ndandawamalenja
JF-Expert Member
- Nov 1, 2012
- 548
- 658
USIMWAMINI MWANAMKE HATA SIKU MOJA!
TRUE STORY
Nilikutana na Sharifa mwaka 2015 akiwa anafanya kazi mgahawani maeneo ya posta ya zamani. Nilipomuona tu siku ya kwanza nikampenda. Baada ya siku 3 za kwenda kula pale tukazoeana nikamuomba namba akanipa tukaanza mawasiliano ya mara kwa mara. Baada ya mwezi tukaanza mahusiano. Mapenzi yalikuwa motomoto, karibu kutwa zima tunachati. Muda wote ambao haudumii wateja na mimi nikiwa free tunachati tu, mpaka wenzake wakawa wanamshangaa wanamwambia huyo aliyempata safari hii kanasa pabaya (Nikienda pale kazini kwake kuna rafiki yake alikuwa ananipa udaku).
Nikamuuliza ilikuwaje akawa singo, akasema AMEACHANA NA JAMAA YAKE SIKU SI NYINGI KABLA HAJAKUTANA NA MIMI. Penzi lilikolea hakuna mfano, baada ya miezi miwili tu alikuwa muda wote yupo kichwani mwangu (naamini hata yeye kwake ilikuwa hivo kwa sababu nisipomtafuta masaa mawili mfululizo ni kesi). Nakumbuka kuna siku sijui kulitokea nini sikumtafuta toka asubuhi mpaka jioni, nikampigia saa 3 usiku video call, hicho kilio alicholia ni kama amefiwa.
Toka siku hiyo nikaahidi haitatokea tena kutomtafuta kutwa nzima. (Kumbuka yeye hawezi kunitafuta kwa sababu hajui niko kwenye mazingira gani, nina mke na mtoto). NILIPOMUULIZA ANAKAA WAPI AKASEMA ANAKAA KWA DADA YAKE TEMEKE. Kwamba huyo ni dada yake wa pili kuzaliwa ndani mwao (KUMBE NI MPANGAJI MWENZIE). Wa kwanza yupo kijijini, wa pili ndio huyo anaekaa kwake, wa tatu anakaa Mbagala, wa nne kaka yake anakaa Mbezi na wa tano ni yeye (wa mwisho).
Mapenzi yakapamba moto, kukutana ni jumamosi au jumapili, au wiki zingine jumamosi na jumapili. Tukikutana tunashinda ndani (lodge) mpaka usiku ndio anaondoka kwenda kwao na mimi naenda kwangu. Kwa miaka miwili mfululizo nadhani hatujawahi kuruka jumamosi hata moja bila kukutana. Sijawahi kutaka kufika anakokaa kwa sababu niliona ni mapema kuanza kutaka kwenda kwa dadake, na kuna namna ni kama alikuwa anapotezea nikiuliza habari za anakokaa na mimi nikawa sitilii maanani sana Kwenda kwao.
Lakini kidogo kidogo akawa ananipa maelezo ambayo naweza kufika mpaka mtaani anakokaa. Ila hakuwahi kunikaribisha huko kwao. Tulipendana mnooo, kwa siku alikuwa ananitumia picha hata kumi akiwa kwenye mazingira tofauti. Nikiuliza yuko wapi anafanya nini muda huo jibu lake inakuja picha (selfie). Halafu tunaendelea kuchati. Siku za kukutana mara nyingi yeye ndio alikuwa anakuja maeneo ya Sinza ndio tunakutania huko, ikafika kipindi nikawa naenda maeneo ya Temeke tunaingia gesti za huko, sio mbali sana na anakokaa. Ratiba ikawa inabadilika badilika.
Pamoja na kukutania lodge za maeneo ya kwao, hakuwahi kunikaribisha nikapajue kwao. Ila alinionyesha kwa mbali sana mnara wa simu (vodacom) akasema anakaa karibu kabisa na huo mnara, akanitajia na rangi ya nyumba wanayokaa.
Picha lilikuja kuanza mwaka 2017. Nilipata safari ya kuzunguka mikoa mitano ya Tanzania bara nikaamua kusafiri nae tukale Maisha. Hizo zilikuwa wiki 3 za furaha kubwa kuliko kipindi chochote kwenye maisha yangu, siji kuzisahau.
Baada ya kurudi safari haikupita wiki mbili akaniambia ni mjamzito. Nikafurahi sana, kwa sababu nilikuwa natamani siku zote anizalie mtoto na kama sio kipingamizi cha ndoa nadhani ningemuoa haraka sana tulivokutana. Tatizo nilikuwa na mke tayari. Kuna siku nilienda kufanya mishe Mbagala na yeye asubuhi alikuwa ameniambia anaumwa (mimba ilikuwa inamsumbua sana ile), basi nikaamua kwenda pale bila kumwambia.
Nikafika mpaka pale bila yeye kunielekeza, nilipofika koridoni nikamkuta jirani yao akanionyesha chumba chao nikaingia. Akashangaa sana kwa sababu hakujua kuwa naenda pale, lakini akanipokea vizuri tu tukapiga stori tukatoka wote tukaenda duka la madawa tukanunua dawa akarudi kwao mi nikarudi zangu ofisini.
Sasa humo alimonikaribisha aliniambia ndio sebuleni kwa dada ake, chumba cha pili ndio cha kulala. Ila yeye analala sebuleni (kulikuwa na kila kitu mpaka kitanda). KUMBE NI CHUMBA CHAKE alichopangishiwa na yule jamaa aliyeniambia waliachana (MPAKA WAKATI HUO WALIKUWA BADO WAKO PAMOJA na sikuwahi kushtuka kuwa yuko na mtu na jamaa hajawahi kushtuka kuwa anaibiwa). Jamaa nae alikuwa na mke wake hivo anakujaga mara moja moja sana. Akija anapiga zake bao chap anarudi kwake, halafu haonekani tena mpaka baada ya mwezi au miwili (alikuwa dereva wa magari ya safari ndefu).
Kilichofanya nisishtuke kabisa kuwa tuko wawili ni kwamba jamaa yake hanaga mawasiliano ya simu ya mara kwa mara. Nadhani akimhitaji alikuwa anaenda tu geto alikompangishia bila kupiga simu wala kutuma meseji. Na akienda hakagui simu hata mara moja kwa sababu angekuwa anakagua angeshajua kitambo kuwa demu wake yuko na mimi. Demu hajawahi kufuta meseji yangu hata moja toka tulipokutana. Na picha zote alizonitumia wasap hajawahi kufuta kwenye simu yake hata moja hata zangu nilizomtumia mimi.
Na kumbukumbu ya simu nilizompigia hajawahi kufuta hata moja. Kitu kingine, nikiwa nae lodge simu yake inakaa hapo mezani muda wote haigusi hata mara moja, na ikipigwa au ikiingia meseji na mimi niko karibu nayo, ataniuliza mimi ni nani anapiga au nani katuma meseji. Yani alikuwa demu ambaye hana mambo mengi kabisa, nilimpenda mnooo na alijenga mazingira ya mimi kumuamini asilimia 100 (sipendi kabisa madem ambaye ukiwa naye muda wote yuko na simu mkononi, huyu alikuwa wa kwanza kukutana nae wa aina ya pekee). Kama mara mbili imewahi kupigwa simu tukiwa pamoja, aliempigia akamfokea sana, halafu yeye hakujibu. Nilipokuwa namuuliza huyo nani akawa anasema ni yule jamaa waliyeachana siku hizi anamsumbua sana anataka warudiane, na yeye hataki kwa sababu ameshakuwa na mimi. (KUMBUKA MPAKA HAPO WALIKUWA HAWAJAACHANA ila mimi nilikuja kujua baadae sana walipochana kweli baada ya demu kujifungua na mimi kumuhamisha demu kutoka pale (”KWA DADA YAKE”) nikamleta maeneo ya jirani na ninakokaa ili iwe rahisi kuwaona na mtoto kila siku).
Kuna wakati akaniambia dadake amesafiri kaenda nyumbani Iringa. Basi siku moja asubuhi tu kabla hajaamka nikaenda pale (Kazi alikuwa ashasimama kwa ajili ya ujauzito). Toka siku hiyo tukaacha kwenda lodge, mambo yote tunamalizia hapo (KUMBUKA KAPANGISHIWA NA MWANAUME ila mimi najua ni kwa dada yake). Nikawa naenda mara kwa mara naingiaga tu kama kwangu.
Aliyejifanya dada ake ananipokea fresh nashinda hapo. Wanapika misosi tunakula kila nikienda. Tunakaa chumbani tukitosheka tunakaa koridoni tukichoka tunakaa nje, yani nikawa huru mno. ILA KUNA MACHO WAPANGAJI WENZIE WALIKUWA WANANIANGALIA KAMA YA KUNIAMBIA KITU mi sina hili wala lile, nimezama kwenye penzi zito. Kabla ya hapo nilikuwa nishaanza hata kuchangia kodi, kwamba mle sebleni anamolala kodi nalipa mimi, nikamwambia amwambie kabisa dadake. Na alikuwa na mtoto yuko darasa la sita huko kijijini kwao (kwa bibi yake huyo mwanamke wangu) nikawa nasaidia kumhudumia.
Picha likaendelea. Siku moja akaniambia anaumwa, mimi mapema tu nikatokea pale. Nikaingia chumbani nikavua zangu shati nikabaki na singlet, akaniandalia chai nikanywa baadae tukatoka tukakaa koridoni, nikamwambia sikai sana ntaondoka muda si mrefu.
Tukiwa hapo koridoni akaingia jamaa, alipofika karibu na chumba cha demu (WAKATI HUO MI NAJUA NI SEBLENI KWA DADAKE) akanisalimia mimi HALAFU BILA KUPIGA HODI WALA NINI akaingia humo chumbani. Demu akasimama akamfuata huko ndani, nikasikia jamaa anaunguruma kama analalamika kitu kama dakika moja nzima, ila maneno nilikuwa siyasikii. Halfu demu akatoka akamuacha jamaa huko ndani. Akaniuliza kama anisindikize au vipi kwa sababu nilikuwa nimemwambia naondoka sasa hivi.
Kwa namna yule jamaa alivoingia nikawa na maswali mengi kichwani nikawa nimeghairi kuondoka ili jamaa aondoke nimuulize demu yule ni nani. Kwa hiyo nikamjibu kuwa nimeghairi kuondoka ntaondoka jioni (Hiyo ilikuwa saa 5 hivi asubuhi). Kwa unyonge akarudi kule ndani, nikasikia jamaa sasa linatukana matusi, kuwa halipendi ujinga na u.s.e.n.g.e u.s.e.n.g.e, na maneno mengine makali makali. Mengine nikawa sisikii mengine nasikia, kama dakika 2 hivi. Halafu jamaa likatoka likabamiza mlango kwa nguvu huku linaondoka linamwambia demu aache upumbavu wake kabisa. Hilooooooo likapotea zake……
ITAENDELEA KESHO***

nimesoma tu neno itaendelea kesho