Ujue mtaa ambao Kila Mwananchi anamiliki ndege nyumbani kwake

george aloyce

JF-Expert Member
Aug 22, 2017
1,187
1,834
ENEO AMBALO KILA MKAZI ANA MILIKI NDEGE

Tumezoea kuona ukipita mitaani utakuta nje ya makazi ya watu kuna maegesho ya magari lakini imekuwa tofauti kidogo kwa eneo la Cameron Park, lililopo California, nchini Marekani ambapo wakazi wake wengi wanamiliki zaidi ndege kuliko magari, na kwamba wameweka maegesho ya ndege zao pembeni mwa nyumba zao.
.
Eneo hilo ambalo hujulikana zaidi kama Cameron Airpark Estates, lilijengwa mnamo mwaka 1963 na lina nyumba zaidi ya 100, na barabara zake za mitaani zimejengwa kwa upana zaidi kuliko njia ya kawaida ya kurukia ndege, ili magari yapite kwa usalama na wanaoendesha ndege waweze kuendesha ndege zao kutoka kwenye nyumba zao kuelekea kwenye njia ya kurukia ndege, kwa usalama bila kupata changamoto.
.
Eneo hilo lina vitu vingi vya kuvutia na kipekee, ukilinganisha na mitaa mingine ambapo wakazi wake wengi wanadaiwa kuwa ni Marubani na Marubani wastaafu, pia alama za barabarani kwenye eneo hilo zimetengenezwa kwa urefu wa chini ya futi 3, ili zisiguse mabawa ya ndege, na kwamba majina ya barabara za mitaa kwenye eneo hilo ni ya makampuni yanayojishughulisha na uundaji wa ndege mfano Boeing Road.

1710654578561.jpg
 
Back
Top Bottom