Kikwava
JF-Expert Member
- Sep 6, 2015
- 1,121
- 527
Habari.
Kwasasa dunia inafanya mapitio ya mitaala ya kufundshia/kujifunza huko mashuleni, huku swala la elimu za walimu ambao ndio wadau wa mitaala hiyo likiwa gizani. Kwa mfano, kwa Tanzania muundo wa kiutumishi wa walimu wa shule za msingi na sekondari unaanzia elimu ya cheti hadi shahada ya kwanza tu, ambapo mwalimu akiwa na shahada ya pili (masters/PhD), mfumo haumtambui kimasilahi na kimuundo, tofauti na nchi zingine kama Kenya, South Africa, Nigeria, Zimbabwe na kwingineko.
Serikali ingelitazama hili swala kwa jicho la utatu kwa kuwaandalia muundo wa kiutumishi na kimasilahi walimu wenye shahada ya pili (masters/PhD) waliopo huko mashuleni. Ifikie kipindi sasa iwe ni kawaida kumwona mwalimu mwenye PhD anafundsha shule za msingi huko. Hii ishu italeta mapinduzi makubwa sana kwenye idara ya elimu na ualimu hasa huko mashuleni, tofauti na sasa ambapo mwalimu akishapata shahada ya pili tu huanza kuomba kuhamia idara zingine ambapo anaona atapata maslahi kulingana na elimu aliyonayo. Wakati huo elimu yake (masters/PhD) ingetambulika kimuundo na kimasilahi, angepata utulivu kituoni pale alipokuwa anafundisha bila kutafuta fursa mahali pengine.
Napenda kuwasilisha.