Usiri wa mali katika ndoa

Usiri wa mali katika ndoa

Unakuta mtu anahangaika na kukazana kumficha au kutokumruhusu mwenzake aishike simu yake.

Na unakuta anaiwekea sijui namba ya siri....

Kwa nini hataki mwenzake awe huru na simu yake kama hana la kuficha?

Ni hivi vitu vidogo vidogo ndo hupelekea usiri kwenye mambo makubwa makubwa.

Ndo yale yale kama mambo ya simu.

Watu mmeoana lakini eti kila mtu ana simu yake ambayo mwenzake haruhusiwi kuigusa!

Kuna nini humo kwenye simu ambayo hutaki mwenzio ayaone?

Eti simu yangu ni yangu na yake ni yake.

Alaaaa! Mbona papuchi ni yako na mboli ni yake lakini mnaachiana mshikane.....

N.ngabu Unaongea kwa dhati mno kuhusu swala la simu. Limekutokea nini? Pole mkuu.
 
Unasikia kutoka kwa jamaa za mbali mme ana kiwanja we unaelala nae chumba kimoja hauji ....kuna watu wana roho za ubinafsi sana aaagrrrr hasara roho tu wafiche salama ikibidi hata salary slip zikakae makwao

Hawa watu ni kizunguzungu, mtu mbinafsi inatakiwa usimfuatilie unakomaa kama hujui na hujali, ili kila mtu afanye yake ili tusirudishane nyuma tu.
 
N.ngabu Unaongea kwa dhati mno kuhusu swala la simu. Limekutokea nini? Pole mkuu.

Wala halijanitokea.

Nadhani umeona nimeongea [andika] kwa dhati kwa sababu nilichokisema ni cha ukweli.

Kama kweli mtu huna cha kuficha humo kwenye simu kwa nini upatwe shida endapo mwenzako ataishika simu yako?

Ni suala la common sense tu.
 
Bravo.
 
Habarini wana MMU,Natumai wote ni wazima kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu na wale ambao si wazima Mungu awaponye.

Wapendwa leo ningependa tujadili juu ya usiri wa mali katika ndoa,Katika jamii ambayo imenizunguka kwa mwaka huu tu nimepata kuona jambo hili likijitokeza mara tano katika misiba tofauti tofauti iliyotokea na mingine ikiwa ni ya ndugu zangu jamaa na marafiki, na katika misiba hiyo bahati mbaya yote inawahusu wanaume ambao wametangulia mbele ya haki huku wakiwa wameacha watoto pamoja na wake zao.

Mbaya zaidi katika familia hizo hakuna yoyote hata wake zao anayejua Mali za hao waume zao ziko wapi zaidi ya Nyumba wanazoishi walizoachiwa na marehemu,moja ya msiba ulionishangaza na kunisikitisha sana ni kuona rafiki ya marehemu anajua Mali nyingi karibu kila kitu cha marehemu alichoacha kuliko hata mkewe na la zaidi marehemu ana watoto wakubwa tu ambao angeweza kuwaambia au kuwashirikisha mambo yake.

Mwanaume na mwanamke wanapoamua kuungana nakuwa mwili mmoja ina maana wamekuwa ni wamoja ,chochote kinachopatikana kinakuwa ni mali ya wote, Ina maana mmeridhiana na kuaminiana na kuamua kukabidhiana maisha yenu kwa faida ya ninyi wote wawili,mtu ambaye umemkabidhi maisha yako unalala naye,anaujua undani wako ,ana usalama wa afya yako, amebeba dhamana ya maisha yako na uzao wako unamficha mali ulizonazo kweli? Hajui hata kama una au huna account bank? Sasa unatafuta kwaajili ya nani na ili iweje?

Basi kama mwanaume una hofu na mwanamke uliye naye basi weka Mali zako kimaandishi kuliko kuweka siri mwisho unaacha kizazi chako kikiteseka ili hali Mali zinapotea bure wanafaidi wengine ambao hata hawakuhusu. Na hiyo hofu inatoka wapi? Ili hali mwanaume wewe ndo kichwa cha Nyumba na mtawala Mkuu, ule utawala wa chini utaenda vile utawala wa juu uko,kama mwanamke amekuwa hajitambui au ana hila ni makosa ya mwanaume katika utawala wake. Tunajua upendo wa kweli ni utimilifu wa mambo yote, na katika Pendo Hamna hofu na huyo mwenye hofu hakukamilika katika Pendo.

Ni wito wangu wanandoa tuache usiri usio na tija,mshirikishe mkeo au mumeo kwa Mali ulizonazo,tuambiane kweli,mpaka mtu unaamua kuingia katika ndoa ina maana umeridhika na huyo uliyemchagua,usiri hauna maana yoyote zaidi ya kuwatesa tu watoto na kuwaacha katika mateso makubwa,hakuna mwenye dhamana ya maisha akajua anaondoka lini duniani,hatukuja na kitu duniani na hatutaondoka na kitu vyote tutaviacha.

Wanaume wafundisheni wake zenu kutafuta ili wajue kuheshimu na kuvitunza vile vinavyopatikana kwaajili ya familia,msiwafungie wake zenu majumbani mwenu kama mifugo matokeo yake Mungu anapowachukua mnawaacha wanateseka na watoto wenu maana walizoea kuletewa kila kitu,na wakati mwingine hata zile Mali mlizoziacha zinapotea maana zinakuwa hazina msimamizi tena kwasababu kila kitu kiliendeshwa na mwanaume.

Nawatakia ndoa zenye furaha,amani na baraka tele, Mwenyezi Mungu awe nanyi daima.karibuni wote kwa mjadala zaidi.

Mkuu,

Ina maana sisi wanaume ndio wa kutangulia kila siku? Yaani sababu ni "Ili mume akifa asipate shida na watoto? Ndio sababu kuambiwa orodha ya Mali za Mume wake?

Japo ujumbe ni mzuri, ila sababu na imemtizama mwanaume kama anaetarajiwa kufa wa haraka. Nadhani hiyo sababu ndio sababu wanaume wengi hawataji mali zao.
 
Weee!!! Acha my dia, hii dunia imegeuka sana, watu wanaona ili kuzaa tu, mambo mengine ndugu na marafiki ndio wanajua, jitu la hivyo ikitokea bahati mambaya mauti imemchukua loh!!! Wakati mwingine ndugu hata hawasemi lolote, hasa ukizingatia familia nying zinaashumu mtu ukifiwa na mume utaenda kuolewa tena.

Wakati Mwingine Wanawake ndio mnachangia hiyo hali. Umeolewa halafu unajaza ndugu zako tuu wa mumeo hutaki kuwaona, inafika mahala Mwanaume anaamua kutafuta namna ya ku balance mambo bila ww kushirikishwa.

Usiishie kulaumu, hebu kwanza thibitisha kuwa ww ni Mke mwema ambae umestahili kufahamu hayo yote lakini hujapata toka kwa Mumeo.

Wanawake mnadai haki zenu utadhan mko hundred percent perfect ktk ndoa zenu.

Kwann sababu ya kuambiwa iwe ili akifa usipate shida?
 
Hawa watu ni kizunguzungu, mtu mbinafsi inatakiwa usimfuatilie unakomaa kama hujui na hujali, ili kila mtu afanye yake ili tusirudishane nyuma tu.

Nyie warembo, wangapi mnajenga kwa mama zenu bila mume kujua? Mnafungulia wadogo zenu biashara kwa pesa za mume bila yy kufahamu? Wapo waliopata kazi zenye mishahara kuliko waume zao na wanafanya mengi bila waumezao kujua.

Una mke, wote mnafanya kazi lakini kutwa yy hana hela. Anakula zako, zake anafanya mambo kimya.

Kuna jamaa, alikuja stukia Nyumba inazungushiwa ukuta, Mke kajenga bila kumwambia hata neno moja.

Jamaa akamwambia mwanamke achague, kuiuza hiyo nyumba au kuachana na jamaa.

Haya Mambo hutokea kutokana na sababu nyingi sana. Wanawake wengi sana hufika nia zao mpaka wakishaingia kwenye ndoa.

Maisha ya ndoa za siku hizi yamekaa kimaslahi sana. Sio wanawake, sio wanaume. ILa wanawake ndio hasa wamezidi ktk kutegemea kunufaika kimaslahi ktk mahusiano yao na waume au wapenzi wao.
 
Wakati Mwingine Wanawake ndio mnachangia hiyo hali. Umeolewa halafu unajaza ndugu zako tuu wa mumeo hutaki kuwaona, inafika mahala Mwanaume anaamua kutafuta namna ya ku balance mambo bila ww kushirikishwa.

Usiishie kulaumu, hebu kwanza thibitisha kuwa ww ni Mke mwema ambae umestahili kufahamu hayo yote lakini hujapata toka kwa Mumeo.

Wanawake mnadai haki zenu utadhan mko hundred percent perfect ktk ndoa zenu.

Kwann sababu ya kuambiwa iwe ili akifa usipate shida?

Nyie warembo, wangapi mnajenga kwa mama zenu bila mume kujua? Mnafungulia wadogo zenu biashara kwa pesa za mume bila yy kufahamu? Wapo waliopata kazi zenye mishahara kuliko waume zao na wanafanya mengi bila waumezao kujua.

Una mke, wote mnafanya kazi lakini kutwa yy hana hela. Anakula zako, zake anafanya mambo kimya.

Kuna jamaa, alikuja stukia Nyumba inazungushiwa ukuta, Mke kajenga bila kumwambia hata neno moja.

Jamaa akamwambia mwanamke achague, kuiuza hiyo nyumba au kuachana na jamaa.

Haya Mambo hutokea kutokana na sababu nyingi sana. Wanawake wengi sana hufika nia zao mpaka wakishaingia kwenye ndoa.

Maisha ya ndoa za siku hizi yamekaa kimaslahi sana. Sio wanawake, sio wanaume. ILa wanawake ndio hasa wamezidi ktk kutegemea kunufaika kimaslahi ktk mahusiano yao na waume au wapenzi wao.

Naona una jazbaaa sana. rejea vitabu vitakatifu vinamtaka mwanaume afanye nini na mwanamke afanye nini.
 
Kama umeshindwa kujibu hilo,
Basi kubali kupokea mabadiliko ya kidunia, over

Wewe umefanikiwa kujibu langu? Ni mwanamke unaejishughulisha kweli na kutimiza wajibu wako, kwann uhofie mali baada ya kufiwa na Mumeo? Kwann mali ambazo hukuambiwa zikuumize kuliko tukio la kufiwa na mumeo?

Ukweli ni kwamba Mpo kimaslahi. Ndio maana mnaanin mtaishi zaidi ya waume zenu hivyo ni haki ukajua kila kilichochake, akifa usipate shida.
 
Nitasoma kesho, maana hata nikisoma sitaelewa, ngoja nilale.
 
Mkuu,

Ina maana sisi wanaume ndio wa kutangulia kila siku? Yaani sababu ni "Ili mume akifa asipate shida na watoto? Ndio sababu kuambiwa orodha ya Mali za Mume wake?

Japo ujumbe ni mzuri, ila sababu na imemtizama mwanaume kama anaetarajiwa kufa wa haraka. Nadhani hiyo sababu ndio sababu wanaume wengi hawataji mali zao.

Pole sana Mkuu japo mada ilijikita huko zaidi ila katika aya yangu ya tano nimeligusia pande zote mbili, ila pia nadhani kwasababu na matukio yote yaliyotokea yalihusisha wanaume tu kutangulia mbele za haki.

Jambo lingine sijawahi ona katika misiba yoyote ambayo mwanamke ametangulia kufariki akamwacha mume swala la Mali likajadilika kwamba marehemu ana Mali gani maana vyote huhesabika ni vya mume,sana sana kama alikuwa mfanyakazi wa kuajiriwa Swala la Mirathi ya mafao ndo itajadiliwa nini kifanyike .
 
Hata kabla sijasoma michango ya wadau, kwenye uzi huu natamani sana kumsikia NANDERA
atoto najua msimamo wake hata bila ya kusoma alichoandika kwenye uzi huu, kuna uzi wake mahali alishawahi kuweka kila kitu hadharani

Mito nilipotezwa na majukumu na nadhani mada ishanipita hii na siwezi kusoma kila mchango. Binafsi mali zangu zinajulikana na ndugu na rafiki zangu wa karibu. Ni kwamba sina tabia ya usiri, na mali nazipenda ila sipendi zininyime usingizi sijui nani atachukua, nani atafanya nini. Hatukuja na kitu, hatutaondoka na kitu na hatuna control ya mali zetu zitumikeje sisi tukishaondoka. hata ukimwachia mkeo anaweza kuzihonga kwa kina marioo, watoto wanaweza kuzitapanya tu, zinaweza kustawi na kuendelea kuzaa....Maadam uko hai tunza uhai sana, uelimishe watoto wako na uwalee vizuri kimaadili, utumie mali zako kusaidia na wengine na kwingine. Baaas! Nshaakwambia kesho ni ya manyani.

Kuhusu wanandoa wanaoficha mali zao mimi nitakuwa wa mwisho kuhukumu. Kwa uzoefu wangu nimeona wanaoficha kwa sababu ni wabinafsi tu au wachoyo na tabia dawa yake ghali, na kuna ambao wake au waume zao ni wafujaji - wakiona hela tu wanakimbilia shopping na anasa zingine. Hivyo wanandoa wenye wenza wa aina hii mara nyingi hushirikisha watu wa nje (ndugu na marafiki). Anakwambia "nimepata hela flani hapa ila staki yahaya ajue kama ninazo. nisindikize nikanunue shamba....". Mi nasema watu waenende na mali zao wanavyotaka maana hatuwezi kufanana wote ila wakumbuke kuandika wosia.
 
Unajisikia vibaya ndio
Hapa ndo kwenye ugomvi wangu na NANDERA namsubiria kwa hamu sana nisikie atasemaje leo
utajiskiaje vibaya na mali za mwenzio?? tafuta zako. kwani mlioana ili urithi mali au umrithishe za kwako? ah! sijui bwana, mtajua wenyewe na ndoa zenu huko. Mi nahaingikia zangu kivyangu upande huu mwingine.
 
Wakati Mwingine Wanawake ndio mnachangia hiyo hali. Umeolewa halafu unajaza ndugu zako tuu wa mumeo hutaki kuwaona, inafika mahala Mwanaume anaamua kutafuta namna ya ku balance mambo bila ww kushirikishwa.

Usiishie kulaumu, hebu kwanza thibitisha kuwa ww ni Mke mwema ambae umestahili kufahamu hayo yote lakini hujapata toka kwa Mumeo.

Wanawake mnadai haki zenu utadhan mko hundred percent perfect ktk ndoa zenu.

Kwann sababu ya kuambiwa iwe ili akifa usipate shida?

"imeandikwa" kwamba sisi ndo wa kwanza kufa......:A S-rap:
 
Back
Top Bottom