Usifanye Masters kama lengo lako sio kutafuta PHD

hizo managerial post utazipata serikalini labda.. kwa magu mpenda vyeti... huku private sector kama voda, puma, airtel, tigo. wanataka output.. yaani mtengeneza pesa.. ndie wanampa ma vyeo.. kina kelvin twissa, hawana hata hizo master zenu.. ceo wa safari com hata degree moja hana..

voda ceo hana masters, airtel ceo hana masters, juzi voda walimpa u bosi mama lishe.. na degree yake ya kupika ugali.. sababu ni anajua kuuza na kuleta pesa...

ukitaka ma vyeo zama hizi jifunze kuuza bidhaa,,, na kuletea kampuni mahela... mambo ya masters ni theory tupu achana nayo

Logic yako ni nini hasa ?
Unadhani kampuni zote za direct marketing haziitaji sana mwenye elimu sasa nini maana ya kusoma
 
Habari wadau;
Wikiendi iliopita nilikuwa katika mjadala na Rafiki yangu wa siku nyingi ambaye tulipotezana zaidi ya miaka 10 iliopita.Tulikuwa tukijadili safari ya kitaaluma na swala la Masomo.Katika Mjadala tuligusia swala elimu ya Ngazi ya Masters Degree na katika mjadala nilimucha na changamoto moja kwamba,Inapendeza na ni busara zaidi unapoamua kujiunga kwa ajili ya Masomo ya Masters katika Fani yoyote basi lengo lako lisiwe kuishia kwenye Masters bali uwe unalenga kutafuta PHD.

Kwa maana hio nilimwambia ni vizuri eneo utakalochagua kulifanyia utafiti liwe ni eneo ambalo unaweza kuzama zaidi na hata kutoa andika linalofaa kwa ajili ya PHD

Nilimsisitizia kwamba ukweli ni kwamba unaposoma Masters kwa ajili ya kutafuta PHD basi unakuwa na nafasi kubwa zaidi ya kupata PHD kuliko unaposoma masters kwa sababu unao uwezo wa kulipa ada au kwa sababu unafikiri utapata Mshahara Mkubwa.

Ingawa Mjadala haukufika mwisho ila nimesema niuliete hapa Jamvini kama ni busara kwa mtu kusoma Masters akiwa hana hata wazo wala mpango wa kusoma PHD.Si ni bora akasubiri mpaka ule wakati ambapo atakauwa na maono ya kupata PHD no aingie kilingeni?
Umemdanganya sana huyo jamaa yako, na umechanganya sana madesa. Si lazima usome Masters kwa lengo la kuwa na PhD. Ila ni muhimu ukasoma PhD ukiwa na sababu za msingi za kufanya hivyo, vinginevyo utakuwa umepoteza muda wako na rasilimali pesa bure, kwani inaweza isikulipe kabisa.
 
Back
Top Bottom