Usiri wa mali katika ndoa

everlenk

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
11,627
15,017
Habarini wana MMU,Natumai wote ni wazima kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu na wale ambao si wazima Mungu awaponye.

Wapendwa leo ningependa tujadili juu ya usiri wa mali katika ndoa,Katika jamii ambayo imenizunguka kwa mwaka huu tu nimepata kuona jambo hili likijitokeza mara tano katika misiba tofauti tofauti iliyotokea na mingine ikiwa ni ya ndugu zangu jamaa na marafiki, na katika misiba hiyo bahati mbaya yote inawahusu wanaume ambao wametangulia mbele ya haki huku wakiwa wameacha watoto pamoja na wake zao.

Mbaya zaidi katika familia hizo hakuna yoyote hata wake zao anayejua Mali za hao waume zao ziko wapi zaidi ya Nyumba wanazoishi walizoachiwa na marehemu,moja ya msiba ulionishangaza na kunisikitisha sana ni kuona rafiki ya marehemu anajua Mali nyingi karibu kila kitu cha marehemu alichoacha kuliko hata mkewe na la zaidi marehemu ana watoto wakubwa tu ambao angeweza kuwaambia au kuwashirikisha mambo yake.

Mwanaume na mwanamke wanapoamua kuungana nakuwa mwili mmoja ina maana wamekuwa ni wamoja ,chochote kinachopatikana kinakuwa ni mali ya wote, Ina maana mmeridhiana na kuaminiana na kuamua kukabidhiana maisha yenu kwa faida ya ninyi wote wawili,mtu ambaye umemkabidhi maisha yako unalala naye,anaujua undani wako ,ana usalama wa afya yako, amebeba dhamana ya maisha yako na uzao wako unamficha mali ulizonazo kweli? Hajui hata kama una au huna account bank? Sasa unatafuta kwaajili ya nani na ili iweje?

Basi kama mwanaume una hofu na mwanamke uliye naye basi weka Mali zako kimaandishi kuliko kuweka siri mwisho unaacha kizazi chako kikiteseka ili hali Mali zinapotea bure wanafaidi wengine ambao hata hawakuhusu. Na hiyo hofu inatoka wapi? Ili hali mwanaume wewe ndo kichwa cha Nyumba na mtawala Mkuu, ule utawala wa chini utaenda vile utawala wa juu uko,kama mwanamke amekuwa hajitambui au ana hila ni makosa ya mwanaume katika utawala wake. Tunajua upendo wa kweli ni utimilifu wa mambo yote, na katika Pendo Hamna hofu na huyo mwenye hofu hakukamilika katika Pendo.

Ni wito wangu wanandoa tuache usiri usio na tija,mshirikishe mkeo au mumeo kwa Mali ulizonazo,tuambiane kweli,mpaka mtu unaamua kuingia katika ndoa ina maana umeridhika na huyo uliyemchagua,usiri hauna maana yoyote zaidi ya kuwatesa tu watoto na kuwaacha katika mateso makubwa,hakuna mwenye dhamana ya maisha akajua anaondoka lini duniani,hatukuja na kitu duniani na hatutaondoka na kitu vyote tutaviacha.

Wanaume wafundisheni wake zenu kutafuta ili wajue kuheshimu na kuvitunza vile vinavyopatikana kwaajili ya familia,msiwafungie wake zenu majumbani mwenu kama mifugo matokeo yake Mungu anapowachukua mnawaacha wanateseka na watoto wenu maana walizoea kuletewa kila kitu,na wakati mwingine hata zile Mali mlizoziacha zinapotea maana zinakuwa hazina msimamizi tena kwasababu kila kitu kiliendeshwa na mwanaume.

Nawatakia ndoa zenye furaha,amani na baraka tele, Mwenyezi Mungu awe nanyi daima.karibuni wote kwa mjadala zaidi.
 
Kwa sasa ubinafsi umekithiri, mtu mpo pamoja kila anachotaka kufanya anaenda kuwashirikisha kwao sio wewe, khaa!!!


Yaani, yapo ya pamoja na yapo ya kila mtu peke yake.

Kwa kweli hii ni hatari sana,na kama unajijua ni mbinafsi unaoa kwaajili gani? Ni bora mwanaume huyo aendelee kutafuta kwaajili ya hiyo familia yake tu aliyozaliwa nayo......Ila bora hata huyo anawaambia hata ndugu zake mwingine hata ndugu zake hawaambii chochote mambo yake anafanya siri tu.
 
Ubinafsi........
Uchoyo.........
Kutokuaminiana......
Ufujaji.........

Mwisho watu baki wanafaidi mali ulizoacha wakati wanao wakiomba omba kwa ndugu jamaa na marafiki

Kweli kabisa BADILI TABIA ,na hao jamaa na marafiki wanakuwa hawana msaada tena maana urafiki wa sasa ni wa vitu,mtu atakusaidia akijua lipo ambalo atalipata kutoka kwako.
 
Last edited by a moderator:
Ndo yale yale kama mambo ya simu.

Watu mmeoana lakini eti kila mtu ana simu yake ambayo mwenzake haruhusiwi kuigusa!

Kuna nini humo kwenye simu ambayo hutaki mwenzio ayaone?

Eti simu yangu ni yangu na yake ni yake.

Alaaaa! Mbona papuchi ni yako na mboli ni yake lakini mnaachiana mshikane.....
 
Kwa kweli hii ni hatari sana,na kama unajijua ni mbinafsi unaoa kwaajili gani? Ni bora mwanaume huyo aendelee kutafuta kwaajili ya hiyo familia yake tu aliyozaliwa nayo......Ila bora hata huyo anawaambia hata ndugu zake mwingine hata ndugu zake hawaambii chochote mambo yake anafanya siri tu.

Weee!!! Acha my dia, hii dunia imegeuka sana, watu wanaona ili kuzaa tu, mambo mengine ndugu na marafiki ndio wanajua, jitu la hivyo ikitokea bahati mambaya mauti imemchukua loh!!! Wakati mwingine ndugu hata hawasemi lolote, hasa ukizingatia familia nying zinaashumu mtu ukifiwa na mume utaenda kuolewa tena.
 
Ndo yale yale kama mambo ya simu.

Watu mmeoana lakini eti kila mtu ana simu yake ambayo mwenzake haruhusiwi kuigusa!

Kuna nini humo kwenye simu ambayo hutaki mwenzio ayaone?

Eti simu yangu ni yangu na yake ni yake.

Alaaaa! Mbona papuchi ni yako na mboli ni yake lakini mnaachiana mshikane.....


Hahahaha Nyani Ngabu umeniacha hoi, ni kweli kabisa usemayo usiri usiyo na tija hauna maana yoyote.
 
Last edited by a moderator:
Hapa kuna jamaa alikuwa na Ushirika na kijana mmoja chokoraa bila kumshirikisha ndugu hawakujua, kafa karithi Huyo dogo
 
Kwa sasa ubinafsi umekithiri, mtu mpo pamoja kila anachotaka kufanya anaenda kuwashirikisha kwao sio wewe, khaa!!!


Yaani, yapo ya pamoja na yapo ya kila mtu peke yake.

Huwa inategemea na mwanamke unayetaka kufunguka kwake na kumtajia mali zako zote...kama si kichwa maji na anamjali mumewe sio mbaya akijua.

Ila just imagine ni wale wanawake wa kule wanapoua wame zao baada ya kutajirika na kujua mali za mume JE UTAMTAJIA MALI ZAKO ZOTE? common sense needs to be applied there aisee,
 
Kama huwezi muamini mkeo basi usioe......


Kumuamwini mke ni sawa na kumusomesha demu wako.

Nyie ndio ambao marafiki na ndugu wanajifaidia mali zenu....

Kuna mmoja aliacha mgorofa huko kawe....kaka yake wa damu alifukuza kwa mapanga mke na watoto walipogundua na kwenda....

Mwingine alijenga kisiri akimshirikisha rafiki yake...alichokifanya rafiki kubadilisha ownership anajua ila watoto wanebaki kutoa macho.
 
Weee!!! Acha my dia, hii dunia imegeuka sana, watu wanaona ili kuzaa tu, mambo mengine ndugu na marafiki ndio wanajua, jitu la hivyo ikitokea bahati mambaya mauti imemchukua loh!!! Wakati mwingine ndugu hata hawasemi lolote, hasa ukizingatia familia nying zinaashumu mtu ukifiwa na mume utaenda kuolewa tena.

Hii ni shidaa !! Sasa anazaa halafu anamficha mkewe Mali zake sasa ili iweje? Basi katika msiba mmojawapo tukiwa katika kikao cha familia ikasemekana Marehemu ameacha kiwanja mkewe anabaki anatoa macho hajui chochote anashangaa tu. Sasa ni hilo tu lililosemwa mengine yakapigwa kimya tu. Mke kila analoulizwa anashangaa tu hajui chochote.
 
Back
Top Bottom