MziziMkavu nimeipenda sana hadithi yako.Wahusika Wakuu wote wamelipwa kulingana na Matendo yao.Deo amepata mateso makubwa kwa kosa la kutaka kumsaliti Levina,Cleopartra nae kapata Maumivu makubwa kwa Kosa la kutaka kumdhulumu rafiki yake Boyfriend,Levina amepata Mateso makubwa Moyoni kwa Kosa la Kumzushia Uongo Mtumishi wao mwaminifu Rashid.KwaMaumivu hayo kila Mtu amepata somo.Somo lingine tunalolipata hapa ni kutoka kwa Levina kwamba kila kitu ukikiwekea malengo ya dhati utafanikiwa.Nakushukuru sana Mzizimkavu kwa Mafundisho uliyotupatia.