki ya kiingereza, anaweza kuelewa movies bila tafsiri, n.k. Hata nikimletea mitihani ya kiingereza ya shule kama st mary anabutua vizuri kabisa.

SHULE YA SEKONDARI - Hapa mtaji wa kujua lugha ya kiingereza unahitajika sanaili kumpiga jeki asome kwa urahisi, Hapa nasihi sana asome shule ya day, aidha iwe ni shule yenye walimu wa kutosha na inafanya vizuri mitihani ya taifa iwe ni shule ya serikali aliyochaguliwa au hizi shule za umoja wa wazazi ambazo mara nyingi hazizidi laki 4.

Binafsi enzi zangu wazazi wangu walinipeleka shule za boarding za gharama kwa sababu wazazi wenzao wengi walifanya hivyo (mkumbo) pia wakiamini kwamba ndio ntajifunza maisha na kuepukana na vishawishi, Mimi muhusika nilieenda huko nlikutana na hali tofauti kabisa, ukiwa mlegevu utaonewa, ukiwa mtu wa makundi utavuta bangi, kulikuwa na mashoga, n.k. watoto wa ma rpc, majaji, wabunge, wakurugenzi wa taasisi, n.k walikuwepo. Kuna ile dhana ya kwamba mtoto aende huku kwa lengo la kupata marafiki wazito, hii nayo siwezi kuipa uzito maana kuna watoto wa vigogo walikuwa wakikuona unawalamba lamba wananyanyasa sana wenzao na kuwafanya kuwa watumwa.

Kiufupi mambo ya boaring hayana sana umuhimu kwa sasa, baki na moto wako nyumbani, Siku hizi kuna vitabu vya maswali na majibu vya kumuandaa mwanafunzi kujua kuyajibu kwenye chumba cha mtihani, Tuition zipo kibao nyingi sana, mtoto anafeli vipi???

FORM 5 NI TAKATAKA PELEKA CHUO - Kuliko kujiminya kumsomesha mtoto shule ya milioni 2 ni heri umpeleke chuoni kwa milioni 1 aanze kujifunza taaluma yake mapema, hata serikali yenyewe huwa inatoa selection chache sana mithiri ya bahati nasibu kuwafadhili wanafunzi kwenda kusoma vyuoni, hii ni sababu tosha kwamba chuoni ndio kuna elimu bora kuzidi form 5.

Nakumbuka hata nilivyomaliza form 6 na kuingia chuo, wale watu waliosomea certificate na diploma badala ya kwenda form 5, kwao karibu kila kitu kilikuwa ni marudio, maisha ya uhuru wa chuoni walikuwa wameshayazoea, walikuwa tayari wameanza taaluma zao mapema huku sisi tunasomea kombi, walikuwa wameshafanya mazoezi ya kazi kwa vitendo huko maoofisini kuvimbishia cv huku sisi ni weupe, vyeti vyao vilikuwa vina hadhi ya kuajiriwa serikalini wakati sisi na vyeti vyetu vya form 6 hata kiwe na division 1 hupati ajira, n.k. Pia nao wanapata mikopo kama waliomaliza form 6.

VITABU - Hakikisha mtoto wako anasoma vitabu kwajili ya elimu binafsi, kuna vitabu kama rich dad poor dad, How to make friends and influence people, n.k hakikisha anasoma hivi, Mwanangu napanga aanze kusoma hicho cha how to influence people mwakani. vitabu ni resource muhimu zaidi, ajabu ni kwamba kuna wahitimu wengi wa vyuoni hawajawahi hata kujisomea kitabu kimoja

Kwa mtinfdo huu utaweza kupunguza gharama
Chuo kikuu wazazi wasitarajie watoto kupata mkopo asee na mtoto atasom kwa shida sana
 
Ni aibu sana kwa vijana kukosa ajira huku raslimali zetu zinaoza tu hii Ina maanisha hatuna viongozi wanaofikiri.
 
Gari sio anasa ni basic needs hayo makodi komozi ya nn sasa, kwann zisiingie bure Ili mafundi,vituo vya mafuta,wauza spea, parking,nk zije zipate mapato at the end import duty iwe imejilipa humo humo.
 
Wala sio sababu! Kama nna hela why mtoto wangu akasome shule anayoenda na mifagio na vidumu vya maji kila siku?Why aende shule yenye huaba wa walimu wa sayansi na hisabati?? kisa nisionekane naringia pesa¿ haya ni mawazo ya kimaskini
Somesha mtu Ili akacheze na wenzie shuleni kuepusha kelele nyumbani pili imsaidie atengeneze connection maana watoto wa leo ndio viongozi wa kesho.Na sio kusomesha Ili akapate ajira,ajira ni matokeo.
 
Kule anakutana na watoto wa matajiri, wanasiasa na wa viongozi mbali mbali anapata future connections. Akisoma Kayumba kama mimi baba ake anakutana na kina Siyawezi, Avinitishi, Mwajuma ndala ndefu,mtoto wa mama Mudy muuza Kangala,Mtoto wa mzee Juma muuza genge etc.....

Sijutii kumpeleka mtoto wangu shule nzuri na zenye garama. Kama wewe kipato kidogo sawa mpeleke unapoweza ila usishauri wengine kufuata unavyofikiria.

Huu ni Umaskini ndo unaokusumbuwa na kukufanya uone hii ni sawa mtoto kwenda na fagio na dumu la maji shule
Ndo na ndio lengo hasa la kunukia uwaridi.
 
Wanasomesha huko ki ufahari na ulimbukeni tu waonekane wana hela na pia watoto wao wajue english, kumbe hakuna lolote huko. Kama mtoto ana akili, ana akili tu hata akisoma shule za kawaida atafaulu
Somesha mtoto shule za hela akachangamane na watoto wa matajiri, viongozi, wanasiasa Ili apate exposure na connection,kwani bila connection life haiendi.
 
Mtoto akifika darasa la7 anajua kusoma na kuandika hiyo elimu inamtosha sana, muachishe shule, peleka chuo cha ufundi veta ama college yoyote akasomee kwa vitendo, akitoka hapo tyr ana ujuzi na anauwezo wa kuanza maisha yake, mtaftie mtaji na urith mapema, then fanya kunawa mikono maana kazi yako kwake unakuwa umeimaliza kama mzaz.

or otherwise kama unajua una connection ya mwanao kwenda kufanya kaz ktk nchi za kigeni ama biashara basi msome izo english medium mpka form4 then achisha shule mpeke short coz ya ujasiliamali miez3-6 then baada ya hapo mkatie urithi wake na mtaji wa kuanzia maisha..

tusiish kwa kukalil maisha kuwa hii mifumo nikama misaafu kwamba huruhusiw kuibadiri ama kufikil nje ya box.

mim nkifanikiwa kupata mtot bas atasoma kwa bata sana, yaan hata shulen atakuwa akienda mara moja kwa wiki, eeh mara moja maana sitaki aende kusomea ajira, bal akasomee kujua kuandika na kusoma tu chazaid akachangamshe akili na watoto wenzake huko, hata mtian wa darasa la7 sitotaka aufanye, maana nikumpotezea muda.

Tuish kiuhalisia jmn maisha ni mafupi why tuteseke?
View attachment 2015279
Wewe jamaa!!! Sasa tukienda hivyo, madaktari, wahandishi na hao watakaofundisha hizo kozi za ujasiriamali watatoka wapi baada ya miaka ishirini kupita?
 
44 Reactions
Reply
Back
Top Bottom