Ushauri wa bure kwa ATC

Mparee2

JF-Expert Member
Sep 2, 2012
2,586
4,274
Baada ya shirika letu pendwa kuendelea kushusha vyombo (madege mapya na ya kisasa) ni wakati sahihi wa Kuajiri Marketing Manager Mzungu na pengine Ops Manager. Wenzetu wapo smart sana, anapewa malengo asipofikia anaondoka, tunaleta mwingine hadi kieleweke.... (Ila asiingiliwe mipango yake na ndege zikikodishwa, zilipwe) au pengine itengwe Ndege moja kabisa kwa ajili ya shuhuli za Serikali kuepuka malumbano

Siwachukii wa Afrika ila kwa hii Elimu yetu ya kujifunza kucopy na kupaste wanachofanya wengine; haina nafasi tena ukisha ingia kwenye soko la ushindani wa kimataifa kwani, unatakiwa uje na strategies zako mwenyewe....

Ikiwapendeza apatikane mtu ambaye hajafanya kazi ukanda wa Eastern and Southern Africa kwani mashirika mengi ya ndege ya ukanda huu yanaboronga kasoro ya ET pekee.

Hali inayo endelea kwa sasa hapo ATC sioni ikiwa na Afya kwani wana Cancel sana Safari, hata hiyo faida wanayosema wanapata haiwezi kuwa endelevu, kwani uki cancel ukaunganisha ndege unapata faida ila inakuwa ya muda mfupi tu; kwani baada ya muda wateja wengi wanahama na hivyo kufulululiza hasara....
 
Back
Top Bottom