Nindo
Member
- Aug 23, 2016
- 71
- 117
Amani kuu na iwe juu yenu,mabibi na mabwana wa JF.Tunapo upa mkono wa buriani 2017,ni vyema kukumbushana baadhi ya mambo muhimu katika maisha yetu ya kila siku.
Ndoa ni taasisi muhimu kwa ukuaji wa jamii yoyote ile.kwa mujibu wa sheria na amri za Mwenyezi MUNGU ndoa ni muungano baina ya mwanaume na mwanamke.
Msingi wa ndoa yoyote ule hujengwa katika misingi ya upendo,heshima na uwajibikaji.Mathalani kwa utamaduni wetu ni kuwa mwanaume anawajibika kuihudumia familia yake mahitaji yote muhimu na hiyo ndiyo asili ya msemo usemao,Baba ni kichwa cha familia!!.
Lazima tukubaliane kuwa kwa kiasi kikubwa Maisha yetu huwakilisha uhalisia wa maisha yetu ya awali.wapo watu wanaotokea katika familia zenye uwezo wa kifedha na wapo watu wanaotokea kwenye familia za hali ya kawaida kiuchumi,Lakini mapenzi hayachagui na mapenzi hushinda vyote.
Ni wazi kuwa,watoto wa kizazi hiki wa kiume,wanakosa misingi ya muhimu katika maisha.pengine ni kwa kutoenda jandoni ama ni kujitoa ufahamu ima ni uzembe tu.
Kumekuwa na dhana potofu inayowasumbua vijana wengi wenye imani kuwa ukipata mwanamke ambaye kwao wana uwezo wa kifedha utakuwa umetoka kimaisha.Hili limewatafuna wengi na linawatafuna wengi walioingia kwenye ndoa kwa ajili ya kutafuta nafuu ya maisha.
Sisemi kuwa ni makosa kuoa mwanamke ambaye anatoka kwenye familia yenye ukwasi,tatizo na makosa ni kuingia kwenye ndoa kwa kufuata pesa za mwanamke na sio kuishi maisha .
Ndoa ni Maisha halisi, katika uhalisia wa maisha mwanaume ndiye kichwa cha familia,kwahiyo ndani ya ndoa utatakiwa kusimamia majukumu yote na endapo utashindwa kwa sababu uliingia ndani ya ndoa ukizitazama fedha za mwanamke,utu na heshima yako vitakuwa rehani na njia panda.
Uvivu ni starehe,wengi huwa wavivu ati kwa kuwa mwanamke anauwezo,wengi wanalia na kuteseka kwani mwanamke akiwa ana provide kila kitu haitakuwa na maana tena kwa uwepo wako kwake,na kiifuatacho ni dharau,masimango na vitimbwi.
Mtoto wa kiume,unapooa lazima upambane kwa ajili ya familia yako,acha kuangalia Mali za mke wako,la sivyo utajitia matatani kwa kuuza utu wako.
Namalizia kwa andiko la biblia kutoka kitabu cha 1 Wakorintho 11,3-12
3 Lakini nataka mjue ya kuwa kichwa cha kila mwanamume ni Kristo, na kichwa cha mwanamke ni mwanamume, na kichwa cha Kristo ni Mungu.
4 Kila mwanamume, asalipo, au anapohutubu, naye amefunikwa kichwa, yuaaibisha kichwa chake.
5 Bali kila mwanamke asalipo, au anapohutubu, bila kufunika kichwa, yuaaibisha kichwa chake; kwa maana ni sawasawa na yule aliyenyolewa.
6 Maana mwanamke asipofunikwa na akatwe nywele. Au ikiwa ni aibu mwanamke kukatwa nywele zake au kunyolewa, na afunikwe.
7 Kwa maana kweli haimpasi mwanamume kufunikwa kichwa, kwa sababu yeye ni mfano na utukufu wa Mungu. Lakini mwanamke ni utukufu wa mwanamume.
8 Maana mwanamume hakutoka katika mwanamke, bali mwanamke katika mwanamume.
9 Wala mwanamume hakuumbwa kwa ajili ya mwanamke, bali mwanamke kwa ajili ya mwanamume.
10 Kwa hiyo imempasa mwanamke awe na dalili ya kumilikiwa kichwani, kwa ajili ya malaika.
11 Walakini si mwanamke pasipo mwanamume, wala mwanamume pasipo mwanamke, katika Bwana.
12 Maana kama mwanamke alitoka katika mwanamume, vile vile mwanamume naye huzaliwa na mwanamke; na vitu vyote asili yake hutoka kwa Mungu. Hukumuni ninyi wenyewe katika nafsi zenu.
Mwanaume ameumbwa kupambana na kulea familia sio kulelewa na mwanamke