Usiombe yakukute jamani, daah!!!

Usiombe yakukute jamani, daah!!!

Duuu pole mkuu yalishanikuta mwezako mpk Leo nawaogopa nilitamn kuama mji mkuu ila nashukur mungu uzim upo
 
Mkuu mwanamke anajileta analala akutege kwa ujasiri bila aibu, nawe una uvaa mkenge 😱.
Kwa ujasiri alioufanya huyo mwanamke ulitakiwa ushtuke na umpeleleze zaidi.
nikarudi kama saa nne usiku,nikamkuta amelala kabisa,amevua blauzia na amevaa chupi na kanga tu!
 
Hii ni psychiatric case mpeleke Bombo aonwe na wataalamu wa ubongo na fahamu.
 
Kupitia somo lako hope wengi watajifunza, jambo hili ni common sana kwa maisha ya sasa ambapo ajira zinachangia kutenganisha wazazi, ntakushauri nikipata muda ila cha kwanza acha Tamaa ya zinaa
 
Mimi nina kisa changu kiasi flani kinataka kufanana na chako. Nikiamua kukielezea hapa jukwaa litasimama.
Ni historia ambayo imenifanya niyaone mapenzi yanaweza kuleta huzuni kubwa sana. Unajikuta upo katikati na kila mtu anakuhitaji na unashindwa umchukue yupi umwache yupi. Acha kabisa.
Ndugu zangu,ukisikia njia panda Kali ndiyo hii!!
Mwaka 2010 niliachana na mpnz wangu nliyempenda sanaaa,ktk kipindi hicho cha mpito nilikutana na msichana mmoja mkoani huko,nikamtongoza ki-maskhara sana,(sikuwa serious kwa sababu sikumpenda kwa kweli) akakubali,nikajisemea moyoni huyu nakula then simrudii tena!

Kweli,nikamla msichana yule,(alikuwa mwaka wa kwanza Chuo cha diploma huko Mkoani),kwa uzembe wetu hatukutumia kinga,baada ya miezi kadhaa akaniambia anahisi ni mjamzito,nilishtuka kweli kwa sababu sikutaka kabisa kuwa na mtoto japo sikuchukua tahadhari kuliepuka hilo. Sikuikataa bali nilimshawishi atoe ile mimba,nikamtumia mpaka pesa ya kutolea,akakataa kabisa kuitoa na pesa yangu akanirudishia!(nikamtumia tena imsaidie kwa mambo yake mengine)

Baada ya mwaka mmoja,alijifungua mtoto anafanana na mimi sanaaa,hata kukataa isingewezekana,nikakubali kulea mtoto. Miaka miwili baadaye nikaanzisha mahusiano mengine,hayakudumu kwa sababu ya huyu mama wa mtoto wangu alikuwa karibu sana nami kimawasiliano juu ya maswala ya mtoto,jambo ambalo lilimkera mpnz wangu hiyo,akaamua kuachana na mimi!

Miaka yote hiyo tulikuwa tunakaa mbali mbali na huyo mama wa mtoto wangu,kutokana na upweke nilimuita Hugo mama wa mtoto nikae naye angalau kidogo niweze kutafuta kumpenda,then tuangalie uwezekano wa kuishi pamoja.(tulikaa kama miezi mitatu hivi kwa matazamio)

Ukweli alikuwa msichana mpole asiye na makuu,nikaamua kumtambulisha nyumbani rasmi,na kutambulika kuwa Huyo ndiye mchumba wangu!(akarejea kwao)

Baada ya mwaka mmoja,nikaenda kwa wazazi wake kuomba ridhaa ya kutambulika pia,wakanipa faini ya kumzalisha binti yao,nikatozwa kiasi fulani cha pesa,baada ya hapo ikawa rasmi pande zote mbili,japo nafsi yangu haikuwa imempenda kwa kweli!!

Mwaka 2014 mimi nilipata kazi,mkoani Tanga,yeye akapangwa Singida (yeye ni mwalimu),basi akawa ananitembelea Tanga mara kadhaa na maisha yakawa yanasonga!
Nilipoanzia kazi kuna binti mmoja alihamia akitokea mkoani Dodoma,tukawa tunasaidiana kazi pale ofisini lakini kwa kweli Moyo wangu ulimpenda yule Dada sanaaa!!(nikawa najizuia sana kuwa naye karibu ili nisijihusishe naye kimapenzi) pasipo kujua kumbe na yeye alikuwa ananipenda sana ila sikuwahi kujua!

Nikawa mwepesi sana kumzungumzia mwanamke wangu(mama mtoto wangu wa Singida) mara kwa mara namuweka profile picture kuongea naye japo ukweli sikuwa na hisia naye kabisa!!!

Kumbe yule dada mgeni alikuwa anakuwa disappointed sana kuona vile,akaomba nimsaidie kutafuta nyumba kwani hakuwa mwenyeji Tanga,nikamuunganisha na mzee mwenye nyumba yangu,akapata apartment pacha na yangu,(hapo ndipo matatizo yalipoanzia)

Tukawa watu wa karibu sana,akija mama wa mtoto wangu wanaongea pamoja na kuishi kiundugu kabisa,na baadaye akiondoka mke wangu anamsifia kuwa mke wangu ni mpole sana!

Akaanza kunisaidia kupika then tunakula wote,kwa kipindi cha kama miezi sita hivi,siku moja tukiwa tunaangalia filamu sebuleni,alionekana kuwa mnyonge sana,akanambia anaomba apumzike chumbani kwangu,nikamruhusu,ilikuwa jioni sana kama saa moja hivi,alipoingia chumbani kwangu mimi nikatoka kwenda kutafuta chakula kwa sababu hatukupika siku hiyo!nilikula huko nikarudi kama saa nne usiku,nikamkuta amelala kabisa,amevua blauzia na amevaa chupi na kanga tu!(kwa kweli nilishtuka nikajikuta kama sipo sawa hivi.

Nilimwamsha lakini hakuamka,niakaingia bafuni kuoga niliporudi alikuwa bado kitandani,nikapanda kitandani nikalala,ilipofika saa saba za usiku uvumilivu ulinishinda nikaanza kumshika maziwa,mapaja,na hatimaye tukaanza romance, na kuivunja amri ya sita!(kumbe lilikuwa kosa kubwa sanaaa)

Tukaingia kwenye mahusiano na ukawa mchezo wetu wa kila siku! Akija mama mtoto wangu ana-pretend kama hakuna kinachoendelea baina yetu,mwaka 2015 miezi ya saba nikata kuvunja mahusiano na mama wa mtoto,nilimshirikisha akaniomba aje tuzungumze juu ya maamuzi hayo,akaja mwezi wa 8/2015,alikaa mwezi mmoja,tuliongea kuhusu kuvunja uhusiano,akaongea kwa Huruma sana na mchozi mengi nikaamua kuahirisha maamuzi yangu,akaondoka!

Mwezi mmoja baadaye akaniambia anahisi ni mjamzito,(mtoto wa pili),nilisononeka sana lakini sikuwa na jinsi,ilibidi nikubaliane na uhalisia,baada ya kuondoka mke wangu tukaendelea na mchezo wetu na co-worker,mara akaanza wivu hataki niongee na mama wa mtoto wangu,nikamwambia ni bora tuachane kuliko kunipa masharti ya eti nisiongee na mpnz wangu mbele yake,na nikamwambia kuwa mchumba wangu ana mimba ya pili,hakufurahia kabisa habari hiyo akaniambia anatamani pia azae,(japo aliongea kiutani utani sana!)

Heeh,mwezi January 2016 co-worker akaniambia amenasa,khaaaa!!!!nikajaribu mbinu zangu zote kumwambia atoe,akasema hawezi kutoa kama sitaki mtoto atamlea mwenyewe,(Jamani wanaume wenzangu,usithubutu kukubali kauli hii kutoka kwa mwanamke,utajuta)

Baada ya miezi kwenda nikajikuta dilemma moja mbaya,huyu wa Tanga,nampenda sana,(sijui kama ndo limbwata au mapenzi natural,nampenda sana!) Wote wana watoto,ila wa Singida anao 2 japo simpendi sana,huyu wa Tanga ana mtoto 1 (nampenda sana,lakini kikwazo kwake ni kwamba kumbe kabla ya kuja Tanga alikuwa ameacha watoto wengine 2 huko kwao,japo hakuolewa)
Kutokana na mazingira aliyopo yule mama watoto wangu wa Singida ilibidi nimnunulie jiko la gas na baadhi ya vitu,jamaa yangu alikuwa anaenda huko nikamuomba niondoke naye kwenda Singida then nichangie mafuta!
Mama yanguuuu!huyu wa Tanga ameleta janga,maana amekuwa akinizuia nisiende Singida tangu juzi,na mimi kwa misimamo yangu nikamwambia siwezi kuacha kwenda ile ni familia yangu,akaniambia ukirudi utanikuta maiti hapa ndani kwako,nikampuuza,nimetoka kununua baadhi ya vitu narudi nyumbani nimemkuta chumbani kwangu akiwa anavuja damu nyingi,(naambatanisha picha mnisamehe wenye hisia kali kuona damu)

Amejichinja mshipa mkuu wa mkono wake wa kushoto,nimepata hofu sana kwa sababu sasa nagundua nipo na mtu hatari sana,kitendo alichofanya leo kimefanya nijutie maamuzi yangu ya mwanzo kabisa,kwanini nilikubali kukaa naye karibu na kuanza naye mahusiano!
Kitendo cha kujichinja mwenyewe si kuna siku anaweza kunivizia aniue huyu mwanamke jamaniii,nawezaje kumtoka mtu huyu katika mazingira haya,na kazini tupi pamoja kila siku!!!

Jamani ndugu zangu natamani siku zirudi nyuma nibadili mfumo wa maisha ila ndo siwezi tena,naombeni mawazo yenu ndugu zangu kwa sababu uwezo wangu wa kufikiri umekoma kabisaaa!!!
 
Back
Top Bottom