ERTUGRUL BEY
JF-Expert Member
- Aug 6, 2020
- 11,529
- 21,530
My people,
Hii ni kwa watafutaji na wahangaikaji wote popote mlipo,endeleeni kupambana.Kwa watu ambao wana vipato vizur hawawezi kujua kwamba kuna watu ambao inabidi mida ya lunch time wakaushe kimya bila kula,sio kwamba hawapendi ila ni kwasababu hisabati hairuhusu kupata mlo wa mchana.
Unakuta mtu akifanya hisabati zake za kula home,Bill mbali mbali bila kusahau nauli ya kwendea mzigoni,anajikuta bajeti iko tight kinoma,tukio lolote la kucheza na bajeti hiyo,inahatarisha ratiba nyengine za maisha
Watafutaji wote msikate tamaa wala msijisikie vibaya,hizo ni stage za maisha tu,wengi sana wameyapitia hayo akiwemo the bey himself,kwahiyo hakuna kujisikia unyonge keep head up,yatapita tu,siku zote tambua maisha ni mchakato kwahiyo nawe upo kwenye mchakato,ipo siku itakuwa historia kwako.
Endelea kupambana,hata huko mambele kuna watu wanaskip meals kama kawaida na wanasongesha maisha kama kawa,wewe sio wa kwanza kuna mamia ya watu wapo hivyo pia.
Kataa unyonge na endelea kupambana one day itakuwa historia,itabaki kuwa sehemu ya mapito ambayo uliwahi kupitia katika maisha yako
Ni hayo tu!