Usife kwanza mpenzi wangu

Usife kwanza mpenzi wangu

[h=1]Usife kwanza mpenzi wangu (29).....[/h]
Siku chache baada ya Levina kumtambulisha mpenzi wake Deo kwa Cleopatra na kufanikisha kumpatia kazi kwenye ofisi ya baba yake, dhambi ya usaliti inachukua nafasi yake.

Cleopatra anatumia ushawishi wa pesa na madaraka yake kumpata Deo kirahisi na kufanikiwa kujivinjari naye. Levina anahisi kitu ingawa anakosa ushahidi. Wazazi wake bado wanamuandama wakimtaka aachane kabisa na Deo kwa kuwa hana hadhi ya kumuoa.
Je, nini kitandelea? Shuka nayo…

"Huwa unatumia kinywaji gani? Namaanisha bia gani?"
"Pombe huwa sinywi, labda soda tu."

"Leo kwa kuwa uko na mimi , naomba unywe japo kidogo uchangamshe akili," alisema Cleopatra huku akiendesha gari lake kuelekea Kunduchi Wet and Wild Hotel. Mawazoni mwake, alikuwa akipanga mengine, na aliamini ile ndiyo siku yake ya kumfaidi Deo.

"Twende tukakae kule pembeni," alisema Cleopatra kwa sauti iliyojaa mbwembwe za kimalavidavi. Akamshika mkono Deo na kumuelekeza mahali pa kukaa.

Walienda kukaa kwenye kona moja iliyokuwa imejificha, wakaanza kupiga stori huku Cleopatra akitumia uwezo wake wote kumtega Deo.
"Tuongeze raundi nyingine," alisema Cleopatra huku akimalizia chupa ya kwanza ya kilevi alichozoea kukitumia.

Japokuwa Deo hakuwa na kawaida ya kunywa pombe, kutokana na ushawishi wa Cleopatra alijikuta akipiga ‘moja moja' kukwepa kuonekana dhaifu mbele ya mrembo yule. Kadri muda ulivyokuwa unazidi kusonga mbele, ndivyo pombe zilivyokuwa zinawakolea vichwani mwao. Wakaacha kuoneana aibu kama ilivyokuwa wakati wanaingia eneo hilo.

"Deo! Naomba nikwambie kitu."
"Niambie Cleopatra, nakusikiliza."
"Naomba usinifikirie vibaya kwa hili nitakalokueleza, nimevumilia nimeshindwa mwenzio."

"Wala usijali. Jisikie huru kuzungumza chochote."
"Deo, nakupenda Deo. Naomba uwe wangu mahabuba."
"Lakini Cleopatra, si unajua kuwa mi niko na rafiki yako Levina na ndiye aliyenikutanisha na wewe?"

"Najua sana Deo, lakini Levina ana nafasi yake, na mimi naomba unipe nafasi yangu."
"Hapana Cleopatra, sipendi kumkosea Levina, amenisaidia vingi sana."
"Nikubali Deo, itakuwa siri yetu, hakuna atakayejua."

Licha ya Deo kujivunga sana, Cleopatra aliendelea kumganda kama ruba akimtaka akubali ombi lake la kuwa wapenzi. Kwa kuwa tayari kilevi kilikuwa kimeanza kukolea ndani ya vichwa vyao, Cleopatra hakuona aibu tena na hakutaka kulaza damu, akajisogeza mwilini mwa Deo na kujilaza kifuani.

Uvumilivu ulianza kumshinda Deo, akawa haeleweki anachokiongea kama amemkubali Cleopatra au la.
"Tuondoke dear, mi nimechoka nataka kwenda kulala."
"Si utanifikisha nyumbani kwanza ndiyo wewe uelekee kwako."
"Hapana Deo, mwenzio naogopa peke yangu. Nifikishe kwanza nyumbani kwangu."

Cleopatra na Deo waliondoka eneo lile wakiwa wamekumbatiana, wakaongozana hadi kwenye gari walilokuja nalo. Deo akakaa pembeni huku Cleopatra akiwa nyuma ya usukani.

Breki ya kwanza ilikuwa nyumbani kwa Cleopatra. Walipofika tu, Cleopatra alishuka haraka haraka na kumshika Deo mkono, akawa anamvutia ndani kama kondoo anayepelekwa machinjioni.

Deo hakuwa na ujanja tena, yeye mwenyewe alishadatishwa na yote yaliyokuwa yanafanywa na Cleopatra.
Akaamua kujiachia. Dakika chache baadaye, walikuwa juu ya uwanja mkubwa wa fundi seremala, chumbani kwa Cleopatra, wakiwa na suti za kulalia.

***
Levina alikuwa chumbani kwake, akifanya usafi wa kawaida. Pingamizi la wazazi wake juu ya kumpenda Deo, lilimfanya muda mwingi awe anajifungia chumbani peke yake.

Mawazo na fikra zake zote zilikuwa juu ya Deo, alimpenda kiukweli na moyoni alijiwekea nadhiri kuwa lazima aolewe naye.
"Nimemkumbuka Deo wangu, ngoja nimcheki hewani," alijisemea Levina huku akijilaza kitandani na kuchukua simu yake ya mkononi.

Simu ya Deo ilikuwa ikiita bila kupokelewa, hali iliyomtia hofu Levina. Alirudia mara ya pili lakini hali ikawa ni ile ile. Aliendelea kujaribu mara kadhaa lakini haikupokelewa.

"Amepatwa na nini Deo wangu? Siyo kawaida yake."
Aliongea Levina huku akitafuta viatu vyake kutoka chini ya kitanda. Alishindwa kuvumilia, akahisi labda Deo amepatwa na tatizo hivyo akaamua kumfuata nyumbani kwake. Alitoka nyumbani kwao bila kuaga, akanyata hadi mlango wa nje na kuwaacha baba na mama yake wamekaa sebuleni.

Alipofika kwa Deo, alikutana na ukimya wa ajabu ambao uliashiria kuwa Deo hakuwemo ndani, hali iliyozidi kumtia hofu.
"Atakuwa wapi muda huu?" Alijiuliza Levina bila kupata majibu.

Alijaribu tena kupiga namba yake, lakini safari hii simu ya Deo ikawa haipatikani kabisa. Akahisi labda huenda amezidiwa na kazi ofisini kwao ndiyo maana amechelewa kurudi. Akaamua kumpigia simu shoga yake Cleopatra ili kujua kulikoni.

"Namba ya mteja unayempigia, haipatikani kwa sasa, jaribu tena baadaye," majibu yale kutoka kwenye simu yake ya mkononi yalimmaliza nguvu kabisa.
Akilini mwake kengele ya hatari ilishaanza kulia, akahisi huenda shoga yake anamzunguka kwa kutoka na Deo kwani tangu siku ya kwanza wakati anamtambulisha kwake, Cleopatra alionekana kumzimikia.

Hakutaka kuamini kuwa muda huo inawezekana wakawa pamoja kutokana na jinsi alivyokuwa anamuamini Deo. Kitu pekee alichoona kinafaa ilikuwa ni kurudi nyumbani kwao kupumzika kwani hakuaga wakati anaondoka, jambo ambalo alijua litawaudhi wazazi wake.

Moyoni alikuwa anaumia sana kumkosa Deo, kipenzi cha nafsi yake usiku ule, akawa hapati majibu ni wapi aliko, yuko na nani na anafanya nini. Wivu wa mapenzi uliwaka mtimani mwake.

"Ulikuwa wapi usiku wote huu?" Baba yake Levina, Mzee Msammu alimpokea kwa maswali makali.

"Na wewe Levina, mpaka nashindwa kukutetea kwa baba yako. Ulikuwa wapi saa hizi? Au ndiyo huyo ‘shamba boy' wako anakuzuzua?" Alidakia mama yake. Levina hakuwa na jibu, akainamisha kichwa chake chini.

Akilini hakuwa anajali alivyowaudhi wazazi wake kwa kuondoka bila kuaga, ila alikuwa akifikiria kwa nini Deo hayuko nyumbani kwake usiku kama ule, huku simu yake ikiwa inaita bila kupokelewa na baadaye ikawa haipatikani.
"Si tunaongea na wewe? Mbona hujibu? Kiburi siyo?"

***
Deo alishtuka kutoka kwenye usingizi mzito na kujikuta yuko mikononi mwa mwanamke tofauti na yule aliyemzoea.
"Hee! Imekuwaje tena?" Alijiuliza Deo huku akiitazama saa ndogo iliyokuwa pembeni ya kitanda. Ilikuwa ni tayari saa sita za usiku."

"Oooh! Shit." Alijisemea baada ya kugundua kuwa kumbe alikuwa amelala na Cleopatra kitanda kimoja, tena wote wakiwa kama walivyozaliwa. Hakutaka kuamini kama amemsaliti kirahisi namna ile mpenzi wake aliyemtoa mbali, Levina.


Je, nini kitaendelea? Usikose
 
USIFE KWANZA MPENZI WANGU....EPISODE.30.

Bila kutarajia Deo amejikuta akitoka na bosi wake Cleopatra. Haikuwa dhamira yake, ni baada ya kuleweshwa na mwanamke huyo.

Siku nyingine, Deo akiwa ametoka na Levina, simu yake inaita, alipoangalia jina la mpigaji akaona ni Cleopatra, akaogopa kupokea.

Kitendo hicho kikasababisha Levina amnyang'anye ile simu. Je, nini kitaendelea?
Sasa endelea...

LEVINA alikuwa amevimba kwa hasira, alianza kuhisi mchezo mbaya ukiendelea kati ya Cleopatra na Deo wake. Aliiangalia ile simu mpaka ikakatika yenyewe.

"Hebu niambie ukweli, anataka nini kwako huyu mwanamke?" Levina akamwuliza Deo.

"Hapo utakuwa unanionea mpenzi wangu, unadhani ni rahisi kugundua kitu kilichopo ndani ya kichwa cha mtu mwingine? Sijui ana shida gani, lakini itakuwa ni mambo ya ofisini!"
"Ofisini mpaka Jumapili?"

"Sijajua mpenzi wangu. We' achana naye bwana..."
"Niachane naye kirahisi-rahisi tu!" Levina akasema kwa hasira na muda huo huo tena simu ikaanza kuita.

Safari hii Levina akaipokea haraka...
"Cleopatra habari yako?" Sauti yake ilionesha kabisa ilikuwa ya shari.

"Poa shoga, enheee vipi mzima wewe?"
"Mzima. Vipi tena simu na shemeji yako saa hizi?"
"Kwani vipi Levina? Inamaana hatuaminiani? Nataka kumpa maagizo muhimu ya kesho, maana kuna mahali nitapitia asubuhi, naomba kuzungumza naye!" Cleopatra akasema kwa kujiamini sana.

"Ok! Ongea naye huyu hapa..." akasema akimpatia simu Deo.
Cleopatra hakuwa na lolote, zaidi ya habari za mapenzi, lakini kwa sababu tayari alishasikia sauti ya Levina, hakutaka matatizo, akajifanya kumuagiza Deo kazi fulani za ofisini.

Ilikuwa kama kipande kwenye sinema ambacho kilipata wasanii walioweza kuuvaa vyema uhusika.

Deo aliweza kuzungumza na Cleopatra na kujifanya kweli walikuwa na mazungumzo ya kikazi. Kwa kiasi kikubwa walifanikiwa kumfumba macho Levina, ingawa naye hakuwa na uhakika wa asimilia mia moja.

Baada ya mazungumzo kukamilika, Levina alionekana hana furaha kabisa, lakini akajitahidi kuilazimisha.
"Kwani mpenzi wangu, bado unamuwaza vibaya Cleopatra?"

"Hata kama ungekuwa ni wewe ungeweza kama ninavyowaza mimi."
"Lakini si ulisema Cleopatra ni rafiki yako na mnaaminiana?"
"Ndiyo."

"Sasa kwa nini unamfikiria mabaya? Wakati mwingine ukimfikiria mwenzako mabaya, hata kama alikuwa hana mpango wa kufanya kitu kibaya anaweza akafanya."

"Lakini mimi ndiyo namjua Cleopatra, naufahamu udhaifu wake na aina ya wanaume anaowapenda!"

"Ndiyo kusema mimi nachukuliwa tu kama mzigo, yaani sina hisia wala uamuzi wangu peke yangu kama mwanaume? Unadhani anaweza kunikokota tu bila uamuzi wangu mwenyewe?

"Kwani unanichukuliaje Levina? Au kwa sababu ulinipata kirahisi ndiyo maana unahisi mwanamke yeyote pia anaweza kunipata? Kumbuka mimi nilikupenda kwa mapenzi ya dhati ndiyo maana nipo na wewe muda huu.

"Sijafurahishwa kabisa na maneno yako, siamini kama kweli hatuamini kwa kiwango cha juu kiasi hicho. Tafadhali sana Levina usinivunjie heshima yangu! Naumia sana moyoni mwangu kwa jinsi unavyonihisi, usivyoniamini!" Deo aliongea maneno hayo kwa uchungu sana.

Yalikuwa yanatokea kinywani tu, ndani ya moyo wake kulikuwa na kitu kingine kabisa. Deo alikuwa ameshatekwa na Cleopatra.
"Samahani sana mpenzi wangu, sikuwa na nia ya kukuudhi, lakini Cleopatra ndiyo amenipa wasiwasi."

"Hata kama...huyo ni Cleopatra. Inamaana mimi huniamini kwa sababu tu Cleopatra anaonekana labda kuwa na nia ya kuninasa?"
"Sijasema hivyo dear...naomba unisamehe mpenzi wangu!"
"Ok! Yaishe!"

Mahali pale hapakuwa na amani tena kwao, wakaamua kuondoka zao. Safari yao iliishia nyumbani kwa Deo, Sinza, ambapo walikaa hadi usiku wa saa 3, ndipo Levina aliondoka.

***
"Vipi yule ---- alishtuka?" Cleopatra alimwuliza Deo, asubuhi wakiwa ofisini.
"Kama ni sanaa, hapa ndiyo nyumbani. Nimemuweka sawa, hajashtuka kabisa."

"Safi sana...sasa Deo mpenzi wangu nimekupandisha mshahara mara mbili ya ule uliokuwa unapata awali. Katika barua yako nimeandika kwamba umepandishwa kutokana na kutimiza vyema majukumu yako ya kazi.

"Nimeandika hivyo lakini ukweli ni kwamba, nimekuongeza mshahara kwa sababu umeweza kutimiza majukumu yako vyema ya kimapenzi kwangu. Hongera sana..." akasema Cleopatra akimkabidhi Deo barua yake.

Deo hakuamini!
Akabaki anaikodolea macho ile barua akitamani kuifungua. Akiwa anataka kuifungua, Cleopatra akamzuia.

"Utafungua ofisini kwako, haraka ya nini mwanaume?"
"Poa mpenzi wangu!"
"Kazi njema."
"Ok!"

***
Penzi la siri kati ya Cleopatra na Deo lilizidi kukolea siku hadi siku. Miezi sita imekatika tangu walipofungua ukurasa huo wa mapenzi. Deo amekuwa muda mwingi zaidi na Cleopatra kuliko Levina.

Mapenzi yake kwa Levina yamefifia kabisa, hachagui majibu ya kumpa na hamjali kabisa. Jambo hilo linamuumiza sana Levina moyo wake lakini Deo hajali.

Ndani ya moyo wake, anashangaa akimpenda zaidi Cleopatra ambaye alikuwa mkali zaidi faragha kuliko Levina. Alishindwa kuelewa jambo moja; Deo hakumpenda Cleopatra kwa mapenzi ya dhati, fedha na mapenzi ndivyo vilivyomchanganya.

Usiku huu akiwa amelala, anagutuswa na simu yake ya mkononi iliyokuwa ikiita. Akajivuta taratibu na kuuruhusu mkono wake kuchukua simu iliyokuwa pembeni ya mto na kuangalia jina la mpigaji!

Ni Cleopatra!
Usiku huu?
Akapokea...

"Nina jambo moja muhimu sana nataka kukuambia Deo...nimechagua muda huu, maana naamini akili yako itakuwa imetulia na majibu utakayonipa yatakuwa yanatoka moyoni mwako..." Cleopatra alianza kusema mara baada ya Deo kupokea simu.

"Ni nini mpenzi wangu?" Deo akauliza.
"Naomba UACHANE na LEVINA ili UNIOE mimi, tafadhali sana nakuomba.

Kumbuka mimi na wewe tunapendana na sioni sababu ya kuendelea kuibana. Nina mali nyingi za wazazi wangu ambazo kwa kutumia akili yako, tutaziendeleza na kuishi maisha mazuri.

Tafadhali mpenzi usiseme hapana...naomba unikubalie!" Sauti laini ya Cleopatra ilisikika kwenye spika ya simu ya Deo.

Deo hakuwa na jibu la haraka. Haikuwa rahisi kiasi kile kumjibu Cleopatra! Kila alipokumbuka alipotoka na Levina, alichanganyikiwa na kinywa chake kuwa kizito kufunguka.

Je, nini kitatokea? Itaendelea Leo jioni.............



 
Hii hadithi,ni nzuri jamani acheni!! Na Mapenzi yana Wigo mpana!sana,Ukiwa hujaingia kwenye Mapenzi ukasoma hii kitu! Lazima moyo wako upate Shokk!
Vilevile ukiwa kwenye mapenzi na ci ndoa ukasoma hii ki2 lazima moyo wako upate Taharuki kwa asilimia fulani!,Big up Mzizi mkavu
 
Last edited by a moderator:
Mzizi leta stori? maana hii stori inaanza kufanana na maisha yangu kimtindo
 
Usife kwanza mpenzi wangu (31)



Bila kutarajia Deo amejikuta akitoka na bosi wake Cleopatra. Haikuwa dhamira yake, ni baada ya kuleweshwa na mwanamke huyo.

Siku nyingine, Deo akiwa ametoka na Levina, simu yake inaita, alipoangalia jina la mpigaji akaona ni Cleopatra, akaogopa kupokea.

Kitendo hicho kikasababisha Levina amnyang’anye ile simu. Je, nini kitaendelea?
Sasa endelea...

LEVINA alikuwa amevimba kwa hasira, alianza kuhisi mchezo mbaya ukiendelea kati ya Cleopatra na Deo wake. Aliiangalia ile simu mpaka ikakatika yenyewe.

“Hebu niambie ukweli, anataka nini kwako huyu mwanamke?” Levina akamwuliza Deo.

“Hapo utakuwa unanionea mpenzi wangu, unadhani ni rahisi kugundua kitu kilichopo ndani ya kichwa cha mtu mwingine? Sijui ana shida gani, lakini itakuwa ni mambo ya ofisini!”
“Ofisini mpaka Jumapili?”

“Sijajua mpenzi wangu. We’ achana naye bwana...”
“Niachane naye kirahisi-rahisi tu!” Levina akasema kwa hasira na muda huo huo tena simu ikaanza kuita.

Safari hii Levina akaipokea haraka...
“Cleopatra habari yako?” Sauti yake ilionesha kabisa ilikuwa ya shari.

“Poa shoga, enheee vipi mzima wewe?”
“Mzima. Vipi tena simu na shemeji yako saa hizi?”
“Kwani vipi Levina? Inamaana hatuaminiani? Nataka kumpa maagizo muhimu ya kesho, maana kuna mahali nitapitia asubuhi, naomba kuzungumza naye!” Cleopatra akasema kwa kujiamini sana.

“Ok! Ongea naye huyu hapa...” akasema akimpatia simu Deo.
Cleopatra hakuwa na lolote, zaidi ya habari za mapenzi, lakini kwa sababu tayari alishasikia sauti ya Levina, hakutaka matatizo, akajifanya kumuagiza Deo kazi fulani za ofisini.

Ilikuwa kama kipande kwenye sinema ambacho kilipata wasanii walioweza kuuvaa vyema uhusika.

Deo aliweza kuzungumza na Cleopatra na kujifanya kweli walikuwa na mazungumzo ya kikazi. Kwa kiasi kikubwa walifanikiwa kumfumba macho Levina, ingawa naye hakuwa na uhakika wa asimilia mia moja.

Baada ya mazungumzo kukamilika, Levina alionekana hana furaha kabisa, lakini akajitahidi kuilazimisha.
“Kwani mpenzi wangu, bado unamuwaza vibaya Cleopatra?”

“Hata kama ungekuwa ni wewe ungeweza kama ninavyowaza mimi.”
“Lakini si ulisema Cleopatra ni rafiki yako na mnaaminiana?”
“Ndiyo.”

“Sasa kwa nini unamfikiria mabaya? Wakati mwingine ukimfikiria mwenzako mabaya, hata kama alikuwa hana mpango wa kufanya kitu kibaya anaweza akafanya.”

“Lakini mimi ndiyo namjua Cleopatra, naufahamu udhaifu wake na aina ya wanaume anaowapenda!”

“Ndiyo kusema mimi nachukuliwa tu kama mzigo, yaani sina hisia wala uamuzi wangu peke yangu kama mwanaume? Unadhani anaweza kunikokota tu bila uamuzi wangu mwenyewe?

“Kwani unanichukuliaje Levina? Au kwa sababu ulinipata kirahisi ndiyo maana unahisi mwanamke yeyote pia anaweza kunipata? Kumbuka mimi nilikupenda kwa mapenzi ya dhati ndiyo maana nipo na wewe muda huu.

“Sijafurahishwa kabisa na maneno yako, siamini kama kweli hatuamini kwa kiwango cha juu kiasi hicho. Tafadhali sana Levina usinivunjie heshima yangu! Naumia sana moyoni mwangu kwa jinsi unavyonihisi, usivyoniamini!” Deo aliongea maneno hayo kwa uchungu sana.

Yalikuwa yanatokea kinywani tu, ndani ya moyo wake kulikuwa na kitu kingine kabisa. Deo alikuwa ameshatekwa na Cleopatra.
“Samahani sana mpenzi wangu, sikuwa na nia ya kukuudhi, lakini Cleopatra ndiyo amenipa wasiwasi.”

“Hata kama...huyo ni Cleopatra. Inamaana mimi huniamini kwa sababu tu Cleopatra anaonekana labda kuwa na nia ya kuninasa?”
“Sijasema hivyo dear...naomba unisamehe mpenzi wangu!”
“Ok! Yaishe!”

Mahali pale hapakuwa na amani tena kwao, wakaamua kuondoka zao. Safari yao iliishia nyumbani kwa Deo, Sinza, ambapo walikaa hadi usiku wa saa 3, ndipo Levina aliondoka.

***
“Vipi yule ---- alishtuka?” Cleopatra alimwuliza Deo, asubuhi wakiwa ofisini.
“Kama ni sanaa, hapa ndiyo nyumbani. Nimemuweka sawa, hajashtuka kabisa.”

“Safi sana...sasa Deo mpenzi wangu nimekupandisha mshahara mara mbili ya ule uliokuwa unapata awali. Katika barua yako nimeandika kwamba umepandishwa kutokana na kutimiza vyema majukumu yako ya kazi.

“Nimeandika hivyo lakini ukweli ni kwamba, nimekuongeza mshahara kwa sababu umeweza kutimiza majukumu yako vyema ya kimapenzi kwangu. Hongera sana...” akasema Cleopatra akimkabidhi Deo barua yake.

Deo hakuamini!
Akabaki anaikodolea macho ile barua akitamani kuifungua. Akiwa anataka kuifungua, Cleopatra akamzuia.

“Utafungua ofisini kwako, haraka ya nini mwanaume?”
“Poa mpenzi wangu!”
“Kazi njema.”
“Ok!”

***
Penzi la siri kati ya Cleopatra na Deo lilizidi kukolea siku hadi siku. Miezi sita imekatika tangu walipofungua ukurasa huo wa mapenzi. Deo amekuwa muda mwingi zaidi na Cleopatra kuliko Levina.

Mapenzi yake kwa Levina yamefifia kabisa, hachagui majibu ya kumpa na hamjali kabisa. Jambo hilo linamuumiza sana Levina moyo wake lakini Deo hajali.

Ndani ya moyo wake, anashangaa akimpenda zaidi Cleopatra ambaye alikuwa mkali zaidi faragha kuliko Levina. Alishindwa kuelewa jambo moja; Deo hakumpenda Cleopatra kwa mapenzi ya dhati, fedha na mapenzi ndivyo vilivyomchanganya.

Usiku huu akiwa amelala, anagutuswa na simu yake ya mkononi iliyokuwa ikiita. Akajivuta taratibu na kuuruhusu mkono wake kuchukua simu iliyokuwa pembeni ya mto na kuangalia jina la mpigaji!

Ni Cleopatra!
Usiku huu?
Akapokea...

“Nina jambo moja muhimu sana nataka kukuambia Deo...nimechagua muda huu, maana naamini akili yako itakuwa imetulia na majibu utakayonipa yatakuwa yanatoka moyoni mwako...” Cleopatra alianza kusema mara baada ya Deo kupokea simu.

“Ni nini mpenzi wangu?” Deo akauliza.
“Naomba UACHANE na LEVINA ili UNIOE mimi, tafadhali sana nakuomba.

Kumbuka mimi na wewe tunapendana na sioni sababu ya kuendelea kuibana. Nina mali nyingi za wazazi wangu ambazo kwa kutumia akili yako, tutaziendeleza na kuishi maisha mazuri.

Tafadhali mpenzi usiseme hapana...naomba unikubalie!” Sauti laini ya Cleopatra ilisikika kwenye spika ya simu ya Deo.

Deo hakuwa na jibu la haraka. Haikuwa rahisi kiasi kile kumjibu Cleopatra! Kila alipokumbuka alipotoka na Levina, alichanganyikiwa na kinywa chake kuwa kizito kufunguka.

Je, nini kitatokea? Usikose kufuatilia baadae....

 
[h=1]Usife kwanza mpenzi wangu (32)....[/h]Fedha ndiyo chanzo cha usaliti wa Deo kwa Cleopatra. Hakuwa na mpango wa kumsaliti mpenzi wake Levina, lakini fedha zilizungumza na kununua penzi.

Cleopatra amekolea kabisa katika penzi la Deo, kiasi cha kuamua kumpigia simu usiku na kumwambia kwamba aachane na Levina ili amuoe yeye!

Unakuwa mtihani mkubwa sana kwa Deo ambaye anakosa kitu cha kufanya.Je, nini kitatokea?
SASA ENDELEA...

KWA kiasi kikubwa Deo alijitahidi sana kubana pumzi zake, lakini alishindwa kabisa! Alijikuta akishusha pumzi ndefu sana alizokuwa amezibana kwa muda mrefu.

Pumzi hizo zilizotoka bila hiyari, ziliweza kumfikia Cleoptara na kuzisikia vyema kupitia simu.
"Deo!" Cleopatra akaita simuni.
"Ndiyo mpenzi wangu."

"Mbona hivyo?"
"Vipi?"
"Umehema kwa kasi sana, kwani kuna nini?"

"Cleopatra jambo ulilonieleza ni zito sana, linahitaji muda wa kutosha kuweza kulifikiria kabla ya kutoa maamuzi. Si jambo jepesi hakika."
"Kwa nini?"

"Kumbuka nilipotoka na Levina, amenisaidia mangapi, leo hii kweli nimsaliti? No...roho yangu inakataa kabisa, moyo wangu hautaki!"
"Kwani hunipendi?"

"Najua nakupenda, lakini tulikubaliana tangu mapema kwamba penzi letu ni la siri na Levina hatakiwi kujua, sasa leo itawezekanaje mimi niwe mumeo?"

"Acha ujinga Deo, bado unapenda maisha ya shida? Nataka kubadilisha maisha yako. Kwa kuishi na mimi utakuwa mpya. Kama nilivyokuambia, wazazi wangu wana mali nyingi sana, hakuna mrithi pekee zaidi yangu. Kubali kunioa tafadhali!"

"Natakiwa kufikiria zaidi Cleopatra!"
"Mpaka lini?"
"Asubuhi nikija ofisini nitakuwa na jibu!"
"Kweli?"

"Niamini."
"Ok! Usiku mwema, jua nakupenda sana Deo!"
"Nakupenda pia Cleopatra!"

Deo alibaki na maswali mengi sana baada ya Cleopatra kukata simu. Kichwani alikuwa na mawazo yasiyo na majibu sahihi.

Alikiri kumpenda, lakini si kwa kumuoa na kuachana moja kwa moja na Levina. Alikumbuka vizuri sana wema aliofanyiwa na mwanamke huyo, kumuacha ilikuwa ni sawa na kumtakia kifo.

"Nitafanyaje mimi jamani? Lakini mpaka kesho lazima nitakuwa na majibu sahihi juu ya jambo hili..." akajisemea moyoni mwake na kulazimisha usingizi ambao ulikuwa mgumu sana kupatikana.

***
Simu ya mezani kwake ndiyo iliyomnasua Deo mawazoni, bado alikuwa akiwaza kuhusu ombi la Cleopatra. Akanyanyua mkonga wa simu na kupeleka sikioni. Akakutana na sauti ya mwanamke.
"Vipi Deo?"

"Poa Cleopatra, habari za asubuhi?"
"Zitakuwa nzuri iwapo utanipa jibu zuri juu ya yale tuliyoongea jana usiku!"
Deo akanyamaza!

Hakuwa na jibu!
"Deo..." Cleopatra akaita simuni.
"Nakusikia Cleopatra."
"Labda kama vipi uje ofisini kwangu!"

"Hapana naweza kukujibu hata hapa."
"Haya niambie!"
"NIMEKUBALI!"
"Unasemaje?"
"Nimekubali Cleopatra!"

"Kwa hiyo upo tayari kufunga ndoa na mimi?"
"Bila shaka."
"Umenifurahisha sana, sasa utakapokuwa tayari kuja kwetu utaniambia sawa mpenzi?"
"Nimekuelewa."

"Nitakuwa na zawadi yako nzuri sana kwa kukubaliana na ombi langu, umenifurahisha sana kwakweli!"
"Nitashukuru sana dear."

"Unaweza kuchagua au nikuchagulie mwenyewe?"
"Yoyote utakayopenda wewe naamini itakuwa nzuri na bora kwangu. Nakupa uhuru mpenzi wangu!"
"Sawa."

Ukurasa mpya wa mapenzi kati ya Cleopatra na Deo ukafunguka. Sasa hawakuwa kama wapenzi wa kuibana tena, walikubaliana kuoana!

***
Ni kumbukumbu zinazomtesa sana Deo, ambaye yupo kitandani amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili siku chache kabla ya ndoa yake baada ya kupigwa risasi ya bega!
Cleopatra yupo mbele yake akimwangalia..

"Mbona kama una mawazo sana?" Cleopatra akamwuliza.
"Hapana nipo sawa, ni maumivu tu!"
"Lakini unajisikiaje sasa?"

"Kwakweli bado naumwa, ingawa nafuu yangu ni kubwa sana."
"Sawa, acha mimi niende, nitakuja kukuona tena kesho mpenzi wangu!" Akasema Cleopatra na kuondoka zake.

Usiku mzima Deo alikuwa akifikiria kuhusu Levina, mwanamke ambaye alikuwa msaada mkubwa katika maisha yake halafu akamuacha na kutaka kumuoa Cleopatra.

Hakujua ni kwa nini mawazo haya yamemjia wakati huu anaoumwa. Muda huu ambao yupo kitandani akiugulia maumivu ya kupigwa risasi! Wakati huu wa kuelekea kwenye ndoa yake na Cleopatra!
Alijaribu kuwaza kichwani mwake lakini majibu yalikuwa magumu kupatikana.

***
Ni kama alikuwa kwenye ndoto, akihisi mikono laini yenye joto ikipapasa kifua chake, lakini alipojaribu kutuliza kichwa chake na kuhisi vizuri mikono ile laini ikipapasa kifuani mwake, akagundua kwamba, hakuwa ndotoni!

Hapo Deo akafumbua macho yake haraka. Hakutegemea kumuona mtu aliyekuwa amesimama mbele yake. Alikuwa ni Levina.
Levina Massamu.
"Habari za asubuhi Deo?" Levina alimsalimia Deo kwa sauti ya taratibu sana.

"Salama, vipi? Ni saa ngapi saa hizi?" Deo aliitikia na kuuliza maswali hayo mfululizo.
"Ni saa 12:15 za asubuhi Deo!"
"Mapema sana!"

"Ndiyo...mtu mwenye mgonjwa ambaye kwake ni muhimu, hupenda kuwa wa kwanza kwenda kumuona hospitalini. Hufika mapema kwa ajili ya kumuamsha na kuhakikisha anakuwa msafi.

"...hata hivyo usijali najua hiyo ni kazi ya Cleopatra, lakini nimekuja na ujumbe mmoja tu kwako...baada ya leo sitakuja tena kukuona hospitalini..." akasema Levina kwa sauti ya taratibu sana.

Deo hakuweza kufungua kinywa chake kusema chochote, aligeuza macho na kutingisha kichwa chake kuashiria kukukubaliana na maneno yake.

"fikiria upya kuhusu suala la kumuoa cleopatra. najua zimebaki siku chache sana kabla ya kufunga naye ndoa, lakini fikiria zaidi kama kuna uhalali wa kumuoa na kuniacha nikidondosha machozi. nikisononeka na kunyanyasika! nakutakia siku njema!"

Levina alitamka maneno hayo kwa simanzi nzito kisha akaondoka na kumuacha Deo akimuita, lakini Levina hakugeuka nyuma.
Akiwa anakaribia mlango mkubwa wa kutokea wodini, macho yakagongana na ya Cleopatra aliyekuwa akiingia.

Hakuna aliyemsemesha mwenzake, zaidi Cleopatra alisimama na kumsindikiza Levina kwa macho mpaka alipopotea machoni mwake.
"Huyu mwanamke hajui kuachwa? Mbona anajipendekeza hivyo?" Akawaza Cleopatra akielekea kilipo kitanda cha Deo.

Kumbuka matukio yote haya Deo anayakumbuka akiwa amelazwa baada ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana. Je, nini kitaendelea? Levina atafanikiwa kumpata Deo? Usikose baadae
 
[h=1]Usife kwanza mpenzi wangu (33)..[/h]
Deo yupo hospitalini amelazwa baada ya kupigwa risasi ya begani, siku chache kabla ya ndoa yake na Cleopatra! Akiwa hospitalini hapo, kumbukumbu za jinsi alivyokutana na Levina, akamsaidia kupata kazi, elimu na maisha mazuri, lakini baadaye akamsaliti na kuwa na Cleopatra.

Ni kumbukumbu asizozipenda kabisa, lakini zinajirudia kila wakati. Asubuhi moja Levina anakwenda kumtembea wodini, lakini siku hiyo Levina anamwambia afikirie upya kuhusu kumuoa Cleopatra na kumuacha yeye akiteseka na kulia!

Muda mfupi baadaye Levina anaondoka, njiani anakutana na Cleopatra ambaye hazungumzi kitu! Wanapishana kama mabubu! Nini kitatokea?
SASA ENDELEA...

AKIWA kitandani amelala, Deo aliweza kumsindikiza Levina kwa macho mpaka alipofika kwenye mlango mkubwa wa kutokea wodini, akamuona alivyokutana na Cleopatra.
Akakaza macho!

Alitegemea kuona ugomvi, lakini hilo halikutokea. Akatulia kitandani, akizidi kuandamwa na mawazo. Tangu ameamua kumuoa Cleopatra, hakuwahi kufikiria kuhusu Levina kwa kina kiasi kile, alijishangaa jinsi mawazo ya huruma dhidi ya Levina yalivyoushambulia ubongo wake kwa kasi.

Hakupenda lililotokea litokee, machozi yakaanza kumiminika machoni mwake. Muda kidogo Cleopatra alikuwa ameshafika kitandani kwake.
Akashtuka sana!

"Vipi, mbona unalia?" Cleopatra akamwuliza akitoa kitambaa na kumfuta machozi.
Deo hakujibu.
"Deo!" Cleopatra akaita.
"Nakusikia Patra."

"Nini tatizo?"
"Levina!"
"Levina?!"
"Ndiyo...Levina."
"Amefanya nini huyo Levina? Nimekutana naye hapo mlangoni, amekuambiaje kwani?"

"Hapana...nahitaji kupumzika!"
"Kwahiyo hutaki kuniambia!"
"Nataka!"
"Haya niambie, kuna nini?"
"Ananilalamikia kumuacha!"

"Deo mpenzi wangu, kwani hilo ni jipya? Ni leo ameanza kukulalamikia? Hebu achana naye bwana!"
"Poa."
"Dokta ameshapita round?"
"Bado."

"Ok! Lakini jana nilipozungumza naye, alisema kwamba kama hali itakuwa kama jana, basi anaweza kukuruhusu leo!"
"Nitafurahi sana, nimeshachoka kukaa hapa hospitalini, nikilala na leo tena, nitakuwa nimekamilisha wiki mbili!"
"Ni kweli, tuombe Mungu uruhusiwe ili kama hali itakuwa nzuri tufunge ndoa yetu!"

"Sawa!"
"Ngoja nikaonane naye!"
"Sawa mpenzi wangu!"
Cleopatra akatoka akielekea ofisini kwa Dk. Pallangyo. Huku nyuma akamuacha Deo akizidi kuwa na mawazo kichwani mwake. Wema wa Levina ulimchanganya.

Alianza kumfikiria kwa upya tena. Hakutakiwa kulipwa ubaya mkubwa kiasi kile. Levina alikuwa mwema sana kwake. Kumkataa na kumuoa Cleopatra ilikuwa maumivu makali sana moyoni mwake. Moyo wake haukukubaliana kabisa na hilo.

Ni hapo ndipo alipokumbuka siku Levina alipogundua kwamba anatoka na Cleopatra. Kumbukumbu zikarudi upya.

***
Ilikuwa Jumapili jioni, Deo akiwa ametulia sebuleni kwake, kitu kigumu kilichokuwa kikimsumbua ni namna gani angeachana na Levina ili aweze kumuoa Cleopatra. Hilo lilimtesa sana kichwa chake.

Akiwa katikati ya lindi la mawazo, mlango wake ukagongwa. Akatoka na kwenda kufungua. Akashangaa kukutana na Levina. Haikuwa kawaida kwa Levina kugonga mlango, siku zote alikuwa akiingia moja kwa moja!

"Vipi mpenzi, mbona unagonga badala ya kuingia?" Deo akaumwuliza Levina.
"Siku hizi mimi hapa ni mgeni!"
"Mgeni?"

"Ndiyo, kwani wewe hujui kuwa mimi ni mgeni hapa kwako?"
"Sikuelewi mpenzi wangu, kwanini usiniweke bayana kuliko kutumia tungo?"
"Hebu twende ndani," akasema Levina na kuingia ndani.
"Mbona hujaja na gari?" Deo akamwuliza Levina.
"Nimeamua kutumia taxi!"

"Tatizo ni nini mpenzi wangu?"
"Kwani wewe hujui tatizo ni nini? Haya mapenzi yetu siku hizi yanaendeshwaje? Halafu siwaelewi kabisa wewe na Cleopatra au nimefanya makosa kukutafutia kazi kwao?"
"Lakini kwanini humuamini rafiki yako?"

"Kama haaminiki unadhani nitawezaje kumuamini? Cleopatra namjua mwenyewe...namjua vizuri sana, mabadiliko yake na yako, yanaonesha kuna kitu kinaendelea."
"Hakuna mpenzi wangu, niamini mimi!" Deo akasema, lakini ndani ya moyo wake akiwa anaujua ukweli.

Kimya kifupi kikapita, wakiwa katika ukimya ule, wakasikia mlango ukigongwa!
Deo akashtuka sana!
Nyumbani kwake huwa hana wageni zaidi ya Levina na Cleopatra aliyeanza kwenda siku za karibuni.

"Nenda kafungue!" Levina akamwambia.
Deo hakujibu kitu, wala hakusimama. Sekunde chache baadaye, mlango ukafunguliwa. Cleopatra akaingia. Hakushtuka alivyomuona Levina. Akaenda moja kwa moja kukaa kwenye sofa moja.

"Habari yako Levina?" Cleopatra akasalimia kwa dharau.
"Patra najua kilichokuleta, najua kabisa..." Levina akasema kwa uchungu.

"Kama unajua bado unasubiri nini? Acha wenye kisu wale nyama mtoto wa kike!"
"Unasemaje?" Levina akauliza akiwa katika mshangao mkubwa.
Ni muda mrefu alikuwa akihisi Cleopatra anatoka na Deo, lakini siku hiyo, alijihakikishia kuwa hisia zake zilikuwa za kweli.

"Hivi Deo, bado hujamwambia Levina kuwa umepata mchumba mwingine?" Cleopatra akamwuliza Deo.
Deo hakujibu!

"Deo umenisaliti mpenzi wangu? Umesahau nilipokutoa? Umesahau nilivyokusaidia? Wema wangu leo unanilipa ubaya Deo?" Levina alisema kwa uchungu machozi yakimtoka, lakini kwa Deo ni kama maneno yale hayakumuhusu yeye!

"Kwahiyo Levina, kwasababu umenisaidia ndiyo unisimange? Mapenzi ni hisia, mwanzoni zilikuwa kwako, sasa hivi zimehamia kwa Cleopatra basi, elewa hivyo mtoto wa kike..." Deo akasema kwa kujiamini.

"Unasemaje Deo?"
"Ulivyosikia ndiyo hivyo, mapenzi yangu kwako yameisha, sasa nipo na Cleopatra na ni lazima nimuoe!"

"Haya Deo, ahsante sana kwa maneno yako, nashukuru kwa kila kitu, lakini kaa ukijua kwamba, nilifanya yote yale kwa sababu ya mapenzi yangu ya dhati kwako. Mimi nakwenda!"
"Nenda!" Deo akasema kwa dharau.

Cleopatra akaangua kicheko cha dharau. Akasimama na kumfuata Deo, akamrukia na kumkumbatia.
"Huo ndiyo uanaume Deo, sasa kilichobaki ni kufunga ndoa yetu, tufurahie maisha. Achana na huyo masikini, nimemlea sana tangu shuleni, pesa zao za mawazo!"

"Sawa baby, nimefurahi sana kupata mwanamke muelewa kama wewe!"
"Vipi, wapi sasa?"
"Kwani tunatoka?"
"Unauliza majibu tena? Twende zetu kiwanja tukale raha!"
"Poa, ngoja nijiandae fasta tuondoke zetu!"
"Poa!"

***
Mapenzi ya Deo na Cleopatra yalizidi kupamba moto, Deo akamsahau kabisa Levina, hata alipojaribu kumpigia simu, aliambulia matusi. Taratibu za Deo kwenda kujitambulisha nyumbani kwa akina Cleopatra zilifanyika haraka. Deo akatafuta wazee waliotuma posa na kukubaliwa.

Wazazi wa Cleopatra hawakuwa na tabu na posa yake, wakamkubalia. Mara moja taratibu za ndoa zikaanza. Hawakutaka kuchangisha watu michango. Fedha walizokuwa nazo zilitosha kabisa kufanya sherehe hiyo bila michango. Kila kitu kikawa tayari, wakabaki kusubiri tarehe ya ndoa.

***
Levina alikuwa akilia usiku na mchana, hakuwa tayari kumpoteza mpenzi wake Deo, mwanaume aliyempenda na kumuhangaikia kwa muda mrefu. Afya yake ilianza kudhorota, muda wote akawa na mawazo.

"Levina mwanangu una nini? Mbona siku mbili hizi sikuelewi kabisa?" Mama yake alimwuliza Levina jioni moja wakiwa wamekaa sebuleni.
Levina hakuwa na jibu!


Je, nini kitaendelea? Usikose kufuatilia baadae...
 
[h=1]Usife kwanza mpenzi wangu (34)...[/h]Deo yupo kitandani Muhimbili, matukio yote katika maisha yake ya kimapenzi na Levina yanaonekana kama sinema. Anakumbuka siku Levina alipogundua rasmi kwamba anatoka kimapenzi na Cleopatra.

Levina akiwa mezani na mama yake wakipata chakula cha usiku, mama yake anagundua tofauti ambayo mtoto wake anayo. Anajaribu kumuuliza lakini hasemi kitu.
SASA ENDELEA...

MAMA Levina akaacha chakula na kumwangalia mwanaye vizuri machoni, ambaye alionekana wazi kuwa na jambo zito linalomsumbua. Alitaka kujua namna ambavyo angeweza kumsaidia.

"Levina, lazima uniambie ukweli!"
"Unataka ukweli gani mama?"

"Nataka kujua nini kinakusumbua, maana naona haupo sawa. Kuna jambo linakutatiza. Lazima."
"Hapana mama."

"Wewe ni mwanangu, nimekuzaa na kukulea mwenyewe, sijasaidiwa na mtu, hivyo nakujua ulivyo. Hapo una tatizo lakini hutaki kusema. Hebu kuwa wazi, mama una nini?"

"Nothing mom, niamini."
"Wewe utakuwa na mimba!"
"Mama!"

"Mama what? You must have a pregnant!"
"Hapana mama, sina mimba. Kwa nini unanifikiria hivyo?"
"Sasa nifikirie nini?"

"Mama ni kweli nina tatizo, lakini si mimba."
"Ok! Niambie, ni nini kinakusumbua?"
"Ni Deo mama."
"Deo? Tena?!"

"Mama nampenda, lazima niwe mkweli bado niliendelea kuwa na uhusiano naye na nilimsaidia sana lakini sasa hivi amenisaliti mama, anatoka na bosi wake ambaye ni rafiki yangu!" Levina akasema kwa uchungu sana akikaribia kudondosha machozi.

Mama yake akaumia sana, moyo wake ukaingiwa na ganzi, pamoja na kwamba mwanaye alimuudhi kwa kukaidi maagizo yao lakini bado aliona ana kila sababu kama mama kumsaidia mwanaye katika hali aliyokuwa nayo.
"Lakini mwanangu, kumbuka kwamba hapa tunatakiwa kujadili kuhusu wewe na siyo huyo Deo tena."
"Kivipi mama?"

"Wewe unazungumzia juu ya mwanaume unayempenda lakini yeye hakupendi, unajua kama ingekuwa ni kesi ya wewe kumpenda na yeye kukupenda, yaani mkapendana, halafu kukawa na tatizo fulani, basi ingekuwa rahisi lakini hapa ni kinyume chake.

"Kifupi Levina binti yangu unatakiwa kufahamu kwamba huyo mwanaume hana mapenzi na wewe, huna haja ya kuendelea kumuweka moyoni mtu ambaye hakupendi. Najua ni kiasi gani unateseka na kuumia. Najua kwa sababu hata mimi nimepita huko lakini huyo Deo si mwanaume sahihi kwako!" Mama yake aliongea kwa sauti ya chini sana akihitaji usikivu wa mwanaye.
"Kweli mama?"

"Ndiyo hivyo mwanangu, si mwanaume atakayeweza kuyashika maisha yako sawasawa, bado una muda wa kusubiri mwanangu!"
"Mama!" Levina akaita.

"Mwanangu!"
"Nitajua mwenyewe cha kufanya!"
"Angalia isiwe kuwa na madhara kwako lakini!"

"Nipo makini kwa kila ninachokifanya mama. Naamini unanifahamu nilivyo, nakupenda na sitakwenda kinyume!"
"Nenda kapumzike mwanangu, kabla hujalala hakikisha unasali. Tuliza kichwa chako mwanangu, usiwe na mawazo sana!"

"Nimekuelewa mama, nakupenda sana."
"Nakupenda pia binti yangu."
Levina akaondoka na kwenda chumbani kwake kulala, kichwa chake kilikuwa kizito kuliko kawaida.

***
Deo alikuwa mezani kwake, akiendelea na kazi kama kawaida, simu yake ikaanza kuita, alipoangalia kwenye kioo cha simu, akagundua ni Levina ndiye alikuwa akimpigia. Deo akashtuka sana!

Ilikuwa ni wiki mbili baada ya Levina kumfuma akiwa na Cleopatra nyumbani kwake, ni siku hiyo ndiyo aliyoamua kuweka ukweli hadharani kwamba yupo na Cleopatra kimapenzi. Pamoja na ujeuri na maneno makali, dhamira iliendelea kumsuta Deo kwa kitendo alichomfanyia Levina.

Hakumtendea sawa, hilo hata moyo wake ulimdhibitishia. Aliiangalia ile simu ikiendelea kuita kwa muda mrefu bila kupokea.

"Nitamwambia nini?" Akawaza akiangalia simu iliyoanza kuita tena kwa mara ya pili.

Levina alikuwa msaada mkubwa katika maisha yake, ni yeye ndiye aliyemtoa kwenye dhiki na shida. Aliyemsomesha na kumtafutia kazi. Kwa hakika hakupaswa kumtenda. Alijishauri sana lakini mwisho wake akaamua kupoikea...

"Haloo!" Sauti ya Deo ilisikika ikionekana dhahiri kuwa na woga ndani yake.
"Deo!"
"Yes!"

"Kwa nini umenitenda hivyo? Kwa nini lakini Deo? Ni kweli nastahili kufanyiwa yote hayo? Wema wangu wote kwako, malipo yake ndiyo haya?"

"Najua nimekukosea Levina, tena nimekosea sana lakini unatakiwa kufahamu kwamba, sikufanya hayo kwa makusudi Levina."

"Unamaanisha nini unaposema hukukusudia?"
"Namaanisha kwamba hayakuwa makusudi yangu mpenzi."
"Kumbe ni nani amefanya hayo."
"Ni mimi lakini kwa shinikizo."

"Shinikizo la nani?"
"Cleopatra."
"Kwa hiyo huyo Cleopatra ndiyo amebeba moyo wako, yeye ndiye anakuamulia mambo yako?"

"Sina maana hiyo lakini nilihofia kupoteza kazi."
"Lakini hiyo kazi si mimi ndiye niliyekutafutia? Kwani ningeshindwa vipi kukutafutia nyingine ili uendelee kuwa wangu?"

"Lakini nilijua kabisa hizo fedha zako za mawazo, mwisho wake ungekuwa mbaya. Levina hata kama umenisaidia unanisimanga sana, bila shaka ungeendelea kunisimanga haya ningekuoa. Kifupi nimeamua kuwa na Cleopatra, haya ni maamuzi yangu na moyo wangu, hayawezi kubadilishwa na mtu yeyote. Nimemaliza!" Akasema Deo kwa hasira na kukata simu.

Levina alijaribu kumpigia kwa mara nyingine, akawa anaiangalia simu bila kupokea. Baadaye akaamua kuzima kabisa.



***
Macho ya Deo yalikuwa yananyemelewa na machozi, moyo wake ulikuwa unapingana kabisa na kitu kilichokuwa mbele yake. Ulikuwa unapingana kabisa na ndoa. Alihisi kumkosea sana Levina ambaye hakuwa na hatia kwa aliyofanyiwa.

Akiwa kwenye kumbukumbu za mawazo hayo, Cleopatra anatokea, tabasamu lake linayeyuka baada ya kuona wekundu katika macho ya Deo. Anakimbia haraka hadi kitandani.

"Kuna nini?" Akauliza.
"Hakuna kitu."

"Hapana mpenzi, kwa nini unajiumiza? Dokta ameshakuruhusu, tafadhali naomba utulize moyo wako, turudi nyumbani."
"Sawa."

"Lakini kuna jambo moja muhimu, nimezungumza na mama kuhusu hali yako, amesema ni vizuri ukapumzike nyumbani kwanza hadi utapopata nafuu, hali yako haikuruhusu kukaa peke yako. Lazima uwe chini ya uangalizi wa karibu."
"Sawa."

Taratibu zote muhimu zikafanyika, Deo akaruhusiwa. Cleopatra akamshika mkono hadi kwenye gari, akamwingiza taratibu na kufunga mlango. Akaendesha gari mpaka nyumbani kwao Mikocheni.

Deo alipokelewa kwa upendo mkubwa, akafikia kwenye moja ya vyumba vya wageni. Cleopatra alikuwa na wasiwasi sana, alitamani mpenzi wake apone haraka ili waweze kupanda madhabahuni kufunga ndoa yao.

***
Mipango yote ilikuwa tayari, Deo alikuwa na hali nzuri zilibaki siku tano tu, kabla ya ndoa. Deo akiwa mwenye mawazo sana, asubuhi ya Jumatatu aliamka akiwa mchovu zaidi kuliko siku zote. Cleopatra alipokwenda kumsalimia chumbani kwake, akashangaa kumkuta Deo katika hali ile.

Hakuwa na furaha, uso wake ulionekana wazi kuwa na jambo zito sana. Cleopatra akakaa kitako kitandani na kumtulizia macho yake usoni.
"Vipi mpenzi wangu? Nahisi kama kuna tatizo."
"Ni kweli kuna tatizo."
"Ni nini?"

"NAJUA HUKUTARAJIA KUSIKIA MANENO HAYA, LAKINI SINA JINSI, LAZIMA NIKUAMBIE. NIMEFIKIRIA KWA MUDA MREFU SANA JUU YA NDOA YETU, NIMEAMUA TUSITISHE. SITAKI KUFUNGA NDOA TENA NA WEWE! SITAKI..." Deo akasema kwa kumaanisha.

Je, nini kitatokea? Usikose kufuatilia simulizi hii ya kusisimua baadae.....

 
Usife kwanza mpenzi wangu (35)..


Deo amesharuhusiwa hospitalini, amepelekwa nyumbani kwa akina Cleopatra Mikocheni. Anajitahidi kwa kila hali kumsahau Levina lakini anashindwa.

Ikiwa zimebaki siku tano tu kabla ya ndoa yao, Deo anabadilisha mawazo, anamweleza ukweli Cleopatra kwamba hataki tena kufunga naye ndoa, sababu kubwa ni Levina.

Levina alikuwa ndani ya moyo wake lakini hakumweleza ukweli Cleopatra kuwa sababu ya kuhairisha ndoa hiyo ni Levina. Cleopatra amechanganyikiwa, haamini alichokisikia. Umeona kazi hiyo?
SASA ENDELEA...

CLEOPATRA alibaki amegandisha macho yake usoni mwa Deo akiwa haamini alichokisikia. Tayari Deo alishaanza kujisikia vibaya, kulikuwa na kila dalili machozi kuanza kuchuruzika machoni mwake.

Cleopatra akatulia kwa muda, akapiga magoti chini na kuanza kumsihi Deo.
"Kuna kitu nimekukosea mpenzi wangu?" Cleopatra akauliza kwa sauti ya taratibu sana.
"Hapana."

"Nimekunyanyasa?"
"Hapana."
"Sasa kwa nini uamuzi huu unakuja kipindi hiki cha mwisho kabla ya kupanda madhabahuni kufunga ndoa yetu mpenzi wangu?"

"Siwezi tena, naomba unisamehe kwa yote, sikujua kama haya yangetokea. Sikujua kama ningebadilisha mawazo lakini kwa sasa sitaki tena."

"Tafadhali Deo, inawezekana kuna mahali nimekukwaza hutaki kuniambia ukweli, tafadhali naomba unieleze ukweli."

"Unataka kujua ukweli?"
"Ndiyo!"
"Una kifua?"

"Ndiyo!"
"Sababu ni Levina."
"Levina?"

"Ndiyo, Levina ndiyo sababu, hata kama sitamuoa yeye lakini kukuoa wewe ni sawa na kumtukana. Hata milango ya riziki zangu inaweza kufungwa kama nikifanya hivyo!"
"Itafungwa vipi? Deo acha ujinga, huoni mali zote nilizonazo, nani anaweza kuzifunga?"

"Yupo wa kuzifunga, yupo Cleopatra. Unajua Levina amenisaidia mambo mengi sana. Kama si yeye, nisingekuwa hivi nilivyo. Sidhani kama nitakuwa namtendea haki kufunga ndoa na wewe.

"Siyo sawa na siwezi kukuoa tena Cleopatra, tafadhali sana, nakuomba unisamehe kwa haya yote lakini sina namna. Haiwezekani tena!" Deo alikuwa akizungumza haraka-haraka tena kwa huzuni.

Cleopatra hakuweza kufanya kitu chochote zaidi ya kuanza kulia. Machozi yakaanza kumtoka machoni mwake. Alianza kwa sauti ya chini lakini muda ulivyozidi kwenda akazidisha kilio na sauti kuwa kubwa zaidi.
Punde mama yake Cleopatra akaingia akiwa anahema kwa kasi ya ajabu.

"Vipi, kuna nini?" Mama Cleopatra akauliza akiwa anahema, woga ulimjaa moyoni akiamini Deo alikuwa amezidiwa.
"Kuna nini nyie watoto?"
Hakuna aliyemjibu.

"Deo!" Hatimaye mama Cleopatra akaita.
"Naam mama!"
"Kuna tatizo gani?"
"Ongea na Patra."
"Niongee na Patra?"

"Ndiyo mama."
"Cleopatra hebu niambie kuna nini mwanangu?" Mama akamwuliza mwanaye.
Hakujibu!
"Cleopatra nongea na wewe...mbona mnanichanganya nyie watoto? Hebu niambie kuna nini?"

"Mama, Deo hataki kufunga ndoa na mimi!"
"Unasemaje?"
"Deo hanitaki tena mama."
"Umemfanya nini mwenzako?"
"Muulize."

"Deo mwanangu, kuna nini?"
"Mama ni kweli sitaki tena kufunga ndoa na Cleopatra, nitakuwa msaliti mama."
"Kivipi?"

"Unajua mama, mwanzoni nilikuwa na mpenzi wangu anayeitwa Levina, huyu msichana naamini utakuwa unamfahamu maana amesoma na Cleopatra na walikuwa marafiki tangu shuleni."
"Levina? Baba yake anaitwa nani?"
"Massamu!"

"Namfahamu, ikawaje?"
"Huyu msichana mama naweza kusema aliniokota sokoni Tandale nikifanya kazi ya kuuza genge la mchele, ni yeye ndiye aliyenisomesha hadi kufikia hivi.

Baada ya kumaliza masomo, akanileta ofisini kwa rafiki yake Cleopatra, kwa kuwa ni marafiki, haikuwa tabu Cleopatra kunipatia kazi lakini sasa mama, tatizo limekuja kwamba, Cleopatra alinishawishi niwe naye.

"Kwa kuwa nilihofia kufukuzwa kazi, nikamkubalia. Baadaye uhusiano wetu ukaja kugundulika na Levina, wakati huo tayari Cleopatra aliniomba nifunge naye ndoa. Mama tulimfukuza Levina kwa maneno makali pale nyumbani, ukawa mwisho wa uhusiano wetu.

"Baada ya kupata haya matatizo na kulazwa, Levina amekuwa akija hospitalini kila siku asubuhi, ananiambia maneno makali ya kuchoma, naona jinsi anavyoteseka, analia, amepungua sana mama. Naamini akisikia nimefunga ndoa na Cleopatra, anaweza hata kuanguka chini na kupoteza maisha.

"Sitaki hilo litokee mama, sitaki kuwa chanzo cha kukatisha uhai wa mtu mama. Hata kama sitamuoa Levina lakini ni bora asisikie kuwa nimefunga ndoa na rafiki yake kipenzi.

Huo ndiyo ukweli wangu mama, naomba unisaidie mama, naomba unisaidie mama yangu!" Alisema Deo akilia muda wote aliokuwa akisimulia.

Mama Cleopatra alitulia kimya kuruhusu masikio yake kumeza maneno yote yaliyokuwa yakitoka kinywani mwa Deo. Yalionekana kumgusa sana, mara kadhaa alikuwa akigeuza macho yake na kumwangalia mwanaye aliyekuwa akilia muda wote.

"Patra ni kweli anayosema mwenzako?"
Cleopatra akatingisha kichwa kuashiria ni kweli. Mama Cleopatra akaangalia chini kwa aibu. Anamjua vizuri sana Levina, aliyekuwa rafiki kipenzi wa mwanaye, hakutegemea kusikia mambo aliyoambiwa na Deo. Muda huo huo, akasimama na kutoka nje.

Deo akajikongoja kitandani na kuamka, akavaa. Hakuwa na nguo nyingi pale kwa akina Cleopatra, hivyo ilikuwa rahisi kuzichukua kwenye mfuko wa rambo. Akamwangalia Cleopatra aliyekuwa akilia pale chini akamwambia:

"Nakwenda zangu, sitaweza kuendelea na wewe, kuhusu kazi, utanijulisha kama nafasi yangu bado ipo au umenifukuza kazi!"
Deo akaondoka zake.
Cleopatra akabaki akilia.
***
"Simama hapo hapo!" Deo alimwambia dereva teksi asimamishe gari mbele ya geti la nyumba anayoishi.
Akashuka na kumlipa fedha zake kisha akaingia ndani mawazo mengi yakiwa yamekizunguka kichwani mwake. Akiwa anakaribia kuufikia mlango wake, simu yake ikaingiza ujumbe mfupi wa maneno.

Ulisomeka: "Deogratius, mwanaume niliyekupenda na nitakayekupenda milele. Nashukuru umeanza hatua moja, huo ni ujasiri wa hali ya juu, nakupongeza kwa kutambua na kuthamini hisia zangu.

"Hata kama hutanioa lakini angalau sitakuwa na maumivu ya kunyang'anywa tonge mdomoni na rafiki yangu kipenzi. Ahsante sana Deo wangu. Ahsante mpenzi!"

Ulikuwa ujumbe kutoka kwa Levina Massamu. Deo akachanganyikiwa! Amejuaje yote hayo? Likabaki kuwa swali kichwani mwake lililokosa majibu!

Je, nini kitatokea? Nani amempa taarifa Levina? Usikose Baadae................
 
[h=1]Usife kwanza mpenzi wangu (36)....[/h]Deo ameamua kutua mzigo mzito moyoni mwake, amemwambia Cleopatra kwa uwazi kabisa kwamba hawezi kumuoa tena kwa kuhofia kumuudhi Levina ambaye alimsaidia sana hadi kupata elimu na baadaye kazi, jambo hilo linaungwa mkono na mama yake Cleopatra. Deo anaondoka zake.

Akiwa ndiyo kwanza anaingia nyumbani kwake, Deo anapokea ujumbe mfupi kutoka kwa Levina ambaye anamshukuru kwa kusikia sauti yake. Kwa Deo inakuwa maajabu, maana hakumweleza chochote kuhusu uamuzi wake. Jambo hilo linamchanganya sana Deo.
SASA ENDELEA…

ALIRUDIA kusoma ule ujumbe mara mbili zaidi, lakini maneno yaliendelea kuwa yale yale, kutoka kwa mtu yule yule, yakiwa ndani ya simu yake yeye mwenyewe! Deo akapigwa na butwaa.

"Amejuaje haya?" Akajiuliza, lakini hakupata majibu.
Akajivuta hadi mlangoni, akafungua mlango na kuingia ndani, akaenda kujitupa kwenye sofa kubwa akihema kwa kasi. Hapo akaanza kumkumbuka kwa upya kabisa Levina. Kuna kitu kilianza kumwingia akilini mwake.

Hakuwaza tena juu ya meseji ile iliyoingia kwenye simu yake kimaajabu, alimuwaza Levina, mwanamke ambaye alimpenda kwa mapenzi yake yote, pasipo shinikizo kutoka kwa mtu yeyote. Pasipo matarajio ya kupata kitu chochote! Alimpenda yeye tu!
Mapenzi tu!

Penzi la dhati!
"Kuna kitu natakiwa kufanya," akawaza akiangalia simu yake.
Wazo la kumpigia Levina likamwingia akilini mwake.

Ilikuwa lazima azungumze naye. Wakati huo hakuwaza tena kuhusu kazi, suala la kazi halikuwa na maana sana kwake. Kwa kutumia vyeti vyake alikuwa na uhakika mkubwa sana wa kupata kazi sehemu nyingine, kuliko kuendelea kukaa na mateso moyoni kwa kuishi na mwanamke ambaye mapenzi yake yalikuwa ya wasiwasi.
Akabonyeza namba za Levina na kumpigia, kiasi cha sekunde nane tu, Levina alikuwa hewani akizungumza na Deo…

"Haloo Levina!"
"Yes Deo, mambo vipi?"
"Poa, lakini sipo sawa sana!"
"Nini tatizo?"
"Kuna kitu nahisi kinaniumiza sana moyoni mwangu, Levina naomba unisamehe kwa yote yaliyotokea, tafadhali sana, nakuomba kwa moyo wangu wote. Mimi ni binadamu na nilipitiwa, siku zote kwenye maisha ni vyema kukosea ili kupata nafasi pia ya kujifunza.

"Waswahili wanasema, watu wanajifunza kutokana na kukosea. Nakuomba unisamahe ili niweze kuishi kwa amani moyoni mwangu!" Deo akasema kwa sauti ya chini sana akionekana kujutia sana yaliyotokea.
"Deo!" Levina akaita.

"Nakusikia mama…"
"Ni kweli unaomba msamaha kwa moyo wako wote?"
"Kweli kabisa, naweza kuapa kwa namna yoyote unayotaka!"
"Hakuna sababu ya kuapa, ni wewe mwenyewe na nafsi yako, kama ni kweli unajua umekosea ni vizuri na ni rahisi kusamehewa."

"Kweli Levina najuta kukukosea, nimetambua kosa langu, nisamehe tafadhali!"
"Nilishakusamehe Deo, lakini ukweli ni kwamba sijakusamehe kikamilifu!"
"Unamaanisha nini?"

"Namaanisha kwamba nilishakusamehe tangu siku nyingi, lakini si kwa moyo wangu!"
"Sawa, naomba basi kuanzia leo uwe umenisamehe kwa moyo wako Levina!"
"Inawezekana Deo, lakini kuna masharti mawili!"
"Masharti?" Deo akauliza kwa mshangao mkubwa.
"Ndiyo kuna masharti mawili, kama ukiweza kuyatimiza, basi nitakusamehe moja kwa moja na nyongo iliyokuwa ndani ya moyo wangu itaondoka."

"Ni masharti gani hayo? Niambie tafadhali!"
"Si kwa haraka kiasi hicho, lakini nitakuambia."
"Lini?"
"Nipe muda, lazima nikutane na wewe, nahitaji kuzungumza na wewe, tena uso kwa uso."
"Itakuwa lini?"
"Nitakujulisha, kwa sasa pumzika kwanza."
"Sawa Levina, lakini nina ombi moja kwako!"
"Nakusikia!"

"Isiwe muda mrefu sana, siwezi kukaa na hili jambo muda mrefu, nahisi moyo wangu unaungua!"
"Usijali najua ni kiasi unateseka, najua pia ni kiasi gani unataka kuishi huru. Yote hayo nayajua na nitayachukulia kwa uzito mkubwa, muda ukifika nitambia!"

"Nimekuelewa vizuri, lakini nilikuwa na lingine!"
"Nini tena?"
"Nimepata meseji yako muda si mrefu!"
"Ndiyo!"
"Umejuaje hayo?"

"Siku zote kama kitu unakipenda, ni rahisi kujua kinavyoendea hata kama hutapewa taarifa. Nimejua kwa sababu nakupenda Deo!"
"Lakini haraka sana!"
"Ni kwa sababu nakupenda sana!"
"Haya bwana."
"Siku njema Deo!"
"Kwako pia."

Deo hakutoa simu haraka sikioni pamoja na kwamba alikuwa ameshaagana na Levina ambaye alishakata simu. Ni kama alikuwa amepigwa bumbuwazi au hajui kinachoendelea. Moyo uliendelea kuteswa na mapenzi, alimtaka sana Levina kwa wakati huu.

Aligundua kwamba penzi lake kwa Levina lilikuwa zito na lenye thamani zaidi ya Cleopatra ambaye alijilazimisha kutokana na mali zake.
"Nitampata Levina wangu, lazima arudi tena kwangu, lazima..." akawaza akisimama na kujivuta chumbani mwake.
***
Mama Cleopatra baada ya kutoka chumbani na kuwaacha Deo na Cleopatra aliifuata simu yake chumbani kwake na kumpigia Levina ili kutafuta ukweli.

"Hujambo mwanangu?"
"Sijambo mama shikamoo..." Levina akasalimia.
"Marhaba...haya mbona mwenzio anafanya mambo ya ajabu unashindwa kuniambia binti yangu?"
"Nani mama? Patra?"
"Ndiyo!"
"Amefanya nini tena?"
"Unamjua Deo?"
"Ndiyo!"
"Unamjuaje?"

"Mama Deo alikuwa mpenzi wangu, lakini Patra kwa sababu ya pesa zake ak...." Levina alishindwa kumalizia sentesi yake na kuanza kulia.


Je, nini kitatokea? Usikose kufuatilia Leo jioni ndio inamalizika.
 
Nasubiri kwa hamu, ngoma imefika kwenye koras, maana kwenda kutoa taarifa kanisan kuwa ndoa imeahirishwa napo patam!
 
nasubilia jioni nione mwisho wake ila naona masaa yanaenda taratibu sana, ngoja niende kwa wakala wa shetani nikaenjoy
 
[h=1]Usife kwanza mpenzi wangu (37)....[/h]
Mama Cleopatra baada ya kutoka chumbani na kuwaacha Deo na Cleopatra aliifuata simu yake chumbani kwake na kumpigia Levina ili kutafuta ukweli.
"Hujambo mwanangu?"

"Sijambo mama shikamoo..." Levina akasalimia.
"Marhaba...haya mbona mwenzio anafanya mambo ya ajabu unashindwa kuniambia binti yangu?"
"Nani mama? Patra?"
"Ndiyo!"

"Amefanya nini tena?"
"Unamjua Deo?"
"Ndiyo!"
"Unamjuaje?"

"Mama Deo alikuwa mpenzi wangu, lakini Patra kwa sababu ya fedha zake ak...." Levina alishindwa kumalizia sentesi yake na kuanza kulia.
SASA ENDELEA...

YALIKUWA maumivu makali sana kwa Levina ambaye alianza kukumbuka tangu siku ya kwanza alipokutana na Deo sokoni na kuvutiwa naye. Akakumbuka jinsi alivyofanya mbinu na kuhakikisha anaingia nyumbani kwao kama mfanyakazi wa ndani lakini ndani ya moyo wake akiwa na kitu tofauti kabisa na hicho.

Ni Levina huyo huyo ndiye aliyejitolea kumsomesha Deo hadi kufikia mafanikio na kupata kazi. Kunyang'anywa na rafiki yake mpenzi, waliokua na kusoma pamoja kulimuuma sana ndani ya nafsi yake. Alishindwa kuzuia hisia zake na kujikuta akianza kulia kwenye simu.

Alianza kwa sauti ndogo, lakini jinsi kumbukumbu zile mbaya zilivyozidi kumsumbua, ndivyo alivyozidisha kilio chake.
Mama Cleopatra akapata kazi ya kumbembeleza Levina.

"Pole sana mwanangu, naomba usilie, nimeshajua kila kitu na huyu kijana mwenyewe ameamua kuachana na Patra na kwa jinsi anavyoonekana, anajutia sana kitendo alichokifanya. Nahisi bado anakupenda na ni mapenzi hayo ndiyo yanayomsukuma kusema ukweli leo hii na kuamua kuachana naye.

"Kuna uwezekano mkubwa sana akarudi kwako na kukuomba msamaha, tafadhali naomba umsamehe na nitakuwa tayari kuwasaidia kwa namna yoyote. Najua thamani ya mapenzi mwanangu, najua maumivu ya kunyang'anywa mpenzi. Tafadhali mwanangu rudisha moyo wako, naomba umkubalie huyo kijana!" Mama Levina akasema kwa sauti ya utulivu sana.

"Kweli mama?"
"Ndiyo mwanangu!"
"Lakini unadhani Deo ana mapenzi ya kweli mama? Si ni aina ya wanaume ambao wanaweza kuyumbishwa ovyo?"
"Ni tamaa tu, halafu ukumbuke kwamba alikuwa na hofu ya kufukuzwa kazi."

"Mama, sasa ni kwanini asiwe na hofu na mimi ambaye ndiye niliyemtafutia hiyo kazi, akawa na wasiwasi wa kupoteza tu hiyo kazi bila kumkumbuka aliyemfanya akaipata?"

"Umeongea jambo la msingi sana mama, lakini ujue kwamba, shetani naye ana mambo yake. Naweza kusema kwamba alipitiwa, lakini kiukweli mwanangu mpatie nafasi nyingine, utaona mabadiliko yake. Atakuwa amejifunza."
"Sawa mama, nitajitahidi!"

"Siyo kujitahidi, naomba iwe hivyo!"
"Sawa mama."
"Niahidi Levina!"
"I promise you mom!" (Nakuahidi mama)
"Thank you my daughter!" (Nashukuru binti yangu)

Kila mmoja alikuwa na lake kichwani mwake, mama Cleopatra alikuwa na nia ya dhati ya kumsaidia Levina ambaye alikuwa sawa na mwanaye kwa namna walivyokuwa marafiki wakubwa. Bado aliona thamani yake kama mwanaye.

Hakufikiria juu ya aibu ya watu wengi walioalikwa kwa ajili ya sherehe hiyo, kwake yeye sherehe hiyo isingekuwa na maana kama ingefungwa ndoa huku Levina akilalamika.

Levina alifurahishwa sana na maelezo ya mama yake Cleopatra, alimuona mzazi bora ambaye anaangalia usawa na kuonesha mapenzi yake kwa watoto wake wote. Bado alikuwa akifikiri vizuri suala la kurudiana na Deo.
Moyoni mwake Deo alikuwepo!
Amejaa tele!

***
Mawimbi yalikuwa yanapiga kwa kasi sana ufukweni mwa Bahari ya Hindi eneo la Coco. Watu walikuwa wengi sana Jumamosi hiyo walipunga upepo baharini. Ilikuwa jioni, mishale ya saa 11:30, jua likianza kung'ang'ania kupotea na giza kusita kuchukua anga!

Ni kama vitu hivi viwili vilikuwa vikishindana, mashindano hayo yalifanya ufukwe kuwa na rangi kama ya dhahabu, mwanga kuwa hafifu kiasi na kupendezesha mandhari ya Ufukwe wa Coco.

Pembeni kabisa, juu ya jiwe kubwa, walikuwa wamekaa Deo na Levina, mikononi mwao kila mmoja alikuwa ameshika box lenye maji ya matunda wakinya taratibu kwa mrija. Levina ndiye aliyemwalika Deo kwa mtoko huo akitaka kuzungumza naye na kumpa masharti yake aliyosema anataka kumpa.

Deo alikuwa kimya akisubiri kusikia masharti ya Levina ambaye alikuwa amependeza sana jioni hiyo. Tayari Deo alikuwa ameshapona kabisa, afya yake ikianza kunawiri na makunyanzi usoni yakianza kupotea.

"Kwanza kabisa, naomba unisamehe kwa kukukosesha kazi. Najua kama siyo mimi, ungekuwa unaendelea na kazi yako. Kwa hilo naomba sana unisamehe Deo!" Levina alianza kwa kutamka maneno hayo.

"Hapana Levina usiseme hivyo, mimi ndiye mkosaji. Halafu hiyo kazi haina maana yoyote kwangu kama wewe hutakuwa na amani na mimi. Hutakuwa na furaha na mimi. Haitakuwa na maana yoyote kabisa. Napenda kuona unafurahi!"

"Deo lazima utambue kwamba nakupenda sana, nilikupenda kwa moyo wangu wote na nimeshindwa kukutoa moyoni mwangu!"
"Najua!"

"Nitakupa masharti mawili, najua ni magumu sana, lakini ukiyaweza nitakusamehe milele."
"Nipo tayari Levina niambie tu mama!"
"Labda nisisitize tena kwamba, nakupenda sana, siwezi kuacha kukupenda katika maisha yangu yote, sharti la kwanza ili nikusamehe Deo, unatakiwa ukubali kufunga ndoa na mimi!" Levina akasema akimwangalia Deo usoni.

"Kwa hilo nipo tayari, sijui kuhusu wazazi wako!"
"Mambo ya wazazi niachie mimi, kama umekubali basi vizuri, sharti la pili ni gumu kidogo, lakini nalo ukikubaliana nalo nitakusamehe!"
"Sema mpenzi, nipo tayari kwa chochote!"

"Deo naomba unisamehe kwa nitakalokuambia, najua litakuumiza na hutanielewa kirahisi, lakini ndiyo ukweli wenyewe. Naomba unielewe kwamba sikuwa na nia mbaya, nia yangu ilikuwa nzuri kabisa, lakini lazima unisamehe Deo!"
"Ni nini? Hebu niambie basi Levina..." akasema Deo akimkazia macho Levina.

"MIMI NDIYE NILIYEKODI WATU WAKUPIGE RISASI KWENYE LIFTI!" Levina akasema akilia.
"Unasemaje?" Deo akauliza kwa sauti ya ukali sana.


Je, nini kitatokea? Kwanini Levina alifanya yote hayo? Fuatilia sehemu ya mwisho baadae. Pia jiandae kusoma kitu kipya ‘THE DOUBLE FACE' (Sura Mbili) itakayoanza baada ya hii kuisha. Utaipenda!
 
[h=1]Usife kwanza mpenzi wangu (38)....[/h]
"Deo naomba unisamehe kwa nitakalokuambia, najua litakuumiza na hutanielewa kirahisi, lakini ndiyo ukweli wenyewe. Naomba unielewe kwamba sikuwa na nia mbaya, nia yangu ilikuwa nzuri kabisa, lakini lazima unisamehe Deo!"

"Ni nini? Hebu niambie basi Levina..." akasema Deo akimkazia macho Levina.
"MIMI NDIYE NILIYEKODI WATU WAKUPIGE RISASI KWENYE LIFTI!" Levina akasema akilia.
"Unasemaje?" Deo akauliza kwa sauti ya ukali sana.
SASA ENDELEA...

HAIKUWA rahisi kwa Deo kuamini kwamba Levina ndiye aliyefanya jaribio la kutaka kumuua, moyo wake ulibadilisha mapigo na hasira yake kuwa kubwa. Aliyatoa macho yake akimwangalia Levina, akiwa haamini kabisa kwamba angeweza kufanya kitendo kile.

"Levina ulitaka kuniua?" Deo akauliza kwa hasira.
"Siyo hivyo mpenzi wangu!"
"Siyo hivyo vipi na umekiri kwamba ulituma watu wanipige risasi.
"Deo kabla sijakuambia lazima nikupe masharti ili nikusamehe. Ni kweli nilifanya kosa, lakini kosa lenyewe ni katika kulinda penzi langu!"
"Ulitaka kuniua au kunilinda?"

"Kwani uliuawa?"
"Hapana."
"Kuna kitu uliibiwa?"
"Hapana!"

"Basi ndiyo unatakiwa kufahamu kwamba nilifanya hivyo kwa ajili ya kukupata. Deo sikuwa na njia nyingine, vinginevyo wewe ungefunga ndoa na Cleopatra. Sikiliza nikuambie Deo, mimi nakupenda sana, moyo wangu una mzigo mzito wa mapenzi ambayo siwezi kufananisha na kitu chochote."
"Sijui kama ni rahisi kukuelewa!"

"Lakini unataka kuelewa?"
"Ndiyo!"
"Ngoja nikusimulie..." Levina akasema akikaa sawa sawa kwa ajili ya kumweleza kisa kizima kilivyokuwa.

***
Alikuwa amekaa mwenyewe kwenye meza ya peke yake, macho yake yakiangaza kila upande, ni kama alikuwa anawasubiri watu wafike katika baa ile. Ilikuwa ni usiku wa saa mbili na dakika zake, Levina ametulia kwenye kona akinywa soda yake taratibu kabisa.

Akiwa anaendelea kuangaza macho yake, simu yake ikaita. Haraka akapokea akiangalia kwenye mlango mkubwa wa kuingilia pale baa.
"Yes..." akatamka Levina akisubiri sauti ya upande wa pili.
"Ni wewe uliyekaa hapo kwenye kona peke yako?"
"Ndiyo!"

"Ok! Tunakuja, nimeshakuona!" Sauti nzito ya kiume ilisikika kwenye spika za simu ya Levina.
Dakika moja baadaye, wanaume watatu walikuwa wamekaa kwenye viti kuizunguka meza aliyokuwa amekaa yeye. Walisalimiana kisha wote wakakaa kimya.

"Karibuni sana, mimi ndiye Levina niliyemuagiza Asnath awatafute, nimefurahi kukutana nanyi!" Akasema Levina.
"Hata sisi pia."
"Kama Asnath alivyowaambia, sina haja ya kumuua huyo jamaa, hakikisheni mnampiga risasi ya bega, nataka alazwe, mambo mengine nitamaliza mwenyewe!"

"Unataka hiyo kazi ikamilike baada ya muda gani?" Mmoja wao akauliza.
"Ndani ya wiki moja kutoka sasa, unajua amebakiza siku chache sana kabla ya kufunga ndoa, ni hiyo ndiyo ambayo sitaki ifungwe!"
"Sawa, chetu?"

"Ninazo...naona niwalipe nusu kwanza, kazi ikikamilika nitawamalizia. Chukua hii..." akasema Levina akimkabidhi bahasha iliyovimba!
"Ahsante sana, hatuna muda wa kusubiri zaidi, kila kitu umeshatuelekeza kwenye simu, namba yake ya simu tunayo, anapofanyia kazi tunapajua, kazi iliyobaki ni ndogo sana, ni kumfuatilia baasi!"

"Sawa, nawatakieni kazi njema yenye mafanikio!"
"Itakuwa hivyo, usijali!"
"Ok! Poa."
Wale vijana wakasimama na kumuacha Levina akiwa amekaa kimya sehemu ile. Moyoni mwake alitamani sana zoezi lile likamilike, hakutaka kabisa Cleopatra afunge ndoa na Deo, mwanaume wa maisha yake.

"Tutaona sasa, mimi si katili, lakini wakati mwingine inabidi ili niweze kutetea penzi langu, naamini sasa nitafanikiwa," akawaza Levina akisimama na kutoka katika baa hiyo.

***
Deo aligandisha macho yake usoni mwa Levina akiwa haamini kabisa anachosimuliwa, hakutegemea kama Levina angefanya tukio kubwa kiasi kile.
"Lakini levina hukuwa na njia nyingine zaidi ya hiyo?" Deo akamwuliza akiwa ameyatoa macho yake.

"Unadhani ningetumia njia gani hapo? Hata kama ni wewe ungetumia njia gani?"
"Kwanini usingenitafuta tukaongea?"
"Deo ulikuwa unatafutika wewe? Hata simu yangu ulikuwa unaiona kama kinyaa, sikuwa na njia nyingine Deo, naomba unisamehe lakini nitakusamehe kama na wewe utanisamehe na kutimiza ahadi zako zote!"

Deo akatulia kwa muda akatafakari, aliyaona makosa yake lakini pia aligundua kwamba Levina hakuwa na njia nyingine ya kufanya zaidi ya tukio alilolifanya ambalo liliweza kuwarudisha tena pamoja.

Alipata maumivu makali sana, aliteseka sana hospitalini, lakini mwisho wa siku aligundua wakulaumiwa ni yeye mwenyewe. "Nimekusamehe Levina!"
"Nimekusamehe pia Deo!"
"Sasa?" Deo akauliza akiwa anamwangalia Levina machoni.
"Nini tena mpenzi wangu?"

"Kuhusu ndoa, itawezekana kweli kuoana?"
"Nini kinachoshindikana chini ya jua?"
"Wazazi wako baby, hawanitaki kabisa hilo ndiyo tatizo."
"Kuna kitu nilikuwa sijakuambia sweetie!"
"Kitu gani?"

"Nilishaongea na mama kila kitu...hakuna tatizo tena, mzee Massamu huwa haongei kwa mkewe Diana. Lazima kieleweke, kwa hiyo ondoa shaka mpenzi wangu. Tutapanda madhabahuni na kufunga ndoa yetu!"
"Kweli dear?" Deo akauliza akiwa ametoa macho.
"Niamini mimi mpenzi wangu!"

Deo na Levina wakasimama, kisha wakakumbatiana. Hawakuogopa macho ya watu. Walichojua wao ni kitu kimoja tu, kuwa wanapendana!
Kama Levina alivyosema, haikuwa kazi ngumu mama yake kumshawishi baba yake mzee Massamu kuhusu Deo kumuoa Levina hasa kwa kuwa tayari alikuwa na sifa walizokuwa wanazihitaji.

Deo akasafiri hadi nyumbani kwao Singida, akawaeleza wazazi wake juu ya kupata mchumba, hakuna aliyepingana naye. Taratibu zote zikafanyika, ndoa ya kifahari ikafungwa jijini Dar es Salaam.

Watu wengi sana walihudhuria, akiwemo Cleopatra ambaye tayari walishaweka mambo sawa. Mama yake Cleopatra ndiye aliyewakutanisha na kuwapatanisha. Jambo la kushangaza zaidi, Cleopatra ndiye alikuwa Mweka Hazina wa kamati ya sherehe ya Deo na Levina.

Ukawa mwisho wa machozi kwa Levina na mwanzo wa maisha ya furaha, akiwa na mwanaume aliyeota kuwa naye, mwanaume aliyemuhangaikia kwa muda; aliyekuwa tayari kufanya chochote kwa ajili yake.
Mwanaume wa maisha yake!


...Mwisho...

Nawashukuru sana wasomaji wangu wapenzi kwa kufuatilia simulizi hii kuanzia mwanzo hadi mwisho, naamini haijakuacha kama ulivyokuwa, kuna kitu umejifunza. Wiki ijayo naanza simulizi yangu mpya ya kusisimua zaidi ya hii, inaitwa ‘THE DOUBLE FACE' (Sura Mbili) USIKOSE!
 
***
MIAKA MITATU BAADAYE
Deo alifanikiwa kumaliza salama masomo yake
na kupata kazi kama mhasibu wa Kampuni ya
Usafirishaji Mizigo ya Snox Carries LTD ya jijini
Dar es Salaam. Kwa upande wa Levina tayari
alishajifungua mtoto wa kike aliyekuwa na umri
wa mwaka mmoja na miezi kadhaa, waliyempa
jina la Precious wakiwa na maana ya kitu cha
thamani.
Baada ya kupata mtoto, maisha yalibadilika
sana na sasa wakawa wanatumia muda mwingi
kumuhudumia na kumfikiria mtoto wao kuliko
wanavyojijali wao.
Deo alikuwa akirudi nyumbani kutoka kazini
anamsaidia mkewe malezi ya mtoto wao
Precious. Pesa walizopata walizitumia pamoja
kufanya mambo mbalimbali ya kimaendeleo.
Maisha yao kwa ujumla yalibadilika na
usingeweza kudhani kuwa huyu ndiye Deo wa
miaka ile.
“Levina! Nadhani sasa wewe ni mke wangu na
nina mamlaka yote juu yako na wewe una
mamlaka juu yangu,” aliongea Deo jioni moja
wakiwa wanapunga upepo kwenye bustani ya
maua nje ya nyumba wanayoishi.
“Ni kweli mume wangu!”
“Lakini mbona siku hizi hutaki mimi niguse
simu yako kama zamani, unapigiwa simu usiku
halafu unaenda kupokelea nje na wakati
mwingine unaikata mbele ya macho yangu,
tatizo nini?”
“Wewe nawe kwa wivuu! Hakuna anayekuzidi
mume wangu kwa kila kitu, siwezi kutoka nje
na kukusaliti, amini nakwambia Deo, mimi ni
wako peke yako…” alisema Levina huku
akimsugua sugua mumewe mgongoni kimahaba.
Licha ya kujibiwa hivyo, Deo alibaki na
dukuduku moyoni kwani mabadiliko ya mkewe
yalishaanza kumtia hofu. Tangu mkewe aache
kunyonyesha miezi michache iliyopita, alianza
tabia za ajabu ambazo zilimfanya ahisi anaibiwa
mali zake. Mkewe alikuwa akichelewa kurudi
nyumbani bila sababu za kueleweka, na
alipokuwa akimuuliza kisingizio kikubwa
kilikuwa ni ubize wa kazi.
Siku nyingine alikuwa akirudi nyumbani
ananukia pombe, hali iliyotoa ishara kuwa
tayari mwenzake anamsaliti. Shughuli zote za
kumlea mtoto zikabaki kwa Deo na msichana
wa kazi aliyetafutwa kwa lazima baada ya
kuona Levina ameanza kubadilika. Ilifika
mahali hata suala la kufurahishana faragha
likaanza kupungua taratibu.
“Najua umenisaidia sana maishani Levina, Bila
wewe nisingekuwa hapa nilipo leo, lakini kaa
ukitambua kuwa mabadiliko yako ya tabia
unayonionesha kwa sasa yanauumiza sana
mtima wangu.
“Kama kuna kosa nililokuudhi niambie na
naahidi nitajirekebisha kwani bado nakuhitaji
Levina wangu.” Uzalendo ulishaanza kumshinda
Deo, ikafika mahali akawa anamwaga machozi
mbele ya mkewe akimsihi ajirudi kama
alivyokuwa hapo mwanzo.
Jibu la Levina siku zote lilikuwa ni kwamba
anampenda Deo na kamwe hawezi kumsaliti,
lakini kumbe nyuma ya pazia alikuwa
akimfanyia mambo ya kusikitisha sana.
Usiku mmoja, Deo akiwa na mwanae mdogo
Precious sebuleni, mkewe alichelewa kurudi,
na hata aliporudi saa tano usiku alikuwa
akipepesuka na kunuka pombe. Alipoingia
ndani, aliweka simu yake mezani na kupitiliza
bafuni kwenda kuoga.
Akiwa bafuni, ujumbe mfupi wa simu uliingia
kwenye simu yake, Deo akaiwahi na kuichukua
kutaka kujua ni nani aliyemtumia meseji mkewe
usiku wote ule.
Alipoifungua na kuisoma, hakuamini macho
yake…akarudia kuisoma tena… akajikuta mwili
wote ukiishiwa nguvu. Wakati anaisoma kwa
mara ya tatu, mkewe akawa anatoka bafuni.
Macho yao yakagongana


(((((((())))))))))
HAPA MKUU MZZ MKAVU...IKIKUWA NDOTO NN MMAANA CJAELEWA MKUU
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom