Usiombe yakukute jamani, daah!!!

Usiombe yakukute jamani, daah!!!

Kwanza nikupe pole kwa mtihani uliokumbana nao, nina hakika yataisha na maisha yataendelea kama kawaida, hakuna changamoto isiyokuwa na ufumbuzi, na natumaini kwamba hili litakapokwisha nawe utakuwa umejifunza kitu. Kama hujajifunza ni kwamba USIFANYE NGONO NA MWANAMKE BILA KUTUMIA KINGA HASA KAMA BADO HUNA HAKIKA KAMA MAHUSIANO YENU NI YA DHATI. Ukiendelea kufanya ngono bila kinga maana yake utaendelea kuzaa watoto bila mpangilio lakini utakuwa unawakwanza wanawake hao unaokutana nao, licha ya hatari unayojitengenezea ya kupata magonjwa.
 
Wewe ulimsaliti sasa yeye kukusaliti hasira unaitoa wap kiongozi, ndege wafananao huruka pamoja
 
Jamani,naomba kuleta mrejesho wa maswahibu yangu!

Baada ya co-worker kujikata mkono kama jaribio la kujitoa uhai wake,nilisitisha safari ya Singida.
Lakini baada ya wiki moja niliamua kutengeneza dharura ya uongo kwa kumpanga rafiki yangu anipigie simu kunipa taarifa kuwa nahitajika kwetu haraka sana!(kwetu ni mkoani)

Basi jioni moja tukiwa tunaongea (huku nikiwa na hasira sana,japo sikutaka ajue),jamaa yangu akanipigia simu,akijifanya kaka yangu,akanambia nijitahidi ndani ya siku mbili nifike nyumbani kuna mambo muhimu yanahitaji uwepo wangu.

Baada ya kumaliza mazungumzo ya simu nikamwambia huyu mpnz wangu kuwa ninahitajika nyumbani haraka,inabidi kesho nipande gari kuelekea nyumbani,hakutia shaka!

Asubuhi ya siku iliyofuata nikapanda gari kuelekea Singida kwa mama watoto wangu.

Nimefika Singida,nikakuta familia yangu ikiwa poa kabisa,nikajisemea moyoni,huyu mwanamke (wa Tanga) anataka kuniharibia familia yangu hakika,kila nikiwaangalia wanangu wanavyofurahia uwepo wangu,na vizawadi kidogo nilivyowabebea nikajisemea hakika sitakubali kuiharibu familia yangu!

Usiku wa saa tano hivi nimelala na mke wangu,sijui shetani gani alinituma kushika simu ya mke wangu,nikaichukua nikaenda sebuleni,(yeye akiwa amelala baada ya game),kufungua inbox yake,loooh!nakuta SMS za wanaume kama 4 hivi,wote wanaonyesha wame-date naye,kwa sababu kila mmoja anasifia kuhusiana na mapenzi aliyopewa!
Mmoja ameandika," Bby una K ya moto sio mchezo,natamani iwe kila siku"

Mwingine,"Kwa ulivyokuwa mtamu,ungekuwa hauna mume ningekuoa kabisa"

Baada ya hapo nikajikuta najawa na hasira mbaya,ukizingatia si mtu niliyempenda ila nililazimika kuweka maslahi yangu kando ili kulinda maslahi ya watoto wetu,(maana bila watoto kiukweli tusingekuwa pamoja mpaka sasa)

Nimeendelea kuwepo mpaka sasa,na Alhamis natarajia kurejea Tanga,ila nina hasira moyoni isiyokifani,mbaya zaidi,kila nikisoma sent items zake kwa hao jamaa,naona anaonyesha ushirikiano chanya kwao!

Kimoyo moyo nawaza nikiondoka nimpotezee moja kwa moja,maana hata hamasa ya kusex naye sina kabisa!!

Nafikiria kuachana na wote nianze upya,(maana wa Tanga nampenda lakini kwa kiasi fulani naona hanifai kuwa mke) japo najiuliza ni mwanamke gani atakayenielewa kuwa nina watoto 3 na aishi nami na kuwapenda hao watoto wangu!!!???
Ushauri zaidi jamani,vijana wenzangu epuka sana kuanzisha mahusiano na mfanyakazi mwenzako,hasa kama hauna mpango wa kumuoa,ni hatari!!
Duuu...we jamaa una gundu!

But aliyekutuma kushika simu ya mkeo huyo tena usiyempenda ni nani? Sasa ulitarajia akae tu bila kuwa na mtu? Mbona we una mwanamke tena ana mimba ako???

Wee una majanga tayari bado unaongezea mengine! Utakuja kujiua ww wee endekeza wanawake na mambo yao
 
Witnessj ndugu yangu,bora ningeona ana-date na mtu mmoja,ningejua ndo ukame wakati mimi sipo,sasa wanaume 4 na bado unamtetea,eboooo!!!
 
Aisee somo la leo wanaume tuache kuchovya chovya ovyo raha ya siku moja inaweza leta shida ya mwaka mzima
 
Kwanza nikupe pole kwa mtihani uliokumbana nao, nina hakika yataisha na maisha yataendelea kama kawaida, hakuna changamoto isiyokuwa na ufumbuzi, na natumaini kwamba hili litakapokwisha nawe utakuwa umejifunza kitu. Kama hujajifunza ni kwamba USIFANYE NGONO NA MWANAMKE BILA KUTUMIA KINGA HASA KAMA BADO HUNA HAKIKA KAMA MAHUSIANO YENU NI YA DHATI. Ukiendelea kufanya ngono bila kinga maana yake utaendelea kuzaa watoto bila mpangilio lakini utakuwa unawakwanza wanawake hao unaokutana nao, licha ya hatari unayojitengenezea ya kupata magonjwa.
Ni kweli,nauchukua ushauri wako,japo nikianzisha mahusiano yakikaa kuanzia miezi 3,matumizi ya kondom kwa kweli yanapungua automatically!!!

Ila kwa hali hii nadhani nitajitahidi sana kuji-control,awali nilikuwa naamini mwanamke hawezi kushika mimba tu pasipo makubaliano,hasa watu wazima na wasomi!

Sasa msomi mzima anajishikia tu mimba pasipo kukubaliana,sio sawa kabisa!
 
Ujanja uliuanza wewe sasa unalia lia
Ushauri muombe msamaha mke wako uanza maisha mapya
 
Back
Top Bottom