Usiombee kukosa hela

Usiombee kukosa hela

Afadhali yako huna familia

Mimi dogo amerudishwa school kisa nimeshidwa kulipa 8000 ya uji

Na mvua ndio zinanyesha hatari, dogo viatu vimechanika maji yanaingia mpaka ndani
,
Nikaenda kukopa vibuti vya kavaa dogo awe anavaa aende navyo shule, yule mama ananidai utazan amenikopesha moyo daily hodi haziishi
Yaani mwanafunzi anarudishwa shule kisa hela ya uji? Hii nchi Hii
Kwani hawezi kusoma bila kunywa uji?
Yani muda wa uji ukifika ambao hawajalipa wasinywe, sasa mwl mkuu anashuhudia hili na anacheka aisee!
 
Mie koote sijawah umia kama kukosa shilingi 100 niongezee 200 nikanunue chumvi mwaka 2010!na hapo nna mgeni shemej yangu kaja kututembelea nimechinja kuku sina chumv na ndo kwanza nna siku kadhaa tu toka nitoke hom kuja kuishi na mshikaji nna katoto kachangaaa nililiaaa alafu mbya zaidi sina mazoea kabs na majirani ..kwanza nilikua sitoki toki nje enzi hizo mtoto wa kishua balaaa shenzi zangu..mshikaj anarud usk namwambia mimi nataka kurudi hom nimemmis baba! Sitak tena yale maisha mm...ya kusubiri upewe!! Yaishie hukooo!nyoko kbs
Hatari sana lakini pia ni bonge la experience kwenye safari ya kuiheshimu hela.
 
Hivi umewahi kukosa hela na huku unanuka madeni mpaka ukatamani hata mtu akosee kutuma mpesa, au tigo pesa, ili hela ije kwako? Au ukatembeatembea ukiamini unaweza hata okota hela mtu aliyedondosha? Kweli wanaume tumeumbwa matesooooo, matessooo kuhangaika.

Nina salio la buku (1000) kwenye wallet ndio kwanza jumatatu. Ee Mola ninusuru. Wangapi tunapitia haya? kama unaamini ni mapito tuu na sisi sikumoja tutakuwa na fedha za kutosheleza mahitaji yetu type Amen.
huo ni ugonjwa usiombe uupate
 
Kukosa hela balaa hata watoto wadogo hawakuamkii shikamoo!! Unapita wao wanaendelea kucheza mpira tu!!
 
Hivi umewahi kukosa hela na huku unanuka madeni mpaka ukatamani hata mtu akosee kutuma mpesa, au tigo pesa, ili hela ije kwako? Au ukatembeatembea ukiamini unaweza hata okota hela mtu aliyedondosha? Kweli wanaume tumeumbwa matesooooo, matessooo kuhangaika.

Nina salio la buku (1000) kwenye wallet ndio kwanza jumatatu. Ee Mola ninusuru. Wangapi tunapitia haya? kama unaamini ni mapito tuu na sisi sikumoja tutakuwa na fedha za kutosheleza mahitaji yetu type Amen.

Unapitia hali hiyo halafu wewe wewe ndio baba mwenye familia, nyumba umepanga, watoto wanahitaji kula.........
 
Ishanitokea kama mara mbili hivi katika kumbukumbu zangu

Mara ya kwanza ilikua mwaka 2011 kipindi hicho nasoma advance Karatu boys. Kuna kipindi kulikua na shida ya maji mno pale shule ilikua chini ya Songoi (mkuu wa shule)wakati huo, hali ikawa tete kufikia hatua hadi vyoo vilifungwa tukagawana viwanja vya kujistiri kwny shamba la don flani hivi wa kule wa kuitwa Shang'lila. Vijana tukaona sio kweli tukaandamana bwana....hahah kilichotokea ilibaki story watu walikula kichapo heavy na siku hiyo hiyo shule ikawa chini ya usimamizi wa askari halafu ikatolewa amri kila mtu kwao untill further notice.....

Nilivyoishiwa sasa
Kwa kuwa nlikua na akiba kidogo nkapiga simu hm wanitumie nauli nikaunga kabisa mpaka Arusha nkachukua room guest ya karibu nkaangusha, morning kumekucha nkakata tiketi kabisa halafu nkafuatilia mchakato wa kutoa pesa nliyotumiwa....sasa sijui wenge au vipi si nikakosea password hadi akaunti ikafungiwa hangaika hangaika na foleni pale mara mda wa safari tayari nkasepa nkasema ntafuatilia hm (dar) ila mfukoni sina kitu.

Basi njiani ilinipiga njaa hiyo mixer kiu ikafikia stage tumeshuka sikumbuki motel gani ile kuchimba dawa kidume nkaingia toilet nkafungua bomba nkakinga maji kunywa sana hadi nkataka kutapika....niliteseka sana ile siku na ule mgari sijui ulikua m'bovu mpaka naingia hm km saa nne na kitu hivi kama sio saa tano kasoro usiku.
 
Ukiwa huna hela hata nyege hazipandagi, Kama Ni mwanaume hata ikikatiza pisi kali yenye chura Ni Kama huioni,, njaa mbaya sana, nawaombea wote mnaopitia magumu ya kiuchumi Mungu atufanyie wepesi maisha magumu sana jamani
 
Tumepokea upako mamaa ya ruvu🤭😅🤣
 
Aisee, ukiwa huna pesa kiufupi moyo unaumaaa, unatamani hata kulia (kwa sauti ya yule dada mbunge😂). Pia unakuwa na hasira za karibu na mawazo mchanganyiko...
 
Back
Top Bottom