Nashauri serikali itumie zaidi wanafunzi wa masters, PhD na PostDoc kufanya tafiti na kuchapisha maandiko kama tunataka kufika mbali katika tafiti

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Jul 7, 2020
6,283
8,196
Kama kweli serikali ina mpango wa kuhamasisha wanazuoni wa vyuo vikuu vya Tanzania kufanya tafiti na kuchapisha maandiko katika majarida makubwa ya kimataifa, napendekeza yafuatayo:

1. Serikali itenge fedha kwa ajili ya ufadhili wa wanafunzi wa masters, PhD na PostDoc kila mwaka kama mataifa mengine yanavyofanya.

2. Serikali itenge fedha za kumzawadia kila mwanazuoni atakayechapisha makala kulingana na sifa ya jarida kwa kuangalia impact factor ya jarida hilo.

3. Serikali iwaajiri zaidi wanafunzi wa PostDoc kwa mkataba kushughulikia suala zima la kufanya tafiti na uchapishaji wa maandiko ili kuhakikisha vyuo vyetu vinachapisha mara kwa mara na kuendelea kubakia kwenye nafasi za juu kidunia.

4. Serikali iweke sharti la kuchapisha angalau andiko moja kwenye jarida lenye sifa ya kimataifa ili mwanafunzi aweze kuhitimu Masters katika vyuo vyetu.

5. Serikali iweke sharti la kuchapisha angalau makala mbili kwenye majarida yenye impact factor kubwa ili mwanafunzi aweze kuhitimu PhD katika vyuo vyetu.

Katika hili, serikali inapaswa kuwatumia zaidi wanafunzi waliofaulu vizuri katika shahada zao, yaani wenye GPA kubwa kutoka vyuo vikuu vikubwa zaidi. Wanafunzi waliofuzu vizuri ndio wenye uwezo wa kuandika zaidi na kufanya tafiti kwa sababu wanapenda kusoma.

Wahadhiri wasisitizwe zaidi kuwa wasimamizi na kuwaongoza wanafunzi katika mchakato mzima wa kufanya tafiti na kuchapisha maandiko. Katika kufanikisha hili, panahitajika ushirikiano mkubwa kati ya serikali, wahadhiri na wanafunzi.

Mwisho, naomba kuishukuru serikali kwa kutambua umuhimu wa suala zima la utafiti katika taifa letu.
 
Kama tu kuweka madawati ya kutosha achilia mbali vitabu vya kujifunzia kwa kila shule nchini wameshindwa, wataweza kuweka Bajeti za ufadhiri wa wanafunzi!!

Tanzania hatuna viongozi bali tuna Wanasiasa wengi ambao kazi yao ni kuwaza uchaguzi na program za Maendeleo za muda mfupi.Viongozi huwa wana tabia ya kuwa na vision ya kupeleka mataifa yao mbele.
Wewe umewahi kumsikia Biden anaongelea uchaguzi ujao?

Rais anaapishwa tu,kesho anaanza kuwaza uchaguzi!!!
 
Wahadhiri wasisitizwe zaidi kuwa wasimamizi na kuwaongoza wanafunzi katika mchakato mzima wa kufanya tafiti na kuchapisha maandiko. Katika kufanikisha hili, panahitajika ushirikiano mkubwa kati ya serikali, wahadhiri na wanafunzi.

Mwisho, naomba kuishukuru serikali kwa kutambua umuhimu wa suala zima la utafiti katika taifa letu.
Serikali na vyuo hapa Tz vinawekeza hasa kwenye majengo lakini allocation of public funding in researches is very minimal
 
tafiti na maendelezo. Research and development.
💯🤝

Hakuna ukuzi ikiwa hakuna uwekezaji kwenye Research and Development (R&D) iwe ni kwa level ya taifa au hata level ya firm

Leo tunaona South Korea, China, India, Singapore uchumi wao na teknolojia vimekuwa kwa kasi sio muujiza ni kwa sababu waliwekeza kwenye R&D

Hata makampuni makubwa kama Apple, SAMSUNG, Microsoft, Huawei, Amazon, Meta n.k yanazidi kufanya vizuri na kuja na new innovations kwa sababu wanamwaga mpunga wa kutosha kwenye R&D
 
Wasomi wa Tanzania, viwango ni vya Chini Sana, hivyo hata hizo research zitakuwa na kiwango Cha Chini Sana, tuwalete Wageni Kutoka Harvard,Waseda, Oxford, waje wafanye research na sio hawa wa Kutafuta uteuzi.
 
Kama kweli serikali ina mpango wa kuhamasisha wanazuoni wa vyuo vikuu vya Tanzania kufanya tafiti na kuchapisha maandiko katika majarida makubwa ya kimataifa, napendekeza yafuatayo:

1. Serikali itenge fedha kwa ajili ya ufadhili wa wanafunzi wa masters, PhD na PostDoc kila mwaka kama mataifa mengine yanavyofanya.

2. Serikali itenge fedha za kumzawadia kila mwanazuoni atakayechapisha makala kulingana na sifa ya jarida kwa kuangalia impact factor ya jarida hilo.

3. Serikali iwaajiri zaidi wanafunzi wa PostDoc kwa mkataba kushughulikia suala zima la kufanya tafiti na uchapishaji wa maandiko ili kuhakikisha vyuo vyetu vinachapisha mara kwa mara na kuendelea kubakia kwenye nafasi za juu kidunia.

4. Serikali iweke sharti la kuchapisha angalau andiko moja kwenye jarida lenye sifa ya kimataifa ili mwanafunzi aweze kuhitimu Masters katika vyuo vyetu.

5. Serikali iweke sharti la kuchapisha angalau makala mbili kwenye majarida yenye impact factor kubwa ili mwanafunzi aweze kuhitimu PhD katika vyuo vyetu.

Katika hili, serikali inapaswa kuwatumia zaidi wanafunzi waliofaulu vizuri katika shahada zao, yaani wenye GPA kubwa kutoka vyuo vikuu vikubwa zaidi. Wanafunzi waliofuzu vizuri ndio wenye uwezo wa kuandika zaidi na kufanya tafiti kwa sababu wanapenda kusoma.

Wahadhiri wasisitizwe zaidi kuwa wasimamizi na kuwaongoza wanafunzi katika mchakato mzima wa kufanya tafiti na kuchapisha maandiko. Katika kufanikisha hili, panahitajika ushirikiano mkubwa kati ya serikali, wahadhiri na wanafunzi.

Mwisho, naomba kuishukuru serikali kwa kutambua umuhimu wa suala zima la utafiti katika taifa letu.
Point 5 nzuri sana. Naomba niongee mbili:

6. Serikali ibadili au kuifuta kabisa Sheria ya ya takwimu iliyotungwa miaka ya karibuni inayosema mtu asichapishe matokeo ya utafiti mpaka ukubaliwe na Mtakwimu Mkuu. Hii tabia ya kutaka ku control knowledge iko kinyume kabisa na knowledge creation.
7. Kuna tatizo kubwa kati ya Research na Development hadi commercialization (wengine wanaita monitization).Research nyingi zinabaki kwenye makaratasi. Serikali itoe ufadhili/tax incentives kwa makampuni makubwa na madogo Ili yashirikiane na Researchers mbali mbali kuwezesha kuhama kutoka kwenye research kwenda kwenye development mpaka commercialization. Mataifa mengi yaliyoendelea Duniani yanafanya hivyo
 
Kama kweli serikali ina mpango wa kuhamasisha wanazuoni wa vyuo vikuu vya Tanzania kufanya tafiti na kuchapisha maandiko katika majarida makubwa ya kimataifa, napendekeza yafuatayo:

1. Serikali itenge fedha kwa ajili ya ufadhili wa wanafunzi wa masters, PhD na PostDoc kila mwaka kama mataifa mengine yanavyofanya.

2. Serikali itenge fedha za kumzawadia kila mwanazuoni atakayechapisha makala kulingana na sifa ya jarida kwa kuangalia impact factor ya jarida hilo.

3. Serikali iwaajiri zaidi wanafunzi wa PostDoc kwa mkataba kushughulikia suala zima la kufanya tafiti na uchapishaji wa maandiko ili kuhakikisha vyuo vyetu vinachapisha mara kwa mara na kuendelea kubakia kwenye nafasi za juu kidunia.

4. Serikali iweke sharti la kuchapisha angalau andiko moja kwenye jarida lenye sifa ya kimataifa ili mwanafunzi aweze kuhitimu Masters katika vyuo vyetu.

5. Serikali iweke sharti la kuchapisha angalau makala mbili kwenye majarida yenye impact factor kubwa ili mwanafunzi aweze kuhitimu PhD katika vyuo vyetu.

Katika hili, serikali inapaswa kuwatumia zaidi wanafunzi waliofaulu vizuri katika shahada zao, yaani wenye GPA kubwa kutoka vyuo vikuu vikubwa zaidi. Wanafunzi waliofuzu vizuri ndio wenye uwezo wa kuandika zaidi na kufanya tafiti kwa sababu wanapenda kusoma.

Wahadhiri wasisitizwe zaidi kuwa wasimamizi na kuwaongoza wanafunzi katika mchakato mzima wa kufanya tafiti na kuchapisha maandiko. Katika kufanikisha hili, panahitajika ushirikiano mkubwa kati ya serikali, wahadhiri na wanafunzi.

Mwisho, naomba kuishukuru serikali kwa kutambua umuhimu wa suala zima la utafiti katika taifa letu.
WASOMI HAWA HAWA WANAOSHINDA WANA BET?
 
Wasomi bongo ni weupe mno kichwani..wengi wanaongeza master na PhD lengo kubwa ni kupanda position.
 
Back
Top Bottom