Usiku wa mwisho wa MH370

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,634
697,867
Ni nini hasa kilitokea kwenye ndege ya MH370, siri kubwa na ya ajabu katika historia ya ndege

"Ndege ya Malaysia MH370 iliruka Machi 28, 2014 na kutoweka na hadi leo, hawajui ilitua wapi, ilikaa wapi. au chochote kuhusu ndege hiyo.

Ikiwa na na idadi ya abiria 239 MH370 ilipaa kutoka Kuala Lumpur na ilitakiwa kuelekea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Beijing nchini China.

safari hiyo ilikuwa na muda wa saa 6 na baada ya dakika 20 kuruka ndege ilifika urefu wa futi 35000 na hatimaye baada ya ndege kufika kwenye mnara wa kuangalia wa Vietnam mida ya saa 6:41 usiku ilipotea kwenye rada, huu Ndio ulikuwa usiku wa mwisho wa ndege iyo iliyo gharumu mabilioni ya pesa.

Pia ulikuwa usiku wa mwisho kwa watu zaidi ya 238 waliokuwemo kwenye ndege hio saa 6: 42 mawasiliano yote kutoka chumba cha marubani na vituo vya rada yalitoweka completely ,

Inakadiliwa kuwa watu wote waliokuwepo kwenye ndege hio wamepoteza maisha , japo hakuna hata mwili mmoja uliopatikana , kwani hakuna hata chembe ya mabaki yaliyosadikika yalikuwa ni ya MH370 kwa wakati huo

Hili ni miongoni mwa matukio ya ajabu katika historia za ajari za ndege Angani .MH370 ilitoweka kwana keamba haijawahi kupaa na hakukuwa na kitu kwenye rada kabisa wakati inapotea.

Kikosi cha uokoaji kilianza kutafuta kila mahali katika Anga na bahari walieneza kila aina ya uokoaj ili kuona kama kuna kitu wangefanikisha , yalitengwa maeneo maalumu kwa ajili ya msako huo , amabako zilitumwa meli 34 na Ndege 28 , kama haikutosha mataifa 7 yaliungana kwa ajili ya zoezi hilo lilokuwa gumu lisilo na hata chembe ya matumaini .

Zaidi ya dola Milioni 200 za kimaerekani , zilisukumiwa huko kama bajeti ya utafutaji wa ndege hio lakini , juhudi hizi ziligonga mwamba

Baada ya wachunguzi, kukagua mfumo wa satelaiti walibaini kuwa ndege hii iliendelea kuruka kwa zaidi ya masaa 7 baada ya kutoweka. Na hili ndilo lililofanya jambo hili kuwa la kustajabisha zaidi

Mwaka 2018 zoezi la utafutwaji wa Ndege hii , ulisitishwa kwani ulionekana kugharimu mabilioni ya pesa bila faida yoyote , mpaka kesho hakuna taarifa yoyote kuhusu sehemu iliyopoNdege hii.

Maelezo yaliyokubalika zaidi ya mkasa huo ni kwamba ndege ilianguka tu baharini, kwa sababu ya kutokana na hitilafu ya mitambo. Katika miaka michache iliyofuata kumekuwa na vipande vitatu vya uchafu vilivyotambuliwa vyema kuwa vinatoka kwenye MH370, na vipande vingine 30 vinavyokisiwa ni vya MH370.

Wizara ya Uchukuzi ya Malaysia ilisema sauti ya mwisho kutoka kwa chumba cha marubani cha Flight 370 ilikuwa ni. (Goodnight three seven zero )

Kwa jumla, familia 19 zilidai simu za wapendwa wao waliopotea ziliita bila majibu kwa siku nne baada ya MH370 kutoweka. Mwanamke mmoja hata alienda kwenye runinga ya China kudhihirishia umma kuwa simu ya kaka yake ilikuwa bado ikiita baada ya ndege kudaiwa kutoweka.

Mbali na kutokupatikana kwa mwili wowote ,Siku 5 baada ya Ndege kupotea , meneja mkuu wa MH370 alitangaza uwezekano mkubwa wa watu wote waliokuwa wakisafiri na MH370 wamepoteza maisha

Nadharia nyingi zimeibuka kujaribu kuelezea siri ya ndege hii MH 370, lakini hadi leo hakuna nadharia hata moja iliyothibitishwa. sababu kubwa ikiwa ni kutokupatikana kwa BLACK BOX ya MH370.
FB_IMG_1698685091502.jpg
 
Hao marubani nahisi wapo hai pahala fulani baharini maana waliagana na ndege na huenda walijirusha na mianvuli kutokomea kusikojulikana baada ya kuona uwezo wao wa kuiongoza three seven zero umeyeyuka.
Wizara ya Uchukuzi ya Malaysia ilisema sauti ya mwisho kutoka kwa chumba cha marubani cha Flight 370 ilikuwa ni. (Goodnight three seven zero )
 
Hao marubani nahisi wapo hai pahala fulani baharini maana waliagana na ndege na huenda walijirusha na mianvuli kutokomea kusikojulikana baada ya kuona uwezo wao wa kuiongoza three seven zero umeyeyuka.
Pia ulikuwa usiku wa mwisho kwa watu zaidi ya 238 waliokuwemo kwenye ndege hio saa 6: 42 mawasiliano yote kutoka chumba cha marubani na vituo vya rada yalitoweka completely ,


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndege Ilitafutwa Na Mataifa Makubwa Duniani Yenye Nguvu Ya Technology

Ila Kadiri Muda Ulivyokwenda Ikawa Kama Usiku Wa Deni.

Hatimaye Miamba Ikakata Tamaa Mpaka Kesho
 
Back
Top Bottom